katuni - The Health COMpass

Transcription

katuni - The Health COMpass
ISSN: 0856-8995
Haliuzwi
KATUNI:
Kilimo
kinalipa
Ramani ya Tanzania
Kilimo kina thamani na kinaweza
kuwa sekta yenye faida kubwa
kwa sababu watu wanahitaji
kula, soko la bidhaa za kilimo
linakuwepo kila wakati hususani
mazao cha ya chakula.
Changamkia jembe
kwa sababu kilimo ni
fedha! Kifanye kuwa
shughuli yako rasmi
ufaidike na kilimo.
2 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013
Si Mchezo! Huzalishwa na
kusambazwa.
Si Mchezo! husambazwa.
Lilikozalishwa toleo hili.
YALIYOMO
4 Stori Yangu: Kilimo kinalipa
6 Mambo Mapya
8 Hadithi ya Picha: Ujanja shambani!
Mhariri
Majuka Ololkeri
12 Je, Wajua: Maofisa ugani ndiyo nguzo ya kilimo
Waandishi
Raphael Nyoni
Rebeca Gyumi
16 Burudani: Moro All Stars
Washauri
Timu ya Femina HIP
Betty Liduke
Mkurugenzi Mtendaji
Dr. Minou Fuglesang
Mkurugenzi wa Habari
Amabilis Batamula
Meneja Machapisho
Jiang Alipo
Meneja Uhusiano
Lilian Nsemwa
Katuni na Usanifu
BabaTau, Inc.
Mpiga Chapa
Jamana Printers Ltd
Usambazaji
EAM Logistic Ltd
Femina HIP na Washirika
Si Mchezo! limefanyika kwa
hisani kubwa ya Serikali za
Sweden (Sida), Denmark
(DANIDA), na mashirika ya
HIVOS, RFSU, Marie Stopes,
Mama Misitu, TWAWEZA na
JHU-CCP/TCCP.
Yaliyomo humu ndani ni
jukumu la Femina HIP na
hayawakilishi maoni au
mitazamo ya wafadhili.
14 Sauti yangu
18 Ruka Juu: Ruka juu na jembe
20 Nguvu za mwanaume
21 Nguvu za mwanamke
22 Chezasalama: Jipange, usije ukavuna mabua!...
24 Katuni: Chakarika jembe likutoe
27 Ukweli wa mambo: Kilimo ni tumaini la wengi
28 Sema Tenda: Kilimobiashara ni zaidi ya ujuavyo
30 Marie Stopes: Waelimisharika Zanzibar, walia na utoaji mimba
31 Ushauri
TAHARIRI
Heri ya Mwaka Mpya wapenzi wasomaji wetu. Mwaka huu tumetuliza
vichwa na kubadilisha vitu vingi kwenye jarida lengo likiwa kukuletea
vitu adimu kivingine. Yote haya yametokana pia na mawazo yenu
mnayotutumia. Toleo hili tumezungumzia masuala ya kilimo. Bila shaka
kila mmoja anajua kuwa kilimo ndiyo uti wa mgongo wa Mtanzania.
Tufunguke katika kilimo! Karibu.
Majuka
Ruka Juu kijanja
Kijana jitume
shambani...
...Peta maishani
Wasiliana nasi kwa:
S.L.P. 2065, Dar es Salaam
Simu: (22) 212 8265, 2126851/2
Fax: (22) 2110842
email: simchezo@feminahip.
or.tz
Si Mchezo! huchapishwa na
Femina HIP.
Sms: Andika SM acha nafasi
andika maoni yako kisha
tuma kwenda 15665
3
STORI YANGU
Kilimo kinalipa
M
tanange wa kusaka maisha nilianza siku
nyingi na niliyoyapitia ni mengi lakini
nataka nizungumzie machache tu kati ya hayo.
Najua vijana wengi tumepitia magumu kama
yangu na ni haki ya kila mmoja kuwa huru
kutoa historia yake. Nimeamua kufunguka
ili kuwaelimisha wengine juu ya umuhimu
wa kubadili uamuzi pale ‘unapobugi step’.
Naitwa Nesho Festo Madepana (25), mzaliwa wa
Kijiji cha Zombo, Kilosa. Nilimaliza elimu ya msingi
mwaka 2002 hapa Zombo na sikufaulu kuendelea
na elimu ya sekondari. ingawa nilikuwa na nia ya
kujiendeleza kielimu. Nilijishughulisha na vibarua
mbalimbali nikiwa na lengo la kuwa na pesa ya
kianzio kwani wazazi wangu hawakuwa na uwezo
wa kunisomesha. Nilipata pesa kiasi ambazo
nilitumia kufuatilia kujiunga VETA Mikumi
ambapo baba alikubali kunilipia ada. Nilikubaliwa
chuoni hapo nikaanza masomo ya ufundi magari
mwaka 2003. Baada ya miezi kadhaa nilifukuzwa
chuo kwani baba hakuweza kulipa ada na sikuwa
na uwezo wa kujilipia. Hapo ndipo nikaanza
kuonja ‘joto ya jiwe’ katika maisha.
Nilikaa Mikumi kwa kipindi fulani nikisoma
‘ramani’ ya jinsi gani naweza kuendelea. Nilijiunga
na Kikundi cha Sanaa cha Wanyonge Family
kama mwanamuziki nikawa natunga na kuimba
nyimbo. Hatukufanikiwa kiviile kwani hatukuwa
na mtaji. Mwaka 2004 nikarudi nyumbani, safari
hii nikamuomba baba shamba la kulima na
akanipatia hekari moja.
Nilianza kulima mahindi peke yake, nilipovuna
mara ya kwanza nilipata magunia 12 kwa hekari
4 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013
Mambo yote shambani: Nesho akiwa na mkewe
wakionyesha mazao yao.
moja. Niliuza yote nikapata 230,000/- nikiwa na
lengo la kwenda Bongo kufungua biashara ya kuuza
chipsi. Nilitua Jijini mwaka 2005 nikaweka kambi
Tabata. Nilijaribu zali la chipsi pale Mwenge lakini
niligonga mwamba baada ya kupiga mahesabu
na kugundua kuwa gharama za kufungua banda
la kuuzia chipsi ni 180,000/- na pesa nitakazobaki
nazo hazitanitosha kujikimu Jijini. Nilipoona
hivyo nilibadilisha mawazo na kwenda Kariakoo,
nikanunua belo la suruali kadhaa za ‘jeans’ kwa ajili
ya biashara, nikanunulia na mbegu za matikiti maji,
nikaamua kurudi nyumbani.
hatua kimaendeleo. Waliniumiza akili sana. Niliuza
zile jeans na pesa hiyo nikafungua banda la kuuza
chipsi hapa Zombo huku nikiendelea na kilimo.
Mwanzoni tulishirikiana na baba kulima pilipili
kwa ajili ya biashara. Nilikuwa nikizipeleka Bongo
tatizo likawa soko duni. Hatukuwahi kupata faida
Niliporudi nyumbani mwaka 2006 niliwakuta kwani bei zilikuwa ndogo sana. Biashara ya chipsi
wenzangu ambao tulimaliza wote elimu ya msingi haikuendelea kwani nilishindwa kuendesha zote
waliotulia wakaamua kuwa wakulima wamepiga kwa pamoja. Niliamua kulima nyanya maji, huku
nikijishughulisha na vibarua ili niweze kupata pesa
za kununua dawa ya kuua wadudu shambani.
Nilipovuna, nikabahatisha msimu mzuri wa
biashara nikauza plastiki moja kwa bei ya 4000/nikapata 280,000/-. Nikaanza kujitegemea mwaka
2007. Nilinunua shamba la hekari tatu. Baadaye
nikaweza kununua pampu ya kumwagilia. Mpaka
sasa nimegundua siri iliyopo kwenye kilimo
kuwa kinalipa! Imenifanya niwe na matumaini ya
maendeleo hapo baadaye. Mbali na kilimo hicho
pia nafuga nguruwe watatu sasa.
Wengine wana fikra potofu kuwa kilimo hakina tija
lakini nimekuwa mmoja wa wale wanaoombwa
buku kitaani! Hivyo kijana jipange na anza
upya sasa. Nina mengi ya kuwashauri vijana.
Unapojaribu kitu ukagundua kuwa hakina tija,
usione ujinga kuanza upya! Tuepukane na makundi
rika yanayotupotosha.
Maisha ni kupeta kwa Nesho na mkewe, baada ya
kujikita kwenye kilimo.
Nimeoa, mimi na mke wangu tunapendana,
tunaheshimiana, tunalindana na tunasaidiana kazi.
Najipanga ili niweze kujenga nyumba ya kuishi
na pia kujiendeleza kielimu ili kuongeza ufanisi
kwenye kilimo.
JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo!
5
mambo mapya
Uchumi Flower
Majengo yanakaa bure haya!
Hivi Tanzania tutaendelea kutegemea misaada
mpaka lini? Yaani inatia uchungu kuona haya
majengo ya Ilonga Youth Centre yamekaa tu bila
ya hata ya kutumika kwa kukosa fedha na hata
yakitumika basi ni kwa kipindi kifupi cha mafunzo
ya wiki mbili tu! Majengo haya pamoja na mandhari yake yanafaa yakatumika kwa kuwa chuo cha
elimu ya juu kuanzia ngazi ya stashahada ya kilimo
kama tu wizara husika itaamua kufanya kweli.
Wajumbe walikaa na kuunda kikundi
cha Uchumi Flower mwaka 2009
chenye makao yake makuu kijiji cha
Mhenda, Kilosa. Jamaa wamejipanga
ile mbaya kujikwamua kwa kutumia
mashamba ya wanachama kulima
alizeti. Penye nia pana njia, wamepata mkopo wa mashine ya kukamua
alizeti kutoka halmashauri ya wilaya.
Unajua nini? Imesaidia sana wanakijiji kupunguza gharama za kwenda
kukamua alizeti na wao wanajiingizia
kipato kutokana na kilimo.
Boda boda
Waendesha pikipiki wa mikoani
wanasifika kwa kuzingatia sheria za
barabarani, lakini huyu braza wa Gairo
yeye sijui vipi? Lori linaovateki na jamaa
nae akaona ‘apige mande,. Haraka izingatie usalama na sheria za barabarani.
Wakati unawahi ishu zako, kumbuka
na majukumu yako kwa watu wanaokutegemea katika jamii.
6 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013
RUKA jUU
Young Farmers
in Business
Kuanzia Machi 2013,
Femina itakuletea Ruka Juu TV show
Usicheze mbali na luninga yako
ITV kila Jumamosi saa 1 usiku
TBC1 Kila Jumapili saa 3 usiku
Funguka shambani peta maishani na Fema Radio.
RFA kila Jumatatu saa 2.45 usiku
TBC FM kila Jumanne saa 3 usiku
JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo!
7
unauhakika nae? shauri
yako! baadae usije lia
wakati mwenzio
nachekelea mavuno!
azikiwe na wanija ni
marafiki tangu
wanasoma.wanashiriki
shana mambo mengi,
japo wanasikilizana na
wakati mwingine
kutofautiana.
Wamemaliza kidato cha
nne na sasa
wameanza maisha
ambayo ni funzo
kwetu sote kujua ni
jinsi gani kila mmoja
alivyoanza maisha ya
mtaani na sasa
anafanya nini.
Tufuatilie mchezo huu
na tujielimishe
haya sasa,
azikiwe na wanija
wamemaliza
masomo na
matokeo ya
mtihani
yameshatoka na
wamefeli.Changa
moto iko mbele
yao juu ya maisha
ya baadae, hebu
tuwafuatilie
kuona nini
kitajiri kwao
unaonaje
tukianzisha bustani ya
mbogamboga ili
tujipatie kipato?
shoga
mbona hivyo!
subiri majibu
yatoke ndio
tutajua
aku
bibi eeh! ya nini
kujizeesha na juma
ananihudumia kila
kitu?
…baba
hekari moja tu
inatosha kwa
kuanzia.
he, yule sio
shoga yako?
mbona na jembe
jioni yote hii?
sawa
mwanangu,
usihofu umeshapata
hilo
azikiwe akiwa na bwana shamba
wanija akionywa na wazazi
bora
useme wewe
hivi kwa nini
umekuwa mazururaji,
siku nne sasa
hujaonekana hapa
nyumbani
8 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013
mtaalamu
msaidie mwanangu
awe mkulima wa
kisasa
akizingatia
haya, atavuna
vizuri
baada ya matokeo ya mtihani
hata kama
nimepata division
four. Siwezi nikashika
jembe
kwani jembe
litakataa?
kufeli
mtihani sio
kufeli maisha
sasa
kulima ndio
kufeli maisha?
kulima ndio
mpango mzima,
utaona!
basi eti
azikiwe alinishauri
tulime, mi
nkakataa .
achana naye,
kafulia yule
panda
mbegu kwenye
mstari kwa kuzipa
nafasi ili zistawi
vizuri
ungezeeka,
shauri yako
haya sasa, kila
mmoja yuko bize na
maisha yake. kuna
aliyepanda kwenye
starehe na
aliyepanda kwenye
kilimo, tuone
watavuna nini?
kilimo ni
suluhu ya
ajira kwa
vijana
duh! kumbe
bora nimestuka
mapema
baada ya miezi kadhaa
ameukataa huu
ujauzito, sijui
nifanyaje
jikaze
hivyo hivyo
mpaka ujifungue
mwaya
JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo!
9
azikiwe akimshukuru bwana shamba
baada ya miezi kadhaa : kila mmoja amevuna
alichokipanda
Karibuni
wageni,
wanijaaa,kuna
wageni
asante
sana maana
ushauri wako
umenisaidia
kuongeza
mavuno
ushauri wa
wataalamu wa
kilimo ni
muhimu
kuuzingatia
fumanizi!!!
karibuni,
waoo, na
zawadi kabisa
asante,
hongera
jamani
nimeshasema
mimi na wewe
sasa bhaaaas!
naomba
unisamehe
mpenzi
usikate tamaa,
kwa kilimo unaweza
kumudu familia na
kujisomesha pia.
nimeshajenga,na
sasa naenda
kusomea kilimo
herí
yako, mi na
hawa watoto
siwezi
tena
10 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013
dah!
sijui kwa
nini sikuanza
mapema
sawa
nitajitahidi
maisha
yananamchapa
wanija,. anaamua
kujirahisisha kwa
wanaume ili aweze
kumhudumia
mwanae, je hili
ndio suluhisho?
hebu tujionee
mazao
yako tayari,
tuma gari lije
kubeba
baada ya kipindi flani
acha tu, kwa kuwa
sasa ni wapenzi, wewe
chukua tu
baada ya misukosuko
mingi ya kimaisha,
wanija ameamua
kutafakari upya
maisha yake,Je
atabadilika? hebu
tuendelee na stori
mmh! hivi
nitaishi
maisha haya
mpaka lini?
baada ya miezi 3
Kilimo
kinalipa,ingia
shambani tu!
…watoto baba
zao wamewakataa, maisha
yamekuwa magumu sana
kwangu
miaka miwili baadae
huku
mambo shwari,
na mimi nataka
kuja kusoma
huko
Haya
nikiuza
yatanisaidia
sana
asante
sana
jitahidi na
kilimo uje, elimu
ndio mpango
mzima
haya,mambo ya kilimo
hayo. Wanija
amebadilika na sasa ni
mkulima mzuri
kabisa.huu ni mfano
mzuri
vijana wengi
wanaona
kama kilimo
hakilipi. ila
ukweli ni
kwamba
Ukizingatia
njia za kilimo
cha kisasa
unatoka
JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo!
11
JE, WAJUA?
Maofisa ugani ndio nguzo ya kilimo vijijini
K
atika mchezo huu tumeona
jinsi Azikiwe alivyopiga hatua
kwa kujikita katika kilimo. Wanija
‘alibugi step’ alivyokuwa akivinjari
kwenye uhusiano, baadaye alijutia
uamuzi wake. Kuna mengi tunaweza
kujifunza katika mchezo huu lakini
ningependa tujadili kidogo kuhusu
umuhimu wa maofisa ugani ambao
ndiyo waliompiga tafu kubwa
Azikiwe katika mafanikio yake.
Hawa ndiyo wanaweza kuwa maafisa ugani...
Maofisa ugani wapo katika sekta nyingi. Wanaweza kuwa;
• Washauri wa misitu
• Washauri wa Ukimwi kwenye jamii
• Washauri wa kilimo
• Maofisa mifugo kwenye jamii
• Maofisa afya katika jamii
• Wakunga wa jadi
Lakini katika stori hii, tunazungumzia wale wanaohusika na kilimo tu.
Maofisa ugani ni nani?
Ofisa ugani ni mshiriki mkuu, anayeishi na kupata
riziki kwenye jamii, lakini si lazima awe mzaliwa
wa eneo hilo. Anatakiwa awe anapatikana na
anaelewa uwezo, udhaifu na matarajio ya jamii
hiyo kwa kutumia utaalamu alioupata na kuwa
wakala wa kilimo. Awe anafahamu lugha, awe
na uelewa halisi wa utamaduni, kanuni, mila
na desturi za jamii hiyo. Awe na uwezo wa
kuhamasisha kushawishi au kuwavutia wengine
kutumia njia sahihi za kilimo kwa kuwafundisha,
kuwatembelea na kuwaonyesha katika mchakato
wa kufanya kazi zao za kilimo.
Jamii ina nafasi kubwa katika
kuchagua ofisa ugani
Yapo mambo mengi ambayo jamii inatakiwa kushiriki katika mchakato wa kumchagua ofisa ugani. Haya ni machache tu;
• Jamii iwe mstari wa mbele kushiriki
kwenye uteuzi, ufuatiliaji na tathmini
ya shughuli za maofisa ugani ili kuhakikisha ubora wa utoaji huduma.
• Muhimu kujua mipaka ya huduma
zinazotakiwa kutolewa na maofisa
ugani.
• Jamii itoe motisha kwa maofisa
ugani kwa kutoa ushirikiano mzuri ili
wafurahie kazi zao.
Shughuli zao hizi hapa;
Pamoja na kwamba maofisa ugani wana shughuli nyingi kwenye jamii,
hizi ni baadhi tu;
• Kutoa habari na kueneza teknolojia katika jamii
• Kuunganisha jamii na masoko, jamii nyingine na watoa huduma
• Kuhamasisha jamii kujifunza mambo mbalimbali
• Kuwezesha uundwaji wa vikundi
• Kutoa mafunzo katika jamii na kufuatilia
• Kutoa ufafanuzi kwa kutumia mashamba yao wenyewe
12 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013
Swali;
Je unawajua maofisa ugani
wa eneo lako? Wanakusaidiaje? Jadili na wenzako
na utuambie kwa kutuma
ujumbe mfupi; andika SM
acha nafasi, andikia maoni
yako kisha tuma kwenda
namba 15665
JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo!
13
SAUTI YANGU
Kama una chochote
unachotaka kusema
tuandikie ili upate
fursa ya kuwaelimisha
wengine
Si Mchezo!
Femina HIP
SLP 2065,
DSM
Maoni yaliyotolewa katika ukurasa huu
ni ya wasomaji, si lazima yalingane na
msimamo wa Femina.
Wadada mnaojiuza
badilikeni
Migongano ya wafugaji na
wakulima itakwisha lini?
Serikali itusaidie kutatua suala la
uhaba wa maji kwenye wilaya yetu
ya Kilosa kwani hali hii inatusababishia kutokuelewana baina ya sisi
wafugaji na wakulima pindi tunapotumia chanzo cha maji pamoja.
Endapo kitatengenezwa chanzo
kingine cha maji kwa ajili ya mifugo,
itaepusha migongano na tutaishi
kwa amani na
upendo.
Dani Zakayo
Mumbi
Kimamba, Kilosa
Mabosi wengine ni kero!
Kuna mabosi wengine ni wasumbufu sana hasa ukifika wakati wa
kutoa posho au mishahara ya
wafanyakazi wao. Mara ukatwe
mshahara na kutafutiwa sababu
zisizo na msingi ili mradi tu
asikupe posho yako yote. Wakati
mwingine anakuja na vitisho na
kutaka ufanye naye ngono ndio
akupe mshahara wako. Hii ni kero
hasa kwa vijana wa kike walioajiriwa na wanaume.
Eda Joseph Ibaraja
Kilosa
Tabia ya wadada wengine
kujiingiza katika biashara
ya ngono si jambo jema na
linapingana na maadili ya
Kitanzania. Mnatoa thamani ya utu wenu na kujidhalilisha kijinsia na kuwa
watumwa. Mara nyingi
wakihojiwa wanasingizia
ugumu wa maisha lakini
pesa wanayoipata haibadilishi mfumo wa maisha yao,
bali huishia kununua mavazi
na mapambo ili kuwavutia
wateja wao.
Elizabeth J. Mollel
Kilosa
Jembe ndiyo mpango mzima!
Wewe pia unaweza kulonga na vijana
wenzako. Tuandike maoni, ushauri,
vichekesho,maswali nk, weka anuani
yako na tuma ukiambatanisha
na picha yako kwa Mhariri,
Jarida la Si Mchezo!,
S.L.P 2065 Dar es Salaam.
[email protected]
Au tumbukiza katika boksi
la Si Mchezo! kama lipo katika
eneo unaloishi.
14 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013
Vijana wenzangu tutumie sana ardhi aliyotupatia Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kilimo ili
kitusaidie kwa maisha yetu ya kila siku na siyo
kukimbilia mjini bila kuwa na mipango. Serikali
iwafuatilie mawakala wa mbegu na dawa ili watusambazie bidhaa zenye ubora pia ikumbuke
kuwa vijana ni Taifa la leo na si la kesho.
Francis Denis Mtawatawa
Kilosa
Wazazi Nipende Advert
Saumu
dhi Buguruni,
iu
b
A
ais
an
,
19
a
ak
Mi
DSM
Ana ujauzito wa miezi
“Niliamua kuja kliniki kujua kama mtoto aliye tumboni ni mzima, kupima damu
pamoja na virusi vya ukimwi, kupewa dawa za malaria na vidonge vya kuongeza
damu”
“Nilimwambia mume wangu, siku ya kwanza alinileta hapa hospital kufanya vipimo”
sita
“Wanawake wajawazito waje kliniki kupata chanjo ili kuwakinga watoto kutokupata
magonjwa, kujua afya zao kama hawana maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na kujua
siku zao za kujifungua”
Thuweba
Abbas
Miaka 27, anaishi Buguruni Kisiwani, DSM
Ana ujauzito wa miezi nane na mtoto wa kike
aitwaye Nahia mwenye miaka mitatu. ameolewa
na Bw. Hassan Rashid mwenye miaka 30.
“Nilikuja kliniki kupata huduma za afya na kutaka kujua mwanangu
anaendeleaje, pia kupimwa damu na kujua umri wa mimba”
“Kwa kuwa nilikuja mara ya kwanza kliniki na wifi yangu, alikuwa wa
kwanza kujua nina ujauzito baada ya kupimwa. Niilipofika nyumbani
nilimwambia mume wangu”
“Akina mama waje kliniki kwa sababu ni hatari. Unaweza kujifungua
bila kujua siku yako ila ukija hospitali unajua mambo yote”
Salma Ally Tunu RBuagum
aMaddenghe,aDSnM i
a Saruni,liDSm
Hali30,m
i
run
M
Miaka 20, anaishi
anaishi Bugu
Miaka 22, anaish
i Buguruni, DSM
Ana ujauzito wa miezi mitano. Ana mtoto wa
kike Amina mwenye miaka sita, ameolewa
na Hamis Said mwenye miaka 30
“Ni muhimu kwenda kliniki mara baada ya
kugundua u-mjamzito. Nilikwenda kupata
matibabu ili kukilinda kiumbe kilichopo
tumboni. Nilipimwa Virusi vya Ukimwi,
magonjwa ya zinaa pamoja na kupewa
dawa za malaria na za kuongeza kiwango
cha damu kwa kuwa nilikuwa na upungufu”
Ana ujauzito wa miezi tisa. Ana mtoto
Kiume Arafat mwenye miaka mitatu,
Salama na mumewe Said Kassim
wanaishi Buguruni, Dar es Salaam
“Sababu ya mimi kuja kliniki ni kutaka
kujua maendeleo ya ujauzito wangu na
kufahamu mtoto anavyokua, wingi wa
damu, kupima Virusi vya Ukimwi. Baada
ya kupatiwa huduma huwa napatiwa
kadi ndogo yenye tarehe ya kurudi”
“Ushauri wangu kwa akina mama
wajawazito na wale wanaopanga kuwa na
watoto, waende kliniki kujua afya zao. Hii
itawapa fursa kujua kama wana
maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na
kupewa ushauri wa namna ya kumlinda
mtoto asipate maambukizi”
“Mtu wa kwanza kumwambia nina
ujauzito alikuwa mume wangu kwa
sababu ndiye mtu wa karibu sana
kwangu na mtu muhimu katika maisha
yangu. Mume wangu ndiye mhusika
mkubwa wa mimba hii. Lakini
nakwenda kliniki peke yangu. Hajawahi
kunisindikiza kutokana na kazi yake,
mara nyingi huwa anakuwa safarini”
“Mume wangu alikuwa wa kwanza
kumtaarifu kwamba nina ujauzito. Alifurahi
sana ukizingatia kwamba tumekaa muda
mrefu bila kupata mtoto mwingine.
Alizipokea habari hizi kwa mtazamo
chanya”
“Nawashauri akina mama wajawazito
waende kliniki wapime afya na umri wa
mimba zao. Pia wataweza kujikinga na
maambukizi ya magonjwa kwa kupata
kinga sahihi na ushauri toka kwa watoa
huduma”
Ana ujauzito wa miezi mitano. Ameolewa na Ramadhani
Shabani ambae ana miaka 30
“Niliamua kuja kliniki ili kujua maendeleo ya ujauzito
wangu, kupima damu na kujua kama
nimeambukizwa VVU. Ningegundulika kuwa nina
maambukizi ya VVU, ingekuwa rahisi kumlinda mtoto
asipate maambukizi hasa wakati wa kujifungua.
Nimepata ushauri mzuri sana kutoka kwa watoa
huduma, na nina amani sana baada ya kujua
sijaambukizwa VVU”
“Hii ni mimba yangu ya kwanza. Nilimweleza mume
wangu baada ya kugundua, yeye akamwomba dada
yake anisindikize kituo cha afya kwa ajili ya kupima.
Imekuwa ni vigumu yeye [mume wangu]
kunisindikiza kutokana na majukumu ya kazi kwani
inabidi awe dukani na hakuna mtu wa kumsaidia na
hawezi kufunga duka”
“Ushauri wangu kwa akina mama ni kwamba
waende kliniki. Huduma ni nzuri, unapata kujua
maendeleo ya afya zao. Pia nimefahamu damu yangu
ni kundi gani, na nimeanza kujiandaa kwa kuwa
nimefahamu tarehe ya kujifungua”
Picha zote na Zechariah Mlacha
Miaka
Tuma SMS neno “mtoto” BURE kwenda 15001 kwa taarifa zaidi
JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo!
15
BURUDANI
Wimbo: Moro All Stars
Wasanii: Afande Selle, Stamina, O – Ten,Belle 9,Samir, Chriss Wamaria, Nassa, Dynna na Zilla
hapa kwetu mtapata furaha, x2
Urithi burudani vyote shwariiiiii, karibu mji kasoro,
Udzungwa ujionee ehee hee hee hee
hee heee he mwenyewe,
Usisubiri usimuliweee, mwenyeweee
(Yoo) Njooow
Na na na na na na na naa na na na
na naaa M-O-R-OOoh,
moro town yeah! Home sweet home
x2 (uuh)
Ubeti wa kwanza - Stamina
Chunga usipitilize stendi suka acha
watu msamvu,
Moro imenipa mengi, washkaji pesa
na shavu,
hatuna mpango na bahari, Mbona
hata mindu ina fukwe,
Milima kwetu fahari, mwaka mzima
kwetu full kipupwe,
Ausindile anoga ndio swagga za
waluguru,
hata ufunge kwa kuroga ila Moro
itaniacha huru,
sihitaji tena Baga utamu naupata
Gairo,
Masai wote huu wana swagga karibu
kama upo Njiro,
16 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013
Toka enzi za Mbaraka mpaka wajukuu wa Mwinshehe,
Mkude kusimama Pastor, Mbokeleni
kuwa sheikh,
Nina haki ya kujisifu, Moro imenipa
kitalu,
Namwaga Pombe kwa Chifu wa Moro
Babu Kingalu,
Sina bifu na Mngoni, Mpogoro ndio
napodeka,
Anzisha tifu ulingoni usande tukupe
Cheka,
Mliotutoka kimwili kiroho tupo
pamoja,
Karibu Moro mswahili uzalendo uende
kwa hoja,
(uuuuuh hu huuu)
Kiitikio
Karibu Morogoro, watu wote wa bara,
visiwani mpaka Zanzibar,
Bahari sio kasoro, wageni karibuni
Ubeti wa pili – O - ten
Yeah! mji unaweza poa, niko rock juu
mlimani,
Na mimi ndio mkuu wa mkoa karibuni madizini,
Matonya alifukuzwa Dar breki ya
kwanza akaja shaini,
Mandela alikuwa shujaa, moro
akaifanya maskani,
Si unajua? Miji kibao haipati mvua,
tofauti kubwa hapa kwetu inanyesha
mpaka inaua,
Mzinga, Ndigutu, Kichangani, Kiguru
nyembe, hapa kwetu haina uzembe,
Hata star anashika jembe, Natokea
matombo kilosa narudi mzumbe,
Nampitia Mkude, makala yuko wapi
Msinde,
Moro Bambam ila vichwa visivimbe,
narudi shamba hata muziki nisiimbe,
No, mi na moro tupo kama pacha, yes
karibu moro tuishi kama kacha,
Mbuga zipo na hata madini yapo,
palipo na amani ndo mi nilipo
Kiitikio
Ubeti wa tatu- Afande Sele
Morogoro,mjini kwetu,
Karibuni wote rafiki na ndugu
zetu(shua)
Toka pande zote iwe ndani, mpaka nje
ya nchi yetu,
Karibuni kwetu mtembeee, harakati
zetu mjionee,
Kama mimi na mtu chee, kuna
mashamba tunalimaga,
Mboga mboga na mipunga, kuna
mahindi, kuna matunda, viazi miwa
na karanga,
Karibuni nyote Morogoro mchote,
hekima za Selemani mtangaze
mataifa yote,
Mkawaambie, mlichokiona hapa,
mkawasimulie siri ya cheka kuwa
chapa,
Na habari kibao za wakali wa hapahapa, kwa soka kwa hip hop, ma
streika marapa,
Maboxer, madensa wote waliotoka
hapa, wahapahapa, tangu kitambo
kile,
Kabla ya Afande Sele, Kabla ya O ten
na Belle, kabla ya Supa Ngedere Moro
Bado Chapa Ilale
Ngoma inogile, tuna historia tele,
hata Mwalimu Nyerere alikuwaga
mbunge wa kwanza wa Moro miaka
ile,
kwa wasiotambua hilo. Karibuni Moro,
hata tommorow
karibuni mjionee maajabu ya mzimu
wa Kolelo, Ifakara Kilombero,
Turiani, Mvomero, Kilosa na Msowero,
Masombo mpaka Gairo
Yeaaah hii ndio Morogoro mpaka
Nyachiro kwa mjomba Kobelo
Na Mahenge kwa shangazi wa kipogoro, twende mahewaa
Kiitikio
Kibwagizo
Morogoro mji kasoro bahari kwetu
bado shwari
Morogoro, Mgeta Mzumbe Mlali Moro
imetulea
Nilipokula gimbi na kachumbari,
mwenzenu mimi naona fahari
Hata ninapokwenda mbali nitarudi
moro nyumbani
Nimelelewa angali bado kichanga,
bado mimi sijajua kuimba
Mpaka sasa mimi natamba, tena
Moro nimepata Mchumba mie x2
Nitazikwa Moro, Nitakufa Moro,
Naipenda Moro, nitaishi Moro
!! !!
Muulize mama’ko...
J
Baba flani mlevi alirudi nyumbani
mwake jioni akamkuta mwanawe
anafanya ‘homework’.
Mtoto akamuuliza babake, “Baba
Indian ocean iko wapi?”
Baba akajibu “Muulize mamako
sababu ye ndio anapenda kusafisha nyumba saa zote,hata mimi
viatu vyangu sivioni!”
J
Nakusaidia hata nikiwa
gerezani
Mzee mmoja alimtumia mjukuu
wake aliyefungwa gerezani barua,
na ilisomeka hivi:-
Nafata chenji yangu!
J
Basi lilipata ajali katika daraja likazama kwenye mto...watu wakaanza
kuogelea kujitoa nje.
Jamaa mmoja akajitahidi kujitoa.
Alipofika nje ya mto ghafla akavua
nguo na kujitupa tena kwenye mto.
Rafiki yake alipomuona akashangaa
akamuuliza,”JUMA unaenda wapi?”
JUMA,”Nataka kumtafuta konda...
hajanirudishia chenji yangu!”
“Mjukuu wangu mpendwa
nina huzuni sana mwaka huu
sitoweza kulima viazi kwenye
shamba kwa sababu wewe
uko gerezani na sina uwezo wa
kulima shamba lote peke yangu”.
Mjukuu alipopata barua akajibu
hivi:“Babu usijaribu hata kidogo
kulima hilo shamba...zile pesa
zote nilizoiba nilizificha kwenye
hilo shamba”.
Mapolisi wa gereza walipoona ile
barua kesho yake wakaenda kwenye shamba la mzee wakalilima
lote wakitafuta pesa.
Baada ya wiki mjukuu akamuandikia babu yake barua nyingine:“Unaweza kupanda viazi vyako
sasa babu...unaona jinsi ninavyoweza kukusaidia hata nikiwa
huku gerezani?
JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo!
17
RUKA JUU
Ruka Juu na jembe!
Unakumbuka shindano la ujasiriamali la Ruka Juu, kwenye luninga mwaka 2010? Habari ya mjini ndio
hii, Ruka Juu imerudi tenaaa… na sasa ni kuhusu vijana wanaofanya kilimo kama biashara. Kipindi
kipya cha radio pia kitazinduliwa kikilenga kuelimisha kwenye masuala haya haya ya kilimo.
Kilimo ni utajiri:
Kila mtu ni lazima ale ili aishi,
hakuna kazi nyingine yenye
umuhimu kuliko kilimo. Soko la
kilimo haliishi, kuna kipato kwenye
kilimo. Lima kwa usahihi na ubora.
Kilimo ni maisha:
Chakula kinajenga miili yetu,
kinatupa nguvu. Kwa kutumia
chakula tunakua, tunakidhi
njaa zetu, tunaponya magonjwa
mbalimbali. Tupo tulivyo kwa
sababu ya chakula.
18 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013
Kilimo ni uti wa mgongo:
Unafahamu kuwa 85% ya
Watanzania wanaishi kwa
kutegemea ardhi? Muda umefika
wote tuweke msisitizo kwenye
kilimo na kukifanya kiwe na
faida.
Msimu mpya
Msimu mpya utakaoanza kurushwa Machi, 2013,
umejaa mambo kibao ya kijanja, tumezunguka sehemu
mbalimbali Tanzania na kukutana na vijana wakulima
ambao wako tayari kukushirikisha mbinu za kutoka na
kilimo.
Amabilis Batamula, mtangazaji wako wa msimu uliopita
amerudi tena akiwa na Bwana Ishi anayetaka kuingia
kwenye kilimo. Bila kumsahau Bahati, atawabahatisha
wote watakaowasiliana nasi kupitia Wasiliana na Bahati
Ubahatike.
Kwenye redio utakutana na vijana wenzako; Michael
Baruti na Rebeca Gyumi wakiwa tayari kukuelimisha
kuhusu masuala mbalimbali ya kilimo. Hii si ya kukosa.
Ardhi kubwa yenye rutuba:
Nchi yetu imebarikiwa ardhi yenye
fursa kibao za kuendeleza kilimo.
Wakulima wajanja wanaofahamu
nini cha kupanda wanaweza
kubadilisha ardhi hii kuwa pesa.
Kilimo Bomba!
J Kum b uk a
Unaweza kuita kilimo bomba au
Kilimo Kwanza, kama kampeni
inayoendeshwa na serikali.
Tuungane wote na kukipa kilimo
kipaumbele. Tulishe kizazi
kijacho, tujenge maisha yetu.
Kilimo siyo ushamba,
kilimo ni ajira na
kinaweza badili
maisha yako.
JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo!
19
NGUVU ZA MWANAmUME
Imeshalipiwa hiyo, unaitaka?
P
wani kuna msemo unaosema “Ushalipiwa weye”ambao watu wengi wakiambiwa, hung’aka na kuwa
wakali kama vile wamekula pilipili mbuzi. Ndiyo. Hata wewe unapopewa ofa zisizoeleweka na watu
unaowafahamu au usiowafahamu. Kuwa makini. Chunga sana hizo ofa, wengi huwa wanakuja kudai vyao
na kutaka vyako pia.
Vijana wengi wa kiume hudhani
kuwa ofa kwao ni “zali la
mentali” na ni akina dada peke
yao ndiyo wanaohongwa na
hizo ofa huwatokea puani hao
kina dada, Hapana! Hata wewe
kidume unaweza kukumbwa
na madhara yale yale ambayo
yanaweza kuwakumba akina dada
ukiangukiwa na hilo zali la ofa,
mentali.
Kupenda ofa husababisha:
• Kuwa mtumwa wa ngono, hasa pale unapolazimishwa
kulipa vitu ambavyo ulipewa
kama ofa na huna uwezo wa
kuvilipa, hii inakuweka katika
mazingira hatarishi.
• Vijana wengi kudhani kuwa
zali la mentali litawadondokea na kufanikiwa kimaisha
bila ya kufanya kazi na kuwajibika kikamilifu na matokeo yake ni kukosa ubunifu
wa kukabiliana na changamoto za maisha na ‘fainali’ ni
uzeeni.
• Kutokuwa na misimamo
thabiti juu ya maisha yako.
• Kujiingiza katika tabia hatarishi.
20 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013
Jihadhari
• Kama mtu usiyemfahamu anakupa ofa, kabla
ya kukubali muulize
kwanza ana lengo gani
hadi anatoa ofa kwako.
• Ni muhimu kutafakari
mahusiano uliyonayo na
huyo mtu anayekupa ofa
J Ku m b uk a
Ofa zinatengeneza
mazingira ya kukosa
utashi na ufinyu wa
maamuzi. Tafakari
kabla ya kutenda.
NGUVU ZA MWANAMKE
Wazazi nipendeni!
Huzuni kubwa imetanda. Ni vilio huku na kule, wakubwa kwa watoto,
wote wanalia. “Mama Wawili umetutoka, Mama Wawili” wanasikika
wanawake wakilia.
Mama Wawili, mwanamke mcheshi, mama wa watoto wawili
amefariki wakati akijifungua mtoto wa tatu. Mtoto pia amefariki.
Mama na mtoto kufariki wakati wa uzazi si mara ya kwanza kutokea
katika kijiji hicho; na wala si jambo jipya nchini kwetu, lakini si jambo
la kuvumilia.
Ni wajibu wetu sote
Pamoja na juhudi za serikali kuimarisha huduma za afya kwa
wajawazito, mafanikio bado ni kidogo. Kina mama na watoto
wengi wanaendelea kufa kutokana na matatizo wakati wa
ujauzito na kujifungua!
Ila serikali haiwezi kufanya juhudi za kupambana na tatizo hilo
peke yake. Ni wajibu wa kila mmoja wetu, kama taifa zima,
jamii, familia, baba wa mtoto na mama mjamzito pia.
Kuhudhuria kliniki mapema ndiyo usalama wako!
Kwa mjamzito ni muhimu
kutambua mapema kwamba
u-mjamzito. Hii itakusaidia
kujiwekea mikakati ya jinsi
ya kutunza mimba yako na
maandalizi ya kuhakikisha
kwamba unajifungua salama.
Tufanyeje?
Hakuna anayependa kifo, hasa
pale uhai mpya unapotazamiwa
kuchipua. Wazazi na jamii
nzima mpendeni huyo mtoto
kabla na baada ya kuzaliwa.
Kliniki kwanza
Mjamzito anatakiwa
kuhudhuria kliniki
katika wiki 16 (miezi
minne) za kwanza za
ujauzito. Pia mjamzito
anatakiwa ahudhurie
kliniki angalau mara nne
katika kipindi chote cha
ujauzito.
Mahudhurio ya kliniki
kwa wakati unaofaaa
yatamuweka mjamzito
pamoja na mtoto wake
katika nafasi bora zaidi
ya uzazi salama.
Wazazi Nipendeni
ni nini?
Kampeni ya “Wazazi
Nipendeni” ina lengo
la kutekeleza kampeni
ya kupunguza vifo
vinavyotokana na uzazi
Afrika, kwa kuwawezesha
wajawazito na wenza
wao kuchukua hatua
muhimu kwa afya ya mama
mjamzito na uzazi salama.
J Kum b uk a
Maandalizi ni kitu
muhimu kwenye
kila kitu. Kwa mama
mjamzito, maandalizi
ya uzazi salama
yanaanza kwa
kuhudhuria kliniki
mapema.
JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo!
21
CHEZASALAMA
Jipange, usije ukavuna mabua!...
Baada ya kuisha kwa msimu wa
mavuno, wakulima hupata muda wa
kufanya tathmini na kupumzika kwa
ajili ya kujiandaa na msimu mwingine
wa kilimo. Kipindi hiki mara nyingi
hutawaliwa na chereko chereko kwani
mazao yanakuwa yameshauzwa na
watu wameshavuta mkwanja wao na
kuusunda kibindoni. Kinachofuata…
Msimu wa sherehe
Hapa ndio utasikia ‘vishughuli’
kila nyumba;
• kumtoa mwali,
• ngoma,
• ndoa/harusi
• Safari za kwenda mjini
kusalimia ndugu
Na siyo kwamba huwa
zinafanyika hivihivi tu, bali
wengine hutafuta hata sababu
ili mradi tu wafanye sherehe.
Hatari ipo jirani!
Ushauri wa bure
Utumiaji wa vileo kama vile pombe huongezeka
sawa sawa na idadi ya wapenzi, ukizingatia
pesa ipo. Kipindi hiki ndio utasikia, Tumia
pesa ikuzoee, jenga heshima baa! Vipi lakini
jembe, umeshajiandaa kwa kilimo katika msimu
unaofuata? Una uhakika msimu unaokuja
utakuwa wa neema kama huu ulioisha? Jihadhari
kabla ya hatari!
Ukilima na kuvuna, pesa inayopatikana ni
bora ikaongezewa katika mtaji wa kilimo kwa
kununua mbegu na pembejeo nyingine za
kilimo. Kumbuka kuwa msimu wa kilimo ni
mrefu zaidi kuliko msimu wa mavuno. Ni vyema
basi ukajiandaa mapema kwa msimu unaofuata
badala ya kujisahau na kujirusha kwa sana.
22 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013
Muhimu kuzingatia
Baada ya kuuza mazao na kudaka huo mkwanja, tuliza
ubongo na kujiongeza kifikra namna ya kujiletea maendeleo.
Fikiria kuhusu biashara nyingine ambazo zinalipa msimu
wa mavuno ili kujazia kwenye kilimo. Achana na mawazo
potofu ya ushawishi kutoka kwa marafiki wanaokutaka
mkapige ‘tungi’ au kushinda kijiweni kutwa nzima bila
kuwa na shughuli ya kufanya.
Msimu wa kilimo ni mfupi lakini ni mrefu kama hautakuwa
makini upande wa matumizi ya fedha, Usije ukashtuka
wakati jua ndio linaanza kuchwa, pasua kichwa.
J K umb u ka
Kuna mabadiliko ya hali
ya hewa, mabadiliko ya
bei ya mazao sokoni,
mabadiliko ya bei
za zana za kilimo na
magonjwa ya mazao.
Jipange kwa msimu
ujao!
JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo!
23
chakarika na jembe likutoe!
K
Michoro: babatau cartoons 2013
ijana Chema anatafuta jinsi ya kutoka kimaisha na washkaji.
Ametoka kijijini kwenda mjini kucheza mdundo wa muziki wa
mjini. Ni muziki gani huo? Je, atatoka? Fuatilia...
baada kushindwa muziki wa mjini
24 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013
chama akikomaa na mteja
balaa!
kilimo kimejibu, chema anasafirisha mazao kwenda
kuuza mjini
JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo!
25
anakutana na washkaji, bado wanahangaika na mdundo wa muziki wa mjini
Umeonaeee? Michongo ya
maisha si lazima kuifukuzia
mjini, hata kijijini ipo.
Umemwona Chema? Wengine
tulibugi kama Chema, tuko
mjini tunasota, kila kukicha
afadhali ya jana! Umeshafikiria
kuhusu kilimo? Tafakari!
26 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013
UKWELI WA MAMBO
Kilimo ni tumaini la wengi
W
engi wetu tumekuwa tukiimba nyimbo lakini hatuujui tunachezaje, kwa kuwa hata
mdundo wake hiyo inatupiga chenga. Kwa kawaida kila wimbo una uchezaji wake na
hivyo kama wimbo utabadilishwa ghafla basi ni wazi kuwa hata uchezaji utabadilika.Vijana
wanakimbilia mjini wakidai kuwa eti kilimo hakilipi wakidhani mjini ndiko maisha bora yaliko.
Twende sawa basi;
• Vijana tukiachana na vurugu
za mgambo wa jiji na kurudi
mashambani tutakuwa na
wimbo mmoja, tutacheza
pamoja na kitaeleweka.
• Tuanze kubadilika tuchangamkie kilimo cha umwagiliaji na kuacha kutegemea
mvua za msimu
• Tukope pesa kwenye asasi
mbalimbali ili tuwekeze katika
kilimo.
J Ku m b uk a
Tudadisi haya yanayotokea
• Vijana kukimbilia mjini kumefanya kilimo kudumaa
na kusababisha wakulima wengi na wengine ambao
maisha yao yanategemea kilimo wakaanza kubadilisha wimbo
• Wakati kilimo kinadumaa kutokana na vijana wenye
nguvu kukimbilia mjini mambo yakabadilika na
kutokea kwa nyimbo mbili tofauti. Ukaanza ule
wimbo wa ukitaka maisha mazuri yapo mjini
• Huko mjini nako vijana walikimbilia kazi ya kuuza
nguo yaani umachinga, ulinzi n.k baadaye wakajikuta wakilazimika kuimba wimbo mmoja na askari
wa jiji yaani Jeshi la Mgambo.
• Sasa wimbo huu wa mgambo si wa kawaida kwani
uliwafanya baadhi ya vijana kuukumbuka ule wa
shambani ambao ulikuwa rahisi hata kuucheza.
Wapo vijana ambao
wameweza kunufaika
kupitia kilimo na sasa
wanaendesha maisha yao
vizuri. Usikubali kuachwa
nyuma, kilimo ndio
mdundo wa uhakika!
JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo!
27
sema. tenda!
Kilimobiashara ni zaidi ya ujuavyo
M
engi yanasemwa kuhusu kujihusisha na kilimo. Wengine wanakandia
kilimo na saa nyingine wana sababu ambazo zinaweza zikakushawishi
kukubaliana nao. Tulitia timu Kilosa na tukachonga na vijana kuhusiana
na kilimo, soko lake, namna ya kujiendeleza katika kilimo na kadhalika.
Changamoto zinazo wakabili wakulima ni hizi
• Wakulima wengi wanalima bila kuwa na malengo
• Hakuna mfumo wa taarifa za masoko kuwawezesha wakulima kujua
watauza wapi
• Elimu ndogo juu ya jinsi ya kuongeza thamani mazao wanayolima
kama vile usindikaji
• Hakuna utunzaji mzuri wa mazao
• Kutojua umuhimu na faida za kujihusisha kwenye vikundi na taasisi za
kifedha kama vile SACCOS na VICOBA
• Kutokuwa na uwezo wa kupanga bei ya mazao
• Miundombinu duni hasa ya barabara na mawasiliano mbovu
• Ukosefu wa vyombo vya usafirishaji kutoka maeneo ya uzalishaji
• Kutojua namna ya kutumia simu za mikononi kibiashara katika kupata
taarifa
• Ubora wa mazao kupungua pale yanapofika sokoni
Mbegu mbalimbali
za mahindi
Moja ya pembejeo
za kilimo ambao ni
mbolea ya chumvi
chumvi kwenye
moja duka la
pembejeo za kilimo,
katika Kijiji cha
Msalabani, Kilosa
28 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013
Nini kifanyike?
Kikundi cha Jitegemee wakiwa mbele ya duka la mmoja wa
wanakikundi hicho. Hawa wanajihusisha na kilimo biashara
Matokeo yake ni nini?
• Vijana wengi hukata tamaa kujishughulisha na kilimo kwa madai
kwamba hakilipi
• Wakulima hukata tamaa kuendeleza kilimo hata kuuza mashamba
• Vijana kukimbilia mijini bila kuwa
na malengo
• Wengi hulima kwa ajili ya chakula
tu
• Sekta zinazohusika zitoe elimu ya kilimo
biashara ili wakulima wanufaike na kilimo
• Kuwe na msukumo wa matumizi ya
teknolojia sahihi za kilimo kama vile kilimo
cha umwagiliaji, mbegu sahihi kulingana
na udongo na hali ya hewa ya eneo lako.
• Wakulima wajifunze namna ya kutafuta
masoko na biashara juu ya kilimo stahiki
kinacholenga hitaji la soko na walaji
• Kuwaunganisha wakulima kwenye masoko
kwa kutumia teknolojia na mawasiliano
mfano vipindi vya redio na simu za mkononi
• Kufanye tafiti za kuendeleza kilimo biashara
• Miundombinu ya barabara, vyombo vya
usafiri n.k iboreshwe
• Elimu ya usindikaji itolewe kwa wakulima
• Suala la kilimobiashara lipewe kipaumbele
katika ngazi zote ili wakulima waweze
kuingia katika soko la ushindani
• Huduma za pembejeo za kilimo zisogee
zaidi vijijini na ziwalenge wakulima
Swali
Je, ni changamoto zipi wanazokutana
nazo wakulima wa eneo lako? Unadhani
nini kifanyike kutatua changamoto hizo?
Tuambie kwa kutumia mawasiliano hapa
chini:
Barua pepe: [email protected]
Sms: andika SM acha nafasi, andikia maoni yako kisha tuma kwenda namba 15665
S.L.P. 2065, Dar es Salaam.
JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo!
29
MARIE STOPES
Waelimishaji rika Zanzibar, walia na utoaji mimba
Suala la utoaji mimba kwa njia zisizo salama, limekuwa likipigiwa kelele kila mara hapa Tanzania.
Vijana waelimishaji rika huko Zanzibar wamefunguka na kuwaomba wazazi, viongozi wa dini na
Serikali kuwasaidia kupambana na vifo vitokanavyo na utoaji mimba usio salama.
Kuna madhara ukijihusisha na
uhusiano wa kimapenzi kwenye
umri mdogo
• Kupata mimba katika umri mdogo
• Kujiingiza katika mazingira hatarishi ya kutoa mimba kwa njia zisizo
salama.
• Kujishushia heshima mbele ya jamii
yako
• Kujiongezea majukumu katika umri
mdogo
Vijana hao wametoa ushauri huu...
Muelimisharika akizungumza na wazazi kuhusu madhara ya
utoaji mimba.
Kuna usiri mkubwa
“Vijana wengi hushirikiana kutoa mimba kwa
kutumia miti shamba,” alisema mmoja wa
waelimishaji rika. Akaongeza, “vitendo hivi
hufanyika kwa kificho sana ili wazazi na jamii kwa
ujumla isijue. Hii hupelekea hatari ya vifo pale
watoaji wanapozidiwa.”
Walizungumzia pia kuhusu mila na desturi za jamii
yao kuwa zinamzuia kijana kuanza mapenzi kabla
ya ndoa, kwa hiyo vijana hutoa mimba mafichoni
na kwa usiri ili kuepuka aibu na adhabu.
Kwa huduma za kuokoa maisha kwa walioharibikiwa mimba fika kituo cha Marie
Stopes Tanzania kilichopo Kilimani Mnara wa Mbao au kliniki yoyote ya serikali.
Kwa mawasiliano piga 0767160038 au tuma ujumbe au kwa njia ya baruapepe
[email protected]
30 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013
• Wazazi kuwa karibu na vijana ili kuwafundisha kuhusu afya ya uzazi kwa
kuwaruhusu kupata elimu hiyo kwenye
vituo vya afya ya uzazi.
• Serikali na viongozi wa dini mbalimbali
walihimizwa kuweka sera itakayomlinda kijana hasa wa kike kupata huduma
bora hasa baada ya mimba kuharibika
ili wasipoteze maisha. Jamii pia ielimishwe juu ya matumizi ya njia za uzazi
wa mpango.
J Ku m b uk a
Maandalizi ya mafanikio ya
baadaye ya kijana, huanza akiwa
mdogo. Sote tuwalinde vijana
ili tuwe na Taifa lenye vijana
wanaofaidi matunda ya malezi ya
wakubwa wao.
USHAURI
Mimi ni msichana wa miaka 24. Nilibahatika kumpata mvulana ambaye tulianza
Swali uhusiano. Katika uhusiano wetu sikuwa na haraka ya kutambulishwa kwani nilijua
kila kitu kinakwenda na wakati. Mpenzi wangu aliniambia anakaa na mama yake na dada yake na mimi
nilimweleza kuwa naishi na mama. Baada ya miaka miwili pamoja ndipo nilipogundua kuwa mpenzi
wangu ameoa na ana mtoto mmoja. Mama alinishauri niachane naye lakini nampenda sana huyo kijana
na sidhani kama kuna mwanamume atakayechukua nafasi yake. Naomba ushauri.
Msomaji wa Si mchezo, Mburu-Manyara.
Tafuta muda ukae naye,
muulize kama yupo tayari
kuendelea na mwanamke aliyezaa naye au kuwa na wewe
na akupe sababu za msingi
kwa nini amemchagua aliyemchagua, ndipo
ufanye maamuzi.
Abdulrazaaq Ngowo
Kilosa
Nashukuru kwa swali. Ukweli ni kwamba mtu anayekupenda kwa dhati
hawezi kukudanganya huyaweka mambo yake wazi ili muweze kuyajadili pamoja.
Ingawa unampenda sana jiulize; ‘kwa mfano mimi ningekuwa mke
wa huyu bwana nitakaposikia habari hizi nitajisikiaje?’ Pia kumbuka
kwamba mahusiano na watu wengi, kama anavyofanya huyo
mwanaume huchangia sana katika kueneza magonjwa ya zinaa pamoja
na VVU. Tafakari kabla ya kuchukua hatua hata kama unampenda.
Asante.
Ningependa kukwambia uondoe
mawazo kwake na amini kuwa
yupo mvulana mwenye mapenzi
ya kweli, na muaminifu na huyo
ndiye atakayekufaa.
Vumilia tu utampata.
Mwanahamisi Rajabu
Kilosa
SWALI LA
TOLEO LIJALO
Nina miaka 21, nina rafikiwa kike ambaye
tumejuana kwa muda wa mwaka mmoja
hadi sasa. Nampenda ila naogopa kumueleza
kwani nitavunja urafiki wetu. Pia kuna mwanamke anayenipenda sana ila mie simpendi
na yupo jirani sana na mimi kuliko yule
nimpendae ambaye ni rafiki yangu, vijana
wenzangu naomba mnishauri nifanye nini
katika suala hili?
Hantish Jozack
Njombe.
Huyo hana mapenzi ya kweli
kwako, mpe nafasi mwingine,
utampata anayekupenda.
Umeshajifunza, kwa huyo
mwingine
utakuwa
makini zaidi.
Pili George
Kilosa
Kama unaishi naye sehemu moja
ondoka ili kumsahau kirahisi.
Jishughulishe na kazi na siyo
mapenzi. Ukisema ukae nae
bado itakusumbua kwani bado
utakuwa kama mke mwenza na
utaumia
zaidi.
Steven F.
Mbwiss
Kilosa
Betty Liduke ni rafiki
mkubwa wa vijana, hata
wewe unaweza kulonga naye.
Ni msambazaji mkubwa wa
Jarida la Si Mchezo! Mkoani
Njombe. Ni mshauri nasaha
na ni Mratibu wa Kitengo
cha Udhibiti Ukimwi katika
Kampuni ya TANWAT,
Njombe.
Mwandikie kupitia
Jarida la Si Mchezo!
Si Mchezo!
S. L. P. 2065
Dar es Salaam
SMS; andika SM acha nafasi
andika ujumbe wako kisha
tuma kwenda namba
15665 na utuambie kama
ungependa uchapishwe.
JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo!
31