YALIYOMO Jamsii ya Wasangu ukurasa Jamii ya Wasafwa

Transcription

YALIYOMO Jamsii ya Wasangu ukurasa Jamii ya Wasafwa
YALIYOMO
Jamsii ya Wasangu
ukurasa
1. Utangulizi ........................................................................................................................
1
2. Wasangu wanapokaa ......................................................................................................... 1
3. Mito Mikuu ya Bonde la Usangu......................................................................................... 2
4. Bonde la Usangu ................................................................................................................ 3
5. Ramani ionyeshayo Eneo la Usangu ................................................................................. 3
6. Udongo wa Bonde la Usangu............................................................................................. 4
7. Magonjwa ........................................................................................................................... 4
8. Historia .............................................................................................................................. 5
9. Misafara ya kwanza ya Kiarabu .......................................................................................... 6
10. Kuja kwa Wangoni.............................................................................................................. 6
11. Wasangu wapigana na Amrani Masudi ........................................................... :................ 6
12. Kindumbwe ndumbwena Wahehe ................................................................................... 8
13. Merere akiwa Ukimbu......................................................................................................... 9
14. Merere akiwa Mfumbi ........................................................................................................ 9
15. Merere atawala nchi ya Wasafwa........................................................................................ 10
16. Wajerumani waja mwaka wa 1892 ..................................................................................... 10
17. Kilimo katika Bonde la Usangu ......................................................................................... 11
18. Historia ya kilimo cha mpunga ...................................................................................... 11
19. Ndoa za Wabaluchi .......................................................................................................... 12
20. Kilimo kinachoendeshwa sasa Usangu.............................................................................. 13
21. Sehemu zihazopandwa mpunga katika Bonde la Usangu.................................................. 14
22. Kilimo kwa jumla ............................................................................................................. 17
23. Kilimo cha mpunga.............................................................................................................. 17
24. Matatizo ya kilimo cha mpunga ................................................................................... 18
25. Mifugo katika Bonde la Usangu........................................................................................ 19
26. Magonjwa ya Mifugo......................................................................................................... 19
27. Matatizo kuhusu Mifugo .................................................................................................... 19
28. Kilimo cha Wasangu ......................................................................................................... 20
29. Ghala za Chakula ............................................................................................................... 21
30. Ufugaji wa ng'ombe .......................................................................................................... 22
31. Shabaha ya kufuga ng'ombe.............................................................................................. 22
32. Utawala wa Wasangu......................................................................................................... 22
33. Sifa kuu za Mwene
........................................................................................................ 23
34. Familiana ndoa ya Kisangu ........................................................................................... 23
35. Imani na Dini ....................................................................................................................... 24
36. Uchawi ................................................................................................................................ 24
37. Nyumba za Wasangu.......................................................................................................... 24
38. Mavazi yao ya jadi .............................................................................................................. 25
39. Michezo ya Wasangu ........................................................................................................ 25
40. Miiko ya Ngoma ................................................................................................................. ..25
41. Mapendekezo ..................................................................................................................... .25
Jamii ya Wasafwa
42.
43.
44.
45.
46.
Utangulizi..................................................................................……………………………..29
Jamii ya Wasafwa ilipo...................................................................................................... 30
Historia fupi ya Wasafwa .................................................................................................. 31
Kipindi cha majilio ya Wageni na Vita.......................................................................... 33
Kuja kwa Wamishonari ...................................................................................................... 34
47.
48.
49.
50.
51.
52.
53.
54.
55.
56.
57.
58.
59.
60.
61.
62.
63.
64.
65.
66.
67.
68.
69.
70.
71.
72.
73.
74.
75.
76.
Serikali ya Kijerumani ..........................................................................................................
Kilimo ....................................................................................................................................
Mgawanyo wa kazi ...............................................................................................................
Kuvuna ..................................................................................................................................
Ghala ya mazao ....................................................................................................................
Kuhama hama kwa watu .......................................................................................................
Wanyama Waf ugwao ...........................................................................................................
Umbo la familia ya Kisafwa .................................................................................................
Ndoa .....................................................................................................................................
Ndoa ya siku hizi ..................................................................................................................
Sifa za wachumba ................................................................................................................
Talaka ...................................................................................................................................
Desturi za kula chakula ........................................................................................................
Mama anayezaa Mapacha ...................................................................................................
Mama aliyefiwa na bwana yake ...........................................................................................
Mama kupata mimba bila kupitia hali yake .........................................................................
Kuotesha meno ya juu kwanza ............................................................................................
Utawala.................................................................................................................................
Kifo .............................. , .......................................................................................................
Kuzika...................................................................................................................................
Mavazi...................................................................................................................................
Miiko.....................................................................................................................................
Imani .....................................................................................................................................
Kutambikia Mvua .................................................................................................................
Maana .......................................................................................................................................
Maji .......................................................................................................................................
Elimu yaWatoto ...................................................................................................................
Kumpeleka mtoto shuleni ....................................................................................................
Nyumba za Wasafwa............................................................................................................
Orodha ya vitabu vya kumbukumbu.....................................................................................
34
35
36
36
36
37
37
38
39
40
41
41
42
42
43
43
43
44
44
45
45
45
46
46
47
48
49
49
50
Jamii ya Wasagara
77.
78.
79.
80.
81.
82.
83.
84.
85.
86.
87.
88.
89.
90.
91.
92.
93.
94.
95.
Historia ya Wasagara........................................................................................................... 51
Imani ..................................................................................................................................... 53
Tambiko la Mvua.................................................................................................................. 54
Uchawi .................................................................................................................................. 55
Desturi za Wasagara ............................................................................................................ 55
Chakula cha Wasagara ........................................................................................................ 56
Mwanamke mwenye mimba ............................................................................................... 56
Mtoto .................................................................................................................................... 56
Jando.................................................................................................................................... 57
Siku ya kutoka...................................................................................................................... 57
Wakati wa Posa...................................................................................................................58
Kuvunjika ndoa ................................................................................................................... 59
Mahari ................................................................................................................................. 59
Msichana .............................................................................................................................. 59
Kifo ....................................................................................................................................... 60
Ufundi ............................................................................................................................... 61
Utani wa Wakaguru na Wasagara ....................................................................................... 61
M ichezo ya Wasagara ........................................................................................................ 62
Kilimo chajadi cha Wasagara ............................................................................................. 62
96.
97.
98.
99.
100.
101.
102.
103.
104.
105.
106.
107.
108.
109.
110.
111.
Mgawanyo wa kazi ...............................................................................................................
Plani ya ghala ......................................................................................................................
Chama cha Ushirika cha wilaya ya Kilosa............................................................................
Hudumaza chama cha ushirikakwa wakulimawa Kilosa ..................................................
Wanyama.............................................................................................................................
Familia ...............................................................................................................................
Nyumba za Wasagara..........................................................................................................
Milango-aina ya mbila .....................................................................................................
Ndoa ....................................................................................................................................
Desturi za kuamkiana .. .....................................................................................................
Utawala ...............................................................................................................................
Kiapo ....................................................................................................................................
Mali ...................................................................................................................................
Mavazi ya Wasagara ............................................................................................................
Mapambo .............................................................................................................................
Mwisho .
........................................................................
65
66
67
68
69
69
69
70
70
72
72
73
73
74
74
74
Sura ya Kwanza
JAMII YA WASANGU
UTANGULIZI
Makala haya yanazungumzia habari za Wasangu waishio katika bonde la Usangu katika Wilaya
ya Mbeya. Kama inavyojulikana Utafiti huu, ambao unaendelea, wafanywa kwa shida nyingi za
usafiri kutoka mahali fulani hadi pengine ambapo utafiti watakiwa ufanyike. Magari hatuna ambayo
yangalituwezesha kufika mahali pa utafiti kwa urahisi zaidi. Safari zotezafanywa kwa miguu na watu
ambao pengine wangesaidia kutoa habari wanashindwa kutembea au sisi wenyewe watafiti
tunashindwa kuwafikia kwa wakati unaofaa.
Zaidi ya hayo, habari nyingi zimesahauliwa sana kwa sababu hakuna mtu aliyejishughulisha
kuzitafuta na kuzihifadhi kwa sababu Wazungu walipofika huku kwetu waliziita hizo habari ni za
kishenzi. Basi watu wakaziacha na habari zake zikapotea kabisa.
Shukurani nyingi ziwaendee wazee wote wa Jamii ya Wasangu ambao walijitahidi sana
kukumbuka habari kiasi walichoweza na kupoteza muda wao mwingi ambao wangeliutumia kwa
shughuli zao za kuinua maisha yao. Shukurani nyingi zaidi zimwendee Mzee Merere — ambaye ni
Katibu Tarafa wa Chimala na ambaye alikuwa Chifu wa jadi wa Wasangu kabla ya kupata Uhuru 1961,
kwa msaada wake mwingi sana katika kutoa habari nyingi za Wasangu, katika kuwa mkalimani wetu
kati yetu na Wazee wa Kisangu, pia katika uwezo wake wa kuweza kuwakusanya watu wanaofahamu
habari nyingi za Jamii ya Wasangu. Bila ya msaada wa Mzee Merere pengine sehemu kubwa ya kazi
yangu kuhusu utafiti juu ya Mila za Wasangu isingeliweza kufanyika.
MITO MIKUU YA BONDE LA USANGU
BONDE LA USANGU
Jumla ya Wakaaji wa bonde la Usangu ni zaidi ya watu 74,000 Kama ilivyohesabiwa mwaka
1972. Lakini jumla ya watu kamaSerikali ilivyohesabu mwaka 1967 ni watu 56,743, kwahiyo jumlaya
watu katika bonde la Wasangu yaongezeka kwa haraka sana kuliko jumla ya watu inavyoongezeka
katika sehemu zingine za Tanzania. Sababu zinazofanya watu waongezeke upesi sana katika bonde
hili ni nyingi sana; na baadhi yasababu zenyewe ni kama hizi hapachini:Sababu ya kwanza ni kwamba bonde hili la Usangu tangu zamani lilikuwa halijulikani sawasawa
na watu wengi jinsi lilivyo na manufaa kwa shughuli mbali mbali za uzalishaji mali kwa sababu
Wasangu walikuwa wapiganaji hodari wa vita kwa hiyo ilikuwa ni vigumu sana kwa jatnii zingine
kwenda kufanya mastaakimu yao huko. Hata baada ya Wakoloni kukomesha vita vya jamii
mbalimbali za Nyanda za juu za Kusini, jamii zilikuwa hazijui habari kamili kuhusu bonde hili. Baada
ya Uhuru tu, mawasiliano katika bonde hili na nje ya mbugaza Usangu yakabadilika sana na kuwa
bora zaidi yaliyoletwa na Chama chaTANU katika kuhudumia watu wake sawasawa. Pili, udongo wa
mbuga za Usangu ni nzuri sana kwa hiyo mkulima halazimiki kutia mbolea hata kidogo katika
mashamba yake. Mbolea ya asili ni nyingi mno katika udongo na mimea ikipandwa hustawi sana.
Tatu, kuna mito mingi yenye maji kwa matumizi ya watu na mifugo pia, kwa hiyo watu wamevutiwa
sana na mali ya asili ya namna hii. Nne, Mbuga za Usangu zinafaa sana kwa ufugaji wa mifugo —
hasa ng'ombe, mbuzi na kondoo. Manyasi yanapatikana kwa urahisi na maji kwa ajili ya mifugo
kwa hiyo wafugaji wamevutiwa sana na mbuga hizi kutoka wilaya za jirani na za mbali pia. Tano,
mbuga za Usangu ni kubwa sana na zina nafasi kubwa za kustawisha malisho ya mifugo na ulimaji
wa mazao mbalimbali. Mvua zanyesha kiasi cha kutosha bali kuna jua kali sana wakati wa kiangazi.
Hali kadhalika ziko sababu zingine nyingi zilizowavutia watu kuja kukaa katika mbuga za Usangu
3
toka Mikoa mingine.
Jamii zinazoishi katika bonde la Usangu ni Wasangu ambao ni wenyeji wa mbugaza Usangu
Wanyakyusa ambao wamehamia mbuga za Usangu toka Rungwe kuja kulima mashamba ya mpunga
na mimea mingine; Wabena ambao wamehamia mbuga hizo toka Wilaya ya Njombe na hushughulika
zaidi na kilimo cha mpunga na mazao mengineyo. Wakinga toka Wilaya ya Njombe, nao
hujishughulisha sana na biashara — hasa biashara ya samaki; Wahehe toka Wilaya ya Iringa —
hujishughulisha na kilimo pamoja na ufugaji; Wahehe wanafanana sana na Wasangu katika mila na
desturi; Wamasai na Wasukuma, ambao hasa walianza kuhamia katika mbuga za Usangu tangu
mwaka1973, mwezi Septemba. Jamii hizi mbili zimehamia mbugaza Usangu juzi juzi tu, lakini jamii
zingine zilihamia mbuga za Usangu miaka mingi kidogo iliyokwisha pita. Wamasai hujishughulisha
zaidi na ufugaji na Wasukuma hujishughulisha na mambo yote mawili, ufugaji na ukulima. Jamii
nyingine ambayo imekaa sana katika bonde la Usangu ni jamii ya Wabaluchi ambao wanaitwa kama
"Maburushi". Jamii hii imekaa katika mbuga za Usangu tangu karne ya 19 na tangu wakati huo jamii
hii imejishughulisha sana na kilimo cha mpunga na pia mazao mengine. Walikuwa watu wa kwanza
katika bonde ia Usangu Kutumia kilimo cha kumwagilia maji katika mashamba kwa njia ya mifereji
iliyochimbwatoka mto Mbarali. Angalia habari zao hapa chini.
UDONGO WA BONDE LA USANGU
Bonde la Usangu lilikuwa na mi to ambayo maji yake yalikuwa yanatiririkia kuelekea katika
bonde la Ziwa Rukwa naZiwa Nyasa. Milipuko ya Volkano ya mlima Rungwe ikaizuia mito hiyo kwa
mwinuko wa ardhi halafu mito ikatiririka katika bonde la Usangu na kulifanya bonde la Usangu kuwa
ziwa. Katika mabadiliko ya ardhi, udongo, changarawe na michanga ikaletwachini yaziwa lenyewe.
Mito ambayo ilikuwa inatiririkia katika bonde la ziwa Rukwa na ziwa Nyasa, sasaziwa lililokuwapo
katika bonde la Usangu (mahali ambapo mbuga za Usangu zipo sasa) likapata nafasi ya kuyamwaga
maji yote kwa njia ya mito upande wa Kaskazini — Mashariki, na mbuga zikatokea toka kwenye
mchanga wa ziwa lenyewe. Na udongo na matope na udongo wa mfinyanzi unaopatikana katika
mbuga za Usangu umeletwa na mito mbali mbali inayotiririkia katike. bonde hili la Usangu.
Udongo wa mbuga za Usangu ni wa aina nyingi na unafaa sana kwa mazao. Kuna udongo wa
mfinyanzi, udongo wa mbuga, na udongo mweusi wenye rutuba sana. Udongo waainazote hizi una
rutuba nyingi sana kwa mazao.
Mazao yapandwayo katika bonde hili ni mpunga, mahindi, viazi vitamu, viazi ulaya, ulezi,
migomba, maharage, karanga, miwa, mihogo na maboga mbalimbali.
MAGONJWA
Mbuga za Usangu zina maradhi mengi sana, magonjwa ambayo yanawasumbua sana watu ni
homa, kichocho, safura, surua, homa ya papasi, ugonjwa wa kuhara na magonjwa ya minyoo ya aina
mbalimbali. Walakini magonjwa mabaya sana ambayo yanammalizia mkulima wakati wake mwingi
sana ni kichocho, homa, safura na ugonjwa wa kuhara. Sababu ya kupatikana kichocho kwa wingi
sana katika mbuga za Usangu ni kwamba mbuga za Usangu zina matopematope mengi sana na pia
kuna majimaji mengi ambayo yamekwama hayatembei. Konokono ambao ndio hueneza vidudu vya
ugonjwa wa kichocho hupenda sana kuogelea katika maji ambayo yamekwama na kwa jinsi hii
vidudu vya kichocho huachwa humohumo majini vikingojea mwanadamu yeyote kupitia katika maji
hayo au kuogelea katika maji hayo na wakati huo vidudu vya kichocho vyamrukia mtu na kupenyeza
katika mwili wake hadi kibofuni na kwenye matumbo ambako vyazaliana sana na kuanza kula
sehemu ya ngozi ya sehemu hizo. Kuutibu ugonjwa wa kichocho ni kazi ngumu sana lakini waweza
kuzuiliwa kwa urahisi sana kwa kutumia njia zilizo rahisi sana za kiafya.
Ugonjwa mwingine unaowasumbua sana watu waishio katika mbuga hizi ni homa ya mbu. Mbu
nao huzaliana kwa wingi sana kwa sababu ya unyevunyevu mwingi unaopatikana katika mbuga hizi
— hasa katika mashamba ya mpunga ambayo yana maji ya kumwagilia mashamba yakaayo kwa
4
muda mrefu hata kuwawezesha mbu kuzaliana kwa muda mrefu sana. Penye maji yaliyosimama
ndipo mbu huzaliana haraka sana na kwa urahisi mno. Kama nilivyosema hapo juu, mbuga za
Usangu zina matopematope mengi na madimbwimadimbwi mengi yaliyokwama ambayo yanafaa
sana kwa mbu kuzaliana.
Ugonjwa mwingine wa watu wa Usangu unaowasumbua sana ni ugonjwa wa kuhara. Ugonjwa
huu watokana na kunywa maji machafu, na mbuga za Usangu nyingi zina maji yaliyo machafu na
hayafai kunywa binadamu.
Lakini watu hawana njia nyingine ya kupatia maji yaliyo safi isipokuwa hiyo tu. Maji ya mto
ambayo ni maji safi kidogo kuliko maji yaliyotuama yanapitia kwa mbali sana na ni watu wachache
tu wanaonufaika na maji haya ambazo wanaishi karibu ya hiyo mito.
Kwa sasa hivi Wizara ya Afya inatoa mafunzo ya afya kwa akina mama walio karibu na kituo cha
afya cha Rujewa na vijiji vingine. Pia kituo hicho kinatoa dawa za kukinga maradhi ya surua,
kifaduro, ndui, polio na kifua kikuu. Tatizo kubwa kwa upande wa utumishi ni kwamba wafanyakazi
ni wachache sana.
HISTORIA
Wasangu ni watu ambao wametokana na jamii za Kihehe, Kisafwa, Kibena, Kinyakyusa na
kidogo jamii ya Kingoni. Jamii zote hizi, isipokuwa Wangoni, ni jirani za Wasangu, na kwa jumla
Wasangu walikuwa ni watu ambao walijulikana sana katika nyanda za juu za Kusini katika karne ya
18 na karne ya 19. Mali kadhalika walikuwa ni jamii iliyokuwa na nguvu nyingi sana ya utawala na
kivita. Hawa watu walikuwa wanaishi sehemu ya llamba iliyo karibu maili 60 Kaskazini ya Utengule
kabla ya kuja Waarabu na Wajerumani, na kila mahali walipofanya maskani yao walipaita
"Utengule", mahali paamani.
Waarabu walipokuwa wanaingia katika nchi ya Usangu waliingia kufanya biashara. Hawa
Waarabu walikuwa wanauza nguo, magobole, baruti na shanga. Kutoka kwa Wasangu, Waarabu
walipata meno ya tembo. Hapo awali mbuga zote za Usangu zilikuwa na wanyama wa kila aina na
ndovu walienea kila mahali katika mbuga hizi za Usangu, kwa hiyo ilikuwa rahisi sana kwa Wasangu
kuwaua tembo na kupata meno yao ill wayauze kwa Waarabu.
Biashara nyingine kubwa ambayo ilikuwa inafanywa na Waarabu katika mbuga hizi za Usangu
ilikuwa biashara ya utumwa. Wasangu walikuwa ni watu ambao walijua namna ya kupigana vita
sawasawa na kwa kuwa walikuwa na chifu wao mmoja tu ilikuwa rahisi kwao kuungana pamoja na
kufanya jeshi moja kali na lenye nguvu sana kuliko jamii zingine walizopakana nazo ambazo zilikuwa
hazina utawala mmoja kama vile Wanyakyusa, Wasafwa na kadhalika. Lakini Wahehe na Wakimbu
walikuwa na utawala mmoja sawa kama Wasangu walivyokuwa.
Kwa kuwa utawala wa Wasangu ulikuwa na nguvu na umoja mkubwa, waliweza kupigana vita
kwa nguvu moja na jamii zingine zilizokuwa jirani nao. Chifu Merere, ambaye ndiye aliyekuwa
mtawala wa Wasangu, alikuwa mtawala shupavu na mpenda raia wake. Kwa kuwa alikuwa anapata
silaha bora toka kwa Waarabu alipowauzia meno ya tembo, aliweza kuwashinda maadui zake bila
taabu kubwa na mateka waliuzwa kwa Waarabu wafanya biashara ya utumwa. Hasa Merere aliwauza
utumwani watoto wa Kisafwa na Kihehe ambao aliwateka wakati wa vita. Uwezo wake Merere katika
kupigana na jirani zake ulisaidiwa sana na ushauri aliokuwa anaupata toka kwa wazee wa Kisangu na
pia toka Mbaluchi ambaye alikwenda Usangu na kuwa Mshauri Mkuu wa Vita wa Chifu Merere I
ambaye yaaminiwaaliingia nchi ya Usangu kati yamwaka1878 na mwaka1880. Mbaluchi (Mburushi)
huyu aliitwa Jemadariambaye kufika kwake Utengule/Usangu kulisababisha Wabaluchi (Maburushi)
wengine kuja Usangu na kuanza shughuli za kilimocha mpunga (angaliachini ya kilimo hapachini).
Wasangu wenyewe wanasimulia kuwa Waarabu walianza kuingia nchi ya Usangu wakati wa utawala
wa Chifu Njali aliyewazaa akina Merere.
5
siri na kupita huko. Si njia ya kutoka pwani tu iliyohatarishwa na Wasangu ball hata njia ya kuelekea
nchi ya Wabemba kuelekea Zambia ilitiwa msukosuko.
Mara kwa mara Wasangu waliuteka utawala wa Kiwele uliokuwa sehemu ya kati ya Ukimbu
ambao ulikuwa njiani Kusini ya Tabora. Mara baada ya Chifu Kilanga kutawala katika nchi ya
Ubungu, Wasangu walimshambulia katika mwaka wa 1856 — 1857 wakimsaidia ndugu yake Kafwimbi, na ingawa Wasangu walishindwa, Kafwimbi alitorokea nchi ya Usangu tena.
Kati ya mwaka 1859 wakati Bwana Burton alipoondoka Afrika ya Mashariki na mwaka 1866 Tippu
Tip alipotembelea reli ya Usangu chifu Muigumba akafariki wakati akipigana na Wahehe. Binini,
ndugu ya Mihwela alikuwa amejifunza sana maarifa ya kupigana vita, na kwa kuwa alikuwa na ari
kubwa ya kutaka kutawala Uhehe nzima. Wakati fulani karibu ya miaka ya 1860 alifanya vita na
Wasangu na alifanikiwa kuviteka vijiji vingi sana na kuwateka wanawake na mifugo yao. Binini
mwenyewe alimwua kiongozi wao Muigumba na akachukua jina lake na kujiita yeye mwenyewe
Munyigumba kama ukumbusho wa ushindi wa kuwatawala Wahehe wote. Huyu Binini
(Munyigumba) ndiye aliyekuwa baba wa chifu Mkwawa na ndiye chifu mkuu wa kwanza wa Wahehe
wote.
Baada ya kifo cha Muigumba vita vikali sana vya urithi wa utawala vikatokea na mjukuu wake
Muigumba kwa jina Merere Towelamahamba akatokea kuwa mshindi na akawaua jamaa zake wengi
sana ambao alishindana nao katika kurithi utawala. Ugomvi wa urithi wa utawala uliwadhoofisha
sana Wasangu katika kupigana vita na majirani zao.
Kati ya mwaka wa 1866 na mwaka wa 1872 Wasangu wakatokea jamii yenye nguvu sana chini ya
chifu Merere wa kwanza kuliko hapo awali, na wakawashambulia majirani zao na kuziteka nchi zao
zote hasa upande wa Mashariki Kusini na upande wa katikati wa nchi ya Wakimbu. Wak&ti huu
Wasangu walikuwa wamefikia kilele cha nguvu zao na hakuna jamii nyingine yoyote iliyoweza
kuikabili jamii ya Kisangu katika pande hizo za Tanzania.
Katika mwaka wa 1867 Bwana Livingstone aliambiwa na Waarabu katika nchi ya Ubungu
kwamba Wasangu walikuwa ni wapole kwa wageni wowote, na kwamba Merere mara nyingi alifanya
mashambulizi kwa machifu wa jirani ili ateke mifugo na watumwa na kuwauza kwa wafanya biashara
wa Kiarabu. Katika mwezi wa Agosti Bwana Livingstone alisikia habari nyingi zaidi za kupendeza
kuhusu chifu Merere na alichelea kuwa huenda akaharibiwa na Waarabu. Walakini katika mwaka wa
1871 habari zikafika Mayema kwamba Merere kisha kosana na Waarabu akiwatuhumu kwamba
walikuwa wanafanya njama ya kumshambulia ili Goambari, mmojawapo wa Wajukuu wa Muigumba
aweze kutawala. Kwa ajili ya sababu hii Merere akawashambulia Waarabu na marafiki zao wote.
Akamwua Mwarabu mmoja naakawanyang'anya Waarabu wenginemali yote waliyokuwa nayo.
Wakati huu Amrani Masudi akajitokeza kwenye uwanja wa vita. Amrani alikuwa ni Mwaarabu
toka Zanzibar wakati Zanzibar ilipotawaliwa na Waarabu. Tanzania Bara ilikuwa inatawaliwa na
machifu mbalimbali wa jamii mbali mbali na Waarabu waliokuwa wakiishi Tanzania Bara walikuwa
wafanya biashara tu sio watawala. Kwa jinsi hii Amrani hakupendelea utaratibu huu, kwa hiyo
akaamua kuwafanyia vita machifu wote wa Tanzania Bara na kuwafanya watu wote wawe chini yake
ili baadaye waweze kumleteamenoyatembo bilaya kuyalipiachochote.
Wakati Amrani Masudi alipofika Tabora akaambiwa kuwa kuna machifu wawili wenye nguvu
sana ambao walihatarisha misafara yote ya biashara ya Waarabu na kuwatoza kodi kubwa kabla ya
kuwaruhusu kupita katika nchi zao. Machifu wenyewe ni Nyungu-ya-Mawe wa Kiwele katika nchi ya
Ukimbu na Merere wa Usangu. Lakini chifu wa hatari kabisa na mwenye nguvu zaidi kuliko mwenzake alikuwa Merere. Baada ya kupata habari hizo, Amrani akalichukuwa jeshi lake na akaomba
kuongezewa askari toka kwa machifu waliomwogopa kupigana naye ili aende na jeshi kubwa la
kuweza kumshambulia Merere vilivyo. Alipoondoka Tabora, alipita Ngulu, Unyangwila, Itumba,
Kipembawe na Igunda mpaka akafika Usangu. Maluteni wake walipita Ukonongo, Isamba,
Wikangulu, Ubungu na Uguruke. Wengine walipitia Ugogo. Kila chifu wa sehemu za Magharibi na
kati na Kusini ya Tanzania alitoa kwa Amrani askari wa kumsaidia katika vita kati yake na Wasangu.
Lakini Nyungu-ya-Mawe hakutoa hata askari mmoja wa kumpa Bwana Amrani.
7
MISAFARA YA KWANZA YA KIARABU
1850 - 1929
Njia ya kwanza ya biashara ya Waarabu kutoka Pwani hadi Unyamwezi ilipita Ukimbu karibu na
mpaka wa Wasangu, na mpaka katikati ya miaka 1830 Waarabu wafanya biashara walifika katika
utawala wa Isenge na Isange upande wa Mashariki wa nchi ya Ukimbu. Huko waliweza kukutana na
Wanyamwezi ambao walibadilishana nao bidhaa — hasa Waarabu wakabadilishana nao bunduki na
bidhaa na meno ya tembo. Baada ya mwaka 1835 waliendelea na safari yao hadi Unyamwezi
yenyewe. Mahali paitwapo Isenga na Isange ndipo njia ya kuelekea Pwani ilipogawanyika: njia ya
Kaskazini iliyokwenda Mbwamaji na njiaya Kusini ikipita Usangu kwenda Kilwa.
Wakati huo kulikuwapo Chifu mmoja maarufu sana aliyeitwa Munyugumba aliyewashinda
majirani zake wote waliokuwa wakiishi katika bonde la Ruaha na akaifanya jamii ya Kisangu kama
jamii ya kivitaambayo iliogopwa sana na majirani na misafara ya biashara hali kadhalika.
Ari ya kivita ya Wasangu ilisababishwa na silaha zenye nguvu zaidi walizopata toka kwa
Waarabu na pia mshawasha walioupata katika vita vya kijamii ambamo waliwateka watu wengi na
kuwauza utumwani. Angalia maelezo zaidi hapo juu. Utawala wa Wakimbu wa Isange na Isenga
ambapo palikuwa kituo cha mwisho cha njia ya biashara ya Waarabu ulikuwa sasa katika hatari
kubwa ya kuvamiwa na Wasangu na Waarabu wakalazimika kutafuta njia nyingine ya kufanyia
biashara yao ambayo baadaye ikasababisha kuanzisha kituo cha Tabora na mji wa Tabora ukaanzishwa wakati huo kama kituo kipya cha kufanyia biashara yao.
KUJA KWA WANGONI
Baada ya Wangoni kuondoka Ufipa, kundi moja likaenda upande wa Kusini hadi Songea ambako
walifanya maskani yao katika miaka 1850, Wakiwa katika safari yao kuelekea Kusini wakapitia nchi
ya Usangu na kuwashambulia vikali sana Wasangu na Wasangu wakakimbilia Usavila Magharibi ya
Uhehe. Wasangu wakiwa Usavila wakayaunganisha majeshi yao pamoja na majeshi ya Wasavila ili
waweze kumpiga vita Chifu wa Wahehe aliyeitwa Mihwela aliyeishi sehemu za Udongwe. Kwa bahati
nzuri chifu Mihwela akasikia habari hizi na akafanya mpango wa kuhamisha ng'ombe wote na
kuwaweka mahali pa salama ili wasije wakatekwa na Wasangu. Wasangu wakafanya kambi yao
Ipagala sehemu iliyo kati ya Tosamaganga na Kalenga. Walakini asubuhi na mapema chifu Mihwela,
ambaye alikuwa chifu wa kwanza wa Wahehe aliwakomoa sana hawa Wasangu kwa kuwatandika
barabara.
Wangoni walipoondoka nchi ya Usangu basi nao Wasangu wakarudi nchini mwao na chifu
Muyugumba akajenga ngome mpya upande wa Mashariki wa llamba mahali ambapo Mto Ruaha
waingia penye bwawa. Sasa Wasangu wakaanza kulijenga jeshi lao upya kwa kufuata utaratibu wa
majeshi ya Wangoni kwa' kutumia mikuki mikubwa na ngao kubwa za ngozi za wanyama. Wasangu
walijifunza maarifa mengi ya kupigana vita na maarifa hayo yakawafanya Wasangu waweze kuwa
watu wenye jeshi la nguvu sana kupita majeshi yote katika nyandaza juu za Kusini.
WASANGU WAPIGANA NA AMRANI MASUDI
NA KILANGA WA KWANZA 1855—1875
Wasangu walikuwa wamenyamazishwa kidogo na Wangoni katika kuishambulia misafara
iliyopitia katika nchi walizozitawala. Walakini Wangoni walipocndoka tu toka nchi ya Usangu basi
Wasangu wakavifufua vita upya na katika mwaka wa 1855 waliweza kuwaua wafanya biashara wa
Kiarabu kutoka Mbwamaji. Wakati Bwana Burton alipoweza kutembelea pande hizi za Tanzania
katika mwaka wa 1857 Waarabu hawakuthubutu kupitia karibu na nchi ya Usangu wakichukuwa
bidhaa zao za kibiashara toka pwani ingawa misafara michache michache iliweza kujipenyeza kwa
6
^
Habari za kuja kwa jeshi la Amrani zikamfikia chifu Merere, kwa hiyo Merere akawaambia watu
waliokuwa mipakani mwake kuwa wasiwashambulie maadui hao mara tu wawaonapo, ball wao
waende Makao Makuu llamba (Utengule Usangu) alipokuwa anaishi chifu. Ujanja huu ulikuwa wa
kumlazimisha Amrani Masudi aondoke sehemu za milimani na zenye misitu ill ateremke katika
Mbuga za Usangu ambazo zilikuwa hazina misitu. Baada ya kuambiwa hivyo, watu wa Merere
walipowaona maadui wanakuja wakakimbilia Utenguie Makao Makuu ya Wasangu. Amrani Masudi
aliingia ndani ya nyumba za Wasangu na kuchukuwa chakula na mifugo ya kuwalisha askari wake.
Wakazidi kuwafuata Wasangu ambao kwa sasa walikuwa wanakimbilia Utengule mpaka jeshi lake
Amrani likafika Utengule Makao Makuu ya Merere. Wakati majeshi ya Amrani yalipokaribia Utengule,
Merere akawaamuru watu wake waanze kuwashambulia watu wa Amrani.
Yasemekana kuwa vita ilipiganwa toka asubuhi hadi jioni. Kesho yake vita ikaanza asubuhi
mpaka jioni tena. Siku ya tatu ya vita, Amrani akauawa na Wasangu na vita ikasimama kwa mara ya
kwanza tangu ianze. Chifu Kilanga ambaye alikuwa anaongozaria na Amrani akimsaidia, akaamua
kuendelea kupigana na Wasangu, ambapo machifu wengine wakaamua kukimbia kwa sababu
kiongozi wao wa vita Amrani alikuwa ameuawa. Walakini Kilanga peke yake asingeweza kumshinda
Merere kwa hiyo akauawa hapo hapo vitani. Baada ya hapo maadui walipoona mambo
yamewaelemea vibaya wakaanza kukimbia na huku Wasangu wakiwafukuza nyuma na kumwua mtu
yeyote wanayemkamata.
Amrani alitaka kupigana kwanza na Merere kwa sababu Merere alikuwa ni chifu mwenye nguvu
zaidi kuwashinda machifu wote. Kama angalimshinda Merere^basi Amrani angalikwenda kupigana
na chifu Nyungu-ya-Mawe ambaye alikuwa anatawala Ukimbu wakati huo. Tangu wakati huo, wakati
Amrani Masudi alipopata cha mtema kuni na kunyolewa kikavu na chifu Merere, hakuna Mwaarabu
yeyote aliyejaribu kuitawala Tanzania Bara na kuanzisha serikali yao wenyewe. Vita hii kubwa
yawezekana ilipiganwa mwanzoni mwa mwezi Oktoba, 1873.
KINDUMBWENDUMBWE NA WAHEHE1875
Kushindwa kwa Amrani Masudi kulisaidia kuongeza na kueneza umaarufu wa chifu Merere
ingawa baadaye kidogo alikiona kindumbwendumbwe akichezeshwa na Wahehe. Kati ya mwaka
1860 na 1880 Wahehe nao walitokea kuwa watu wenye nguvu sawa na nguvu za Merere. Wakati wa
miaka ya 1860 Munyigumba aliziteka tawala za Kihehe na aliweza kuanzisha utawala wake katika
nchi ya Uhehe. Kufaulu kwake kulisababishwa na mambo mawili, wasifu mzuri na watu wengi
walikuwa tayari kuukubali utawala wake kwa sababu aliweza mara nyingi sana kuyazuia
mashambulizi ya Wasangu ya mara kwa mara na baadaye mashambulizi ya Wangoni. Pili alikuwa
amejifunza maarifamengi ya kivitatoka kwa Wasangu ambao nao waliigatoka kwa Wangoni.
Wahehe waliiga sana utawala wa Wasangu na utaratibu wa majeshi yao. Wahehe walijifunza
toka kwa Wasangu namna ya kuwatia ari wapiganaji vita kama ilivyotumiwa na Wasangu wakati wa
vita na kwa kuwa Wahehe walikuwa wamejifunza Kisangu kwa hiyo wakajivunia sana lugha hii mpya
ya Kisangu. Wasangu na Wahehe waliyagawanya majeshi yao katika makundi makundi ya askari
ambayo yalikuwa na majina maalum. Mikuki mikubwa na matumizi ya ngao za ngozi za wanyama
ziliigwa toka kwa Wangoni. Wasangu na Wahehe wanafanana sana katika desturi zao.
Mmoja wa mabinti wa chifu Munyigumba alikuwa ametolewa na wakampa Chifu Merere
Towalahamba ill awe mkewe. Yasemekana kwamba chifu Merere alikuwa na zaidi ya wake 300, kwa
sababu chifu aliyeshindwa na Merere vitani alilazimishwa kumtoa binti yake mmoja au zaidi na
kumpa Merere. Na zaidi ya hayo, Merere mwenyewe alijigawia wanawake wengine aliowateka wakati
wa vita na jirani zake. Wakati binti huyo wa Munyigumba ambaye alikuwa mke wa Merere
alipopofushwa macho na ndui akamuudhi Munyigumba kwa kumrudishia binti yake akiwa katika hali
ya upofu. Kwa hiyo naye Munyigumba akamrudishia tusi hili kwa kumshambulia Merere katika
mwaka 1875. Merere alitwangwa vizuri sana na ikambidi akimbie kuokoa maisha yake. Kuanzia
wakati huo Wahehe ndio wakawa jeshi lenye nguvu kushinda majeshi ya jirani zao na wakati Merere
aliposhambuliwa akakimbilia Kiloli katika nchi ya Ukimbu pamoja na wafuasi wake ambako akawa
mgeni wa Nyungu-ya-Mawe.
8
MERERE AKIWA IIKJMBU MWAKA 1875
Nyungu-ya-Mawe alikuwa rafiki mkubwa wa Merere na wakati Amrani alipofunga safari ya
kwenda kumshambulia Merere, Nyungu-ya-Mawe alikataa kutoa msaada kwa Amrani kwa kujua yeye
mwenyewe angalishambuliwa na Waarabu baadaye. Nyungu ya Mawe alikuwa ameziteka tawala za
Ukimbu kati ya mwaka wa 1871 na mwaka wa 1881.
Merere na Wasangu hawakuwa wageni sana katika nchi ya Ukimbu. Babu yake Merere kwa jina
Mui'gumbi alikuwa ametembelea tawala za Ukimbu kabla ya Merere kufika huko na alikuwa amekwisha pigana na Kilanga katika nchi yaWabungu. Kabla ya Nyungu-ya-Mawe kuwa mtawala mwenye
nguvu Wasangu walikuwa wameshinda machifu wote wa Ukimbu ya kati na kusini na mashariki mwa
nchi na machifu wa Kikimbu wa Kipembawe, Igunda, na Hume (Chunya) walikuwa wanatawala nchi
hizo kwa ruhusa ya Wasangu. Katika nchi ya Kiwele machifu llaasi na Kupumpa walikuwa marafiki
wakubwa wa Merere na kwa msaada wake Merere hawa machifu waliweza kuwatia wasiwasi machifu wa
Wakimbu kwa upande wa kaskazini.
Kati ya mwaka wa 1871 na mwaka wa 1875, Nyungu-ya-Mawe aliupanua utawala katika tawaia za
Wakimbu. Alivanya mpango wa kuishambulia Kiwele lakini kabla ya kufanya hivyo akanuia
kuwaomba Wasangu ambao kwa wakati huo walikuwa wanapigana na Wahehe na kusema kweli
walikuwa tayari kuupokea msaada wake Nyungu-ya-Mawe, tena mmojawapo wa mabinti wa Nyungu-yaMawe alikuwa ametolewa na kumpa Merere awe mke wake.
Merere alipopigwa na Wahehe katika mwaka wa 1875, aliweza kutoroka na wapiganaji wake
wachache. Baada ya kukaa kwa muda mfupi katika nchi ya Ubungu ambako watu wa Ubungu
walikuwa wanamchukia, Merere akaenda kujificha chini ya ulinzi wa Nyungu-ya-Mawe Kiwele. Huko
alikaa kwa muda wa mwaka mmoja na akaweza kuanzisha jeshi jingine jipya kabla ya kurudi kwake
Usangu. Wakati alipokuwa akiishi Ukimbu, aliweza kumsaidia Nyungu-ya-Mawe katika kuishinda nchi
nzima ya Wakimbu. Kijiji alichokijenga Merere sehemu ya Kiwele bado kinaitwa Kiloli mpaka sasa
likiwa na maana ya "WALOLI". Katika mwaka wa 1877 Merere alirudi nchini kwake naakajenga ngome
nyingine mpya chini ya Milima ya Mporoto pahala paitwapo MFUMBI.
MERERE AKIWA MFUMBI
Wakati Merere aliporejeshewa mamlaka yake, Wavumbuzi wa Kiingereza Elton na Cotteril!
walifika Mfumbi mwezi wa Oktoba 1877. Na kuweza kuishi kwa muda wa wiki mbili katika ngome yake
hiyo. Mara tu baada ya kuondoka Mfumbi. Elton naCotterill wakasikia ya kuwa Wangoni walikwishapatana na Wasangu kuwaponda Wahehe na kuiteka mifugo yao iliyokwishaibiwa na Wahehe
hapo awalj kitendo ambacho kiliwaudhi sana Wahehe na kuwafanya wawashambulie Wangoni.
Wahehe walifanikiwa katika kuwaponda Wangoni kwa sababu chifu wa Wangoni alikuwa hajawa
tayari kwa vita. Wangoni nao wakaazimu kulipiza kisasi na kuwashambulia Wahehe na
kumlazimisha chifu Munyigumba kwenda kujificha katika mapango yaliyokuwa upande wa kaskazini wa
Uhehe ambako alikufa baada ya kuugua.
Kwa wakati huu utawala wa Wahehe ulikuwa umebadilika sana; badala ya nchi nzima
kutawaliwa na machifu wengi sana Uhehe nzima ilikuwa inatawaliwa na chifu mmoja tu ambaye kwa
sasa watu wake walikuwa wamejifunza sana mambo ya vita na kuwashinda majirani zao vibaya sana
Kama vile watu wa Utemikwila, Wangoni na Wahehe. Chifu mpya wa Uhehe akafanya mapatano na
Wangoni katika mwaka 1881 Hi wasishambuliane mpaka watoto wakue na kwa jinsi hii Wahehe na
Wangoni wakawa watani wao, uhusiano ambao mpaka sasa upo kati ya jamii hizi mbili. Lakini watu
waiiokuwa wamebakia kuwa wa hatari sana kwa Wahehe ni Wasangu.
Baada ya kufa chifu Munyigumba mwaka 1878 watoto wakashindania urithi, na baadaye
Mkwawa akatokea kuwa chifu mwenye nguvu kubwa katika mwaka wa 1883 na vita ya mara kwa mara
ilitokea kati ya Merere na Mkwawa na Mkwawa mara nyingi aliweza kumshinda Merere.
9
MERERE ATAWALA NCHI YA WASAFWA TOKA 1883 - 1898
Mara nyingi sana Mkwawa aliweza kumshambulia Merere na mwishowe Merere akalazimika
kukimbilia nchi ya Wasafwa. Mkwawa akatawala nchi ya Usangu na Merere alishindwa kumwondoa
kutoka katika nchi yake. Baada ya Merere kufanya misafara yake ya vita katika nchi ya Ukukwe,
Umalila, Uhehe na Usafwa mwishowe akajenga ngome yake mpya sehemu ya Mpedjere chini ya
mlima Mbeya na kuiita Utengule mpya. Merere alishindwa kabisa na Mkwawa na ingawa Merere
aliweza kumpa chifu Mkwawa binti zake wawili lakini hawakufanya amani hata siku moja. Akiwa
katika nchi ya Usafwa Merere aliendelea na vitendo vyake vya kuwashambulia majirani zake pande
zote Kusini, Mashariki Kaskazini na Magharibi huku akiwatia katika utawala wake mkali, kama vile
Wanyakyusa wa Kaskazini, Wanyiha na Wasafwa, na mara nyingi alikuwa na wazo akilini mwake la
kumwondoa chifu Mkwawa kutoka katika nchi yake ya Usangu.
WAJERUMANI WAJA MWAKA WA 1892
Katika mwezi wa Januari mwaka wa 1892, Wamishonari wa kwanza walifika Utengule, nao ni
Merensky na Nauhaus wa misheni ya Berlin. Baada ya mwaka mmoja kupita Wamishonari wengine
wa Moravian walifika Utengule, hao ni Meyer na Richard na Kootz. Katika mwaka huo huo alifika
MejaVon Wissman na DK. Bumiller nakamanda wakampuni Meja Von Prince.
Wajerumani walikuwa wamepata habari za kuhusu vita vya Merere vya kuwashambulia Wahehe
mara kwa mara. Ingawa Merere alisababisha matata mengi kwa jamii za jirani lakini chifu Mkwawa
alid.haniwa na Wajerumani ni mtu wa hatari kubwa kwa utawala wao, nao kwa jinsi hii, Wajerumani
walikuwa tayari kumsaidia Merere katika kila hali. Wajerumani walikuwa na matumaini kupata
msaada wa Wasangu katika kumtia adabu chifu Mkwawa, naye Merere alitumaini kuwatumia
Wajerumani ili aweze kumfukuza adui yake mkubwa kutoka katika nchi yake. Katika mwaka huo huo
wa 1893 Merere wa kwanza akafariki nakurithiwa na mtoto wake Merere wa pili Mgandilwa.
Von Wissman akaanzisha uhusiano mzuri na chifu Merere wa pili ambaye alikuwa bado mmoja
wapo wa machifu wenye nguvu sana pande hizo za Tanzania kabla ya kumshambulia chifu Mkwawa.
Von Wissman akaona afadhali aende ziwa Rukwa na kumwadhibu Bwana KIMALAUNGA
ambaye alikuwa ni mnyanganyi na ambaye alijiimarisha mwenyewe kama mtawala wa bonde la Ziwa
Rukwa. Von Wissman akamtuma msaidizi wake DK. Bumiller kwa Merere ili akamwombe msaada
wa askari 100 wa Kisangu. Kusikia haya, Merere akafurahi sana na kuona ndiyo nafasi yake naye ya
kujiimarisha katika utawala wake. Kwa hiyo Merere akamshauri DK. Bumiller awashambulie
Wanyiha chini ya chifu NZUNDA. Wakamshambulia chifu Nzunda na kumshinda lakini gharama ya
kumshinda ilikuwa kubwa mno na ikawalazimu waahirishe safari yao ya kwenda kumtwanga
Kimalaunga. Vita waliyomfanyia Nzunda ilimtingisha sana chifu Merere kwa sababu ya kuwapoteza
askari wengi waliokufa wakati huo, lakini hata hivyo chifu Merere aliwahitaji sana Wajerumani ili
waweze kuwashambulia Wahehe.
Mwishowe matumaini ya Merere yakadhihirika wakati Wajerumani walipoanza kufanya mipango
ya kumshambulia chifu Mkwawa. Von Schele akawa ndio kamanda wa msafara wa vita hii na Dk.
Bumiller akawa mkuu wa sehemu nyingine ya jeshi. Wakati wa kiangazi cha mwaka wa 1894 Von
Schele akaanza mashambulizi yake juu ya chifu Mkwawa na akaiharibu kabisa ngome ya Mkwawa ya
Kalenga: kuharibiwa kwa ngome ya Kalenga kulimaanisha kuwa mwisho wa nguvu za utawala
umefika ingawa chifu Mkwawa aliendelea kuitawala nchi ya Uhehe kwa muda wa miaka mingine
minne baadaye na ilikuwa mwaka wa 1898 Mkwawa alipojiua yeye mwenyewe wakati Wajeruman
walipokuwa wakimtafuta.
Kifo cha Mkwawa kilimaanisha mwisho wa vipingamizi vya Wahehe kwaserikali ya Wajeruman
na hii ikasababisha Wahehe kuondoka katika nchi ya Usangu ambayo ikarudishwa kwa chifu
Merere ambaye akafanya maskani yake au makao yake Makuu Utengule (Usangu). Utawala wa
Usafwa na Makao yake Makuu Utengule (Usongwe) ukarudishwa kwa Wasafwa chini ya chifu wao
Mwalyego.
10
Wakati wa vita vya Uhuru vya Maji maji Wajerumani walitiwa wasiwasi mkubwa na chifu Merere
kwa sababu yeye ndiye aliyekuwa chifu mwenye nguvu zaidi katika Wilaya ya Iringa ambaye alikuwa
amejijengea ngome ya makao yake Makuu. Mara mbili chifu Merere alilazimishwa na Wajerumani
kutoa askari. "Hi waende kuwasaidia Wajerumani katika shughuli zao za Vita na jamii zingine za
Tanzania. Hata baada ya kufariki Merere wa nne katika mwaka wa 1906 kutokana na sumu wasiwasi
wa Wajerumani ulizidi kuongezeka hata Katibu Mkuu wa Serikali ya Kijerumani alisema", ili
kuhakikisha utii wa Wasangu ni lazima ngome ya askari ianzishwe ama sivyo utii wa Wasangu
hautajulikana sawasawa". Ingawa ngome ya askari ilianzishwa lakini hata hivyo mambo yakazidi
kuwa mabaya zaidi mpaka mwisho wa mwaka wa 1909 ambapo Wasangu wakafikiriwa kuwa ni wa
hatari sana kwa utawala wa Wajerumani. Merere wa tano alikuwa ni mtu mvivu, na ambaye hakuwa
mwangalifu na kawatawala watu wake katika njia mbaya sana. Alichukiwa sana na Wajerumani
kuliko mtu yeyote katika nchi nzima na Wajerumani wakamwondoa kutoka katika nchi yake na
kumpeleka katika kisiwa cha Mafia mwezi wa Oktoba 1910 kwa sababu ya utawala wake mbaya, na
badala yake ndugu yake Mtengela akatawala.
KILIMO KATIKA BONDE LA USANGU
Katika kueleza kilimo kinachoendeshwa katika bonde la Usangu nitajaribu kueleza hictoria ya
kilimo cha mpunga ambacho ndicho kilimo kikubwa kushinda vilimo vyote vinavyoendeshwa katika
bonde hili na halafu nitajaribu kuelezea jinsi kinavyoendeshwa kwa sasa hivi na hapo baadaye
nitaelezea kilimo cha jadi cha Wasangu wenyewe ambao ndio wenyeji wa Mbuga za Usangu.
HISTORIA YA KILIMO CHA MPUNGA
Yaaminiwa kuwa mpunga ulipandwa katika bonde la Usangu kwa mara ya kwanza na mfanya
biashara ya utumwa Mwaarabu kwa jina TIPP TIP ambaye katika mwaka wa 1968 aliwaacha watu
katika bonde la Usangu ili wapande mpunga; na kilimo hiki cha mpunga kikaweza kuendelezwa zaidi
na jamii ya Wabaluchi (Maburushi)ambapo Mbaluchi wa kwanza kufika Utengule/Usangu alikuwa
bwana Jemadari ambaye alifika Utengule kuwa mshauri Mkuu wa vita wa chifu Merere wa kwanza.
Baada ya miaka kumi baadaye, kuja kwake Mbaluchi (Mburushi) huyu katika nchi ya Wasangu
kuliwavutia Wabaluchi (Maburushi) wengine kuja kukaa katika Usangu, na mwisho wa karne ya19
familia za Kibaluchi zikaingia katika bonde la Usangu na kuanza kulima kilimo cha mpunga.
Mbaluchi (Mburushi) aliyeacha historia nzuri ya kilimo cha mpunga cha kumwagilia maji
alikuwa Bwana MOOLAR ABDALLAHIM PREMOHAMED, ambaye mpaka sasa kizazi chake yaani
wajukuu zake, bado wanaishi Rujewa wakishughulikia kilimo cha kumwagilia maji.
Bwana Moolar Abdballahim Premohamed alifika nchini Tanzania mwaka wa 1920, na baadaye
akaamua kwenda kukaa Usangu katika bonde la Usangu na kuanza kulima kilimo cha mpunga katika
mwaka wa 1928. Katika mwaka wa 1940 akaomba ruhusa kutoka kwa serikali ya kikoloni ya
Kiingereza ili aweze kuchimba mfereji wa maji kwa ajili ya kilimo cha kiangazi cha mpunga. Bwana
Moolar alipewa masharti na Serikali ya Kiingereza kwamba kwa kuwa kaomba kuchimba mfereji wa
maji ni lazima aumalize mfereji huo katika muda wa miezi kumi na mbili tu, si zaidi ya hapo. Baada
ya kupata ruhusa akaanza kuuchimba mfereji huo na kuumaliza katika mwaka wa 1941 na alitumia
miezi kumi na moja tu katika kuumaliza mfereji wenyewe. Zana alizozitumia katika kuuchimba
mfereji huo ni sululu, majembe, nyundo na maji ambayo yalitumiwa kumwagia miamba ya mawe ili
iweze kupasuka kwa urahisi huku wakiipasha moto tena. Mfereji huo ambao mpaka sasa unatumika
una urefu wa maili saba.
Serikali ya Kiingereza ilitoa sheria kuwa si ruhusa kwa mtu ambaye si Mzungu kulima eka zaidi
ya kumi. Kwa hiyo, bwana Moolar aliruhusiwa kulima eka 10 tu kwa sababu hakuwa Mzungu. Lakini
Mbaluchi (Mburushi) huyo aliweza kupata eka 40 badala ya eka 10 kwa kutumia majina ya shemeji
na watoto wake; na aina za mpunga zilizopandwa wakati huo ni Kahogo na faya. Na katika mwaka
wa 1945 bwana Moolar aliruhusiwa na serikali ya Kiingereza kupata shamba lake mwenyewe baada
ya kuona juhudi zake kubwa katika kuuchimba huo mfereji wa maji ambao bado unatumika wakati
huu.
11
Tabia ya Wabaluchi (Maburushi) ni kwamba huweka chakula cha akiba cha kutosha miaka miwili
inayokuja ill kuepukana na maafa ya vita, njaa, nzige na majira mabaya ya hali ya hewa. Wenyeji wa
Usangu wameiga mambo mengi — hasa ufundi na ujuzi mwingi sana wa kuchimba mifereji ya maji
ya kumwagilia mashamba yao ya mpunga. Hali kadhalika utaalam wa kutumia trakta na jembe ulaya
la kukokotwa na ng'ombe umeigwa na wenyeji fulani fulani wanaolima kilimo cha kisasa waishio
Usangu.
Hapo awali hawa Wabaluchi (Maburushi) walikuwa wanakodisha plau za Wabena ambazo ndizo
zilizolima mashamba yao ya mpunga. Wabena walikuwa na maplau na ng'ombe wa kuyakokota
maplau, halafu waliwalimia mashamba yao hawa Wabaluchi (Maburushi) kwa kulipwa fedha.
Baadaye, katika mwaka wa 1958 Wabaluchi (Maburushi) wa Rujewa walinunua trakta lao la kulimia
na mpaka wakati wa kuandika habari hizi, Februari, 1975. Wabaluchi (Maburushi) wana matrakta
matano ya kulimia ambayo pia yanatumiwa kulimia mashamba ya wenyeji kwa kuyakodi.
Hawa Wabaluchi (Maburushi) walitoka nchi iliyo kati ya Pakistan na Iran iitwayo Baluchistani
ambayo sehemu moja iko Iran na sehemu nyingine iko Pakistan. Huko walikotoka hawa Wabaluchi
(Maburushi) hulima mashamba yao kwa kutumia maplau ya miti yaliyochongwa vizuri na kutiwa
chuma nchani na kukokotwa na ng'ombe. Na mazao yao yalimwayo huko walikotoka ni choroko,
mtama, mpunga na ngano mazao ambayo yanapandwa kwa kufuatana na hali ya nchi. Chakula chao'
kikuu huko walikotoka ni wali, zao ambalo ni zao kuu la watu hawa. Hata huko Usangu kwenyewe
Wabaluchi hawa hupanda sana mpunga na ndilo zao na chakula chao kikuu. Shughuli yao kuu ni
kilimo cha mpunga ingawa mazao mengine pia yanapandwa na watu hawa. Pia wanafuga ng'ombe,
mbuzi na kondoo huko Rujewa na wanakunywa sana maziwa ya ng'ombe. Dini yao kubwani Uislamu
na wanatumia dakika 75 kila siku za kusali na saa za shambani ni saba kwa siku. Halafu wakati
unaobakia unatumiwa katika shughuli zingine kama vile kula chakula, kukamua maziwa, kuongea,
kuuza duka na kuyatengeneza matrakta yao ili yawe katika hali timamu tayari kwa kazi ya kesho yake.
Zana zingine za kilimo chao ni vyombo vya kupandia mbegu, matrakta, na maplau. Vifaa
vinapoharibika vyatengenezwa na wao wenyewe kwani kila Mbaluchi ni makanika mwenyewe wa
trakta lake hapeleki trakta lake kwa mtu mwingine yeyote kumtengenezea, bali hulitengeneza yeye
mwenyewe kama limeharibika.
Kazi ya shambani ni ya wanaume tu na wanawake wa Kibaluchi (Kiburushi) hujishughulisha na
kazi za kinyumbani tu.
NDOA ZA WABALUCHI (MABURUSHI)
Wabaluchi (Maburushi) huoana kwa kufuatana na ubinamu. Kama jamii nyingi za Kiarabu
zinavyofanya. Makusudi ya kufuata ndoa za namna ni kudumisha ukoo wao, pili kuepukana na talaka
nyingi ambazo si za lazima, tatu kupanua ukoo wao; na kadhalika. Wakati wa kuoa, fedha
iliyopangwa na baba ya msichana yatolewa ikiwa kama mahari. Mali hiyo yatumiwa na msichana
katika kununulia vitu vya kwenda navyo kwa bwana yake. Na iwapo kumetokea talaka, basi
bwana hutoa kiasi fulani cha fedha na kumpa mkewe ambaye anatalikiwa naye ili ikamsaidie kule
anakokwenda. Kama ni bibi anataka kumwacha bwana, basi naye bibi hufanya hivyo hivyo kumpa
bwana yake fedha naye ikamsaidie kule anakokwenda. Walakini inatokea mara nyingi sana kwa
bwana kumsamehe bibi asimpe mahari yoyote wakati bibi ataka kuachika na bwana yake. Jamii ya
Wabaluchi (Maburushi) iliyoko Rujewa ni ya ukoo mmoja kwa sababu wamekuwa wakioana wao kwa
wao kwa kufuata ubinamu na hawaoani nje ya utaratibu huu labda itokee kwa bahati mbaya.
12
KILIMO KINACHOENDESHWA SASA USANGU
Jamii zote za Usangu zimegawanyika katika shughuli za uzalishaji mali kama ifuatavyo hapa
chini—
1. Wavuvi wa samaki Usangu na wafanya biashara ya samaki ni WAKINGA.
2. Wakulima ni WANYAKYUSA, WABENA, WABALUCHI (Maburushi) na WASUKUMA.
3. Wafugaji ni WASANGU, WAMASAI na WASUKUMA.
Ufuatao hapa chini ndio utaratibu wa shughuli za kilimo katika Wilaya ya Mbeya:MWEZI
JUNI
JULAI
MAZAO
Kahawa
Ulezi
Mahindi
Maharage
JULAI /AGOSTI
SEPTEMBA
—
MIPANGOYA KAZI
Kuendelea kuvuna na
kuchimba mashimo
Kuvuna
Kuvuna
Kuvuna
Kazi za maendeleo
Kuuza mazao.
OKTOBA
Ulezi
Mahindi
Kutayarisha mashamba
Kutayarisha mashamba
NOVEMBA
Kahawa
Kufukia mashimo, kutia
dawa na kazi za maendeleo
SEHEMU YA MASHARIKI
NOVEMBA
Mahindi
Mpunga
Pamba
Karanga
Kulima na kupanda
Kulima na kupanda
DESEMBA / JANUARI
FEBRUARI / MACHI
Mahindi Pamba
Mpunga Karanga
Kupalilia
Kupalilia
Vitunguu
Viazi Vitamu
Mihogo
Kulima na kupanda
Kulima na kupanda
Kulima na kupanda
JUNI / JULAI / AGOSTI
Mpunga
Mahindi
Karanga
Pamba
Kuvuna
Kuvuna
Kuvuna
Kuvuna
SEPTEMBA / OKTOBA
Vitunguu
Mpunga
Pamba
Mahindi
Kuchimba mifereji na kupanda
Kutayarisha mashamba
Kutayarisha mashamba
Kutayarisha mashamba
MACHI / APRILI /MEI
13
Kama nilivyoeleza hapo juu, kilimo cha mpunga kiliwachwa na Waarabu wafanya biashara ya
utumwa na baadaye kilimo hiki kikaendelezwa zaidi na Wanyakyusa, Wabena, Wahehe, Wasangu na
kufikia kima cha kilimo hiki killchopo sasa. Miche ya mpunga hupandikizwa na kupandwa wakati
mvua zimeanza kunyesha na baadaye umwagiliaji maji watumika sana. Mbolea ya aina yoyote
haitumiwi ili kurutubisha ardhi yake kwa sababu udongo wake una rutuba nyingi mno. Jembe la
mkono ndilo zana kubwa sana ya kulimia ingawa jembe la kukokotwa na ng'ombe na trakta yanazidi
kutumiwa sana siku hizi. Kulima kwa trakta au plau huanza mwezi wa Desemba na katika
kutengeneza majaruba majembe ya mikono yatumiwa kati ya Januari na Machi. Kupandikiza miche
kwafanyika mara tu baada ya kuyasawazisha na kuyatengeneza majaruba. Mpunga wavunwa na
huondolewa kwenye masuke kati ya mwezi wa Juni na mwezi wa Agosti. Mavuno yote ya mpunga
tukiacha shamba la Taifa yaweza kukadiriwa kuwa Tani 24,000 kwa wastani, ambayo asilimia 50
yanauzwa.
Mkulima hutumia familia yake katika kazi za shamba. Wakati wa shughuli nyingi za shamba,
mkulima hupata msaada katika kazi za shambani kwa kuwaalika watu wengine na wakulima
wengine wanaojiweza huwaajiri watu wengine na kuwalipa ujira wao. Umwagiliaji maji wa
mashamba ya mpunga huwa wa lazima kwa sababu aina za mpunga zinazopandwa Usangu
zinahitaji maji mengi mno. Milima ya Mporoto, Kipengere na Milima ya Chunya ndiyo inayotoa mito
ambayo maji yake yanatumika sana katika kumwagilia mashamba ya mpunga kwa kuchlmba
mifereji midogo midogo ambayo inapeleka maji kwenye kila shamba la mkulima wa mpunga.
14
SEHEMU ZINAZOPANDWA MPUNGA KATIKA BONDE LA USANGU
Hizi hapa chini ni takwimu za mpunga ulionunuliwa kutoka bonde la Usangu kufikia Desemba
31,1972.
MWAKA WA KUPANDA MPUNGA
TAN I
WAISHIA 31 MEI
ZILIZONUNULIWA
1964 — 1965
37,780
1965 — 1966
20,580
1966 — 1967
37,550
1967 — 1968
30,160
1968 — 1969
44,440
1969 — 1970
63,353
1970 — 1971
92,240
1971 —1972
69,445
*1972 — 1973
55,121
Toka: Bodi ya Taifa ya
Mazao. * : Mpaka
Desemba, 1972.
15
Takwimu hizi hapa chini zaonyesha ununuzi wa Mpunga na Bodi ya Mazao ya kilimo kwa
kufuata Mkoa katika Tanzania Baratoka mwaka wa 1969 — 1973 katikaTani.
MKOA
1969 — 1970
1970 — 1971
1971 — 1972
1972 — 1973
Mbeya
20,238.6
19,553.9
22,264.8
17,539.2
Tabora
20,437.2
26,812.2
15,291.0
9,352.1
Mwanza
9,296.2
17,870.0
2,723.9
1 ,323.0
Morogoro
2,162.0
4,890.4
10,868.3
9,732.6
Mara
4,344.3
8,992.3
3,811.1
1 ,534.4
Shinyanga
1,975.2
5,820.3
2,820.2
5,732.4
Kilimanjaro
2,196.2
3,623.0
3,630.6
5,224.4
Pwani
235.9
175.8
4,978.9
3,969.0
Iringa
893.0
2,011.4
1,180.9
222.0
Kigoma
812.7
1,327.7
707.7
14.0
Tanga
187.5
903.3
368.8
351.2
Mtwara
447.4
233.0
515.0
—
Ruvuma
126.7
—
234.2
71.9
Arusha
—
24.3
22.5
—
Dodoma
—
2.0
15.9
—
92,239.6
69,444.8
Jumla
63,352.9
55,125.2
Toka: Bodi ya Mazao ya kilimo.
Takwimu hizo hapo juu zaonyesha kuwa Mikoa 15 tu ndio inayotoa mpunga kati ya Mikoa 18
ya Tanzania Bara na Mikoa yote imepangwa kiasi cha tani zilizouzwa katika miaka 4 iliyopita ya
kupanda mpunga. Mkoa wa Mbeya umekuwa wa kwanza kwa kutoa mpunga mwingi uliokwisha
uzwa ukifuatiwa na Mkoa wa Morogoro na Tabora.
Mvua zinapokuwa haba katika mwaka, basi mito yote hii inayopeleka maji katjka bonde la
Usangu hupungua sana kima chake hata husababisha upungufu wa maji kwa ajili ya Wakulima na
wafugaji wa mifugo. Hata hivyo maji huwa hayatoshi kabisa kwa mifugo wakati wa kiangazi kwa
sababu wakulima ambao wana mashamba yao sehemu za upande wa juu wa bonde la Usangu,
ambao wamezibaziba maji mengi kwa ajili ya kunyweshea mashamba yao. Kwa hiyo maji mengi
yanaelekea katika sehemu hizi za mashamba na wafugaji ambao wana mifugo mikubwa sana ya
wanyama wanashindwa kupata maji ya kutosha,kwa ajili ya mifugo; yao. Kuna haja ya kurekebisha
tena utaratibu wa kugawanya maji ili wafugaji, ambao ndio wenyeji bonde-hili la Usangu pamoja na
wakulima wengine, wasipate taabu
KILIMO KWA JUMLA
Wakulima huanza kulima mashamba ya mahindi mara mvua zinyeshapo katika miezi ya
Novemba na Desemba. Katika mashamba haya, maharage na wakati mwingine karanga zapandwa
pamoja na mahindi.katika shamba moja. Wakati huo huo viunga vya kutayarishia miche ya mpunga
yaanzishwa katika majaruba au kati ya matuta mawili ya mihindi kwa kutegemea kiasi cha maji
kinachopatikana wakati huo.
Kilimo cha mpunga chaanza mara tu baada ya ardhi ya shamba kulainika vizuri na pia baada ya
kufanyika kazi ya kulima mashamba ya mahindi. Wakulima wengine hufanya matayarisho ya kilimo
cha kwanza katika mwezi wa Agosti na Septemba wakati ardhi ikiwa bado laini. Jembe la Plau na
wakati mwingine matrekta yaweza kutumiwa wakati wa kilimo hiki cha kwanza. Kilimo cha pili
chafanyika pamoja na kusawazisha udongo katika mwezi wa Januari na Februari hadi katikati ya
mwezi wa Machi na hii ni kazi ya jembe la mkono; kila jaruba lajazwa maji na majani sasa yamekwisha kuwa marefu sana. Majani haya yalimwa na kulundikwa katika mafungu mafungu, na udongo
chini ya mizizi yake watolewa na maji na kisha majani hayo yalundikwa katika matuta yakifanya
majaruba. Kisha kusawazisha kwa-fanyika kwa kulima udongo pamoja na maji na hufanya matope
ambayo huchanganywa vizuri sana mpaka usawa wa maji umefikiwa. Baada ya hapo miche ya
mpunga yapandikizwa.
Wakati wa kupandikiza miche ambayo ni kazi inayofanywa na wanaume halikadhalika
wanawake, vile vile kilimo cha viazi vitamu chafanyika wakati wa miezi hii hii pamoja na kuanzisha
kwa mashamba ya maharage. Wakati wa kusawazisha majaruba kazi hii yaendelea hadi kupalilia
majaruba yaliyotangulia kupandikizwa miche ya mpunga. Wakati wa miezi ya Aprili na Mei, kazi ya
kuamia ndege yaanza na kazi ya kukata miti kwa ajili ya ulezi, na karibu na mwisho wa Juni hadi
Agosti kazi ya kuvuna mpunga huwa imeshamiri barabara. Na kazi ya kupepeta mpunga vile vile
yafanyika wakati wa miezi hii hii. Pia mahindi yanavunwa na kuwekwa katika vihenge. Wakati wa
kiangazi shughuli za kilimo huwa zimepungua sana isipokuwa" kwa wale wakulima ambao wanayo
maji ya akiba ndio huendelea na shughuli za kilimo. Wakati huu wa kiangazi vitunguu vyalimwa na
mwezi wa Novemba, matawi makavu na majani yalfyokauka katika mashamba ya ulezi huchomwa
moto.
KILIMO CHA MPUNGA
Kilimo cha mpunga kama nilivyoeleza hapo mwanzoni ni kikubwa zaidi kuliko kilimo chochote
cha mazao katika bonde la Usangu, lakini kilimo chenyewe kina dosari zake. Kwa mfano, mashamba
yote ya mpunga hayatiwi mbolea ambayo inapatikana kwa wingi sana katika bonde hili. Ingawa'
udongo wa bonde la Usangu una rutuba sana, lakini upo uwezekano mkubwa wa rutuba kupungua
baada ya kupanda mpunga kwa muda wa miaka minne au mitano mfululizo. Mpunga unapovunwa,
wakati, mwingine mpunga wavunwa kabla mabua yake hayajakauka vizuri, kwa hiyo joto na
unyevunyevu waweza kuharibu mpunga wenyewe.
Kuondoa punje za mpunga toka kwenye masuke hufanyiwa ardhini. Wakati mwingine fimbo
zatumiwa ili kuondolea punje za mpunga toka kwenye masuke na kitendo hiki chaufanya mpunga
utakaopepetwa kuchanganyikana na changarawe ndogo ambazo ni za hatari kwa meno na matumbo
pia. Yafaa njia nyingine nzuri itumiwe. Mali kadhalika mpunga wachukuwa wakati mwingi sana wa
mkulima kuliko yanavyomchukuwa mazao mengine katika kuyalima; na pia magonjwa yachukuwa
muda mrefu wa mkulima. Kuna haja ya kufanya kampeni ya magonjwa yanayopatikana katika bonde
hili ili yaweze kushambuliwa au kuzuiwa.
17
MATATIZO YA KILIMO CHA MPUNGA
Wakulima wengi sana wanatumia majembe ya mikono. Hili ni tatizo kwa sababu jembe la
mkono lamchukuwa mkulima wa kawaida saa nyingi kumaliza eka moja na pia anatumia nguvu
nyingi zaidi wakati wa kulima kuliko ambavyo angalitumia kama angalitumia plau au trekta. Kuna
haja vile vile ya kubadili mila na desturi za Wasangu ambao kwa kweli wafuga ng'ombe kwa wingi
sana kwa ajili ya ufahari tu bila ya kuwatumia ipasavyo. Na jamii zingine zilizo katika bonde la
Usangu zatumia zaidi kilimo cha jadi badala ya kilimo cha kisasa. Vijiji vya ujamaa ndivyo ambavyo
vimeendelea mbele kidogo katika kutumia njia za kisasa za kilimo. Lakini watu waishio katika vijiji
vya ujamaa, wengi wao hawana matrekta wala plau.
Tatizo jingine linasababishwa na jua. Kipinrdi cha jua kali ni kirefu zaidi kuliko majira ya mvua.
Kwa kawaida mvua zaanza mwezi Novemba hadi Desemba halafu kuna kipindi cha jua kali na ukame
mwezi Januari hadi Februari. Halafu kuanzia mwezi wa Machi hadi Aprili mvua zanyesha. Baada ya
hapo kipupwe na ukame wafuata ukiambatana na jua kali katika miezi ya Juni hadi Oktoba.
Wengi wa Wasangu na jamii zingine waajiriwa na Wabaluchi katika kulima mashamba ya watu
hawa. Waacha kazi za mashambani mwao na kufanya kazi za kulipwa, kumbe katika kufanya hivyo
kazi zao za mashamba yao zinalala na kazi katika mashamba ya Wabaluchi hazilali hata kidogo. Kwa
hiyo, Waafrika wengi hubakia nyuma siku zote kwa kufanya kazi za kulipwa katika mashamba ya
watu wengine. Si Wabaluchi tu wanaoajiri vibarua bali hata mtu yeyote yule anayejiweza huajiri
vibarua wakumsaidia kazi shambani. Angalia hapo juu chini ya kilimo katika bonde la Usangu.
Tatizo jingine lililo kubwa sana katika bonde hili ni mgawanyo wa maji ya kunyweshea
mashamba mbali mbali ya mpunga na mazao mengine. Kusema kweli watu wengi hawana maji bali
hutegemea sana maji ya mvua. Mvua zisiponyesha, basi wakulima hawa hawawezi kulima na
wakapata mazao mazuri. Pia wale wakulima wachache ambao wanategemea maji ya mito katika
kunyweshea mashamba yao ya mpunga wana matatizo yao, yaani jinsi ya kuwa na utaratibu mzuri
wa kugawana maji ya mito sawa sawa ili wakulima wengine wasipunjike. Mpaka wakati huu kuna
kupunjana sana katika kuyatumia maji ya mito iliyomo katika bonde hili. Kadri nilivyoona na
kuyaangalia mashamba ya mpunga niliona kuwa watu wengine walikuwa na maji ya kutosha katika
mashamba yao yanayoletwa na mifereji ya kuchimbwa kutoka kwenye mito wakati watu wengine
walikuwa hawana tone la maji ingawa nao walichimba mifereji ya kiasi chao. Wakati huo huo
wafugaji wa mifugo walikuwa na shida kubwa ya kukosa maji kwa ajili ya mifugo yao. Maji ya mito
yatakuja leta mzozo mkubwa kati ya wakulima iwapo utaratibu mzuri wa kuyagawanya maji kwa watu
wote waishio katika bonde hili la Usangu hautapatikana. Maji ya mito katika bonde la Usangu
yanathaminiwa sana na watu wote waishio huko kwa sababu ndio mtaji mkubwa sana kwa watu
wote. Kwa jinsi hii, utaratibu mzuri wa kuyagawanya maji wafaa uanzishwe upesi.
Tatizo jingine la wakulima wa Usangu ni kwamba yasemekana wakulima wengine wa Kiafrika
wanafanya magendo ya kuuza mazao yao kwa Wabaluchi bila ya kuyapeleka mazao kwenye chama.
Lakini hili sina hakika nalo iwapo ni kweli kitendo hiki kinafanyika. Iwapo ni kweli jambo hili
linafanyika basi kuna haja kubwa ya kulipiga vita kabisa kwa kutumia njia safi na maarifa mengi.
Tatizo jingine ni kwamba wakulima wengi wanaweka fedha zao kwa Wabaluchi (Maburushi) badala
ya kuziweka katika benki ya biashara. Tabia hii ni mbaya sana kwani inamletea matatizo mengi yule
mtu anayeweka fedha zake kwa Mbaiuchi badala ya kuziweka fedha zake katika benki. Mtu huyo
anayeweka fedha zake kwa Mbaiuchi, anapozitaka hachukuwi fedha taslim bali huambiwa
kuchukuwa vitu kidogo kidogo toka duka la huyo Mbaiuchi mpaka kima chote cha fedha alizoweka
zimekwisha. Bei ya vitu anavyochukuwa toka dukani huandlkwa na mwenye duka na ndiye peke
yake anayejua ni kiasi gani kimebakia katika jumla ya fedha zote zilizowekwa dukani mwake na
mkulima. Sikupata nafasi ya kulithibitisha jambo hili lakini pengine safari ijayo nitaweza
kuthibitisha iwapo jambo hili ni la kweli.
18
MIFUGO KATIKA BONDE LA USANGU
Ifuatayo hapo chini ndiyo idadi ya
iliyohesabiwakabla ya mwaka 1973: —
1. Ng'ombe walikuwa
2. Mbuzi walikuwa
3. Kondoo walikuwa
4. Nguruwe walikuwa
5. Punda walikuwa
6. Kuku walikuwa
Mifugo
yotekatika
Wilaya
yote
ya
Mbeya
250,600
39,080
25,069
1,889
293
42,552
Idadi ya mifugo katika bonde la Usangu peke yake kabla ya Wamasai na Wasukuma kuingia
katika bonde hili mwaka wa 1973.
1. Ng'ombe walikuwa
149,528
2. Mbuzi walikuwa
10,490
3. Kondoo walikuwa
7,543
Takwimu hizi hazina idadi ya ng'ombe wa Wamasai na Wasukuma ambao walianza kuingia
katika bonde la Usangu kuanzia mwezi wa Agosti mwaka 1973 baada ya kuhesabu mifugo yote katika
bonde hili mwaka 1972.
MAGONJWA YA MIFUGO
Magonjwa makubwa yanayoisumbua mifugo katika bonde la Usangu ni haya: —
1. Chambevu (Blackquarter)
2. Kimeta(Anthiax)
3. Ndigana (East Coast Fever)
4. Ndigana Baridi (Anaplasmosis)
5. Ugonjwa wa midomo na miguu (Foot and Mouth)
6. Ndorobo.
MATATIZO KUHUSU MIFUGO
Baada ya Wamasai na Wasukuma kuingia katika bonde hili matatizo mengi yamezuka hasa
kuhusiana na mifugo yao ambayo imesababisha mgongano kidogo na Wasangu ambao pia ni
wafugaji stadi. Wamasai na Wasukuma walianza kuingia bonde la Usangu mwezi wa Agosti mwaka
1973 huku wakiandamana na mifugo yao mikubwa. Walipokuwa wakiingia bonde hili la Usangu
waliweza kueneza ugonjwa wa ng'ombe wa miguu na midomo (Foot and Mouth disease) ugonjwa
ambao ulikuwa haujulikani kabisa katika bonde la Usangu. Ugonjwa huu uliua mifugo mingi ya
Wasangu na jambo hili liliwaudhi wafugaji wa Kisangu. Pia mifugo ya Wamasai na Wasukuma
ilisababisha ukosefu wa malisho ya kutosha kwa Wasangu jambo ambalo hawakulizoea tangu
zamani.
Halikadhalika Wamasai ambao ndio waliotangulia kuingia bonde la Usangu kabla ya Wasukuma
walianza kugongana na Wasukuma wakati Wasukuma wakiingia katika bonde hilo na kuwakuta
tayari Wamasai wamejiimarisha.
Kuyadhibiti maradhi ya ng'ombe huwa ni vigumu sana kwa maafisa wa mifugo kwa sababu hawa
wahamiaji Wamasai na Wasukuma huingia katika bonde hili bila ya utaratibu wowote, na hueneza
magonjwa mengi ya mifugo kwa urahisi sana. Vile vile wafugaji wengine hawanunui dawa za kutibia
na kuzuia magonjwa ya mifugo kwa sababu husema kuwa dawa hizo ni aghali sana ambapo wafugaji
wengine hukubali kununua dawa hizo na kuwatibu wanyama wao.
19
Idara ya mifugo inapatataabu sana katika kutoa huduma safi kwa wafugaji katika bonde hili
kwa sababu wafugaji wenyewe wametawanyika huko na huko pamoja na mifugo yao. Hawakai
pamoja. Kwa jinsi hii, ni vigumu sana kutoa huduma nzuri kwa wafugaji wote pamoja. Hili ni
tatizo linaloikabili Idara ya Mifugo. Halikadhalika barabara hazipitiki wakati wa majira ya mvua.
Kwa hiyo huwa ni vigumu kwa Idara ya Mifugo kuwahudumia wafugaji kwa sababu wanashindwa
kusafiri hadi mahali walipo hao wafugaji.
Zaidi ya hayo kuhamahama kwa wafugaji ambao huhamia bonde la Usangu na mifugo yao na pia
kutoka katika bonde hilo kwafanya kazi ya Idara ya Mifugo kuwa ngumu sana pia kuidhibiti
sawasawa tabia hii ya kuhamia bonde hili bila taarifa yoyote kwa idara ya mifugo katika Wilaya ya
Mbeya huwa ni kazi ngumu. Pia hawa wafugaji ni wagumu sana kuwasikiliza mabwana mifugo
wanapotoa mashauri yao kwa hawa wafugaji. Tatizo jingine ni kwamba wafugaji wenyewe hawana
chama chao cha ushirika kitakachoweza kuwasaidia wafugaji katika shughuli zao za ununuzi na
uuzaji wa wanyama wao. Mpaka wakati wa kuandika habari hizi, Mbaluchi mmoja ndiye
aliyeruhusiwa kununua na kuuza ng'ombe katika Mikoa mingine inayotaka kununua ng'ombe na
kadhalika. Ingawa chama cha wakulima wa Usangu wanajaribu kununua ng'ombe wachache lakini
hakitoshi.
Kwa upande wa utumishi kuna tatizo la upungufu wa watumishi wa Idara ya Mifugo. Wengine
waliopo sasa hivi katika Wilaya ya Mbeya hawajapata nafasi ya kuwaongezea ujuzi wao kama idara
zingine zinavyofanya. Kuna haja ya kuongezea mafunzo watumishi wa mifugo waliopo sasa. Hii
itasaidia kuinua ujuzi wao na kufanya uchumi wa mifugo uweze kuongezeka zaidi. Labda itafaa
kuongeza nafasi kwa watumishi hawa katika vyuo vya Mpwapwa na Morogoro ambavyo hasa ndio
vyuo vyataifa vinavyotegemewa sana kwa kutoa watumishi wa mifugo hapa nchini.
Kwa sasa hivi, Idara ya Mifugo inazo zahanati nne za mifugo katika bonde la Usangu na Idara hii
inao mpango wa kuanzisha kituo cha mafahali wa nyama na kuanzisha kiwanda cha kutengeneza
samli. Vile vile wanatarajia kuanzisha shamba la kufugia ng'ombe (Ranch).
KILIMO CHA WASANGU
Baada ya kusimulia shughuli za uchumi kwa jumla katika bonde hili la Usangu sasa nitasimulia
shughuli za uchumi za Wasangu kama jamii pekee ya asili kabisa katika bonde hili. Kama
ilivyoelezwa katika historia ya Wasangu hapo juu, Wasangu wametokana na jamii za Wasafwa,
Wahehe, Wabena, Wanyakyusa ambao jadi yao ni ukulima wala sio ufugaji. Wasangu tangu awali
walikuwa wanalima na kufuga ng'ombe wachache sana kama jamii zinazowazunguka zilivyokuwa
zinafuga. Utamaduni wa Wasangu wa kufuga ng'ombe wengi na kuacha utamaduni wao wa kwanza
wa kilimo ulianza kutokea wakati wa vita mbalimbali vilivyopiganwa kati ya wao na majirani zao.
Angalia hapa chini. Kilimo chao kilikuwacha majembe ya mikono. Majembe haya yalitengenezwa na
Wakinga kutoka Ukinga na wakayaleta kwa Wasangu ili wayauze. Wakinga walibadilishana majembe
yao na ng'ombe; huyu ng'ombe alichukuliwa na Mkinga aliyeleta majembe, na akakaa naye huyu
ng'ombe mpaka wakati wa kuzaa. Baada ya kuzaa mara moja tu kwa Mkinga, ng'ombe huyo
alirudishwa kwa Msangu maana bei ya jembe au majembe ilikadiriwa kwa mtamba au mitamba. Na
iwapo ng'ombe huyo aliyechukuliwa na Mkinga alifia kwa Mkinga kwa bahati mbaya, basi Mkinga
alilazimika kumchuna ngozi na kuirudisha kwa mwenye ng'ombe pamoja na majembe mawili au
matatu kama malipo.
Mpini wa jembe ulitengenezwa kwa mti uitwao "mshala" na wakati wa kuchomeka jembe
lenyewe katika mpini mlunda, kitu kama msumari mrefu, ambao ulichomwa sana moto, ulitumika
kutobolea shimo kwenye mpini kwa kuuchoma mpini wenyewe. Baada ya hapo jembe nalo
lilichomwa sana na kutiwa kwenye shimo la mpini uliokwisha tobolewa na msumari halafu majani
fulani yaliyochanganywa na mavi ya ng'ombe yalitiwa pamoja kwenye jembe na kutiwa katika shimo
ili jembe liweze kusaki barabara. Kazi hii ilifanywa na mafundi maalum ambao walikuwa wanaishi
kijijini.
20
Wakati wa kuanza shamba jipya, miti na majani hufyekwa kwa kutumia shoka na miundu.
Baada ya hapo miti iliyofyekwa shambani huachwa ili iweze kukauka kwa jua. Wakati majira ya
mvua yanakaribia, majani na matawi yote ya miti huchomwa moto. Shamba hulimwa kwa sesa
na kupandwa ulezi. Katika mwaka wa pili shamba hulimwa matuta na kupandwa mahindi. Kilimo
chao kilifanyika kati ya mwezi wa Januari na Februari katika kila mwaka. Kulima kwao kulikuwa kwa
njia ya kualikana. Pombe ilipikwa ili iweze kunywewa baada ya kazi ya kulima. Siku hizi utaratibu
wa kualikana wakati wa kulima umetoweka na ubinafsi umekuwa mwingi mno.
Wakati wa kuvuna Wasangu hawakualikana; kila familia ya Kisangu ilivuna mavuno yake.
Mashamba ya familia ya Kisangu yaligawanyika sehemu mbili; sehemu ya mke na sehemu ya
bwana, na mavuno pia yalitenganishwa. Mavuno kutoka shamba la mwanamke yaliwekwa katika
kihenge chake na mavuno toka shamba la bwana yaliwekwa katika kihenge cha bwana. Wakati
wageni walipotembelea ndugu zao, waliweza kupewa chakula kwa kufuatana walikuwa ni wageni wa
nani — wageni wa bwana au wageni wa mwanamke. Kama walikuwa wageni wa bwana basi
walipewa chakula toka kwenye ghala ya bwana na kama walikuwa wa mwanamke basi wageni
walipewa chakula toka ghala ya mwanamke.
Watoto hawakushughulika sana na kilimo bali walijishughulisha na kuchunga ndama au
mitamba. Mpaka wakati huu kilimo cha Wasangu hakijabadilika sana yaani matumizi ya jembe la
mkono ni yale yale yaliyokuwapo zamani kabla ya Wasangu hawajaanza kufuga ng'ombe kwa wingi.
Labda kitu kilichobadilika katika kilimo cha Wasangu, ni kuacha kujishughulisha na kilimo zaidi
kama hapo awali na kuanza kujishughulisha na mifugo zaidi katika karne ya 18 na karne ya 19.
GHALA
Ghala za vyakula zajengwa kwa kutumia miti ya MIPEREHEME na huezekwa kwa manyasi
yaitwayo LIPEPETE au LIKUHI. Kamba za kufungia fito ni za MAHANGO na mayota. Ghala hujengwa
kwa kuinuliwa juu ya ardhi kwa kuogopa mchwa. Ghala zenyewe si madhubuti sana kwa kuzuia
panya.
21
UFUGAJI WA NG'OMBE
Kama ilivyoelezwa hapo mwanzoni, Wasangu walikuwasi wafugaji maarufu wa ng'ombe Kama
walivyo sasa, bali walifuga ng'ombe wachache na kwa wastani kila familia iliweza kufuga ng'ombe
wawili au watatu hivi. Lakini kazi yao kubwa sana ilikuwa kilimo. Ufugaji wa mifugo mingi ulianza
Wasangu walipokuwa wanafanya vita na majirani zao katika karne ya 18 na karne ya 19. Shabaha
mojawapo kubwa ya Wasangu kufanya vita na majirani zao ni kuteka mifugo ya maadui. Pia
walikuwa na shabaha ya kuteka wanawake wa maadui na baada ya kuletwa utumwa katika nchi za
jirani, basi wakaanza kuwateka watoto wa maadui ili wakawauze utumwani. Basi ilikuwa wakati huu
wa vita ambapo walijiongezea mifugo kwa wingi sana na kila Msangu aliyeshiriki katika vita
aligawiwa ng'ombe waliowateka vitani. Chifu wao aliwagawia ng'ombe watu wake wote walioshiriki
vitani. Kwa jinsi hii Wasangu waliacha utamaduni wao wa kwanza wa kulima na kuanza kufuga na
kutegemea sana mifugo yao badala ya kulima.
SHABAHA YA KUFUGA NG'OMBE
(i)
Nguo za Wasangu zilitengenezwa kwa kutumia ngozi za ng'ombe, na pia matandiko ya
kitanda yalikuwa ni ngozi.
(ii)
Maziwaya ng'ombe ni mboga kubwa sana kwa Wasangu. (iii)
Ng'ombe wanatumiwa kama
mahari ya kuolea wanawake. (iv)
Ng'ombe huchinjwa kilioni na matambikoni na nyama kuliwa na
watu. ( v )
Kwa siku hizi Wasangu wanauza ng'ombe ili wapate fedha lakini ng'ombe
wanaouzwa ni
wachache sana.
(vi) Kuonyesha ufahari wa utajiri kuliko Wasangu wasiokuwa na ng'ombe wa kutosha. (vii)
Kwa kawaida ng'ombe wa Wasangu hawachinjwi kwa ajili ya nyama, bali ng'ombe wafugwa
ili kuonyesha ufahari wa utajiri katika jamii ya Wasangu na hapo zamani matajiri wa
Kisangu
waliweza kutoa ng'ombe mmoja au wawili kwa chifu wao ili wamwonyeshe utajiri wao.
Halafu chifu wao aliwateua hao matajiri kuwa viongozi wa vijiji na kuweza kutawala baadhi
ya vijiji fulani. ( v i i i ) Kwa wastani familia moja ya Kisangu hufuga kati ya 200 — 300; na
wanaogopa kupanua
Kilimo chao kwa sababu ya kuogopa kumaliza malisho ya mifugo.
Dawa a kutibia magonjwa mbalimbali ya ng'ombe ni
(i) Limulimuli. (ii) Lirungurugu (iii) na dawa ya kutibia ugonjwa wa mlguu na midomo ilikuwa ni
kuwapa wanawake shughuli ya kuwachunga ng'ombe ambayo haikuwa kazi yao hasa. Wanaume
hawakuruhusiwa kupitia sehemu ambako wanawake walikuwa wakichunga hao ng'ombe waliposhikwa na ugonjwa huu. Wakati wa kuchunga ng'ombe, wanawake walivaa nguo za wanaume wakati
ambapo wanaume nao walivaa nguo za kike na walibakia nyumbani na kupika badala ya wanawake
kupika. Yaaminiwa kuwa kwa kufanya hivyo, ng'ombe wa ugonjwa huu walipona kabisa bila ya dawa
yoyote. Kitendo hiki cha kubadilishana kazi ya kuwachunga ng'ombe kati ya wanaume na wanawake
kilitosha kabisa kuwatibu ng'ombe walioshikwa na ugonjwa huu wa miguu na midomo.
UTAWALA WA WASANGU
Kabla ya kuja Waarabu katika bonde hili, Wasangu walikuwa na mtawala mmoja mkuu ambaye
alitawala nchi nzima ya Usangu. Chini ya Mwene alikuwapo jumbe mkuu ambaye ndiye alikuwa
Waziri Mkuu wa serikali ya Kisangu, naye alisaidiwa na wajumbe wadogo walioitwa Watambuli.
Baada ya hawa Watambuli walikuja raia. Wakati wa kumtafuta chifu wa kutawala nchi ya Usangu,
Watambuli (wazee) ndio waliomchagua Mwene wao.
Kwa kawaida chifu katika uhai wake kabla hajafa aliwachagua watoto wake wawili kuwa kati yao
mmoja atatawala, ndipo Watambuli (wazee) humchagua mmoja kati yao aliye na busara.
22
SIFA KUU ZA MWENE
Lazima mtu yule atakayechaguliwa kuwa chifu awe na utii kwa wazee; lazima aweze kuyakubali
yanayosemwa na wazee; lazima huyo chifu awe kiongozi bora katika vita. Kabla yakutawazwa chifu
mteule akae na wazee (Watambuli) kwa muda ili apigwe msasa safi. Siku ya kutawazwa ikiwadia,
Mjumbe Mkuu humchukuwa yule chifu mteule na kumkalisha kitini cha ufalme. Sasa kiapo
chasemwa na wazee wenyewe huku chifu mteule amekaa kimya pale kitini. Baada ya hapo,
wazee wanamwondoa huyo chifu na kumpeleka nyumbani kwake. Shughuli huambatana na sherehe.
kubwa ambapo pombe nyingi hupikwa na vyakula vingi vyaandaliwa. Ng'ombe hao walichinjwa kwa
wingi.
Mambo ya uhalifu yalishughulikiwa zaidi na majumbe na wahalifu walikamatwa na kupelekwa
kwa chifu. Adhabu zilitolewa kwa kufuatana na uzito wa makosa. Aliyeua alipewa adhabu ya
kuwapa ndugu wa marehemu ng'ombe. Katika makosa ya kupigana majembe kutoka Ukinga
yalitumika sana katika kulipia adhabu. Mtu aliyeshikwa ugoni, ng'ombe wake wote walikatwa
mishipa ya miguu kama adhabu. Wakati mwingine vita ilizuka kati ya kijiji na kijiji kwa sababu ya
kuzuia watu wenye mkealiyeshikwa ugoni na bwana mwingine asije akafyeka miguu ya ng'ombe
wao.
Kodi ya nchi ililipwa kwa mwene kwa kulima shamba la mwene. Kila kijiji kilikuwa na zamu ya
kwenda kulima shamba la mwene — kila jumbe alileta watu wake kuja kulima shamba la mwene.
FAMILIA NA NDOA YA KISANGU
Kwa kawaida Msangu wa kawaida alikuwa anaoa mke mmoja tu na mtindo wa kuoa mwanamke
zaidi ya mmoja kwa Msangu wa kawaida ni mtindo ulioigwa siku hizi. Wajumbe wa Kisangu katika
vijiji ndiyo walioweza kuoa wake zaidi ya mmoja kwa sababu hawa walikuwa na nafasi ya kuweza
kupata majembe ya kuolea wake. Hii ilikuwa ni tabaka ya kijamii ya Wasangu ambayo ilifuatana na
utajiri wa kuwa na majembe ya kutosha. Wakati wa kuoa mke, ilimbidi ahamie mji au kijiji cha
bwana. Kwa hiyo familia moja ya Kisangu ilikuwa ni ya namna mbili: familia ndogo na familia
kubwa. Familia ndogo yenye kuwa na mume na mke na watoto wao. Familia kubwa ilikuwa na baba,
mama, watoto — pia kulikuwapo familia alikotoka baba na familia walikotoka mama. Mahari
iliyotolewa wakati huo ilikuwa jembe na ushanga, nakadhalika. Hii ndiyo ilikuwa mahari kubwa ya
Wasangu. Ng'ombe hawakutumika kama mahari. Siku hizi mahari ya jembe na shanga havitumiki
tena ball ng'ombe (mitamba) wawili na kambaku mmoja hutumika badala ya jembe na shanga.
Hapo zamani wavulana ambao walikuwa tayari kuoa waliambiwa na wajumbe wa vijiji kwenda
porini ili kila mmoja akatayarishe mwenge na kuupeleka kwa mwene. Yule mvulana aliyefaulu
kuwasha mwenge na kuufikisha kwa mwene huyo alikuwa anajipatia sifa mojawapo ya kuweza
kumpata mke wa kuoa. Lakini yule aliyeshindwa kuufikisha mwenge kwa mwene, basi alibakia
mgane siku zote. Hali kadhalika wasichana kuolewa walikamatwa na jumbe wa kijiji na kupelekwa
kwa Mwene (chifu) ili waweze kugawiwa mume wa kumwoa.
Baada ya wavulana kupeleka mienge kwa chifu kila jumbe wa kijijini aliulizwa na mwene ana
wavulana wangapi kijijini mwake wa makamo ya kuoa na waliofaulu kupeleka mwenge kwa Mwene.
Baada ya kupata majibu toka kwa wajumbe wa vijiji, kila jumbe aligawiwa wasichana ili akawagawie
wavulana walio na sifa zinazotakiwa. Mahari ya jembe na ushanga ilitoka kwa Mwene na kuwapa
wavulana hao waliopata wake wa kuoa — hao walipeleka mahari kwa wazazi wa wasichana. Vile vile
wavulana hao waliopewa mahari walilazimika kwenda kwa Mwene kulima shamba la chifu kwa muda
wa siku kama mbili hivi kila mmoja. Wakati huo pombe ya kunywa na chakula viliandaliwa kwa ajili
ya walimaji hao. Baada ya hapo, wavulana hao waliwapeleka wake zao katika nyumba ambamo
walikuwa wanalala mitamba mpaka wavulana watakapojenga nyumba zao. Kwa hiyo, binti hao
waliweza kukaa pamoja na wazazi wao kwa muda ili waweze kupevuka zaidi, na wakati huu mvulana
(mme wa msichana) ilimpasa apate mahitaji yake ya chakula toka kwa wazazi wa msichana (mkewe)
na vile vile ilimbidi huyo mvulana awasaidie wakweze katika shughuli za kilimo.
23
Wakati wa arusi watu walicheza zeze (Gombo) ill kufurahia arusi hizo na nyimbo nyingi
ziliimbwa kwa mfano wimbo huu hapa ulitumika sana katika kuimbwa wakati wa arusi: —
Towene mandu lyamlamba lya menda lyahanjika lyagwaa, shoo — shoo.
Maana yake:Tumecheza mno, mpaka jua limetua na kupumzika
(Huu ni wimbo wa kumsifu mtwa wao).
Talaka hazikuwapo wakati huo katika jamii ya Wasangu kwa sababu chifu alikataza kitendo hiki
kisitokee. Lakini siku hizi mambo ya talaka katika jamii ya Wasangu imekuwa ni jambo la kawaida.
Mila ya kudumisha ndoa ya zamani imepotea kabisa. Iwapo mama fulani alipatikana na jambo la
kufiwa na watoto basi huyo mama aliruhusiwa na chifu Hi aende akaolewe mahali pengine na bwana
mwingine. Ilionekana kuwa bwana aliyemwoa huyo mama alikuwa na mkosi wa kuwapoteza watoto
wake. Kwa hiyo mama huyo aliruhusiwa kujaribu bahati yake mahali pengine kwa bwana mwingine.
Bwana mwenye bibi huyo aliyetaka kumwacha bwana yake alikwenda kwa chifu wake kulia hali ill
aweze kupatiwa mke mwingine.
Iwapo bwana ya mke alifariki dunia, basi ndugu wa kwanza wa marehemu aliweza kumrithi mke
wa ndugu marehemu na mwanamke alikuwa hana uchaguzi.
IMANI NA DINI
Dini ya asili ya Wasangu hufanyika mahali watemi wanapozikwa. Kwanza kabla ya kuanza
shughuli za sala ulezi huchangwa na raia halafu ng'ombe wa kuchinjwa wakati wa shughuli hizo
hutolewa kwa kufuata zamu. Kuna vikundi hivi hapa chini vinavyoshughulika na utoaji wa ng'ombe
wa kuchinjwa wakati wa kuomba sala; vikundi hivyo vyaitwa FIPUGA. Navyo viko vinane:1.
2.
3.
4.
Kikundi cha Wanyangamana
Kikundi cha Wanyakulwa
Kikundi cha Wasagarua
Kikundi cha Wanamwani
5. Kikundi cha Wanyakongwe
6. Kikundi cha Wanyawami
7. Kikundi cha Wayegenza
8. Kikundi cha Wanyibanga.
Kasisi Mkuu ni mzee Mfumbulwa. Baada ya kazi ya sala pombe hunywewa na nyama
wanagawana. Hapo zamani mavazi maalum yalitumiwa wakati wa kazi hii. Kasisi alivaa joho jeusi na
ushanga na hujipaka chokaa iitwayo NKENJI. Viatu na vitambaa vilivyovaliwa kichwani hutolewa
halafu ndipo sala zasemwa. Nyimbo fulani zaimbwa na akina mama. Baada ya hapo watu hupata kile
kitu wanachokiomba.
UCHAWI UHABI
Kwa kawaida ramli hupigwa kumtambua mchawi. Baada ya kumtambua mchawi, basi huyo
mchawi alikabiliwa na adhabu ya kifo na mtu maalum aliwekwa kwa ajili ya kutoa adhabu. Mtu
alipokufa alifungwa ndani ya ngozi au kirago na kutupwa porini. Hii ndiyo iliyokuwa njia yao ya
kuzika maiti. Desturi ya kuzika maiti katika makaburi imeanza wakati Wajerumani walipoingia nchi
ya Usangu.
NYUMBA ZA WASANGU
Nyumba za Wasangu ni za aina ya tembe, nazo zajengwa kwa kutumia miti ya "mipecheme"
na huezekwa kwa majani yaitwayo "lipepete" au "likuhi". Kamba za kufungia miti ya kujengea
nyumba za fito ni za mahango na mayota. Mwamba wa nyumba ni "mganga", sakafuni husiliba
udongo uliochanganywa na mavi ya ng'ombe. Ukutani udongo huu huu hutumika kwa kusilibwa.
Mlango wake huwa ni wa matete yaliyosukwa pamoja kwa kutumia kamba. Kwa kawaida mlango
huwa ni mmoja na chumba huwa ni kimoja. Siku hizi Wasangu wengine wamebadili mtindo wa
kujenga nyumba zao kwa kufuatana na nyakati za kisasa na pia kufuatana na utamaduni mpya wa
jamii mbalimbali zilizoingia katika bonde la Usangu.
24
MAVAZI YAO YA JADI
Vazi liitwalo MAJIHU, ainaya usinga, lilivaliwa na Wasangu kuficha sehemu zasiri nachifu wao
ndiye aliweza kununua usinga huu na raia zake wakapewa bure. Chifu alivaanguo na kichwani
alivaa vazi lililoitwa NJORA Akina mama walivaa ngozi za mbuzi.
MICHEZO YA WASANGU
Ngomaza Wasangu zilizo maarufu sana ni:(i) Malenjelana, (ii) Ligombo
MALENJELA ni ngoma ambayo ngoma tano ndogo zapigwa pamoja na kubwa moja, jumla ni
ngoma sita. Ngoma ndogo zapigwa kwa kutumia kijiti kimoja na ngoma kubwa yapigwa kwa kutumia
vijiti viwili. Katika kucheza wanawake hujipanga upande na wanaume hujipanga upande mwingine
halafu ndipo huanza kucheza kwa kutamba.
MIIKO YA NGOMA
Wakati wa kutengeneza ngoma mtu haruhusiwi kupitia mahali hapo ama sivyo atanyang'anywa
nguo zake. Wapiga ngoma hawana ruhusa kutoroka wakati ngoma zinapigwa ama sivyo nguo zao
zitanyang'anywa. Wakati unaofaa kucheza ngoma hizi ni ule baada ya kuvuna mtama halafu ndipo
habari zipelekwe kwa mtemi. Baada ya kufikisha habari kwa mteni na kupata kibali chake ndipo
mpango hutayarishwa ili ngoma ichezwe.
MAPENDEKEZO
Lingalikuwa jambo zuri kama wafugaji wote wanaoishi Usangu wangehimizwa na serikali ili
waunde chama cha Ushirika cha mifugo yao ili kuendeleza shughuli ya ufugaji wa ng'ombe iwe nzuri
na yenye kuwaletea manufaa zaidi kuliko ilivyo sasa. Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.
Wanyama wote ambao kwa sasa hivi wananunuliwa na kuuzwa na mtu mmoja wangaliuzwa kwa
chama na chama kingalikuwa na jukumu la kutafuta masoko ya kuuzia hao, wanyama nje ya Mkoa wa
Mbeya. Chama hiki kingalisaidia sana katika kutoa mashauri mema kwa wanachama wake jinsi ya
kuwatunza wanyama walio bora zaidi. Pia madawa mbalimbali ya kutibia maradhi mbalimbali ya
mifugo yangaliweza kutolewa na chama chao huku wakishirikiana na Idara ya Mifugo katika Mkoa.
Vile vile Idara ya Mifugo ifanye kampeni ya kuwaelimisha wafugaji umuhimu wa kutumia madawa
mbalimbali ya maradhi ya ng'ombe. Kwa sasa hivi wafugaji wengi wanakataa kuzinunua dawa
zinazoletwa na Idara ya Mifugo kwa kuogopa bei za madawa hayo. Kwa jinsi hii maradhi mengi ya
ng'ombe yanabakia pale pale ingawa kuna wafugaji wachache sasa ambao huzinunua dawa hizo na
kuzitumia katika kutibu maradhi ya ng'ombe. Lakini wafugaji wachache hawa hupoteza nguvu zao
bure kwa sababu jirani zao wengine wanakataa kuzinunua hizo dawa.
Pendekezo jingine ni kwamba ingalikuwa jambo zuri iwapo Serikali ingefanya kampeni ya
kutosha kwa wafugaji, ili waweze kuwatumia wanyama wao vizuri. Mpaka sasa wafugaji wote hawa
hawatumii ng'ombe wao kama inavyopasa — yaani, ng'ombe wanafugwa kwa ajili ya ufahari tu na
pengine kuuzwa wachache mara shida zinapowatopea. Ingalifaa hawa ng'ombe wafanywe njia
mojawapo kuu ya kuchuma mali. Kama wafugaji wakifanya hivyo, basi ng'ombe hawa watakuwa wa
manufaa sana kwa wananchi hao.
25
Maziwa ya ng'ombe hao hayatumiwi Kama ipasavyo. Lingekuwa jambo zuri iwapo maziwa
yangalikamuliwa ya kutosha ili yauzwe kwa watu wengine kama njia moja wapo ya kujipatia fedha
kwa wafugaji, na pengine hata kiwanda cha kutengenezea Siagi, Jibini, na Samli kingejengwa katika
bonde hili. Kuna uwezekano wa kupata maziwa mengi sana iwapo ng'ombe watafugwa vizuri zaidi
kuliko ilivyo sasa. Vile vile idadi ya hao ng'ombe ingepunguzwa kwa kuwauza ng'ombe wengine
mnadani, na katika kufanya hivyo hao wafugaji wangaliweza kujipatia fedha ambayo ingalitumika
katika kununulia vifaa vingine vya kusaidia katika kuzalisha mali kwa njia nyingine. Kwa mfano,
matrekta na majembe ya kukokotwa na ng'ombe yangalipatikana, na wafugaji hawa wangeweza pia
kulima mashamba ya vyakula na mimea mingine kuliko ilivyo sasa. Kwa sasa hivi wafugaji wengi
hawapendi kulima, au kama wanapenda, hawalimi sana wakati ambapo ardhi yao ni nzuri sana kwa
kilimo cha mimea mbalimbali. Kwa mfano, Wasangu wameacha utamaduni wao wa kulima na
wakaiga utamaduni wa kufuga ng'ombe na kulima kidogo sana. Nchi ya Wasangu ni nzuri sana kwa
kilimo na ingalifaa sana kama wangalijishughulisha na mambo yote mawili — kilimo na ufugaji
kuliko kujishughulisha sana na mifugo kama wafanyavyo kwa sasa hivi: hufuga zaidi na kulima
kidogo.
Uhamiaji wa wafugaji kuingia katika bonde hili wafaa uthibitishwe sana na Idara ya mifugo ili
waweze kujua idadi ya mifugo inayoingia katika bonde hili na kuweza kujua ni maradhi ya namna
gani yanayoweza kuletwa na mifugo kutoka Mikoa mingine. Lakini iwapo mtindo uliopo sasa wa
kuihamishia mifugo sehemu za Usangu kutoka nje ya Mkoa wa Mbeya bila ya wataalam kujua
utaendelea, itawawia vigumu sana kwa watumishi wa Idara ya Mifugo kuweza kutoa huduma zilizo
bora kwa wafugaji. Mpaka wakati wa kuandika habari hizi mwezi wa Februari 1975, Idara ya Mifugo
ya Mkoa wa Mbeya ilikuwa haijui idadi ya mifugo iliyomo katika bonde la Usangu kwa sababu
imekuwa ni vigumu sana kujua ni lini wafugaji wengine watahamia katika bonde hilo.
Wakati wa kiangazi, maji ya mito inayotiririkia katika bonde la Usangu hupungua sana kima
chake. Kwa hiyo huwa ni vigumu kwa watu wote waishio katika bonde hili kupata sehemu yao ya
maji kwa ajili ya shughuli za uzalishaji mali. Utaratibu uliopo sasa wa kugawanya maji si mzuri kwa
sababu ni watu wachache sana ambao hupata maji kwa ajili ya shughuli ya kilimo na mifugo ambapo
wako upande wa chini wa bonde hili wanapata shida kubwa katika kuyatafuta maji kwa ajili ya
mifugo yao na hali kadhalika kwa ajili ya matumizi yao wenyewe. Pia wakulima ambao mashamba
yao yako upande wa chini ambako wafugaji wako hukosa kabisa maji kwa ajili ya shughuli ya kilimo
chao. Kwa jinsi hii, utaratibu mzuri wa kugawanya maji kwa ajili ya wakulima na wafugaji wote
unafaa uanzishwe upesi na utaratibu uliopo sasa uachwe kwa sababu unawanufaisha watu
wachache sana. Katika kufanya hivyo. wakulima na wafugaji wangeshauriwa ili wakae pamoja na
kuamua jinsi ya kuanzisha sehemu za kilimo na sehemu za kufugia mifugo. Baada ya kufanya hivyo
mifereji ingalichimbwa ambayo itayapeleka maji toka mitoni hadi sehemu hizi za uzalishaji mali na
vile vile habari kamili ziwekwe kuhusu kiasi cha maji yanayotakiwa kwa shughuli hizi — shughuli hii
wataalam wa kilimo na mifugo wangeweza kuandika kila habari katika vitabu ambavyo baadaye
vitasaidia sana kuwa vitabu vya kumbukumbu kwa mtu yeyote yule anayetaka kujua jinsi maji
yanavyotumika kwa kilimo na ufugaji, na iwapo mtu anataka kuanzisha mradi mpya wa uchumi
katika bonde hili. Vile vile utaalam wa kutengeneza mifereji ya maji iliyo bora uweze kutolewa na
wataalam wanaohusika lakini kazi ya kuchimba mifereji iwe ndiyo kazi ya kujitolea kwa wakulima na
wafugaji wenyewe. Kama utaratibu mzuri wa kugawanya maji ukianzishwa matatizo mengi ambayo
yangeweza kutokea au yanayotokea sasa hivi yataepukika.
Zaidi ya hayo, mbolea ya ng'ombe ingalifaa itumiwe ingawa udongo una rutuba sana, mkulima
aweza kulima shamba lake kwa muda wa miaka minne mfululizo, lakini mazao hayawezi kuwa ni yale
yale. Mara nyingi hupungua sana kwa hiyo kama jamaa hawa wakijif unza namna ya kutumia mbolea
ya ng'ombe, basi itakuwa ni rahisi sana kwao kulima shamba mfululizo bila ya kupata mazao hafifu
katika miaka mingine.
Vile vile kampeni ingalifaa sana kuwaelimisha wafugaji wa mifugo ili waweze kutumia madawa
yanayotolewa na idara ya mifugo na kuweza kutibu na kuzuia magonjwa mbalimbali ya mifugo.
26
Mpaka sasa wafugaji wengi wanaogopa kununua dawa hizo eti zauzwa aghali. Siku hizi ni siku za
kupanda kwa bei za vitu mbalimbali hapa duniani, bei zenyewe zapanda kila mwezi. Kwa hiyo bei ya
madawa lazima ipande kwa sababu inatengenezwa na watu ambao hulipwa mishahara. Kwa hiyo si
dawa za ng'ombe tu zinazouzwa aghali ball kila kitu hapa duniani chauzwa aghali.
Zaidi ya hayo, wananchi wa Usangu ambao wanashindwa kutunza fedha zao katika benki na
kuzipeleka kwa tajiri Hi amtunzie, wanayo shida kubwa. Kwa sababu fedha zinazowekwa kwa
Mbaluchi zaleta matatizo mengi ya Uchumi wa mtu. Mtu anayehusika anaweza kuvutiwa na vitu
vilivyomo katika duka la huyo mfanya biashara na kuanza kuvichukuwa vitu hivyo kidogo kidogo
mpaka fedha zake zote zimekwisha. Kwa jinsi hii mtu anayehusika hubakia maskini siku zote. Pia
tatizo jingine linalomkabili huyo mtu anayeweka fedha kwa Mbaluchi ni kwamba bei za vituanavyovichukuwa zapangwa na Mbaluchi mwenyewe bila ya mwenye fedha kushirikishwa. Kwa hiyo.
kuna uwezekano wa ujanja kwa upande wa yule mwenye duka kuweza kuutumia ili zile fedha ziishe
upesi. Pia kuna uwezekano wa kuibiwa huyo Mbaluchi siku yoyote au kuunguliwa duka na moto.
Kwa jinsi hii hasara ni kwa yule mwenye kuziweka fedha kwa huyo Mbaluchi. Kwa hiyo kuna haja
kubwa sana kwa viongozi wa TANU wa pande za Usangu kuwaelimisha wananchi faida ya kuzitunza
fedha zao katika benki kuliko kuzipeleka kwa Mbaluchi ambako zaweza kumletea matatizo mengi ya
kiuchumi. Vile vile watu wanaofanya magendo ya mazao na kuyauza nje ya chama cha Ushirika cha
Chimala na Rujewa yafaa wapigwe vita kwa kutumia maarifa na ujuzi mwingi. Kwenda pupa katika
kukipiga vita kitendo hiki kunaweza kusifanikiwe na nguvu zikapotea bure. Vile vile chama cha
Ushirika pamoja na wazee wa TANU wa pande hizo wapewe semina au njia yoyote ile inayofaa
ili wapewe elimu juu ya manufaaya chama cha Ushirika na hasara za kufanya magendo nchini.
Jam bo hili litawasaidia wananchi wenyewe, chama chao cha Ushirika na nchi nzima kwa jumla.
27
Wazee waliojitolea kutoa habari nyingi sana na misaada mbalimbali kuhusu utafiti wetu ni
hawa:1. Mzee L. Mwandangala — Utengule — Usangu
2. Mzee F. Malisa — Utengule — Usangu
3. Mzee J. Mfumbulwa — Utengule — Usangu
4. Mzee W. Mfumbulwa — Utengule — Usangu
5. Mzee G. Makela — Utengule — Usangu
6. Mzee S. Mbeda — Utengule — Usangu
7. Mzee Yotichuma — Ruiwa — Usangu
8. Mzee Fundi Nasoro — Malanda — Rujewa — Usangu
9. Mzee Mwankili — Rujewa — Zahanati — Usangu
10. Mzee W.K. Simtengo — Bwana Afya — Rujewa
11. Katibu Tarafa — Rujewa — Usangu
12. Bwana Gulam — Mbaluchi — Rujewa
13. Afisa utamaduni — Mkoa wa Mbeya
14. Afisa Kilimo — Wilayani Mbeya
15. Afisa Mifugo—Wilayani Mbeya
I
28
JAMII YA WASAFWA
UTANGULIZI
Makala haya kuhusu jamii ya Wasafwa inayokaa katika Wilaya ya Mbeya ni mojawapo ya
mfululizo wa makala mbalimbali yanayokusanywa na Idara ya Utafiti ya Wizara ya Utamaduni wa
Taifa na Vijana kuhusu jamii mbalimbali za Watanzania.
Makala haya, ambayo ni matokeo ya utafiti uliofanywa na Ndugu J.S. Mwakipesile, yaonyesha
kuwa kuna jamii fulani iitwayo WALUGURU inayopakana na WAWANJI. Jamii hii vile vile
imeonyeshwa katika jarida la Utamaduni la Mkoa wa Mbeya Uk. 28 - 29. Mali kadhalika, Bwana S.R.
Charsley katika kitabu chake, THE PRINCES OF NYAKYUSA, amewaonyesha Waluguru hawa katika
picha inayoelekea ukurasa 48 kama WABUNDUGULU. Kusema kweli, kuna jamii ndogo sana
sehemu za Mporoto na sehemu za mlima Rungwe ambayo inajiita Waluguru tofauti kabisa na
jamii ya WALUGURU wanaoishi katika Wilaya ya Morogoro. Tunaposoma habari za Waluguru wa
Wilaya ya Njombe na Rungwe, tusiwe na mawazo ya Waluguru wa Morogoro. Utafiti zaidi
utafanywa kuhusu jamii hii na historia yake.
Zaidi ya hayo, kuna mam bo mengine katika makala haya hayakukamilika kwa sababu ya ukosefu
wa ukweli safi kwa sababu mambo yamekuwapo au yametokea kila mara na kwamba imekuwa
vigumu sana kujishughulisha ili kutaka kujua maana yake kwa nini mambo yamekuwa hivyo.
Watu waliotoa msaada mkubwa wa kutoa habari hizi, kuhusu jamii ya Wasafwa — mila na
desturi zao, ambao wanapewa shukurani nyingi sana ni kama ifuatavyo hapa chini: —
1.
Andrea Mwanjonga
— Mwalimu washule ya watu wa Inshinshi,
Mbeya.
2.
MzeeY. Mpayo
3.
A. Lyoba
— Afisa utamaduni, Mbeya.
4.
J.Kimamula
— Majengo, Mbeya.
5.
Ndugu Sleet
— Kanisa katoliki, Mbeya.
6.
Ndugu M. Lehner
— Mbalizi Mission.
— Uyole, Iganjo, Mbeya.
29
Sura ya Pili JAMII
YA WASAFWA
HALI YA NCHI
Wilaya ya Mbeya ni Wilaya yenye milima na vilima vingi sana vinavyozungukwa na mabonde
pande zote. Nchi hii ni ya rutuba nyingi sana na udongo wake umetokana na milipuko ya volkano kitu ambacho kinatoa rutuba nyingi sana. Juu ya milima hii kuna baridi nyingi sana na mvua
zinapoanza kunyesha, kupanda milima kwa kutumia magari huwa ni taabu kubwa kwa sababu magari
huteleza. Kwa jinsi hii huwa ni hatari kwa msafiri kwenda huko nyakati za mvua kwa kutumia gari bali
huwa ni salama kwenda katika sehemu hizo kwa njia ya miguu ingawa kuna shida ya kuweza
kuchoka katika kupanda milima yenyewe.
Mji wa Mbeya umekaa katika kitako (Saddle) cha milima ya Mbeya na unaelekea upande wa
Kusini. Mtu anapotaka kuufikia mji wa Mbeya kutoka nje ya sehemu ya Mbeya, yampasa kwanza
apande milima; baada ya kupanda hiyo milima ndipo aweze kuteremka milima hiyo na kuufikia mji
wenyewe. Mji wa Mbeya unapendeza sana usiku na mchana kwa sababu unaonekana wazi wazi
wakati wa kuteremka milima yake.
Jina hili Mbeya limetokana na mlima uitwao "Mlima Mbeya" ambao umebonyezwa na kufanya
kitako ulipojengwa mji wa Mbeya. Asili ya jina hili la "Mbeya" ni kwamba mlima huu ulikuwa na
magadi mengi yanayofaa kwa chumvi na pia mlima huu ulikuwa na panya wengi sana zama hizo,
basi wenyeji wanasema mlima huo uliitwa mlima wa Mbewa (Mlima wa Mapanya) na wenyeji
wengine wanasema kuwa mlima huu uliitwa hivyo kwa sababu ya chumvi nyingi iliyopatikana huko
(Mbeye) (Chumvi). Sasa wakoloni walipofika wenyewe sehemu za Mbeya walishindwa kutamka
sawa sawa jina hili "Mbeye" au "Mbewa" na wakatamka "Mbeya" kama walivyoshindwa kutamka
"Nzovwe" badala yake wakatamka "Nsofe", "Nzombe" wakatamka "Njombe" "Ntwara" wakatamka
"Mtwara", "Riringa" wakatamka "Iringa" (Ngome) Sumbuwanga (tupa uchawi) wakatamka Sumbawanga, nakadhalika.
Wilaya ya Mbeya kwa upande wa Mashariki inapakana na wilaya ya Njombe, Kusini Mashariki
inapakana na wilaya ya Rungwe, Kusini Magharibi inapakana na Wilaya ya Mbozi, Kaskazini'
Magharibi inapakana na Wilaya ya Chunya, na Kaskazini inapakana na Wilaya ya Iringa.
30
Mvua zanyesha kwa wingi katika senemu yote ya Usatwa na zaanza kunyesha mwezi Oktoba na
zinaendelea hadi mwezi wa Mei. Baada ya mwezi wa Mei kipupwe chatokea kikiambatana na baridi
kali sana kwa sababu ya mwiriuko wa nchi yenyewe. Barafu huanguka na kufunika sehemu ya ardhi
kama unga mweupe uliotandazwa, na mimea mingi yaunguzwa sana wakati huu. Milima ya Mporoto
ndiyo inayotia fora kabisa kwa kuwa na baridi kali. Milima hii ina baridi kali karibu wakati wote wa
mwaka. Lakini bonde la Usangu huwa na kipindi kirefu cha ukame na ni joto sana wakati wa kiangazi
kwa sababu sehemu yenyewe ya Usangu iko chini katika Bonde Kuu la Ufa la Afrika Mashariki
linalotoka Ziwa Rudolf. Bonde hili halina rutuba kama ile iliyoko kwenye milima, lakini linaweza
kufaa kabisa iwapo kilimo cha kiangazi kitastawishwa vizuri kwa kutumia utaalamu wa kisasa kwa
kutumia mfano wa mradi wa kilimo cha Mbalari. Katika Bonde hili la Ufa iiitwalo bonde la Usangu
linafaa sana kwa kulima mahindi, mpunga, mtama na kadhalika. Katika sehemu za milimani, mazao
yalimwayo huko ni kahawa, ngano, viazi ulaya au viazi mviringo, njegere, pareto, maharagwe,
mahindi, viazi vitamu, migomba, ulezi, choroko, na kadhalika. Miti mbali mbali ya matunda
inapandwa. Mali kadhalika udongo wa sehemu za milimani unafaa sana kupanda miti mbali mbali
kama vile mikaratusi, miti ya kutengenezea karatasi, miti ya mbao na mingine mingi. Katika sehemu
za Mporoto, kuna mianzi ambayo haikupandwa na mtu, na mianzi hii wenyeji wa huko hutumia kwa
kutengenezea mabomba ya kusafirishia maji toka sehemu yenye kijito au chemchemi. Hutoboa
mianzi hiyo katikati halafu huunganisha pamoja na kutega kwenye chemchemi au kijito halafu maji
husafiri ndani ya mianzi hii mpaka kwenye kila nyumba ya mtu anayetaka maji yafikie nyur.iba yake
ili asipate taabu ya kuyafuata maji huko kuliko na chemchemi au kijito chenyewe. Watu wa sehemu
hizo za Mporoto wameweza kutatua shida ya maji kwa kutumia utaalamu wao huu wa asili.
Mifugo hufugwa lakini si kwa wingi. Ng'ombe, Kondoo, Mbuzi hufugwa na watu wa Mbeya.
Bonde la Usangu linafaa sana kwa ufugaji wa ng'ombe labda shida ya maji ndiyo yaweza kuzuia
ufugaji safi wa ng'ombe kwa sababu ng'ombe wanahitaji maji ya kutosha ili waweze kuwa wanyama
bora wenye manufaa kwa wafugaji. Pia sehemu za milima ya Mporoto zafaa kwa ufugaji wa Kondoo
wa manyoya au wa nyama.
Kilimo cha kiangazi kinaweza kutumiwa wakati wote kwa sababu Mbeya ni nchi yenye bahati ya
kuwa na vijito vingi vinavyotiririka kwenye milima hiyo kila wakati bila kukauka. Wenyeji wengi
hutumia sana vijito hivi kwa kazi mbali mbali zenye manufaa. Kwa mfano, wenyeji hutumia maji
hayo kwa kufyatulia matofali, kufulia nguo, kumwagilia bustani za mboga, na mashamba mengine.
Kwa hiyo mpango huu ungalitiliwa maanani sana katika sehemu zile za Mbeya ambako matumizi ya
maji kwa kumwagilia mashamba hayajaanza bado kama vile sehemu za Utengule, Songwe na
Njerenje.
Kuna barabara madhubuti zinazopitika wakati wote. Barabara moja kuu itokayo Dar es
Salaam kwenda Lusaka, Zambia imetiwa lami, na pia barabara itokayo Mbeya kwenda Kyela imetiwa
lami. Barabara zingine hazijatiwa lami lakini ziko imara na zapitika wakati wote.
HISTORIA
Jamii kubwa kuliko jamii zote katika wilaya ya Mbeya ni Wasafwa. Wasafwa huishi katika
milima ya Mporoto Kaskazini ya mlima Rungwe na katika bonde ambalo laenea kati ya milima ya
Mbeya upande wa Kaskazini na milima ya Umalila na Unyiha kwa upande wa Kusini na Kusini
Magharibi. Mali kadhalika, Wasafwa huishi upande wa Kaskazini wa mlima Mbeya na katika sehemu
ya uwanda wajuu unaopakana na Wilaya ya Chunya.
Wasafwa wanazungukwa na jamii hizi:- Wasangu upande wa Kaskazini, Wanyiha upande wa
Magharibi, Wamalila upande wa Kusini-Magharibi, na Wanyakyusa kwa upande wa Kusini.
Wasafwa hawajapata kuwa chini ya Utawala wa namna moja, bali walikuwa wametawaliwa na
machifu mbali mbali. Machifu wa Kisafwa waliokuwa wanajulikana sana tokea karne ya 19 ni
31
Mwalyego ambaye alijenga nyumba yake kwenye miteremko ya milima ya Mbeya karibu na Utengule,
Chifu Lyoto alitawala sehemu ya mteremko wa mlima Mbeya upande wa Usafwa ya Kaskazini
kuelekea bonde la Usangu, Zambi alitawala sehemu ya upande wa Kaskazini - Mashariki za
miteremko ya milima ya Umalila, Malema alitawala sehemu za Kaskazini - Mashariki za miteremko ya
milima ya Unyiha.
Ingawa ni vigumu sana kujua chimbuko la Wasafwa lakini koo mbali mbali za Wasafwa
zakumbuka wapi zilitoka. Chimbuko la Wasafwa limo katika sehemu tatu. Sehemu ya kwanza ni ile
inayowahusu Wasafwa ambao asili yao ni Ugogo. Ziko sababu nyingi ambazo zilisababisha kwa
Wagogo fulani kwenda kuishi sehemu za Usafwa na kuoana na Wasafwa. Nchi ya Mbeya ilikuwa na
rutuba nyingi kwa kupanda mazao ya chakula, biashara ya utumwa ambayo iliendeshwa zaidi na
Waarabu, na kadhalika. Msafara wa watumwa ulifuata bonde la Usangu kuelekea sehemu za pwani
ambako ndiko yalikuwako masoko ya kuwauzia hao watumwa. Njia hii ya watumwa ilifuatwa wakati
njia ya kupitia Ugogoni ilipoonekana ni ya gharama kubwa sana kwa wafanya biashara hii na wakati
mwingine ilifungwa na jamii za Kigogo kwa sababu mbali mbali za kutoelewana na Waarabu,
Wafanya biashara. Na kama tunavyoelewa machifu wa Kiafrika nao walijitupa barabara katika
biashara hii na kuwauza wenzao. Kwa hiyo, Wagogo waliokwenda sehemu za Mbeya yawezekana
walifuata biashara halafu baadaye wakafanya mastaakimu yao pande hizi za Mbeya na kuweza
kuoana na Wasafwa wa huko na baadaye watoto wao wakafuata malezi ya Kisafwa na kuwa Wasafwa
Kamili. Pengine hao Wagogo walikwenda sehemu hizo za Usafwa kwa sababu ya kukimbia taabu ya
kutiwa utumwani na Waarabu kwa sababu njia kuu ya biashara ya utumwa ilipitia katika nchi yao.
Chimbuko jingine la Wasafwa ni Ukinga. Hasa hili ndilo chimbuko kubwa la Wasafwa ambao
kwa mila na desturi wanafanana nao sana. Wasafwa wanatoa sababu kubwa iliyowafanya waje
sehemu hizi za Mbeya nayo ni sababu ya kupata moto. Kama inavyosimuliwa na wazee wengi wa
Kisafwa, watu wa asili waliokuwa wanakaa pande za Mbeya, walijua jinsi ya kutengeneza moto, na
Wasafwa wengi wakafuata utaalam huo toka pande za Ukinga na baadaye wakafanya maskani yao
huko pengine baada ya kuwafanyia vita wenyeji wa huko halafu wao Wasafwa ndio wakawa watawala
wa nchi yote ya Mbeya. Kwa kawaida Wasafwa wana desturi ya kukoka moto mmoja halafu huo moto
huenea nchi nzima ya Usafwa. Moto huu ulikokwa kwa kufuata sherehe maalum.
Chimbuko la tatu la Wasafwa ni Unyakyusa na pande za Kaskazini za Malawi - Karonga. Kwa
mfano, chifu Mwalyego ambaye baadaye alifanywa na Wajerumani kuwa chifu mkuu wa Wasafwa
katika mwaka wa 1898 yeye husimulia kuwa asili yao ni Karonga na baba mkubwa wa Mwalyego
(great grand father) Bwana Shyungu aliishi Karonga na utawala wake ulienea sehemu yote ya nchi ya
Ukonde. Mtoto wake Mwamwondo alifanya maskani yake Nshorongo sehemu iliyo karibu na milima
ya Igale. Mtu huyu alioa wanawake wengi na pia alioa binti ya Chifu Lyoto ambaye alitawala Usafwa
wakati huo. Baadaye Mwamwondo akaasi na kumpindua mkwewe na yeye akawa ndiyo mtawala wa
sehemu hii ya Usafwa. Mwamwondo alizaa wavulana wengi. Mwamparandje, Mwenipyana na
Nsewe. Mtoto huyu Nsewe alizaliwa na mke wa Mwamwondo ambaye alikuwa binti ya Lyoto.
Mwamwondo alifariki dunia mara baada ya Nsewe kuzaliwa. Mwamparandje akatawala nchi ya
Nshorongo badala ya baba yake. Walakini ndugu yake Mwenipyana alipigana na Mwamparandje na
akamshinda. Kwa hiyo Mwenipyana akatawala sehemu ya Nshorongo na Mwamparandje akakimbilia
katika milima ya Igale.
Wasafwa walimkataa Mwenipyana kwa sababu mama yake hakuwa Msafwa na pia tabia yake
mbaya ilimfanya asikubaliwe kutawaia. Wakati Wangoni walipoingia Mwenipyana aliwasaidia
Wangoni kwa kuwapa chakula ambacho raia wake walikihifadhi. Tabia hii iliwaudhi sana Wasafwa,
kwa hiyo wakamkataa kuwatawala.
Mwamwondo alipofariki mke wake, binti Lyoto alirudi kwa baba yake pamoja na mtoto wake
Nsewe. Nsewe alipokua, babu yake Lyoto alimteua Nsewe kuwa chifu badala ya baba yake Mwamwondo. Baadaye Nsewe akamwasi babu yake na akapigana naye kalazimika kukimbilia
milimani alikofia wakati wa majilio ya Wangoni. Nsewe alizaa watoto wengi:- Mwalyambi, Zambi,
Milambo, Ngaja, Nswila, Mpoli, Mwansonswe, Mwembe, Sidjodjo, Djedjo na Mudjenda. Nsewe
aligawanya sehemu ya Utawala wake na kuwagawia watoto wake hawa.
32
Wasangu chini ya chifu Merere walipoingia katika nchi ya Nsewe, Nsewe alikufa wakati wa
vita na watoto wake wakatoroka. Nswila allkwenda Ukonde, Zambi akakimbilia Unyamwanga na
watoto wengine wakajificha chini ya machifu wengine. Nswila hakukata tamaa na kwa msaada wa
machifu wa Unyamwanga na Unyiha, akawashambulia Wasangu na akawashinda na kuwatoa toka
nchini mwake. Nswila alipotuliza nchi yake, ndugu zake wote wakarudi toka walikokimbilia na
wakamheshimu sana kwa kitendo alichokifanya cha kuwafukuza Wasangu toka Usafwani, lakini
hawakumkubali kama yeye ndiye chifu mkuu wa Usafwani. Badala yake kila mmoja wao alitawala
sehemu aliyopewa na baba yao Nsewe.
KIPINDI CHA MAJILIO YA WAGENI NA VITA 1845 — 1893
Katika mwaka 1845 Wangoni kutoka Ufipa ambako waligawanyika baada ya kufa kiongozi wao,
waliingia katika nchi ya Usafwa na kuishambulia kikatili sana wakiua wanaume na kuwatia utumwani
wanawake na watoto, na huku wakichoma vijiji na kuharibu mimea. Njaa ikatokea na Wasafwa
walilazimika kula mizizi na matunda ya porini. Njaa ilikuwa kali sana hata Wangoni wakalazimika
kuiacha nchi ya Usafwa na kwenda mahaii pengine. Wasafwa ambao walikuwa wamekimbilia milima
ya Igale, Umalila na Mporoto, wakaanza kurudi Usafwani pole pole tena mmoja mmoja. Wakajenga
nyumba, wakalima mashamba na wakawa na amani kwa muda mfupi.
Katika sehemu ya Mashariki ya Usafwa bonde la Ufa lapitia na ndio iliyokuwa njia kuu ya
wafanya biashara ya utumwa na mara nyingi sana Wasangu na Wahehe walipitia katika bonde hili
kuja kuwashambulia Wasafwa. Bonde lenyewe latokea sehemu za Dodoma kuja Iringa - na kuungana
na bonde la Usangu - Laendelea hadi Uyole - Mbalizi - Utengule - hadi Tunduma mpakani mwa
Zambia na Tanzania. Hii ndio iliyokuwa njia yao kubwa na sehemu zingine hazikuwezekana kupitia
kwa sababu ya milima mirefu. Wahehe waliwashambulia Wasangu na walisukumwa mpaka Usafwani
ambako chifu Lyoto alijaribu kuwazuia Wasangu na vita ikapiganwa sana mahaii paitwapo llomba sehemu iliyo karibu sana na mji wa Mbeya. Chifu Lyoto alishindwa na kuuawa. Merere akapeleka
mifugo, wanawake na watu fulani katika uwanda wa Usafwa. Yeye mwenyewe Merere aliendelea
kupigana vita katika milima ya Ukimbu na kumfukuza Chifu Zumba ambaye alikuwa mtawala wa
milima ya Chalangwa, na akapiga kambi yake katika nchi ya Ubungu. Wabungu walipojaribu
kumwua, Merere akaenda Kiwele Kaskazini - Mashariki. Watu wa Merere hawakuipenda hali ya nchi
kwa hiyo Merere akalazimika kurudi Usangu.
Baadaye Mkwawa akaanza tena kutaka kupigana na Merere, lakini safari hii Merere akakimbilia
katika milima ya Mporoto halafu akaingia katika nchi ya Ukukwe ya chifu Mwakalinga ambako
aliwaua Wanyakyusa wengi na kuteka mifugo mingi na kuipeleka Uporoto. Hali ya hewa ya unyevu
unyevu ya milima ya Mporoto haikumpendeza Merere, kwa hiyo akalazimika kwenda katika milima
ya Unyiha katika nchi ya chifu Mwashambwa akipitia milima ya Umalila. Chifu Merere alikaa huko
mpaka alipomshinda chifu Mwashambwa, na baadaye akapigana na chifu Zambi upande wa
Kaskazini Mashariki wa milima ya Umalila. Baadaye akaenda kufanya kambi yake Mpedjere chini ya
mlima Mbeya. Wakati machifu wa Kisafwa waliposhambulia walifikiria kuwa jeshi lake Merere
limedhoofika kwa vita vingi lilivyopigana, lakini chifu Malema ambaye alikuwa mtawala wa Wasafwa
ya Magharibi karibu na milima ya Unyiha aliwahaini watu wake na hakushiriki katika kumshambulia
Merere kama machifu wengine wa Kisafwa walivyoamua kumzunguka. Kwa hiyo Merere akapata
mwanya wa kuweza kuwashinda machifu wa Kisafwa.
Mpedjere, ngome mpya ya Merere, ikaanza kujengwa na kutoka hapo aliweza kuwashambulia
machifu wote wa Kisafwa mpaka wote wakamsujudu. Wakati wavita kule Mpedjere, chifu Mwalyego
alishindwa vita na akakimbilia kwenye utawala wa chifu Zumba Kaskazini ya Mlima Mbeya. Wakati
huu Merere alijijenga sana sana na kuimarisha utawala wake katika nchi ya Wasafwa na akajenga
ngome kubwa sana ya mawe yenye kuta ndefu naakaiita ngome hii mpya "Utengule" ikiwa na maana
"Mahaii pa amani", jina lile lile la mji wake mkuu sehemu za Usangu ulioitwa "Utengule", Kwa jinsi
hii Merere aliuimarisha utawala wake. Katika nchi ya Usafwa na machifu wote wa Kisafwa wakaacha
uchifu wao na kumtambua Merere kama ndiye chifu wa Usafwa ingawa hawakumpenda hata kidogo.
33
Chifu Zambi peke yake, akiwa mtawala wa sehemu ya milima, ya Umalila, alikataa kumtambua
Merere kuwa kama chifu wa Usafwa na akakataa kufanya kazi chini yake. Chifu Zambi alikuwa na
chuki nyingi na kwa ajili ya ujasiri wake akamwomba chifu Mkwawa wa Wahehe ili amsaidie katika
kumshambulia Merere, na kwa bahati chifu Mkwawa akakubali ombi lake. Wahehe, machifu wa
Kisafwa Mwalyego, Zumba, Mbuvi, wakaunganisha majeshi yao nawakauzunguka mji wa Utengule.
Walijaribu kuzuia njia za kupatia chakula cha Wasangu waliokuwa wanaishi katika ngome ya
Utengule na mpango huu uliwachukua miezi minne, na baadaye wakaushambulia mji wa Utengule
lakini jeshi la Merere liliyarudisha nyuma majeshi yote ya Mkwawa. Pengine safari hii majeshi ya
Mkwawa yangeweza kuwashinda majeshi ya Merere kama chifu Malema asingaliwapa chakula
Wasangu wakati majeshi ya Mkwawa na Wasafwa yalipowazunguka. Mwishowe Mkwawa akaamua
kuiacha vita hii na kurudi katika nchi yake. Baada tu Mkwawa kurudi kwake, Merere akaamua kulipiza
kisasi kwa kuwaua Wasafwa wengi sana walioshiriki katika kumshambulia. Wale machifu wa
Kisafwa ambao walishiriki katika kumshambulia Mwalyego, Mbuvi, Zumba, Mpyila na Zambi, kila
mmoja alilazimika kumpa Merere binti yake mmoja ikiwa kama adhabu yao. Malema vile vile alitoa
mabinti wake wawili na kumpa chifu Merere. Pia kila chifu ilimbidi atoe mazao yake ya mwaka na
kumpa Merere. Lakini Merere alikuwa hataki amani, shida yake ilikuwa vita na akaviharibu sana vijiji
vingi sana na kuwauza watu wengi utumwani. Mali hii ya wasi wasi iliendelea mpaka walipofika
Wajerumani.
KUJA KWA WAMISIONARI 1892
Wamisionari wa kwanza walifika katika nchi ya Usafwa mwaka 1892 Januari, wakiwa Merensky
na Nauhaus, ambao walikuwa wa madhehebu ya Misheni ya Berlin. Wamisionari wa Moravian
walikuja baadaye. Mkurugenzi wa Misheni ya Moravian alimwomba Bwana Kootz na mkewe Kretschmer kuja kwenye koloni za Kijerumani za Afrika ya Mashariki mwaka 1894, kuja kufanya kazi
kama Wamisionari kwenye pwani ya Kaskazini ya Ziwa Nyasa. Miaka mitatu ya nyuma kazi ya
Misheni ilikuwa imeanza katika nchi ya Unyakyusa - mahali paitwapo Ipyana. Walianza kazi yao
katika mwaka wa 1894 mwezi wa Julai.
Baada ya kufanya kazi nusu mwaka na Bwana Th.Richard ambaye alikuwa amewasili huko
mwaka wa 1891, waliombwa kwenda kufanya kazi ya kimisheni katika nchi ya Usangu. Wakati huo
chifu Merere alikuwa amefanya urafiki na Wajerumani. Richard alifuatana na Bwana Kootz na
Kretschmer katika safari hii na Misheni ikafunguliwa Utengule makao makuu ya chifu Merere na
mahali ambapo Wasangu walikuwa wanaishi baadaya wao kufukuzwa Usangu na Wahehe. Utengule
ikawa ndio makao makuu ya Misheni ya Moravian katika Usafwa na Usangu.
SERIKALI YA KIJERUMANI
Serikali ya kikoloni ya Kijerumani ilianza kuleta amani katika nchi ya Usafwa kati ya mwaka wa
1895 na 1900. Serikali hiyo ilikomesha vita vya machifu na biashara ya utumwa, na baada ya
kuwashinda Wahehe, serikali hiyo iliwafukuza Wahehe wote kutoka nchi ya Usangu, na pia Wasangu
waliokuwa wanatawala nchi ya Usafwa waliambiwa warudi kwao Usangu, na chifu Mwaiyego
akapewa utawala wake juu ya Wasafwa. Walakini Wasafwa hawakupata kuwa chini ya utawala wa
chifu mmoja, kwa hiyo chifu Mwalyego alipotawazwa na Wajerumani kama chifu mkuu wa Wasafwa,
machifu wengine wa Usafwa walikataa kumtambua.
Basi kwa kufuatana na masimulizi hayo hapo juu utaonaya kuwa jamii ya Kisafwa inachimbuko
lake sehemu tatu, ya kwanza ni kwamba ukoo mmoja wa Kisafwa ulitoka Ugogo, ya pili ni kwamba
ukoo mwingine wa Kisafwa ulitoka Ukinga, na ya tatu ni kwamba ukoo ule ule ulitoka Unyakyusa
sababu nyingi za kihistoria na za Kiutamaduni zimeelezwa kuhusu kufika kwa Wasafwa katika nchi
ya Mbeya na kukaa huko. Lakini sababu zingine zinazohusu jiografia hazikuelezwa kikamilifu - hasa
kuhusu ukoo uliotoka Ukinga. Sababu moja kubwa ya kijiografia ambayo ilisababisha kuondoka kwa
34
Wasafwa kutoka sehemu za Ukinga ni kwamba nchi ya Ukinga imeinuka sana na mwinuko huu
huwagawanya watu kuwa katika pande mbili zilizo tofauti ya hali ya Kijiografia, hata baadaye watu
ambao pengine asili yao ni moja kuwa katika jamii mbili zilizo tofauti kabisa, ambazo lugha zao
zatofautiana. Mambo yanapotokea hivi, basi kutoelewana kwaweza kutokea na kuchukiana pia
kukatokea. Ngazi hii ikifikiwa basi kundi lisilotaka ugomvi huhamia mahali pengine ambapo kuna
usalama zaidi na hali hii yawezekana kabisa iliwapata Wasafwa na kuamua kuhamia sehemu za
Mbeya ambako maskani yao ya kudumu yalifanyika.
Jamii ya Wasafwa yagawanyika katika jamii hizi kubwa:(i)
Wasongwe ambao huishi sehemu za mto Songwe; (ii)
Wamalila ambao wanaishi katika milima ya Umalila. (iii)
Wamporoto ambao huishi kwenye milima ya Mporoto. (iv)
Wambwila ambao huishi kati ya Wasongwe na Wasangu. (v)
Waguluhaambao huishi sehemu za lleya.
KILIMO
Wasafwa walitumia majembe yao ya kwanza ambayo yalikuwa ya miti, yaani miti ilichongwa
vizuri kabisa mithili ya jembe halafu wakayatumia kwa kulimia. Katika kuchonga majembe ya miti,
tezo na mashoka yalitumiwa, zana ambazo zilikuwa za chuma kilichotengenezwa toka Ukinga. Pia
zana hizi hizi, mashoka na tezo, zilitumika katika kuchongea mizinga ya nyuki. Miti iitwayo
'Magambo' na miyombo ilifaa sana kutengenezea majembe. Mizinga ya nyuki ilichongwa kutokana
na mti wowote ule. Baadaye sana, majembe ya miti yakaonekana hayafai ndipo majembe ya chuma
kutoka Ukinga yakatumiwa zaidi na kuonekana bora zaidi.
Katika shughuli za kulima, kwanza walianza kulima mashamba ya chifu wao, yaani "Kwila",
maana yake "Shamba la Chifu". Baada ya hapo kila raia alikwenda kulima shamba lake. Walakini
kualikana katika shughuli za kilimo lilikuwa jambo la kawaida ili mashamba yamalizike upesi. Mtu
alipotaka kualika wenziwe wamsaidie kulima mashamba yake, alipika pombe na chakula cha kutosha
ili baada ya kulima watu waweze kula na kunywa pombe. Wale walioalikwa siku hiyo waliimba
nyimbo wakati wa kula chakula na pia ngoma zilichezwa ili kuonyesha furaha kubwa ya chakula
walichopewa. Iwapo jamaa mmoja alitokea kutokuwa na chochote, yaani hana pombe wala chakula
cha kuwapa watu watakaolima shamba lake, aliweza pia kuwaalika wenziwe hapo kijijini ili wamsaidie kulima na kumaliza shamba lake. Wanakijiji waliweza kulima shamba la mwenzao bure. Baada
ya mavuno kupatikana basi huyo jamaa aliyelimiwa shamba lake bure aliweza sasa kupika pombe na
chakula na kuwakaribisha wale wale jamaa waliomlimia shamba lake hapo awali ili kuonyesha
shukrani zake kwa msaada aliopewa alipokuwa yeye hana kitu cha kuwapa. Ilikuwa ni desturi kwa
kila mwanakijiji kukubali kualikwa na mwanakijiji yeyote, na kukataa kumsaidia mwanakijiji katika
kulima ilikuwa ni mwiko. kitendo hiki cha kulimiwa shamba bure mtu anapokuwa hana pombe wala
chakula kiliitwa "Alimishumiwa", maana yake wanalima bure bila kuwapa chochote cha kula
wanaolima shamba la mtu siku hiyo. Siku hizi Wasafwa wanaalikana katika shughuli za kilimo lakini
si sana kama ilivyokuwa hapo zamani.
Katika nchi ya Usafwa shughuli za kilimo zaendelea wakati wowote katika mwaka kwa sababu
hali ya hewa na ya ardhi yaruhusu sana shughuli ya kilimo iweze kuendelea mwaka mzima, ingawa
sehemu zingine za usafwa hazina bahati ya kuwa na hali hii ya hewa na rnanufaa mengine mengine
ya kuendeleza hali ya kilimo. Kuna mazao ya aina nyingi sana ambayo hulimwa nyakati mbali mbali
tofauti na mazao hayo hupandwa kwa kutegemea ardhi na jiografia ya mahali penyewe kwa sababu
jiografia ya nchi ya Usafwa yahitilafiana toka mahali hadi pengine. Kilimo chao maalum ni cha sesa,
lakini pia wanalima matuta, ufundi ambao wameigatoka kwa Wanyakyusa. Watu wa Mporoto hulima
matuta ya terrace ili kuzuia mmomonyoko wa udongo kando kando ya milima. Karibu robo moja ya.
Wakulima wa Kisafwa hutumia trekta au plau lakini matumizi ya zana hizi mbili hutegemea jiografia
ya mahali shamba lilipo.
35
MGAWANYO WA KAZI
Katika jamii ya Kisafwa, baba huwa na shamba lake na mama huwa na shamba lake pia. Iwapo
baba ametangulia kumaliza shamba lake huenda kumsaidia mkewe. Kufanya hivi hakumfanyi bwana
adai sehemu yoyote juu ya umilikaji wa shamba na mali iliyomo katika shamba hilo. Bali husaidia tu
kwa imani, lakini shamba labakia kuwa ni la mwanamke. Kila mtu alikuwa na mamlaka juu ya
shamba lake hata mavuno yake pia. Mavuno kutoka shamba la baba ndilo lilifanya ghala ya chakula
cha familia nzima. Kama mke mmoja hakuvuna kiasi cha kutosha, basi mwanamke huyo aliweza
kupata chakula toka ghala ya bwana yake. Lakini iwapo kila mwanamke ana chakula cha kutosha
toka shambani mwake, basi bwana aliweza kuuza baadhi ya chakula toka kwenye ghala yake, ill
kupata fedha za kununulia ng'ombe au mbuzi. Pia mwanamke alikuwa haingiliwi na bwana wake
katika umilikaji wa chakula. Alikuwa na uhuru kabisa wa kuweza kuuza chakula chake kama
alipenda. Watoto walikitumia chakula toka kwa mama zao katika 'Ibanza' yao bila wasi wasi bila
kujali mama ya nani kapika chakula hicho. Lakini siku hizi ni vigumu kwa akina mama kulisha watoto
wote sawa. Hujali sana watoto wao tu; wamekuwa wachoyo na hawawezi kuwalisha watoto wa
mwingine kama ambavyo wangaliwalisha watoto wao wenyewe. Ubinafsi umewaingia sana kitu
ambacho hakikujulikana hapo zamani.
Kabla ya kwenda kulima au kuvuna, mama hupika chakula asubuhi Hi waje wale mchana baada
ya kazi. Umwagiliaji wa mashamba ulitumika kama Wasafwa wanavyotumia utaalamu huo kwa sasa.
Mama, baba na watoto hulima pamoja.
KUVUNA
Wakati wa kuvuna, ngano hukatwa shina zima na kisu halafu hulundikwa pamoja. Baada ya
kumaliza kuvuna, ngano yote hupigwa pigwa na mti (threshing) ili itoke kwenye masuke yake. Ulezi
hukatwa vichwa vyake na kisu halafu huwekwa pamoja na baadaye huzitengeneza kwa kutenganisha
punje zake toka kwenye masuke. Mahindi huvunwa kwa kukwanyua vigunzi vyake toka kwenye shina
lake na kuwekwa pamoja. Kazi yote hii hufanywa kwa kualikana. Mtu mmoja peke yake alikuwa
hawezi. Nyimbo ziliimbwa wakati wa kazi ya kuvuna na vyombo hivi, "Indili, Izeze, na Marimba"
yalitumika katika kuwatumbuiza wafanyakazi.
GHALA
Chakula kilihifadhiwa katika ghala maalum zilizotengenezwa kwa kazi hiyo. Ulezi na ngano
vilihifadhiwa katika vilindo vikubwa vilivyotengenezwa kwa kusuka matete pamoja kwa kutumia
kamba za miyombo ambayo zama hizo zilipatikana kwa wingi karibu karibu na vijiji vyao. Mpaka
sasa njia hii ya kuhifadhi mazao yatumika Usafwani kote.
Picha hii yaonyesha kilindo cha matete
36
Mahindi yalivunwa na kuanikwa penye uchanja kwanza ili yapate kukauka sawasawa. Baada ya
hapo, mahindi yaliwekwa ndani ya kihenge kilichojengwa nje ya nyumba ya kulala. Hii ndiyo
iliyokuwa ghala ya mahindi. Zamani hakukuwa na wizi na iwapo mtu fulani alionekana kuwa yu
mwizi mtu huyo alizomewa sana na pia wanakijiji walimnyima mwizi huyu haki yake ya kuoa mke
(Social Control). Kwa hiyo watu waliogopa kuiba ili wasije wakaambiwa ni wezi na kukosa
mwanamke wa kuoa. Siku hizi wezi ni wengi mno hata wananchi huwa na wasiwasi sana katika
kujenga ghala zao mbali na majumba yao. Sababu kubwa zinazofanya wizi uongezeke ni kwamba
viongozi wengi wavijijini huogopa kuwafichua wezi na pia huhongwa pombe na wale ambao ni wezi.
Basi jamaa hawa hushindwa kutekeleza wajibu wao sawasawa. Wakati mwingine mwizi aweza
kukamatwa na wanakijiji na kumpeleka mwizi huyo kwa bwana hakimu. Wanapofika huko naye, hao
wanakijiji wanaulizwa maswali kama wanao ukweli kwamba mtu waliyemleta ni mwizi. Basi
wanakijiji wengi hukata tamaa na mara nyingi wanakijiji wengine hujichukulia madaraka mikononi
mwao na kumwadhibu yule mwizi vibaya sana.
KUHAMA KWA WATU (MIGRATION)
Zamani watu walikuwa wachache sana na kuhamahama kwao kulikuwa kuchache. Kuhamahama
kulitokea tu wakati njaa ilipoingia katika nchi fulani au vita kutokea, basi jamaa walihama.
Kuhamahama kwa Wasafwa twaweza kusema kuwa walihama mara yao ya mwisho walipoingia nchi
ya Usafwa miaka mingi iliyokwishapita. Shida zao zilikuwa ni hizo hapo juu zilizo wafanya watu
wahamehame na kwa jumla kuhamahama kulisababishwa na maafa hayo. Siku hizi Wasafwa wengi,
hasa vijana huhamia sehemu zile zilizo na nafasi ya kazi kama vile mji wa Dar es Salaam, sehemu
zenye mikonge mingi - Tanga - Kilosa - Morogoro na kadhalika. Pia Wasafwa wengi walio vijana
wamehamia nchi za Zambia ambako kazi nyingi zapatikana katika migodi na viwanda. Wasafwa
wazee ndio hubakia nyumbani kwa sababu ya jukumu walilo nalo juu ya familia zao, na pia wao
hawapendi zaidi kuhamia nchi za kigeni ambazo zina watu walio na desturi na mila tofauti na za
kwao. Zaidi na zaidi wazee wa Kisafwa hubakia nyumbani wakilima mashamba yao. Kundi lingine
lililo na uhuru wa kuhamia sehemu zilizo na nafasi za kazi ni wale Wasafwa ambao hawajaoa.' Hawa
huhamia sehemu zilizo na kazi bila taabu kwa sababu hawana matatizo ya familia. Lakini kwa jumla
vijana wa Kisafwa wanaotaka kujaribu bahati yao katika maisha yao ndio wengi huhama kila mwaka.
WANYAMA WAFUGWAO
Wasafwa si wafugaji hodari kama jamii zingine za Watanzania zilivyo. Wamasai, Wambulu,
Wagogo, Wahehe, Wanyiha ni wafugaji wakubwa wa ng'ombe. Lakini Wasafwa walifuga wanyama
wachache sana na mpaka sasa wanafuga wanyama wachache sana katika vijiji vyao. Walifuga.mbuzi
na ng'ombe wachache sana kwa ajili ya kutambika au kuwachinja wakati wa kilioni kwa ajili ya
mboga, kwa wale waliopo kilioni. Siku hizi ng'ombe, mbuzi, kondoo, wanafugwa kwa ajili ya maziwa
na nyama. Pia kuku na nguruwe wafugwa kwa sababu ya mayai na nyama.
37
Familia ya Kisafwa inaweza kuwa na baba mmoja, mama mmoja pamoja nawatoto, au inaweza
kuwa na baba mmoja, mama wawili au watatu pamoja na watoto wao. Hapo zamani familia zilikaa
katika vijiji kwa kufuata ukoo. Kwa hiyo kila kijiji kilikuwa na ukoo fulani. Mtu alipoposa msichana
basi alihamia katika kijiji cha msichana na kukaa huko na kuongeza jumla ya familia. Kwa hiyo
familia iliyokuwa na mabinti wengi iliweza kupanuka sana na kufanya kijiji chao wao wenyewe cha
wakwe na baba na mama mkwe na watoto na wajukuu, na kadhalika. Utaratibu huu wa kuishi pamoja
namna hii kwa kufuata undugu bado unafuatwa na watu wengi katika nchi ya Usafwa. Jamii ya
Wasafwa ni jamii inayofuata urithi kwa upande wa baba. Katika kurithi baba akifa ni lazima mtoto wa
kwanza wa kiume arithi mali ya baba yake. Lakini katika kurithi mall ya baba, yampasa mtoto huyo
aonyeshe busara safi, bila hivyo hawezi kurithi mali ya baba yake kwa sababu ya kukosa busara.
Mtoto wa pili aweza kuchaguliwa na ukoo wa baba ili aweze kurithi iwapo alionyesha busara safi,
zaidi kuliko kaka yake mkubwa. Kwa kawaida warithi walitoka kwa mke mkubwa, na iwapo mke
mkubwa alikosa kuzaa watoto wa kiume na akazaa watoto wa kike, basi mtoto wa kiume wa mke wa
pili aliweza kurithi.
Mirathi iligawanywa kwa ndugu zake wote, lakini yeye mrithi alizidishiwa mirathi zaidi kwa
sababu yeye ndiye aliyebadili nafasi ya baba yake na alipaswa kuwatunza ndugu zake sawa sawa
kama baba yao alivyokuwa akiwatunza alipokuwa bado yu hai. Siku ya kurithi, pombe nyingi
ilipikwa na kutengenezwa na chakula kwa wingi kilipikwa ill watu wale na kunywa na kufurahi sana.
Watu walicheza na kuimba nyimbo za furaha. Utaratibu huu wa kurithi mali ya baba bado
unafuatwa na Wasafwa wengi ingawa yapo mabadiliko mengi.
NDOA
Kwa kawaida mvulana aliweza kusikilizana na msichana anayetaka kumchumbia. Baada ya
hapo, mvulana alikwenda kwa baba yake na kumwambia ya kwamba anamtaka binti ya fulani amchumbie. Basi babake aliweza kumwambia mzee mwenzie pale kijijini kuwa aende akamwambie
baba ya binti kuwa wanamtaka kumchumbia binti yake. Iwapo mzee wa binti huyo anakubali ombi la
wazee wenzie, basi posa inapelekwa.
Njia ya pili ya kumposa msichana ni kwamba mvulana na msichana wanakubaliana waoane.
Baada ya kufanya hivyo, wanaamua wote wawili kutoroshana bila ya wazee kujua, isipokuwa wazee
wanaambiwa baada ya kutoroshana hao vijana. Kwa kawaida msichana hutoroshwa na mvulana
ambaye atakuwa mumewe wa maisha. Mvulana humpeleka msichana huyo aliyetoroshwa kwa baba
yake mvulana. Mzee wa mvulana akishaona mambo yamefikia kiwango hicho, huondoka haraka
kwenda kwa mzee pale kijijini na kumwomba aende mara moja kwa baba ya msichana aliyetoroshwa
na kumwambia ya kuwa wanataka kumuoa binti yake na kwamba kwa sasa binti huyo wamemchukuwa tayari yuko nyumbani kwao hao jamaa. Basi baba ya binti hukubali na kuwaambia ya
kuwa wakalete mahari.
Kwa kawaida mahari ilikuwa kuku au ng'ombe au mbuzi mmoja au jembe lapelekwa kama posa
au mahari. Zamani mahari yalikuwa si mengi na tena yalikuwa hayadaiwi sana kama siku hizi iwapo
mtu aliyehusika alikuwa hana chochote bali alitaka kuoa mwanamke. Vijana wa Kisafwa walikuwa
hawana taabu katika kuoa mke kwa sababu mahari yalikuwa rahisi sana. Lakini siku hizi mahari
yamekuwa makubwa; Ng'ombe sita au zaidi hudaiwa kama mahari na hii yasababisha kushindwa
kwa vijana wengi wa Kisafwa kuoa wanawake na wanawake kushindwa kuolewa. Kwa hiyo namba ya
wanawake wasioolewa huzidi na ya wanaume yaongezeka, na mwishowe umalaya waongezeka
nchini. Kwa jinsi hii, ile mila ya zamani ya Wasafwa ya kuukataa umalaya kabisa katika nchi yao
umeanza kupungua. Yasemekana ya kuwa mtindo huu wa kutoza mahari mengi sana umeigwa na
Wasafwa toka kwa Wanyakyusa ambao wana desturi ya kutoza mahari mengi watoto wao
wanapoolewa. Tabia hii ya kutoza mahari mengi ilianza kuigwa tangu mwaka 1919.
Baada ya mahari kupelekwa kwa baba ya msichana, basi yule kijana huanza kumsaidia kazi
nyingi baba mkwe wake. Wakati mwingine aweza kulima shamba la mkwewe nyumbani kwake.
Iwapo watoto hawakutoroshana, basi baada ya posa kupelekwa kwa baba mkwe, wazazi wa
39
msichana wanaweza kumleta binti yao kwa bwana yake wakati wowote ule na wala hakuna sherehe
kubwa katika kufanya hivi. Baada ya ndoa, mvulana pamoja na msichana (mkewe) huhamia kwa baba
mkwe na kujenga nyumba yao huko. Ilikuwani lazima msichana avunje ungo ndipo aweze kuposwa.
Inampasa mtoto wa kiume amsaidie baba wa msichana kama posa au mahari ilirudishwa kwa
mwenyewe baadae kama alishazaa mara moja kwa baba mkwe. Mtamba alibakia kwa baba mkwe.
NDOA YA SIKU HIZI
Mvulana baada ya kupatana na msichana anayetarajia kumwoa humpa msichana huyo shillngi
ishirini, na msichana huchukua hizo shilingi ishirini na kununua nguo yoyote ile inayompendeza,
bila ya kuwaeleza wazazi wake. Kama wazazi wake wakimwuliza kapata wapi nguo aliyovaa,
huwaambia kauza kuni ndizo zilizomletea fedha za kununulia nguo. Baada ya hapo, mchumba wake
aweza kumchukua mchumba wake bila ya wazazi wa msichana kujua na kumpeleka mchumba wake
hadi kwa mama yake mvulana ambaye naye hutoa shilingi ishirini na kumpa huyo mchumba wa
mtoto wake. Baada ya kufanya hivyo, habari zinaietwa kwa wazazi wa msichana kuwa mtoto wao
wanaye nyumbani kwao na kwamba wanataka kumuoa. Wazazi wa msichana hukubali na baada ya
siku nne hivi, msichana hurudishwa kwa wazazi wake. Siku ya kwanza ambayo msichana
huchukuliwa na mchumba wake, anapofika mlangoni kwa nyumba ya mama ya mchumba lazima
apewe shilingi 150/- na mchumba wake. Safari ya pill, msichana huyo huchukuliwa na mchumba
wake baada ya kukaa kwao msichana miezi mitatu au sita, na sasa msichana hupelekwa moja kwa
moja hadi nyumbani kwa mvulana, ambako hulala siku mbili hivi, halafu baba ya mvulana
huwaambia wazazi wa msichana kuwa binti yao yuko hyumbani kwake. Wazazi wa msichana
humwambia baba ya mvulana kuwa warudishiwe binti yao siku ya pill. Basi msichana hurudishwa
saa za jioni siku hiyo ya pill na msichana hupewa shilingi tatu au nne hivi kama kuku wa kuwapa
wazee wake ikiwa kama ni adhabu. Msichana hukaa kwa wazazi wake kiasi cha miezi miwili au sita
kwa kutegemea mahari aliyonayo mchumba wake. Kama mahari ipo, basi msichana hatakaa miezi
mingi kwao bila kwenda kwa mchumba wake ambayo hupelekwa kidogo kidogo kwa wazazi wake.
Safari ya tatu, msichana huchukuliwa tena na mchumba wake na kupelekwa nyumbani kwa
mchumba wake. Mpaka wakati huu msichana hawezi kupika chakula cha mume wake sababu bado
hajawa ni mke. Wakati wote huu wanapata chakula chao toka kwa mama ya mvulana. Msichana
hukaa siku mbili kwa mchumba wake na siku ya tatu baba ya mvulana hutoa habari kijijini kwao kuwa
waanze kutayarisha pombe na vyakula vichache. Baada ya kuona kuwa pombe imekuwa tayari, baba
wa msichana huwaambia wazazi wa mvulana ya kuwa wawarudishie binti yao. Wakati huu baba wa
mvulana hujitayarisha sawa sawa na huvunja fedha kiasi cha shilingi mia nne ambazo huwa katika
mahela mahela au vikoroti.
Siku hiyo wazazi wa msichana hunywa pombe sana na huwachagua wazee fulani ambao
hutumwa kwa baba ya mvulana na kusema kuwa wanamtaka binti yao. Halafu baba wa mvulana
humchagua mtu mmoja wa kumpeleka msichana kwa wazazi wake. Mtu huyo aneyempeleka
msichana kwa wazazi wake ndiye anayeshika helazote hizi zilizovunjwa na mzazi wa mvulana, na
pia jamaa huyu hufuatana na ndugu wa mvulana wakati wa kumpeleka msichana nyumbani kwao.
Msichana hutembea tembea kidogo kidogo ili aweze kupewa fedha nyingi sana, na hujaribu kutafuta
sababu nyingi na visingizio vingi ill aweze kusimama, na akisimama hupewa fedha ili aweze
kutembea. Kwa njia hii msichana huyo aweza kuchuma fedha nyingi sana kiasi cha shilingi mia tatu
au zaidi kabla hajafika nyumbani kwao. Wafikapo nyumbani kwa wazazi wa msichana, wale
waliokuja kumsindikiza msichana hupewa pombe kiasi cha madebe thelathini hivi na kuyapeleka
nyumbani kwa baba ya mvulana. Huko nyumbani kwa wazazi wa mvulana hunywa pombe
waliyopewa na wazazi wa msichana. Lakini wazazi wengine wa mvulana wanaweza kutoa kila mmoja
shilingi tatu halafu kila mmoja akichukua debe moja la pombe na kwenda nayo nyumbani kwake na
kuinywa. Kila ndugu ya baba ya mvulana aweza kutoa shilingi tatu na kuchukua debe moja la pombe.
Msichana hulala siku moja nyumbani kwao. Baada ya siku hiyo, baba ya mvulana huenda
nyumbani kwa wazazi wa msichana kwenda kumpa baba ya msichana shilingi kumi na tano. Katika
40
safari hii, baba wa mvulana hufuatana na wenzie watatu au watano hivi. Baada ya kupokea zile
shilingi kumi natano, baba wa msichana huwapa binti yake wazazi wa mvulana. Kesho yake, baada
ya msichana kufika nyumbani kwa bwana yake, huanza kutayarisha mafiga na kupika chakula cha
bwana yake kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya kuwa mwanamke aliyeolewa.
Bwana yake hawezi kula chakula hicho kilichopikwa na mke wake mpaka kwanza mke ampe
bwana yake shilingi sitini ndipo ale chakula chake. Chakula kingine kilichopikwa na huyo mke
kinapelekwa kwa baba mkwe. Mali kadhalika baba mkwe hawezi kula chakula cha mkwe wake mpaka
naye apewe na huyo mkwe wake (mke wa mtoto wake) shilingi ishirini na tano ndipo ale chakula
chake. Bila ya kupewa hizi shilingi ishirini na tano baba mkwe hawezi kula chakula cha mkwe wake.
Hizo shilingi ishirini na tano zatiwa pembeni mwa sahani za chakula wakati wa kupeleka chakula
kwa baba mkwe. Baada ya hapo, msichana huyo huendelea kuwapelekea chakula baba na mama
ya bwana yake, mpaka watakapomkataza asiwapelekee chakula tena. Sasa atakuwa mwanamke
kamili nyumbani.
SIFA ZA WACHUMBA
Wachumba wanatakiwa wawe na sifa nzuri kabla ya kuoana, yaani wanatakiwa wasiwe wezi au
wasitoke katika ukoo wa watu walio wezi wasiwe malaya. Wanatakiwa wawe wema na wasiwe
wachoyo bali wawe wakarimu. Inawabidi watoke kwenye koo zilizo nzuri na bora. Magonjwa kama
ukoma yalitiliwa mashaka makubwa katika posa. Iwapo mchumba mmojawapo anatoka katika ukoo
ulio na ugonjwa wa ukoma basi mchumba huyo itamwia vigumu sana kumpata mchumba mwenzie.
Kwa kawaida mkoma hutengwa mbali sana na watu wengine na kujengewa nyumba yake ya pekee
chini ya mti wa mlagalila, na anapokufa mkoma huzikwa chini ya huo huo mti halafu mti wenyewe
hukatwa ili uangukie nyumba yake na vyombo vyake vyote vifunikwe kabisa. Makusudi ya kufanya
hivi ni kwamba Wasafwa wanajaribu sana kuepusha watu wasio na ugonjwa huu wasikamatwe nao.
Walakini sifa zote hizi zilizoelezwa hapo juu kuhusu wachumbazimeanza kusahauliwa, na sasa
watu wengi wa Usafwa hawaangalii sana sifa hizi kwa sababu ya elimu nyingi na pia mwingiliano
wa utamaduni mbali mbali wa kigeni.
Sherehe haikuwa kubwa sana bali kitu kikubwa sana katika ndoa yao kilikuwa kudumisha ndoa
yao kwa wale waliohusika. Ndoa za Kisafwa zilidumu sana bila kuvunjika, lakini siku hizi ndoa
nyingi zinazofungwa hazidumu sana kwa sababu ya mabadiliko ya maendeleo yaliyokwisha tokea
yakiambatana na utamaduni wa kigeni. Ingawa kuna sherehe kubwa zinazofanyika siku hizi wakati
wa arusi, lakini ndoa nyingi hazidumu sana kama zamani. Ingawa kuna mabadiliko mengi ya
utamaduni katika jamii ya Wasafwa lakini Wasafwa ni watu ambao hawakupoteza sana utamaduni
wao kama jamii zingine za mkoa wa Mbeya zilivyopoteza utamaduni wao.
Kila msichana alipimwa bikira yake kabla ya kupelekwa kwa bwana yake. Hii ilikuwa ni desturi
ya jamii nyingi za Mkoa wa Mbeya. Kwa kawaida wasichana wote wa Kisafwa walitunza bikira zao
vizuri sana mpaka siku ya kuolewa. Lakini siku hizi nidhamu hii imeanza kupungua uzito wake kwa
sababu ya mwingiliano wa ustaarabu mbali mbali.
TALAKA
Hapo zamani talaka katika jamii ya Kisafwa zilikuwa nadra sana kupatikana. Mwanamke kutoka
kwa bwana yake na kwenda kwa bwana mwingine ilikuwa shida. Pia bibi kumtoroka bwana na
kutorokea kwa bwana mwingine ilikuwa vigumu sana. Iwapo mwanamke alifanikiwa kufanya hivyo,
vita kati ya kijiji alikotoka na kijiji anakotorokea ilizuka. Ng'ombe na wanawake wa kijiji alikotorokea
walitekwa kwa hiyo kumtorosha mke wa mtu au kumghilibu akili zake, watu waliogopa sana
matokeo yake. Kwa hiyo upuuzi huu wa kutoroshana au kumtaliki mwanamke ovyo ulikuwa nadra
sana. Kwa hiyo vita ilipiganwa na kusababisha hasara kubwa kwa pande zote, hasa kwa
wanakijiji waliom-
41
torosha mwanamke wa kijiji kingine. Kwa jinsi hii, wanawake waliogopa sana kuwatoroka
mabwana zao kwa sababu ya kuepuka vita kati ya kijiji na kijiji, na pia wanaume waliogopa kufanya
kitendo hiki kwasababu hii hii ya kuepukana na vita baina ya kijiji na kijiji. Lakini siku hizi za
mamboleo, mtindo huu wa kuwatorosha wanawake au wanawake kuwatoroka mabwana zao
umeenea sana katika jamii ya Kisafwa. Sababu zilizowafanya baadhi ya Wasafwa kuiacha
nidhamu yao ya bwana kubakia na mke au mke kubakia na bwana yake ni kwamba Elimu ya
kikoloni, mchanganyiko wa jamii mbali mbali; vimedhoofisha nidhamu hii. Na yasemekana kuwa
mtindo huu wa kuachana achana kwingi kati ya bwana na mke hasa kumeanza kwenye miaka
1930. Iwapo bwana na bibi walichoshana kwa amani, basi mahari yote ilirudishwa kwa bwana.
Siku hizi kuna utaratibu mwingine uliowekwa na serikali ya TANU.
DESTURI ZA KULA CHAKULA
Zamani Wasafwa walikuwa wanakula pamoja kijijini. Nyumba ilijengwa katikati ya kijiji na
iliitwa Ibanza, yaani nyumba ya kulia chakula na pia kulala wanaume wote. Ilikuwa vigumu kwa
mwanaume yeyote kwenda kulala katika nyumba ya mkewe. Hii haikuwa desturi yao. Nyumba zao
zilijengwa pamoja. Siku hizi 'Ibanza' imetoweka- bali kila familia inaweza ikawa na Ibanza' yake
kwa ajili ya watoto wake ili waweze kula pamoja. Mtu mkubwa hawezi kula katika Ibanza kwa
sababu utaratibu wa zamani haupo tena.
Maji ya kunawa yaliletwa katika kata na kila mtu alinawa maji, yaliyokuwa safi na maji
machafu yalimwagikia chini halafu kila mtu alikata kipande cha ugali na akakiweka juu ya kiganja
cha mkono wake ndipo akala. Hata kunywa pombe kila mtu alimiminiwa pombe mkononi pake,
ndipo anywe. Lakini siku hizi watu hutia maji ndani ya bakuli na watu wote hunawa maji hayo
hayo ambayo kila mtu ametumbukiza mkono wake na kunawa. Maji hayo huwa ni machafu sana.
Ni rahisi kueneza magonjwa kwa kunawa maji ya namna moja. Watu wanapokunywa pombe
hutumia mkenge mmoja unaotumiwa na kila mmoja.
Wakati wa kula ilikuwa lazima aanze mkubwa ndipo hufuata mtoto. Wakati wa kumaliza kula
ilikuwa lazima mtoto awe wa mwisho kumalizia kula, na ilikuwa ni lazima mtoto aondoe vyombo
vya chakula. Nyama iligawanywa na mkubwa. Watoto wa kike walikula pamoja na mama zao. Lakini
siku hizi desturi hizi zimeanza kusahauliwa kabisa na watu wameiga desturi za kigeni ambazo
baadhi yake si desturi nzuri.
MAMA ANAYEZAA MAPACHA
Mama wa Kisafwa anapozaa mapacha hutengwa na bwana yake na kulala nje ya nyumba
yake, yaani upenuni pamoja na mapacha yake. Kesho yake mbiu yapigwa kijijini kuwa kwa fulani
kuna mapacha na kwa hiyo watu wasiende kulima kwa muda wa siku tatu, kwasababu mtu
akienda kulima wakati mapacha yamezaliwa, yaaminiwa kuwa chakula hakitastawi shambani,
kwa sababu yaonekana kuwa ni mkosi kuzaa mapacha. Wakati wa siku tatu hizo wanakijiji
huwajengea kijumba chao hao jamaa waliozaa mapacha (bwana na bibi) mbali kidogo na kijiji
chenyewe. Halafu bwana na bibi wenye mapacha hukaa katika kijumba chao kwa muda wa miezi
miwili bila kuja kijijini. Chakula wanaletewa na mashamba yao yanalimwa na ndugu zao. Baada ya
hiyo miezi miwili jamaa za hao ndugu hukoroga pombe na huwatangazia wanakijiji kuwa
wanakwenda kuwatoa ndugu zao kule walikowekwa. Halafu siku hiyo nguo za wenye mapacha
zavuliwa na kutupwa huko huko waliko na huvaa nguo mpya au nguo zingine ambazo
hazijatumiwa wakati hao jamaa walipokuwa katika shughuli ya kutengwa. Nywele zao zanyolewa
na ndipo wanapelekwa nyumbani kwao kwa zamani. Baada ya hapo huanza kuishi maisha ya
kawaida na kufanya kazi kama kawaida. Desturi hii yaanza kufa katika sehemu zingine za Usafwa
kwa sababu ya elimu ya siku hizi.
42
MAMA ALIYEFIWA NA BWANA YAKE
Mama aliyefiwa na bwana hutengwa na kujengewa kijumba chake cha muda mbali kidogo
na nyumba yake ya kawaida. Mama huishi katika nyumba hiyo kwa muda wa mwezi mmoja.
Wakati anapokoka moto wake hapulizii na pumzi yake bali hupepea moto huo na kipande cha bati
au debe. Hali kadhalika mama mzaa mapacha hutumia kipande cha bati au debe kupulizia
moto upate kuwaka; baada ya mwezi mmoja, mama mjane hutolewa nje baada ya ndugu zake
kukoroga pombe kwa ajili ya sherehe hii. Mama mjane hunyolewa nywele, nguo zake alizokuwa
akizitumia katika kijumba cha kutengwa zatupwa. Hupewa dawa fulani na mganga ili anywe ili
kuondoa balaa jingine toka mwilini mwake. Baada ya kukaa mwaka mjane anaweza kurithiwa na
ndugu ya marehemu pamoja na watoto wake na watoto watakaozaliwa wataitwa kwa jina la
mrithi. Katika kufanya hivyo lazima pombe ya marehemu ikorogwe na kunywewa.
Iwapo mtoto wa kwanza katika familia amefariki, basi maiti yake itazikwa kwa baba ya
mama yake kwa sababu kwa mila mtoto wa kwanza katika familia ni mtoto wa baba ya mama.
Kwa hiyo anapokufa anazikwa kwa baba ya mama. Mtoto wa pili akifa huzikwa kwa baba ya baba ya
marehemui kwa sababu ndiye mtoto wake kamili. Mtoto wa tatu na kuendelea huwa ndio mtoto
wao, yaani wazazi wa mtoto.
MAMA KUPATA MIMBA BILA KUPITIA HALI YAKE
Mama akipata mimba bila ya kupitia hali hii, watu huwa na mashaka na wasi was! mwingi
sana, kwa sababu hii yaonyesha ni balaa kubwa sana kwa nchi. Ili kuthibitisha kitendo hiki cha
kushika mimba bila kupitia hali yake ya kawaida jamaa huenda kwa mganga kupiga ramli na
baada ya kuthibitishwa na mganga, wananchi waliotumwa kwa ajili ya shughuli hii hurudi kijijini
kwao na kumuuliza mama huyo kama yaliyokwisha semwa na mganga ni kweli na mama,
huitika kuwa yaliyosemwa ni ukweli mtupu. Baada ya mama kukubali hayo, bwana yake hutoa
mbuzi mmoja kwa chifu na kusema maneno haya:—
Chifu tumeharibu nchi yako kwa hiyo tunatubu". Chifu hupokea mbuzi na kuwaita wazee
anaoshirikiana nao katika ibada mbali mbali, halafu mbuzi huyo huchinjwa huku mtawala huyo
akisema maneno machache ya sala kama: —
"Mtu huyu anasema ameharibu nchi na ametoa mbuzi huyu na kutubu.
Kwa hiyo msifanyie lolote baya!"
Basi mbuzi huchinjwa halafu nyama yachomwa na kuliwa na wazee wenyewe. Basi bwana
na bibi wanaohusika wanatengwa, mahali mbali mpaka bibi amejifungua. Baada ya kujifungua
wananyweshwa dawa wote wawili pamoja na mtoto ili wasije wakapatikana tena na janga hili
siku nyingine. Halafu wanarudishwa nyumbani kwao na kuishi maisha ya kawaida.
KUOTESHA MEMO YA JUU KWANZA
Iwapo mtoto mdogo wa mtu fulani ameotesha meno ya juu kwanza, hii huonekana kama ni
mkosi mkubwa katika nchi yote. Mganga hutafutwa ili awanyweshe dawa hao jamaa na
kuwatenga wasichanganyikane na watoto wengine katika nyumba yao wenyewe. Pia
vyombo vyao wanavyotumia huwa ni maalum na hawawezi kutumia vyombo vingine vyo vyote
katika nyumba. Hao jamaa wanaohusika wanakaa katika hali hii kwa muda wa wiki mbili au tatu
hivi. Halafu mganga huwatoa na kuwapa dawa ya kuendelea kumpa mtoto.
43
UTAWALA
Zamani Wasafwa walikuwa na machifu wengi sana kama nilivyoeleza katika historia
yao hapo kwanza. Kila chifu alikuwa na watu wa kumsaidia katika utawala na hasa wazee
ambao wengi wao walishirikiana na chifu wao katika matambiko mbali mbali. Wasafwa
hawajapata kuwa chini ya mtawala mmoja kabla ya kuja wakoloni. Kila sehemu ya
Usafwa ilikuwa na mtawala wake na mtawala alipofariki, jamii yote katika utawala wake
huyo chifu ilimchagua mtu na kutawala. Kwa kawaida Wasafwa walimchagua chifu wa
kuwatawala kwa kufuatana na busara aliyokuwa nayo huyo mtu anayechaguliwa. Uchaguzi
haukufuata mtoto mkubwa tu wa chifu la, ball busara yake aliyoonyesha kwa watu ndiyo
ilikuwa sifa kubwa sana.
Mtu ye yote aliyevunja sheria alihukumiwa kutubu na baadaye kulipa ng'ombe
mmoja kwa wazee (mafumu). Bila ya kulipa ng'ombe, mvunja sheria alilaaniwa. Kodi zama
hizo ilikuwa kila raia kwenda kulima shamba la Mwene (Mtawala), na shamba hili lilikuwa
kama shamba la ushirika hivi. Kama mtu hakuenda kulima shamba la Mwene, kuku wake
alikamatwa kama adhabu yake ya kutofika kulima shamba la Mwene.
Raia walipeleka shida zao kwa mafumu wadogo halafu toka hapo shida zilipelekwa kwa
wafumu wakubwa na kuendelea mpaka kumfikia Mwene mwenyewe.
KIFO
Mtu akifa watu hukusanyika pale kilioni. Watu wengine huleta kuku, wengine huleta
nguo na wengine huleta chakula. Mtu anapokufa sababu inatafutwa kwa nini kwa kupiga
ramli. Kitendo hiki cha kupiga ramli kimeigwa toka kwa Wanyiha, Wakinga na Wanyakyusa.
Zamani kabla ya kuiga, kupiga ramli watu kijijini waliwauliza familia yake kama wametenda
jambo moja ovu ambalo limesababisha kifo cha marehemu. Iwapo mtu mmoja mbaya
aliingia ndani kumtazama mgonjwa na mgonjwa akafa baadaye, mtu huyo mbaya
alilaumiwa sana na kijiji. Ilikuwa ni mwiko kwa mtu anayefahamika kuwa ni mbaya kwenda
kuwaangalia wagonjwa, walimokuwa wanauguzwa kwa kuogopa kuwa hao watu waovu
wangeweza kusababisha vifo vya wagonjwa. Mgonjwa alitunzwa vizuri na watu wabaya
walizuiliwa wasifike kumtazama mgonjwa. Mtu akifa lazima wamzike siku ya pili yake ili
kuwapa nafasi wanaohusika kupashwa habari kuhusu kifo hiki. Iwapo ramli imemtaja mtu
fulani kijijini ndiye kamchawia marehemu basi huyo mchawi hukamatwa na kuzikwa
karibuni akiwa yu hai. Kwa hiyo utaona yakuwa uchawi ulikuwa hautakiwi kabisa katika
jumuia ya Wasafwa. Kumzika mchawi angali hai ni desturi ya zamani ambayo haifuatwi siku
hizi.
Siku hizi mtu anapokufa ghafla wanakijiji huchimba kaburi na mganga huja kupasua
maiti ili kutaka kujua ni nini kilichosababisha kifo cha huyo marehemu. Kama ni uchawi
uliosababisha kifo,
44
wanakijiji huenda kwa mganga kupiga ramli na mganga mwenyewe, kwa kufuatana na ufundi wake,
humtaja yupi ni mchawi ambaye kafanya kitendo hicho. Habari zinazomtaja mchawi zinaletwa
kijijini, na mchawi anayetajwa katika ramli kuhusu kifo cha marehemu huulizwa mbele yahadhara
kama kweli katenda hivi. Mtu huyo akikubali kuhusu jambo hili, basi yeye pamoja na wale wpte
alioshirikiana nao wanafukuzwa kijijini pale kwenda kijiji kingine. Iwapo huyo mchawi anayedhaniwa
katenda jambo hili anataka kuhamatoka kijiji chake alimofanya kitendo cha uchawi, basi, wanakijiji
wanamwambia kuwa wanakijiji wote watamuua kama mpango wao ukifaulu.
KUZIKA
Kwa kawaida Wasafwa hutumia nguo za kawaida kuzikia hasa nguo zilizokwisha tumiwa. Kama
mtu aliyekufa ni mtu mkubwa, kaburi lake huchimbwa ndani ya nyumbayake halafu maiti huzikwa
humo, kama ni Mwene, basi huyu huzikwa mahali.patakatifu na nyumba hujengwa juu yake. Iwapo
mtu amezikwa katika nyumba, nyumba hiyo itaendelea kukaliwa na familia yake.
Iwapo maiti ilipasuliwa, vitu fulani vyatolewa toka kwenye maiti. Baada ya kaburi kumalizika
kuchimbwa maiti inazikwa na inazikwa kiasi cha robo tatu ya kaburi halafu hushindilia sawasawa.
Baada ya hapo wale watu waliokuwa wakipasua maiti huchukuwa sehemu zile zilizotolewa kwenye
maiti ambazo zilikuwa bado kufukiwa kaburini na wanazitia kaburi ni nakuendelea kufukia. Baada ya
hapo waganga huenda kwenye kaburi wakati wa usiku, na kabla ya hapo tangazo latolewa kuwa mtu
yeyote asiwepo mahali karibu na kaburi na hao waganga hutia dawa fulani kwenye kaburi.
Hapo awali mtu aliyeugua ugonjwa unaoponyeka, aliweza kuuguzwa bure bila malipo. Walakini
baada ya kupona ugonjwa wake ndipo mgonjwa, kwa hisani yake kwa msaada alioupata toka kwa
mganga wake, aliweza kutoa mbuzi au chochote kama ndiyo shukrani yake. Mgonjwa wa safura
alipokufa alizikwa pamoja na vyombo vyake vyote asije akawaambukiza watu wengine ugonjwa huo.
Mgonjwa wa ugonjwa wa kawaida alitumia vyombo vyake maalum peke yake wakati wa kuugua
ugonjwa huu.
Siku hizi mambo mengi yameanza kusahauliwa kabisa. Kwa mfano, mchawi hawezi kuzikwa na
wanakijiji akiwa yu hai, wala mtu mwenye safura hatengwi na watu wengine katika familia na
kadhalika.
MAVAZI
Hapo awali mavazi ya wanaume na wanawake wa Kisafwa yalihitilafiana kidogo. Wanawake
nguo zilitengenezwa kwa ngozi ya mbuzi ambazo zilivaliwa mbele na nyuma. Ngozi ililainishwa sana
na baadaye ikapambwa na shanga mbalimbali. Wanaume walivaa adumbwi. Hii ilitengenezwa kwa
kutumia kamba za mti fulani fulani ambazo zililainishwa vizuri kiasi cha kuifanya nguo
inayotengenezwa iweze kuvaliwa, na zaidi vazi hili lilivaliwa kiunoni. Katika kuyalainisha mavazi,
mawe na miti ilitumika na mavazi yakatengenezwa vizuri.
Kichwani wanawake walitumia pambo walilolitengeneza kwa kutumia vijiti walivyovipaka rangi
na halafu wakavaa kichwani. Miguuni walivaa viatu vilivyotengenezwa kwa kutumia ngozi za mbuzi na vazi hili lilitumiwa zaidi na wanaume kwa sababu wao walivitumia kwa kutembeatembea porini
wakati wa kuwinda wanyama ili miguu yao isichomwe na miiba au kuumizwa na mawe. Na
wanawake hawakushiriki hasa katika kazi za uwindaji wa wanyama wa porini, kwa hiyo viatu hivyo
havikuhitajiwa sana nao.
MIIKO
Kama jamii zingine za Watanzania, Wasafwa waliiogopa miiko fulani fulani. Kwa mfano,
wanawake walikataa kula kuku na mayai yake kwa kuogopa kuwa kama wakila, wangegeuka kuwa
wapumbavu. Labda kuku alionekana kuwa ni ndege mpumbavu, kwa jinsi hii wanawake waliogopa
45
kuwa wangalikuwa wapumbavu kama wangalikula nyama na mayai yake. Ajabu yake ni kwamba
katika utafiti wangu sikuambiwa kuwa wanaume nao walikatazwa kula huku. Ukisoma maelezo
yangu hapo juu utaona kuwa kuku alitumiwa sana katika shughuli mbali mbali kama vile kutambikia
mvua na kadhalika, na kuomba sala mbalimbali zilizohusu maafa yao. Lakini sikuona mahali
popote palipoonyesha kuwa hao makasisi waligeuka kuwa wapumbavu baada ya kula nyama ya kuku.
Labda mwiko huu huu uliwapendelea wanaume na kuwatisha wanawake wasifaidi hiyo nyama ya
kuku. Hali kadhalika hata katika shughuli kubwa kubwa za kutambikia mvua au kutakasa nchi
wanawake hawakushirikishwa kikamilifu ball walikujashiriki katika ngazi ya mwisho ya shughuli yote
kama vile kushiriki katika kucheza baada ya sala za mwisho kumalizika. Hii yaonyesha nafasi ya
mwanaume na mwanamke ilikuwa namna gani katika jamii ya Kisafwa. Mwanamke alipokuwa katika
hedhi, ilikuwa ni mwiko kwake kumpikia chakula bwana yake wala hata mwanaume ye yote
hakuruhusiwa kuingia katika nyumba ya mwanamke aliyekuwa katika hali hii mpaka siku saba
zimepita, ambapo mwanamke aliyehusika ilimbidi kusafisha nyumba na kuisiliba upya ndipo
bwana au mwanaume yeyote aruhusiwe kuingia katika nyumba yake. Pia ilikuwako miiko mingine
mingi, lakini miiko yote hii imetoweka kabisa au miiko yote imo katika kutoweka kwa sababu ya
elimu nyingi mpya inayoleta fikra mpya kabisa na kuyakataa yale ya zamani yasiofaa.
IMANI
Hapo zamani kabla ya kuathiriwa na utamaduni wa kikoloni Wasafwa walikuwa ni watu wenye
imani kubwa sana kuliko ilivyo sasa. Kwa mfano, iwapo mtoto aliugua nyumbani, wazazi iliwapasa
waungane kama wamepata kugombana nyumbani ambako huenda ndiko kumesababisha kuugua
kwa mtoto, na walipofanya hivyo, yaani walipoungana, kijiji kizima kiliungana na wazazi hao
waliokuwa wakiuguliwa mtoto katika kuungana na kuomba kwa Mungu mtoto aweze kupona. Kijiji
kilipofanya hivyo, mtoto aliendelea kupona maradhi yake. Hata magonjwa makubwa makubwa kama
vile ndui ambao ni ugonjwa wa hatari sana, haukuweza kumuuwa mgonjwa baada ya kijiji chote
kuungana na kuomba kwa Mungu ugonjwa huo uondoke mara moja. Simba alipokamata ng'ombe
kijijini, wanakijiji waliwachagua vijana wawili wamwendee simba ili wakamuue na kweli wale vijana
wawili waliweza kumuua bila taabu. Hali kadhalika mwanaume aliweza kulala nyumba moja na mke
wa mtu mwingine bila kumtamani. Ilikuwa ni mwiko kwa Msafwa yeyote kufanya hivyo. Mtu
aliyevunja mahindi ya shamba la mtu, aliweza kuvunja hayo mahindi vizuri na kuyalaza mabua yake
pale pale karibu na shamba hilo vizuri ili kuonyesha ya kuwa mtu huyo hakuwa mwizi bali alikuwa na
njaa yake. Wakati wa kuposa msichana, kulikuwa hakuna haja ya kuwepo shahidi kwa sababu
Wasafwa waliaminiana sana, na iwapo ndoa ilivunjika hapo baadaye, mahari ilirudishwa bila ya
kuwapo mashahidi wo wote. Mvua iliposhindwa kunyesha, Wasafwa waliomba na mvua ikanyesha
siku hiyo hiyo. Lakini mpaka sasa sehemu zingine za Usafwa bado watu wanaomba mvua na mvua
inanyesha. Kwa mfano, sehemu za Iganjo na kwa Inshinshi, ni sehemu mojawapo ambako Wasafwa
wanaomba mvua kama imeshindwa kunyesha na mvua hunyesha siku hiyo hiyo.
KUTAMBIKA MVUA
Miaka mingine hutokea kwamba mvua hazinyeshi au zakawia kunyesha. Kama tunavyoelewa,
mvua ni kitu cha lazima kwa binadamu, wanyama, wadudu na mimea kadhalika. Kwa hiyo mvua
zinaposhindwa kunyesha, zasababisha maafa ya kila namna kwa viumbe nilivyovitaja hapo juu. Kwa
jinsi hii, mvua zinaposhindwa kunyesha viumbe mbali mbali na wanyama mbali mbali hustushwa
sana na ukosefu huu wa mvua. Duniani pote hupata pigd kubwa sana iwapo mvua zinashindwa
kunyesha na binadamu hufanya juu chini ili kupigana na mazingira ya namna hii waepukane na
maafa yanayoambatana na ukosefu wa mvua.
Wasafwa wana njia yao ya kupigana na mazingira ya mvua. Mvua zinapokosekana au
zinapochelewa kunyesha, Wazee fulani wa Kisafwa huenda mahali patakatifu na kuomba kwa Mungu
46
mvua iweze kunyesha. Mfano wa sehemu mojawapo zilizo maarufu sana kuomba (kutambikia) mvua
ni Iganjo, sehemu za Uyole karibu na mlima Mbeya. Kwa kawaida chifu wa jadi, ambaye watu wa
sehemu hizo humwita Mfalme, huwa ndio kasisi Mkuu wa matambiko, lakini sehemu zingine za
Usafwa Mzee fulani anayeaminika na kufuatana na chifu wao, ndiye huwa Kasisi Mkuu wa kuomba
mvua. Yeye hutafuta ulezi wa kukorogea pombe na baada ya pombe hii kukorogwa na kuwa tayari
pombe hiyo yatiwa ndani ya vibuyu vitano au sita. Kisha kasisi huwatangazia wazee wanaohusika na
salaza kuombea mvua na sifku huchaguliwa ili kufanya shughuli zote hizi.
Sasa kuku mweusi hutafutwa (sehemu zingine mbuzi au kondoo hutafutwa kwaajili ya shughuli
hizi). Mambo yote yakiwa tayari watu wote wanaohusika hjuenda mahali palipo patakatifu na kuanza
kuomba mvua inyeshe. Kasisi mkuu huanza kusema maneno haya. "Uposhele inguku ini
tuhanzaje hwunzi hwilwipei invula itonye, iviyabo vihwone. Ingukuinj mulyarrje mwendi mwikwizyanajei abantu balalamiha baiga, "Tukosile yenu? Invulayinyu Mhutima?"Tulaba twalamba
sana ngatukosile shimo vyanje. Ngazilipo zimo uvitilwe utuwozye we wewe dada pipo nahumo
uhwinyi washimbilile. Tusubila wenewe ungulubi uwinji numo."
MAANA
"Pokea kuku huyu tunataka nchini kuwe kweupe, Mvua inyeshe vyakuia vinakauka. Watu
wanalalamika wanasema,Tumekosa nini? Kwa nini unatunyima mvua? Tunakuomba sana
kama tumekosa lolote useme. Kama kuna jambo lolote lililokukasirisha
utuambie wewe baba. Kwa sababu hakuna mahali pengine pa kukimbilia. Tunakutegemea wewe
mwenyewe, Mungu mwingine hakuna."
Wakati sala hizi zinaposemwa, pombe iliyo katika vibuyu viwili yamwagwa chini mahali
patakatifu na huku kuku atiwa ndani ya pombe iliyomwagwa chini na hushikiliwa hivyo hivyo mpaka
kuku huyu kukosa hewa kabisa na kufa kwa kushindwa kuvuta hewa. Baada ya kuku kufa manyoya
yake yananyonyolewa na nyama yake huchomwa. Baada ya kumchoma kuku huyo, kasisi
huchukua nyama kidogo na maini yake na kukatakata vipande vidogo vidogo vya nyama ambavyo
vyatiwa pembeni mwa mahali pale pombe imemwagwa. Nyama inayobaki inaliwa na makasisi wadogo waliopo hapo pamoja na kasisi Mkuu, Makasisi hao wadogo huwa watano au kumi hivi kwa
kutegemea na mahali penyewe na watu walivyo na shida zao, na jinsi wanavyotaka kuomba mvua
yenyewe. Lakini kabla ya kusema sala zao, wale makasisi, wengine hucheza cheza kwanza hapo
hapo mahali patakatifu isipokuwa kasisi mkuu na kusema, "Tumefika sisi watoto wenu msije
mkasema ni watoto wengine". Ndipo kasisi mkuu huwaambia makasisi wake wakae chini halafu
huendelea na sala kama ilivyoelezwa hapo juu na mvua hunyesha mara baada ya sala hizo. Wakati
mahindi yamekomaa mashambani hakuna mtu wa kuanza kuvunja mahindi hayo kutoka shambani
mwake na kuanza kula mpaka kwanza sherehe maalum imefanyika. Sherehe ya namna hii hufanyika
sehemu zingine zingine katika nchi ya Usafwa. Mwezi wa tatu ambapo ndiyo wakati mahindi yaanza
kukomaa kiasi cha kuweza kuliwa, Kasisi mkuu huwakusanya watu wote wa sehemu yake na
kuwaambia siku ya kukutana pamoja kwa ajili ya shughuli ya ufunguzi rasmi wa kuanza kula mahindi
mapya. Siku hiyo ikifika watu wote huondoka na kwenda mahali pa kukusanyikiana huku
wakichukuwa mapembe na fimbo na miilini mwao na usoni hujipamba kwa rangi mbali mbaii. Siku
hiyo wanakijiji hao hucheza sana kuanzia saa saba adhuhuri hadi saa moja jioni. Wakati wa
kucheza, watu huwa katika safu - wanaume upande mmoja na wanawake upande mwingine, na wale
walio na mapembe hufanya safu, ya katikati. Wakati wa kucheza watu hawavai mavazi rasmi balil
huvaa mavazi ya kawaida tu. Kasisi Mkuu huvaa shuka na kaptura hukamata mikuki mitatu, halafu
hupanda juu ya mti na huko mtini huchomeka mikuki miwili. Baada ya kufanya hivyo, kasisi
hushuka chini na mkuki mmoja. Saa za jioni huwakusanya watu wote halafu humwaga unga wa
malezi chini na kusema.
"Baba Inshinshi tuongene apa usanyono, Tuhwanza aje iviyabo vimelaye ishinza mwatulima
Idondoma tumanyile aje linanganya, Tulawa ugazije amalondoma gasinanganaye iviyabo
Nantele baba pahandinealine amagonda gao, Iviyabo vyao vyamelile ishi bahwande aje
balyanje. Ovisaye abantu basinanganye, Tumanyile aje balipo abitunga, Tulaba aje ngoshele
balipo abitunga bawoneshe, Utuvuzye aje abitunga babana nganya, balipo abantu bafumu
nutali,
47
Bahwanza aje bananganya insi yitu. Abitunga balogaje abantu babahwinza ananganye insi
itu, Ishi bagosi tumalile ivlyabo vyetu visayirwe".
MAANA: "Baba Inshinshi tumekusanyika hapa leo, Tunataka vyakula vyote vizurl tunamolima.
Tunajua kwamba viwavi vinaharibu, Tunaomba uwazuie viwavi wasiharibu vyakula. Na tena
waliowahi kulima mashamba yao, Vyakula vyao vimekomaa wanataka wale, Uvlbarlki vyakula
wachawi wasijarlbu kuchukua chakula. Tunaomba kama wako wachawl utuombee kwamba
kama kuna watu waliotoka mbali kuja nchini kama wapo wachawi wawaloge hao wageni.
Wachawi wawaloge watu wanaokuja kuharibu nchi yetu." Sasa wakuu tumemaliza kwa hiyo
vyakula vyetu vimebarikiwa. Baada ya kumallza haya, watu wote huondoka na kukimbia
kwenda nyumbani kwao, bila ya kugeuka nyuma. Kaslsl mkuu hubakla mahali pale pale penye
shughuli hii ya sala kwa muda mrefu kldogo. Iwapo mtu aklgeuka nyuma wakatl wa
kukimbllia nyumbani yaaminiwa kuwa mtu huyo hupotea yaani hawezl kujua nyumbani
kwake ni wapi mpaka atakapotafutwa na jamaa zake. Basi baada ya kurudi nyumbani watu
wote wanaweza kuanza kuja chakula chao toka mashambani.
Lakini iwapo mvua ni nyingi sana nazinazidi kunyeshazaidi ya kawaida ya kusaidia mimea,
vile vile lazima tambiko lifanywe. Kasisi mkuu humchagua mfuasi wake mkuu ili akatafute kuku
mweupe kabisa toka kwa wanakijiji na humnunua na kumpeleka kwa kasisi mkuu (ambaye kwa
kawaida huwa ndiyo chifu mwenyewe) na kuku akishapokelewa, kasisi naye humpeleka huyo
kuku mahali patakatifu na kuwaomba mababu, kuwa nchini kuwe kweupe ili jua lije, na mara
nyingi huenda huko mahali patakatifu na wazee 5 na pia pombe lazima itolewe. Kasisi mkuu huanza
sala zake kama hivi:
Kasisi:
Msaidizi:
Kasisi:
Msaidizi:
Kasisi:
Msaidizi:
Kasisi:
Msaidizi:
Kasisi:
Msaidizi:
Kasisi:
Msaidizi:
Kasisi:
Msaidizi:
"ini kuku" (kuku huyu)
"Mumvwaje" (Msikie)
"Tuhwanzaje isanye lihole" (tunatakajua liwake)
"Mumvwaje" (Msikie).
"Imvula inanganya ivi yabo" (mvua inaharibu mazao)
"Mumvwaje" (Msikie)
'Twalamba sana" (Tunaomba sana)
"Mumvwaje" (Msikie)
"Twalamba sana" (Tunaomba sana)
"Mumvwaje" (Msikie)
"Inzagatwenzile izinji" (hatujaja kwa mambo mengine)
"Mumvwaje" (Msikie)
"Basi atwe twamala" (Basi sisi tumemaliza)
"Mumvwaje" (Msikie).
Basi baada ya hapo kuku anachinjwa na kuchomwa nyama yake kuliwa hapo hapo. Kesho
yake jua linawaka sana na linaendelea kuwaka na iwapo lazidi kuwaka na kuwatia wasiwasi
wanakijiji, sala nyingine itafanyika ili kuomba mvua zianze kunyesha. Huu hapo juu ni mfano wa
sala za kuombea mvua uliochukuliwa toka kwa Inshinshi juu ya mlima Mbeya (nyuma yake).
MAJI
Nchi ya Usafwa ilikuwa haina shida ya maji. Maji yalipatikana tele kila mahali katika nchi ya
Usafwa na misitu ilikuwapo mingi iliyohifadhi maji yasikaushwe na jua. Lakini watu walipoanza
kulima karibu na kingo za chemchemi za maji, basi maji yakaanza kupungua kabisa katika sehemu zingine za Usafwa. Mpaka sasa ziko sehemu zingine zenye ukame wa maji kama vile sehemu
zinazopakana na bonde la Usangu na sehemu za Njerenje na za Songwe ambazo ziko mbali na mto
Songwe. Walakini sehemu zingine za Usafwa zina maji chungu mbovu, na maji haya hutumika kwa
matumizi mbali mbali kama vile kumwagilia mashamba wakati wakiangazi hasa sehemu za
Uyolena sehemu za Mporoto. Maji ya sehemu hizi yanatumiwa sana kumwagilia mashamba ya
mboga mbali mbali kama vile kabichi, vitunguu, na kadhalika. Mashamba ya mihindi
yamwagiliwa maji hasa nyakati za kiangazi wakati mvua zimepungua na kuna ukame ukame.
Shughuli hii yapaswa kuen-delezwa vizuri zaidi na wataalamu wa kilimo hasa katika sehemu zile
ambazo mpango huu wa kum48
wagilia mashamba haujaanza bado katika mkoa wa Mbeya. Kwa matumizi ya nyumbani, maji
yanatumiwa kwa kunywa, kunyweshea mifugo, kufulia, kuoga na kadhalika. Kama nilivyosema hapo
'iuu sehemu zingine za Usafwa zina bahati ya kuwa na chemchemi na vijito vingi vinavyo tiririka
miteremko ya milima hudumu daima kwa hiyo, Wasafwa hutumia mianzi na kuitoboa katikati
halafu inaunganishwa na kufanya bomba la maji linalopeleka maji sehemu zile zinazotakiwa - hasa
sehemu zilizo na nyumba za kukaa watu.
Watu wengi wanaoishi sehemu za Mporoto wametatua tatizo la kuyafuata maji yaliko kwa
kuyaleta maji karibu na nyumba zao kwa kutumia mabomba yaliyotengenezwa kwa kutumia mianzi
ambayo inapatikana pande hizi za Usafwa. Matumizi mengine makubwa ya maji ni kujengea nyumba
za kisasa. Watu wengi wa Usafwa, karibu robo tatu ya wakazi wote wa wilaya ya Mbeya wanajenga
nyumba zao kwa kutumia matofali mabichi au yaliyochomwa, na juu ya mapaa ya nyumba zao
huezekea mabati. Kwa kweli watu wa wilaya ya Mbeya wamepiga hatua kubwa katika kujenga
nyumba za kisasa zilizo na nafasi ya kutosha. Maji mengi yanatumiwa katika njia hii kwa sababu
karibu kila mkazi wa Wilaya amejaribu kujenga nyumba ya matofali ya kumtosha yeye na familia
yake.
ELIMU YA WATOTO
Mtoto anapozaliwa hupewa maziwa - yaani mtoto huanza kujifunza kunyonya maziwa toka kwa
mama yake, na huendelea kunyonya mpaka baada ya siku nyingi kidogo ambapo huanza kupewa uji
wa ulezi. Huendelea hivyo hivyo mpaka baadaye atakapoanza kupewa chakula laini laini.
Elimu kubwa kabisa wanayofunzwa watoto wa Kisafwa ni kujifunza kazi zote zinazofanywa na
wazazi. Elimu hii inaanza mapema kabisa tena ni elimu ya kujitegemea. Ni elimu ya kuona na
kufanya, haina nadharia yoyote ndani yake. Kazi kubwa ambayo lazima watoto wajifunze ni kulima.
Hii ni kazi ya kwanza kabisa ambayo mtoto wa Kisafwa anapaswa kujifunza upesi sana ili aweze
kuwasaidia wazazi wake na pia aweze kuwa na kijishamba chake mwenyewe cha mahindi ya
kuchoma. Mvulana na Msichana wote hufundishwa kazi hii mapema sana. Watoto wanaanza
kujifunza kazi hii tokea umri wa miaka mitano na kuenuelea. Watoto wanatengenezewa vijembe
vidogo sana vilivyo na ukubwa wa kiganja cha mkono na mipini yake ni mifupi sana ambayo ina urefu
wa kiasi cha mkono mmoja au mkono na nusu hivi kwa kutegemea kimo na umri wa mtoto
anayetengenezewa kijembe hicho. Jembe ni maisha kwa mtoto yeyote wa Kisafwa.
Mtoto, baada ya kufahamu kazi ya jembe, huanza kujifunza elimu nyingine. Pia, hasa kwa
kufuatana na maisha yake na baadaye atakapokuwa mtu mzima. Elimu yenyewe ni kama vi l e
kujifunza kupika, kusafisha vyombo, kuteka maji, kukandika nyumba, na kadhalika. Elimu hii hasa
yatolewa kwa msichana. Mvulana hujifunza elimu ya kujenga nyumba, kuchonga mizinga ya nyuki,
kukamua maziwa, kuchunga ng'ombe, mbuzi, kondoo, na kadhalika. Elimu yake yote hutolewa kwa
kufuatana na kazi atakayofanya baadaye katika maisha yake. Kwa mfano, mtoto wa kiume
anafunzwa elimu ambayo itamsaidia kuishi na mke na watoto wake, na mtoto wa kike hufunzwa
elimu itakayomsaidia kuishi na bwana yake na jinsi ya kuwalea watoto wake.
Katika jamii ya Kisafwa hamna utaratibu wa marika, bali watoto hula pamoja, hucheza pamoja,
na kulala pamoja na watoto wenzao pale kijijini.
KUMPELEKA MTOTO SHULENI
Siku hizi Wasafwa wengi huwapeleka watoto wao katika shule za serikali kujifunza elimu
nyingine ya kisasa. Lakini hapo nyuma kidogo watu wengine walikuwa wanaogopa kuwapeleka
watoto wao shuleni kwa sababu eti wangelogwa na watu wasiopenda watoto wa watu fulani
waendelee. Wasiwasi huu ulikuwapo sana, lakini siku hizi jambo hili limekufa kabisa kwa sababu
watoto wengi sana wanasoma shule za serikali na hakuna kinachotendeka.
NYUMBA ZA WASAFWA
Nyumba za asili ni za mviringo ingawa siku hizi nyumba za aina nyingine zinajengwa na
Wasafwa. Nyumba za asili zinajengwa mviringo yaani "msonge", na vifaa vitumikavyo katika
kujengea nyumba hizi ni miti, magugu, matete na kamba za miyombo kwa kufungia fito pamoja na
49
miti ya kujengea. Kwa kawaida ndani ya nyumba za asili hazigawanywi vyumba, bali
huachwa hivi hivi na kutumiwa hivyo hivyo. Nyumba zenyewe zakandikwa kwa kutumia
matope kwanza halafu Mpu iliyochanganywa na mavi ya ng'ombe hufuata juu ya matope.
Lipu ya namna hii hulainisha sana ukuta na kuufanya ukae sawasawa. Mlango wa nyumba hizi
huwa ni mmoja. Juu ya nyumba manyasi maalum yaitwayo "Isonze" huezekwa. Manyasi haya
ni laini sana na yanadumu hata miaka sita bila kuharibika. Kutengenezea kenchi na paa
hutumia miti au mianzi nasakafu yake hutengenezwa vizuri kwa kusiriba matope na kuifanya
sakafu iwe sawasawa na kuonekana maridadi na imara.
Siku hizi watu hujenga nyumba za namna nyingine hasa nyumba zenye kuta nne. Kwa
kawaida watu wa wilaya ya Mbeya wanajenga nyumba zao kwa kutumia matofali mabichi au
matofali ya kuchomwa. Maji mengi yanatumika kutengenezea na kufyatulia matofali. Nyumba
za miti zimeach-wa isipokuwa wale watu wanaoishi karibu na mianzi. Hawa hutumia mianzi
au matofali katika kujengea nyumba zao. Kitu kinachowasumbua wakazi wa Mbeya ni saruji
ya kujengea na bati za kuezekea nyumba zao. Shida inayowatokea hawa jamaa ni kwamba
vitu vinapatikana kwa msimu. Ni shida kupatikana wakati wote. Shida ya pili ni ile ambayo kila
mtu anaelewa yaani ya kupanda kwa bei ya vifaa vya kujengea nyumba. Kwa hiyo utaona
kwamba nyumba nyingi zinachelewa kumalizika kujengwa kwa sababu ya shida hizi mbili
zilizotajwa hapo juu.
ORODHA YA KUMBUKUMBU YA VITABU
1.
E.Kootz Kretschmer:
ABRISS EINER LANDESGESCHIEHTE VON
USAFWA IN OSTAFRIKA, 1929.
2.
E.Kootz-Kretschmer:
DIE SAFWA. 3 BANDE, 1933.
3.
TH.SIaats:
PEOPLES OF MBEYA DIOCESE, 1972.
4.
Afisautamaduni:
JARIDA LA UTAMADUNI LA MKOA WA MBEYA,
1970.
5.
Charsley, S.R.
THE PRINCES OF NYAKYUSA, 1969.
50
Sura ya Tatu
JAMII YA WASAGARA
UTAFITI ULIOFANYWA KUHUSU ELIMU YA JADI YA WASAGARA
Wasagara ni jamii inayoishi Wilaya ya Kilosa wakipakana na Wakaguru upande wa Kaskazini na
Wavidunda upande wa Kusini, ha Waluguru upande wa Mashariki na Wagogo upande wa Magharibi.
Nchi yao ni ya rutuba sana tena ni ya tambarare. Udongo wake ni mzuri sana, mimea mbali mbali
hupandwa. Katani kama zao la kuwaletea fedha iimekuwa likipandwa na Makampuni ya kizungu kwa
muda mrefu sana. Wasagara wenyewe wamekuwa hawalishughulikii zaidi zao hili kwa sababu ya
kazi ngumu inayotakiwa katika kulishughulikia zao hili kikamilifu. Kwa hiyo Wasagara wenyewe
wamekuwa wakipanda mazao kama vile mtama, bwembwela, maboga, kunde (safe), mlenda
(hombomgunda), Derega, mwage, tele, kikundembala (mwamizi Mulungu), sunga, mpunga na
pamba, na kadhalika. Mpunga na pamba ni mazao yanayowaletea fedha.
Kwa upande wa Kaskazini, nchi ya Kilosa imeinuka na mwinuko huu huendelea katika milima ya
Kilosa ambayo inaungana na milima ya Mpwapwa na ya Ukaguru. Mvua zanyesha kwa wingi sana
wakati wa masika na maji ya mvua yanatuama sana juu ya udongo na kuifanya ardhi ya nchi ya
Kilosa, ionekane kama yenye matope matope. Wakati wa kiangazi, jua linawaka sana. Reli Kuu ya
Kati imepita hapa na barabara za magari ya kwenda Mpwapwa, Gairo, Morogoro na Mikumi zapitia
katika mji wa Kilosa.
Nchi ya Kilosa ni maarufu sana kwa mashamba ya mkonge ambayo yametapakaa karibu kila
upande wa nchi hiyo. Mashamba ya mkonge kama yale ya Msowero, Kimamba na Kilosa ndiyo
yaliyoifanya nchi ya Kilosa ijulikane sana katika nchi ya Tanzania. Mali kadhalika Reli Kuu ya Kati
imeongezea umaarufu wa nchi hii. Reli iendayo Kilombero kupitia Mikumi, yaanzia Kilosa. Pia
llonga ambacho ni kituo cha kilimo, elimu na mawasiliano, kimeongezea umaarufu wa nchi ya
Kilosa.
Kama inavyofahamika, Wasagara ni watu wapole sana na wema! Watu hawa hawajui vita hata
kidogo na hawataki kumwudhi mtu. Wako tayari kumwachia mali yao adui yeyote anayetaka
kupigana nao. Ni watu wapole sana na waoga kwa vita. Wasagara wengi wanaishi sehemu za
mashambani na wageni karibu wote wanakaa mjini Kilosa. Wasagara ni watu wanaojishughulisha
sana na kilimo. Kwa sasa hivi Wasagara wengi sana wamepiga hatua kubwa ya kuhamia katika vijiji
vya maendeleo ambamo shughuli nyingi za pamoja zafanyika, na Wasagara wengi sana kwa sasa
wananufaika sana kwa kuitikia mwito wa kukaa pamoja katika vijiji hivi.
HISTORIA
Jina hili "Wasagara" lina maana ya "Wachokozi". Asili ya Wasagara yasemekana kuwa ni
Palaulanga. Huko Palaulanga walifanya kambi kubwa kwa sababu walikuwa katika makundi
makubwa makubwa, na kama inavyoeleweka kila mahali penye kundi au makundi makubwa ya watu
hapakosi mgawanyiko wa watu. Kwa sababu kufanya kazi kwa pamoja huwa ni vigumu sana. Basi
hayo makundi yakiwa bado Palaulanga yaligawanyika, na kundi lililoitwa Wasagara lilikaa penye
majani yaliyoitwa mazaganza. Wasagara wengine walikaa mahali palipoitwa Peupe (Nzelu) watu
wenyewe wakaitwa Wanzelu (Weupe). Huu ni ukoo wa Wasagara uliokaa mahali hapa. Watu hawa
wakiwa katika hali ya makundi haya mawili, kundi moja ambalo lilikaa juu ya Mazaganza likaenda
kuwachokoza Wanzelu walipokwenda kuomba moto, tumbaku na vitu vingine vingi. Kuomba kwao
51
vitu hivi kulikuwa ni kwa mara nyingi mno hata Wanzelu wakachoshwa na tabia hii ya kusumbuliwa
na hawa watu. Basi Wanzelu wakaanza kulalamika na kusema kuwa watu hawa ni "Wasagara" - yaani ni
"Wachokozi". Wakubwa wa Wanzelu walipouliza kwa nini watu wao wanalalamika, Wanzelu
wakaelezea kisa chote toka mwanzo hadi mwisho. Basi mkuu wa Wanzelu na mkuu wa Wasagara
wakasikiliza kisa chote na wakaangua kicheko, kuonyesha kuwa basi yote yale yaliyowaudhi
Wanzelu yamekwisha. Tangu hapo wale waliokaa juu ya majani ya mazaganza wakaitwa wachokozi
yaani Wasagara.
Basi makundi ya watu hawa yakazidi kuendelea na safari zao, na walipofika mto Mdukwi
wakatengeneza daraja la kuvukia. Watu wengi walivuka mto Mdukwi kwa kutumia daraja hilo.
Makundi mengine ya watu yakiwa katika kuvuka huo mto, daraja likavunjika. Lite kundi la Wasagara
lililovunja daraja la kuvukia likaitwa Wabenadiloko — yaani Wavunja daraja". Basi watu wote hawa
waliokuwa katika kundi hili wakaitwa "Wabenadiloko" na ukafanywa kuwa ukoo maalum. Daraja
lenyewe lilivunjwa wakati wa safari za hawa Wasagara.
Walipokuwa katika safari zao, njaa ikawashika, nao walikuwa hawana moto wa kupikia ingawa
chakula walikuwa nacho. Kwa hiyo, baadhi ya watu wakafikiria njia ya kupatia moto wa kupikia.
Wakatafuta mti mkavu na mti wa kupekechea na wakaanza kupekecha moto. Baadaya kupata moto,
wakashindwa kuutumia moto huo kwa sababu hawakujua jinsi gani wapike hicho chakula. Mtu
mmoja toka kundi mojawapo ya makundi ya Wasagara akatafuta mawe na kuyapasua na kuyafanya
yaonekane kuwa mafiga ya kutelekea chungu cha chakula, na kweli hayo mawe yakafaa kuwa maf iga
na wakapika chakula chao na baadaye wakashibisha njaa yao. Jambo hili liliwafurahistia na
kuwastaajabisha watu wengi sana. Wakubwa wao wakauliza, "Ni nani kaleta elimu ya kutumia
mafiga"? Watu wakaeleza jinsi watu wa kundi moja kati yao, lilivyoweza kupasua mawe na kufanya
maf iga ya kupikia. Basi kundi lote la yule mtaalamu aliyetafuta hayo mafiga likaitwa ukoo wa
Mahafigwa. watu wenyewe wanaitwa Wahafigwa.
Walipozidi kuendelea na safari yao, makundi fulani ya watu yalishindwa kutwanga unga wa
kutengenezea ugali, basi ikawabidi waende kuomba unga kwa watu wengine waliokuwa katika
misafara hiyo. Hao watu walioombwa unga wakatoa chengachenga za unga badala ya kutoa na
kuwapa unga. Zile chenga zikapikwa na wakala. Baada ya kula zile chenga, wazee wa makundi
yaliyoomba unga wa kupikia ugali wakawauliza watu wao ni nani aliyewapa zile chenga, nao
wakajibiwa na akina mama ya kwamba waliowapa hizo chenga ni wale pale. Wazee wakaonyeshwa
wale watu waliozitoa hizo chenga. Basi wazee wakaamua na kusema kuwa hao watu ni
"Wanyasenga". Basi baadhi ya Wasagara wakaitwa hivyo — Wanyasenga , yaani watu waliotoa
chenga.
Kama tunavyoelewa sote, misafara yoyote huandamwa sana na magonjwa mbali mbali.
Wasagara hawakuepuka maafa hayo. Maradhi mengi yaliwasumbua sana, na mwishowe jamaa fulani
kutoka katika mojawapo ya makundi ya Wasagara wenyewe, akagundua mizizi ya dawa ya
kuponyeshea magonjwa fulani fulani. Basi watu wote waliougua magonjwa fulani fulani walipewa
mizizi kama dawa ya kuponyeshea na wengi walisaidiwa sana. Jamaa wote wakamheshimu sana na
wakakata shauri kuwa kundi lake huyo mganga alimotoka liitwe Wazizimiza. Basi huo ukawa ni
ukoo mmojawapo maarufu sana katika jamii ya Kisagara. Pia palitokea mzee mmoja aliyekwenda
kuwatembelea wenziwe saa za jioni. Alipofika katikati ya safari yake, akasikia harufu mbaya ya
chpo. Jamaa huyo akauliza, "Nani huyo"? Kumbe kulikuwa na mtu ambaye alikuwa anajisaidia
vichakani. Yule mtu kule kichakani akaitikia, "Ni mimi". Akamwuliza, "Unafanya nini?" Yule mtu kule
kichakani akajibu, "Ninakwenda chooni". Basi jamaa akaendelea na safari yake hadi alikokusudia
kwenda. Kumbe alipokuwa anazungumza na yule mtu aliyekuwa anajisaidia vichakani, watu
walimsikia. Alipofika tu wakamwuliza, "Ulikuwa unazungumza na nani huko porini usiku huu?"
Akajibu, "Nimemkuta mtu anajisaidia pale porini usiku huu". Basi wale wenzie wakamwambia kuwa
hao ni "Wanyakilo", yaani watu waendao choo usiku.
52
Katika hizo safari zao, walifika kwenye mto wa Matete, watu walishindwa namna ya kuvuka mto
huo. Basi jamaa mmoja kutoka katika kundi moja akawaonyesha wenzie namna ya kuvuka mto ule
kwa kutumia kushika matete yaliyoota pembeni mwa mto wenyewe. Basi watu wengine walipouliza
ni nani kaleta maarifa haya; jamaa wakamtaja huyo mtu mwenyewe. Basi kundi lake lote yule jamaa
mwenyewe kuleta maarifa haya likaitwa "Wadete". Wakati wakizidi kusafiri katika safari zao jamaa
mmoja alisahau kitu chake nyuma alikotoka. Alipokumbuka ikambidi arudi nyuma akakitafute.
Alipofika mahali penyewe walipotoka, akaanza kukitafuta kitu chenyewe huko na huko huku wenzie
wakimngojea. Walipoona anachelewa kurudi, wakaamua wamfuate ili wamsaidie. Kumbe katika
kufanya hivyo, yale makundi mengine yakawaita watu hao "Wasemwa", yaani "Waliosahau". Basi
ukoo wa "Wasemwa" ukawa umetokea tayari katika jamii ya Wasagara. Wakati huu walikuwa
wamefika kambi ya Kwiva, na sasa wakaanza kusambaasambaa wakikaa pamoja katika makundi
makundi ya watu watano au kumi au zaidi. Basi hivyo ndivyo koo mbali mbali za jamii ya Wasagara
zilivyotokea.
IMANI
Wasagara ni watu ambao hapo awali walikuwa na imani kubwa sana na wenye kushika sana
dini yao ya jadi tena walikuwa waoga wa vitendo viovu. Baadhi za imani za watu hawa zimeelezwa
hapa chini. Mama anapokuwa katika hali mbaya (mwezini) ilikuwa ni mwiko kwake kumpikia
chakula bwana yake, ilikuwa lazima mtu mwingine ampikie chakula bwana yake. Hali kadhalika
mwiko mwingine kuhusu hali hii ulikuwa mwanamke hawezi kumzunguka bwana iwapo alitaka
kupita. Ilimbidi mama apite mbele ya bwana. Iwapo mgonjwa alikuwapo, ilimbidi apakatwe na
Mzelu yaani mtu wa ukoo wa Wanzelu, halafu unga ulinyunyizwa kuzunguka mgonjwa na baadaye
"Mulungu" (Mungu) akaombwa ill amsaidie huyo mgonjwa. Yasemekana kuwa kweli huyo
mgonjwa alipona. Katika kila kijiji alimokuwamo mgonjwa ilipitishwa amri ya kuwa hakuna mtu wa
kuongea na bwana yake au mke wake mpaka mgonjwa amepona na watu wote walishika sana amri
hii. Vile vile iwapo palitokea simba kijijini aliyetaka kukamata mtu, watu wote pale kijijini walitoka
nje ya nyumba zao nakupiga magoti nakumwomba Mungu (Mlungu) amsaidie ndugu huyo ambaye
alikabiliwana janga la kukamatwa na simba na kumwepusha hilo janga. Basi simba hakuweza
kumkamata huyo mtu na akaondoka kijijini bila ya kufanya ghasia zingine tena.
Jamii ya Wasagara ilikuwa inafuata urithi kwa mjomba. Mjomba alikuwa na mamlaka makubwa
na aliogopwa na kuheshimiwa sana na watoto wa dada zake. Mjomba aliweza hata kumchukua
1
mwipwaye na kumtia rehani na hakuna ambaye angalimwuliza kisa cha kufanya hivyo. Baba ya
mtoto hakuwa na la kufanya bali kazi yake huyo baba ilikuwa ni kuzaatu nakusaidia kuwalea watoto
wake, lakini mamlaka juu ya watoto hao alikuwa hana kabisa.
Wasagara walikuwa na imani kubwa sana katika dini yao ya asili na kumwamini Mlungu
(Mungu) ilikuwa kwa njia ya tambiko kuelekea kwa Mwenyezi Mungu. Kuongopa ilikuwa ni mwiko
kwa Msagara yeyote. Iwapo ugonjwa ulitokea kijijini, waiimchukuwa mgonjwa na kumweka chini ya
mti waliouchagua na kumwomba Mungu amsaidie mgonjwa apone haraka, Unga wa mtama,
machicha ya pombe, viazi vikuu, majani ya hozavilinyunyizwa mahali pa tambiko. Muwa mwekundu
uliomenywa, tumbaku ya mkate, viliwekwa mahali pa tambiko. Vitu vyote hivi viliwekwa juu ya
majani ya mgomba yaliyotandikwa chini. Kondoo wa tambiko alichinjwa na kuku mweupe aliweza
kuletwa mahali hapo na kuchinjwa. Lakini shughuli kubwa za tambiko lolote lile ilikuwa lazima
kondoo achinjwe. Zaidi ya hayo bao lilipigwa na mganga kutafuta sababu ill atoe kiini cha ugonjwa
wenyewe, halafu mtani wa mgonjwa alitafutwa ambaye alitakiwa kutafuta unga na kutambikia
Mungu ili mgonjwa apone. Maneno aliyoyasema huyo mtani wa kutambikia ni kama hivi:
"Mulungu mkawage" maana yake, "Mungu mwachilie mgonjwa huyu ili aweze kupona" na huku
baba yake yule mgonjwa hutajwa. Matambiko yalifanywa wakati wowote shida zilipowatopea.
Wakati wa tambiko kubwa, kasisi wa shughuli hizi huvaa ngozi, ushanga na mgobole ulipigwa.
Kondoo huchinjwa kwanza hata kama wanyama wengine wa kuchinjwa wapo. Baada ya tambiko
watu hurudi kijijini kwao na kula chakula pamoja na kunywa pombe.
53
Kabla ya kondoo kuchinjwa, kondoo huyo huzungushwa mahali patakatifu na mtani mara nne
au tano hivi na wakati huo huo manyoya ya kuku mweupe na kuku mweusi hunyonyolewa moja
baada ya moja na huku wimbo ukiimbwa kama hivi:
"Mgole kwega uleke mgole,
Kwega uleke mgole".
Kabla kuku hajachinjwa huzungushwa mahali patakatifu mara saba na mwimbo ukiendelea tu. Na
wakati wa kuwachinja hao kuku mweupe na kuku mweusi, wanachinjwa kidogo tu ili muradi damu
zinamtoka huyo kuku, na huachiliwa ili ajipigepige wakati anapotapatapa halafu ubawa
watakaoangukia basi ndio itakuwa tafsiri ya tambiko lenyewe - kama ni upande wa kuume au upande
wa kushoto. Basi yule mgonjwa, ataambiwa kama ni babu zake ndio waliochukia na kuleta baa hili la
ugonjwa, basi sala zitaelekezwa huko.
TAMBIKO LA MVUA
Iwapo mvua hazikunyesha kama kawaida yake, basi wazee wa sehemu fulani za Usagara ambao
ndio waliohusika waliwaambia vijana wa Kisagara shida iliyokuwa inawakabili katika nchi yao. Basi
vijana wakaamua kuchanga fedha ili wanunue chumvi na kaniki halafu wawakabidhi wazee vitu hivyo
viwili. Basi wazee walimtafuta mtani wao na mtu mwingine kutoka kijijini pao. Hawa watu
walitumwa kwa Mundo ambaye maskani yake yalikuwa Ukaguruni. Yasemekana huyu Mundo
alikuwa mchafu sana kwa kuleta mvua nyingi kila siku. Jamaa hawa wawili walikwenda mpaka
kwa Mundo, mtani "tu ndiye aliyeruhusiwa kuingia mahali alipokuwa anaishi Mundo, na yule
mwanakijiji aliachwa mbali na mahali hapo. Yule mtani alipoingia mahali anapoishi Mundo, alitoa
zawadi hizo kwa Mundo huku akitukana matusi chungu mbovu. Baada ya kumtukana na kumkabidhi
zile zawadi - chumvi, kaniki na tumbaku ya mkate, Mundo alimkabidhi yule mtani Mzimu wa mvua na
kuuwambia, "Haya sasa nenda maombi yenu yamesikilizwa". Basi huyo mtani kabla hajafika
nyumbani mvua zaanza kunyesha nyuma alikotoka na mbele anakokwenda. Basi mtani akifika
nyumbani humkabidhi Mkuu wa sehemu hiyo ulikotoka mzimu wa mvua, wakati huo mvua zinazidi
kunyesha. Lakini lazima Mzee Kutukutu, ambaye ndiye aliyekuwa mtawala wa nchi yote ya Kilosa,
ajulishwe kuhusu shughuli zote hizi, kwamba watu wake wa mahali fulani wanatambikia mvua.
Pia mvua ilitambikiwa kutoka kwa Kingo ambaye maskani yake yalikuwa Morogoro. Kwanza
baada ya kuona kuwa mvua haijapiga kwa muda mrefu, mzee Muhongola ambaye alikuwa waziri wa
Kutukutu, alimwendea na kumwambia kuwa watu watakufa na njaa kwa sababu mvua hazinyeshi na
kwamba ingalifaa atambikie. Basi Muhongola alitumwa Morogoro na Mzee Kutukutu kupeleka
zawadi za mganga Kingo anayeishi Morogoro. Zawadi zenyewe zilikuwa shoka au jembe halafu na
kitambi. Baada ya kuzifikisha hizo zawadi na Bwana Muhongola Kingo mganga wa mvua, alimwambia Muhongola ale kwanza chakula. Lakini Muhongola alikataa kabisa kula chakula kwanza
mpaka apate mvua iliyompeleka huko ndipo ale chakula. Basi baada ya kupokea zawadi zake,
mganga Kingo alitoa dawa yake ya mizimu ya mvua na kumwambia Muhongola aende nayp na
akampe Kutukutu ili ikalale ndani ya maji, na siku ya pili yake mzee Kutukutu aitishe mkutano wa
kupiga gumba, yaani kuchoma sindano kwenye sikio la kila mmoja na iwapo kuna mtu ambaye sikio
lake halipitishi sindano, yaani sindano haipenyi sikio lake, basi mtu huyo atashikwa kuwa ana
mzimu wa mvua atakuwa ndiyo mtu aliyeshika mvua. Sasa Mzee Muhongola hurudi kwa Kutukutu na
kumwelezea yote yale aliyoambiwa. Basi Kutukutu aliitisha mkutano baada ya dawa aliyopewa na
mganga kulala ndani ya maji. Watu wote walikusanyika pamoja na kila mtu alipigwa gumba (sindano) ili kumtafuta nani sindano hiyo ilikataa kuingia ndani ya sikio lake. Kwa kawaida katika nchi ya
Wasagara lilikuwapo jitu moja ambalo lilikuwa haliogi halichani na jitu la kutisha na baya kwa sura.
Hili jitu hasa ndilo lilikuwa na mizimu ya mvua katika nchi hiyo. Jitu hili vile vile lilikuwepo wakati wa
kupiga gumba na siku zote zamu yake ilipofikajitu hili sindano ilikataa kupenya sikio lake. Baada ya
kuona hivyo mtawala Kutukutu alimwambia yule mtu wa kutisha. "Basi nenda kafungue mvua! jioni
yake siku hiyo tambiko la mvua lilifanywa na kesho yake lile jitu lilifunga safari kwenda porini
kufungua mvua. Baada tu ya jitu hili kufungua mvua ilinyesha mfululizo siku saba na ardhi ikajaa
54
maji kila mahali. Baada ya kuona hivi raia wakapatwa na wasi wasi. Basi mzee Muhongola alikwenda
kwa Kutukutu na kumwambia kuwa mvua sasa zinaharibu mashamba ya watu. Kutukutu akaliambia
hili jitu likafunge ile mvua ili ipungue watu wapate nafasi ya kulima na kupanda. Mvua ilifungwatena
na jitu hilo hilo na watu wakapata nafasi ya kupanda mbegu shambani mwao.
UCHAWI
Uchawi ni imani ambayo binadamu huwa nayo kuhusu utaalam wa kufanya mambo kwa njia ya
siri. Katika nchi ya Wasagara uchawi uliogopwa sana na mtu yeyote aliyeonekana na uchawi alikuwa
ni adui mkubwa sana. Kwa jumla wachawi katika vijiji walikuwa wanatafuta visa ili waweze
kuwadhuru watu. Na zaidi ya hayo uchawi ulikuwa mara kwa mara ni wa biashara, yaani watu
waliofanya uchawi walifaidika kwa kupata vipesa kidogo au kupata mbuzi.
Kwa kawaida mtu alipofariki, sababu ya kifo chake ilitafutwa na iwapo kulikuwa na mtu
aliyeshukiwa kuwa katenda kitendo hiki kibaya basi mnong'ono uliweza kusikika wakati wa kilio na
habari zilienea upesi sana kuwa mtu aliyetenda kitendo kile ni fulani. Siku ya kuondoa matanga
wanakijiji walifika matangani na kusema kwa watu wote waliohudhuria matanga hayo kuwa ingawa
walikuwa wanamaliza matanga, lakini mtu fulani ndiye kafanya kitendo kile kibaya. Na sasa wazee
waliamua hapo hapo kumwuuliza jamaa anayeshukiwa kumtendea marehemu uchawi. Lakini huyo
jamaa mtenda mabaya alikataa kabisa kuhusu sababu ya kufariki kwa marehemu. Alisema kuwa
hana habari yoyote kuhusu uchawi, wanakijiji waliwachagua wajumbe wawili waende kwa mganga
wakapige ramli. Waganga mafundi wa kupiga ramli walikuwapo na kusema kweli walikuwa mafundi
sana wa kupiga ramli. Kama Wasagara wenyewe wanavyoelewa hao waganga walikuwa hawakosei
sana katika kazi zao hizo. Mganga alitazama ramli yake na kumtaja mchawi aliyemwua marehemu.
Wajumbe baada ya kusikia hivi hurudi nyumbani kijijini kwao na kutoa taarifa ya ujumbe wao na
kuwaeleza wazee wote kuhusu ramli ya mganga. Mchawi adhaniwaye kuwa ndiye aliyefanya tendo la
kuua huwapo wakati habari hizi zikielezwa. Basi kila anapoulizwa na mchawi hukataa kabisa kuhusu
kitendo hiki. Ujumbe hutumwa kwa mganga na katika msafara huu huwamo yule mchawi ili
akajionee yeye mwenyewe kuhusu ubaya wake. Na iwapo bado mchawi anakataa mbele ya yule
mganga, basi mganga hutafuta dawa ambayo huchemshwa sana na chungu hicho chenye dawa
inayochemka hutiwa kipande cha chuma au kengele na kuchemshwa sana. Baada ya kuchemsha
sana vitu hivi dawa na kengele ya chuma, kila mtu huambiwa kuopoa kile chuma kwa kutumia
mikono mitupu bila chombo cha kuopolea na kitendo hiki hufanywa kwa zamu. Inasemekana kuwa
yule mtu ambaye hana hatia ya uchawi huopoa kile chuma kilichochemshwa bila kuungua, lakini
mtu ambaye ndiye mchawi aliyetenda maovu, hudhurika sana kwa kuunguzwa mkono, na hapo hapo
kukubali kuwa ndiye aliyefanya kitendo cha uchawi na kwamba kamwua marehemu. Baada ya
kuthibitisha yote hayo, ujumbe hurudi kijijini kutoa habari kuwa mchawi kapatikana. Kablaya kurudi
nyumbani kwao mchawi hunyweshwa dawa pamoja na wenziwe walio katika ujumbe huo na wote
kunyolewa hywele zote na kupakwa dawa utosini pao iii wasifanye uchawi tena - hasa yule mchawi.
Basi mashauri hufanywa pale kijijini, yule mchawi huambiwa na wanakijiji kuwalipa jamaa za
marehemu mbuzi kumi au kumi na tano. Baada ya kufanya hivi, yule mchawi hushikana mikono na
jamaa za marehemu kuonyesha kuwa sasa uadui hakuna tena na kwamba hapatakuwepo na
uhasama wowote tena kati ya huyo mchawi na jamaa za marehemu.
DESTURI ZA WASAGARA
1. Wasagara walikuwa na desturi ya kula ugali kuanzia chini na kuendelea. Si desturi kwa
Msagara kula ugali kutoka juu yake. Mtu akifanya hivyo atakuwa amekiuka desturi yao.
2. Kama chakula kimefunikwa, bwana hana ruhusa kukifunua mpaka mama au watoto wake
ndio wanaweza kufunua chakula.
55
3.
Mtu akipiga hodi mara mbili hivi na Kama hakuna jibu, hana ruhusa kuingia ndani.
4. Bwana yeyote wa Kisagara hana ruhusa kufunua funua kitanda chake anacholala na mkewe.
Mkewe tu ndiye anayeweza kufunua funua kitanda hicho.
5.
6.
Wakati wa kula ni mwiko kuvuta sahani ya chakula.
Kwa Msagara ni mwiko kwake kumfyonya mtu yeyote yule.
7. Wakati wa kula chakula, wanaume wote walikuwa wanakula pamoja na wanawake wote pale
kijijini walikuwa wanakula pamoja.
CHAKULA CHA WASAGARA
Chakula cha Wasagara ni kama hiki hapa chini: — ( i )
Ugali wa mtama na Bwembwembela.
nn
Maboga. ( i i i )
Safe (kunde). ( i v )
Mlenda(hombomgunda). ( v )
Derega. ( v i )
Mwage. ( v i i )
Tele. (viii) Kikundambala - Mwamizi Mulungu. Maana yake mboga hii yajiotea
yenyewe na Mungu tu
ndiye anayeiotesha. (ix) Sunga ambacho kiungo chake uf uta.
MWANAMKE MWENYE MIMBA
(i)
(ii)
(iii)
Mwanamke mwenye mimba alikula chochote kile ambacho roho yake ilitaka.
Bwana alikatazwa kumpiga mkewe wakati kama huu.
Mama mja mzito alitembea kwa tahadhari kubwa kwa kuogopa watu waliokuwa wamechanja
dawa mbaya zinazodhuru mimba za watu.
(iv)
Mikuwa ni mwiko kwa mama mja mzito kutembea na wanaume wengine. ( v )
Mali
kadhalika ilikuwa ni mwiko kwa bwana ambaye mkewe ni mja mzito kutembea na
wanawake wengine.
MTOTO
Mtoto anapozaliwa hunyweshwa maji ndipo uji ufuate baadaye. Kama maji hayapiti kwenye koola mtoto, basi yaaminiwa kuwa mtoto huyo labda ni wa kufa au hakukomaa sawasawa. Mtoto
anafunzwa kuanza kutembea na mafunzo hayo yaambatana Sana na nyimbo maalum ambazo
zilitungwa kwa madhumuni hayo. Mfano wa nyimbo hizo ni kama wimbo huu hapa chini: —
"—Do yaya do, Maikoka do, na kadhalika."
Maana yake ni:— "Pengine mimi nitaondoka, Afadhali ujisaidie."
Katika kufunza mtoto namna ya kusema na kutamka maneno, wazazi wa Kisagara hutumia zaidi
maneno haya hapa:
Wize mwisukulu, Wize
mzangazanga, Wize
mbena, na kadhalika.
Jukumu kubwa la mama mzazi ni kumwelekeza mtoto wake ill mtoto huyo afanye matendo kama
anavyoelekezwa na mama. Iwapo mtoto katika kuchezacheza mchangani kazingirwa na Nyoka aitwaye "Moma", katika lugha ya Kisagara ikiwa na maana ya "Kifutu", kama mzazi kaona kuwa mtoto
56
wake kazlngirwa hivyo na huyo nyoka, hana ruhusa ya kupiga kelele kuwa mtoto wake labda
..amekufa. Kitu anachotakiwa huyo mzazi kukifanya ni kunyamaza kimya halafu huyonyoka ataandoka
mwenyewe bila ya kumdhuru mtoto. Lakini kama mzazi kapatwa na woga na kupiga kelele "Mtoto
wangu amekufa jamani" anapoona mtoto wake kazingirwa na "Moma", basi huyo "Moma" atamwuma huyo mtoto na kwa vyo vyote vile yule mtoto atakufa. Kwa hiyo Wasagara hawapigi kelele
iwapo mtoto wao kazingirwa na huyo "Moma" na "Moma" hawezi kumwuma mtoto kama mzazi wake
hakupiga kelele.
JANDO
Watoto walikwenda jandoni kuanzia umri wa miaka kumi na kuendelea. Wazazi wa kila mtoto
walikaa chini na kuamua lini mtoto wao aende jandoni. Baada ya wazazi wa kila mtoto kuamua lini
mtoto wao aende jandoni, ndipo walipofanya mkutano na wazazi wa watoto wengine ili kuamua kwa
pamoja lini watoto wao katika kijiji chao waende kuhudhuria mafunzo ya jando. Jumla ya watoto
wanaotakiwa kwenda jandoni itategemea wako watoto wangapi pale kijijini ambao wamefikia sifa hii
ya kwenda jandoni. Watoto zaidi ya hamsini wanaweza kwenda jandoni mradi wanazo sifa
zinazotakiwa. Muda wa kukaa jandoni ni kutoka mwezi mmoja au zaidi, na mara nyingi mahali pa
kuendeshea mafunzo ya jando huwa ni mbali kidogo na mji wao au kijiji chao. Wakiwa jandoni
hufundishwa elimu ya kuwatayarisha ill waje waishi katika jamii ya Kisagara bila taabu na wasiweze
kuishi maisha kinyume cha maisha ya Wasagara. Baadhi ya mafunzo yanayotolewa wakiwa jandoni
ni: Watoto wanafundishwa kuwa kutukana watu ni makosa, kutukana wakubwa ni mwiko, kupita
mahali anapoogea mama au mtu yeyote mkubwa ni marufuku. Mtoto hatakiwi tena kupita au kupitia
mahali hapo. Mtoto anapoamkia wakubwa lazima kwanza apige magoti, akishapiga magoti yake,
aondoe kofia yake, halafu ndipo aseme "shikamoo". Anapotaka kuingia ndani ya nyumba ya mama
yake lazima abishe hodi naakiambiwa "karibu", yampasa asimame ukumbini tu. Haruhusiwi kuingia
ndani ya chumba wazazi wake walimo sababu yake kubwa ya kufanya hivi ni kwamba hawezi kujua
hao wazazi wake wanafanya nini ndani. Kwa jinsi hii, mtoto yampasa kusimama ukumbini tu, na
wazazi watamwambia la kufanya au yeye atasema shida yake iliyomleta.
Endapo mtoto kavunja sheria au kanuni yamafunzo yake baada ya kumaliza mafunzo, basi
baba anaweza kumchukulia hatua kali mtoto wake ya kumrudisha tena kwa mwalimu wake wa
zamani (mwalimu wa jando). Yule mwalimu akishaona hivi, basi atasema hivi: "Lusimbi nitamwona
tena," huku akitia alama vumbini kwa kutumia kidole kimoja cha mkono wake wa kulia - hasa
kidole cha shahada, halafu hufanya alama kuzunguka shingo yake na kuapa. Neno "Lusimbi"
maana yake ni dawa ya vidonda iliyotumika kuponyeshea vidonda baada ya kutahiriwa. Dawa
yenyewe ilikuwa vumbi la udongo ambalo ndiyo ilikuwa dawa ambalo lilipakwa kwenye vidonda
vya mtoto aliyetahiriwa. Basi yule mtoto ambaye alimaliza mafunzo yake siku nyingi na kufaulu
masomo yake, akivunja au kufanya makosa katika maisha yake ya kawaida, basi anaweza
kurudishwa na baba yake kwa mwalimu wake tena. Yule mwalimu humtia yule mtoto katika kundi
la wanafunzi wajifunzao upya na huyo mtoto mkosaji huanza upya tena kujifunza masomo ambayo
alikuwa ameyamaliza.
Watoto wanapokuwa jandoni wanalala uchi bila chochote cha kujifunika na hupelekwa mtoni
saa kumi na moja kuoga maji ya baridi. Kusudi kubwa la kufanya hivi ni kutaka kuwakomaza watoto
Hi waweze kuwa wakakamavu wa maungo na waweze kujitegemea katika maisha yao ya baadaye.
Zaidi ya hayo, watoto hutandikwa viboko kama wamefanya makosa.
SIKU YA KUTOKA
Siku ya kutoka inapowadia, habari hupelekwa majumbani ikieleza ni lini watoto watatoka
jandoni na hasa siku ambayo ilifaa sana kwa sherehe ya kutoka jandoni ilikuwa siku ya Jumapili.
Baada ya kufahamika siku hiyo, wazazi wote kijijini walitayarisha mtama kwa wingi na uwanja
mkubwa ulitengenezwa kwa ajili ya sherehe hiyo na watoto wanaotoka jandoni hukaa kwa pamoja
hapo uwanjani na wazazi wao (akina mama tu) watafika mahali hapo na kukutana nao. Uwanja wa
shughuli hii waitwa uwanja wa "Mbilu" hapo hapo ndipo ngoma itakapochezwa. Wakati huo watoto
huvaa nguo rasmi iitwayo "Usambo" wa mbuyu, nayo huvaliwa kiunoni na kuzungushwa kichwani.
57
Siku ya Jumamosi akina mama hutayarisha unga wa mtama na nyama na kupikwa ili kuwa chakula cha
sherehe. Siku hiyo hiyo ya Jumamosi akina mama ambao watoto wao ndio wanatoka, kila mmoja
atamwita mtoto wake kwa zamu na kuita huko ni kama hivi: —
"Mwanangu longalonga nhulike", maana yake, "Mwanangu sema nikusikie". Mtoto wake
anapaswa kuitikia hivi: —
"Nabaha mai nabaha, maana yake "Niko hapa mama, niko hapa."
Mama yake akisikia sauti ya mtoto wake, basi hupiga kigelegele cha furaha kubwa kwa sababu
mtoto yupo na pili kamaliza mafunzo yake. Mtoto anaweza kufia huko huko jandoni, lakini mama yake
haambiwi kama mtoto wako amefariki, bali baba yake tu anaambiwa na mazishi yanafanyika kimya
kimya bila ya mama yake kujua. Mkewe haambiwi hata kidogo. Mama anaweza kupeleka chakula cha
mtoto wake huko jandoni hata kama mtoto amefariki kwa sababu hajui wala haambiwi. Ataendelea
kupeleka chakula mpaka siku ya kutoka watoto wote. Siku mama atakapojua kuwa mtoto wake hayupo
ni siku ya kutoka ambapo akina mama wanakusanyika na watoto pia hukusanyika, halafu akina mama
huita jina la mtoto wake. Iwapo mtoto wake haitikii, basi mama huondoka akifahamu kuwa mtoto
wake hayupo na kwamba mtoto wake kafariki. Basi mama ataondoka mahali hapo walipo watoto na
kurudi nyumbani bila ya kuonyesha huzuni yoyote. Pia siku ya Jumapili inayofuata ambayo ndiyo
siku kuu kubwa ya watoto wote atakuwapo kusherehekea na atawapikia chakula watoto wa wenzie kwa sababu katika mila za Wasagara watoto wa familia zingine kijijini wanafikiriwa kama ni watoto wa
kila mmoja pale kijijini wala si watoto wa yule tu aliyezaa. Ni watoto wa kijiji kizima na mama yeyote au
mzazi yeyote kijijini anaweza kuwatuma watoto wowote wam-fanyie kazi na watoto hawawezi kukataa.
Mtoto yeyote anayetumwa kazi na mzazi yeyote ambaye hakumzaa akikataa, anaweza kupewa adhabu
kali kabisa na yule anayemtuma. Kwa hiyo kwa desturi ya Wasagara mtoto yeyote kijijini ni mtoto wa
mzazi yeyote kijijini pake.
Nyama na unga vinavyoletwa pale vyapikwa pamoja ili watoto wale kwa pamoja siku hiyo ya
sherehe. Siku hiyo ya Jumapili kunakuwa na ngoma kubwa sana na watu hucheza sana ngoma hiyo.
Akina baba hali kadhalika akina mama hushiriki katika kucheza ngoma hiyo. Zama hizo ngoma hii
ilichezwa toka saa kumi na mbili ya jioni ya Jumamosi hadi saa kumi na mbili ya Jumapili bila
kupumzika. Baada ya hiyo Jumapili, wazee fulani waliamua kuwapeleka watoto wao kama kumi hivi, kwa
mzee mmoja hivi kwa ajili ya kuonyesha furaha waliyonayo wale wazazi wa watoto hao. Basi mzee
huyo aliyepelekewa watoto hao alishinda nao siku moja na kulala nao usiku mmoja halafu asubuhi
yake aliwarudisha hao watoto kwa wazazi wao. Lakini watoto wengine walirudi kwa wazazi wao siku
hiyo hiyo ya Jumapili.
Baada ya kumaliza mafunzo ya Jandoni mtoto lazima aandamane na baba yake katika kila
shughuli anayofanya, ili naye ajifunze ije imsaidie katika maisha yake ya baadaye. Shughuli hizi ni
kama kujenga nyumba, kulima mashamba na kadhalika.
WAKATI WA POSA
Mtoto akikua na kubalehe, basi baba ya mtoto huzungumza na mkewe na kumwambia kuwa
mtoto wao amekua afadhali achumbiwe msichana. Basi baba yake huchukua jukumu la
kuangazaangaza macho huku na huko kutafuta mtoto wa kike ambaye anafaa na mwenye ukoo wa
heshima. Baada ya kumpata msichana anayefaa, baba mtoto huenda kwa baba ya msichana na
kumwambia kuwa anataka amchumbie mtoto wake binti yake. Basi baba ya binti akikubali, akina
mama - mama ya mvulana na mama ya msichana hukutana peke yao na kuzungumza juu ya jambo hili
na kukubaliana. Baada ya hapo, wazazi wa msichana humwambia binti yao mchumba wake ni nani,
na pia wazazi wa mvulana humwambia mchumba wake ni nani. Baada ya hayo, msichana
anapelekewa mkufu wa kuvaa mkononi na mama ya mvulana kuonyesha kuwa msichana huyo
kafungwa ni wa mtu, hayuko huru. Baada ya msichana kuvikwa mkufu huo na mama ya mvulana,
hupelekwa "Mbopa mkoa" yaani kitambi, kwa mama ya msichana ikiwa ni zawadi yake - shukrani kwa
taabu aliyopata wakati wa kumbeba na kumchafua. Baada ya "mbopa mkoa" kupelekwa, ndipo posa
yenyewe yapelekwa kwa wazazi wa msichana. Mbuzi hupelekwa na kima cha juu sana cha posa
58
ni mbuzi watano. Baada ya hapo, msichana hupelekwa moja kwa moja kwa wazazi wa mvulana
kufunga ndoa na kufanya arusi.
Siku hizi, baada ya kupelekwa posa, Sheikh anaitwa na baba ya binti anatoa idhini kama
amekubali. Basi Sheikh hufukiza ubani na kitezo huku baba ya mtoto hupiga magoti - na ndoa
hufungwa kwa kufuata desturi za Kiisiamu au Kikristo.
Iwapo mvulana hana nyumba siku ya arusi, mvulana atakaa na mkewe katika nyumba ya babu
yake, na kama nyumba ya babu yake haipo, basi nyumba yoyote ya jirani ambaye wanaelewana naye
itafaa mpaka wakati huo mvulana atakapojenga nyumba yake mwenyewe. Na iwapo haiwezekani
kuipata nyumba hiyo basi baba ya mvulana humwachia mtoto wake, chumba kimoja ill waweze
kukaa mpaka watakapojenga nyumba yao.
KUVUNJIKA NDOA
Iwapo ndoa ilivunjika, bibi hampendi bwana, na bwana hampendi bibi, basi kilitafutwa kibua
chochote na kibua chenyewe kilikeketwa vizuri na baba ya mvulana halafu akawapelekea wazazi wa
msichana mbele ya watu na kusema, "Haya chukua kibua, binti yenu simpendi tena". Kama kibua
hakikukeketwa vizuri (ambayo ndiyo talaka hasa ya jadi) basi kibua kilikataliwa kwa sababu
ilionyesha kuwa bado binti yao anapendwa na bwana. Lakini kama kilikeketwa vizuri basi talaka
ilikubaliwa. Basi matumizi ya kibua kwa jamii ya Wasagara yalikuwa ya maana sana. Talaka zote
ziliwekewa msingi na kibua.
MAHARI
Wakati wa kuvunjika ndoa mahari ingaliweza kuachwa yote kwa wazazi wa msichana bila ya
kurudishwa iwapo msichana alikaa vizuri na bwana yake. Mahari hayo huwekwa kama akiba ya
heshima ili watakapotaka kuposa mahali pengine waweze kukubaliwa upesi kama watu wenye
heshima na wasiokuwa na matata yoyote. Kuiacha mahari kwa wazazi wa msichana ilikuwa ni
mojawapo ya sifa maalum kwa ukoo wa mvulana. Wakati mwingine mahari inaachwa nusu tu na
nusu inarudishwa kwa sababu ya utumishi aliotumika kwa bwana yake. Basi baba ya mvulana
huamua kuwa nusu ya mahari irudishwe na nusu yake ibakie. Lakini iwapo wazazi wa mvulana
wamesikia kuwa huyo binti amemwacha mtoto wao kwa sababu kampata bwana mwingine, wazazi
wa mvulana huamua kurudisha mahari yote.
MSICHANA
Wakati msichana alipovunja ungo, wazazi wake walitangaza mji mzima kuwa binti yao kavunja
ungo. Sherehe ilifanyika kufurahia jambo hili. Mara baada ya hiyo sherehe, msichana aliwekwa
ndani kwa mafunzo maalum jinsi ya kuishi na bwana, heshima kwa watu, kazi za nyumbani, na
mambo mengine mengine mengi yanayohusu maisha yake ya baadaye na jinsi ya kuishi na bwana
yake. Wakati anapokuwa "ndani" msichana hufunzwa na waalimu wawili - mama yake na bibi yake.
Akiwa ndani, msichana hujipaka pumba ya mahindi iliyochanganywa na maji na kujisugua sana
mpaka ameiva vizuri kabisa.
Muda wa kukaa ndani ulitegemea nyakati au majira. Iwapo alivunja ungo wakati wa masika, basi
msichana aliwekwa ndani mpaka wakati wa kiangazi kwa sababu watu wote walikuwa na shughuli
nyingi za kilimo mashambani. Lakini iwapo alivunja ungo wakati wa kiangazi basi aliwekwa ndani
mpaka kiangazi kingine. Walakini muda wa kuwekwa ndani ulitegemea zaidi shughuli za wakazi wa
kijiji cha msichana huyo. Iwapo watu walikuwa na shughuli nyingi, basi msichana huyo aliwekwa
ndani kwa muda mrefu zaidi kuliko wakati ambapo shughuli zawanakijiji zilikuwa chache. Shughuli
za kilimo ndizo zilizotawala muda wa msichana kuwekwa ndani.
Wakati wa kutoka msichana huyo alikoshwa vizuri na alivikwa nguo nzuri nzuri, na alipambwa
kwa shanga na nguo mpya mpya alipewa na kuvalishwa siku hiyo. Ngoma zilichezwa sana ikiwa
sherehe kubwa sana kwa siku hiyo wakati msichana akitoka. Wachezaji wa ngoma hii hasa ni akina
mama ambao hushangilia mtoto wao kwa kutoka ndani. Akina mama walikuwa katika hali ya
kucheza kumzunguka mtoto wao na kumzingira kabisa hata akina baba huwa ni vigumu kumwona
59
huyo mwali mwenyewe alipokaa. Iwapo huyo mwali alikuwa ameposwa tayari, basi baadaya sherehe
hiyo yule mwali hupelekwa kwa bwana yake moja kwa moja. Siku ya kutoka msichana huyo, ndugu
za mchumba wake wa klume huwapo kusherehekea kutoka kwa huyo mchumba wao wa kike.
Baada ya ngoma hiyo kubwa, siku ya pill yake msichana huchezewa ngoma ya ndani ya nyumba
tu, ngoma hiyo yaitwa "Goko" au Koko", yaani ngoma ya mafunda. Wanawake wengi huwapo wakati
wa ngoma hii ya ndani ya nyumba, na kila mwanamke wa maana hutoa mafunzo yake ya kumfunda
na kumfunza yule mwali kwa mara ya mwisho. Pia mama ya msichana huwapo wakati huo ill kutoa
mafunzo ya siri kwa mwali. Kwa mfano, mama mmoja hutoa mafunzo namna ya kupika, mama
mwingine hutoa mafunzo namna ya kucheza, mama mwingine hutoa mafunzo jinsi ya kutambua
shida ya bwana yake, nakadhalika. Hii ndiyo ngoma ya mwisho katikaelimu yake yote yule binti. Hli
ndiyo elimu yake ya kumfanya afaulu na kushinda mtihani wake wote. Siku hii ndiyo (graduation
day) siku ya kutoka.
Wakati msichana yumo ndani akihudhuria mafunzo mbali mbali kabla ya kutoka, wakati wa
kulala hujifunika mgololi na nguo moja ya kushindia. Chakula chake wakati wote huo wa kukaa
ndani ni nyama, kuku, maharagwe na chakula kinglne kllicho kizuri klzuri. Baada ya kutoka, na
iwapo huko aliko hafuati yale aliyojifunza wakati akiwa mwali, basi mwalimu wake huambiwa habari
hizi - hata kama ni mke wa mtu sasa. Basi mwalimu wake anangojea siku ambayo kuna mwali
mwingine ambaye ndiyo kwanza anahitimu mafunzo yake, humwita yule mwanafunzi wake wa
zamani ambaye hafuati na kutoitumia elimu yake vizuri na kumwambia aanze kufanya mazoezi upya
tena kama vile mwali anavyofanya ili ajifunze upya kabisa kwa maana elimu yake aliyopata zamani
haikumfaa. Basi huyo mwanamke huyarudia mafunzo yote siku hiyo ya sherehe ya mwali mwingine,
basi siku hiyo wanafunzi wanakuwa wawili. Baada ya kumaliza mafunzo hayo siku hiyo, basi
mwanamke huyo huruhusiwa kurudi kwa bwana yake ili akayatekeleze yale aliyokuwa hayafuati. Kwa
kuwa ni aibu sana kwa mwanamke aliyeolewa kurudi tena kujifunza elimu ya wasichana
wanaotayarishwa, basi hujitahidi sana ili aitumie elimu yake hiyo vizuri.
KIFO
Mtu mara anapokufa huzikwa mara moja - hata kama mtu kafa saa nne za usiku, lazima azikwe
mara moja wakati huo huo, tena huzikwa kimya kimya bila maneno yoyote. Baadaya kuzika, mtama
hutafutwa. Kuku au mbuzi huchinjwa. Iwapo marehemu alikuwa ameoa na kumwacha mke, na
kama huyo mama anataka kurithiwa na ndugu za marehemu basi atarithiwa la kama hataki
atarudishwa kwao. Na iwapo wapo ndugu za marehemu ambao wangependa kurithi mwanamke huyu
mfiwa, basi pale kilioni wakati wakitoa sadaka mtani humwambia mfiwa kuwa kuna mnong'ono wa
maneno wa kutaka kumrithi na kuambiwa kuwa anapewa uchaguzi wa kumchagua yupi ndugu ya
marehemu atafaa kumrithi yule mjane, na wakati wote huu yule mjane hasemi neno ila huitikia tu
kwa kutumia kichwa. Basi baada ya kutolewa taarifa hii mtani huchukuwa kijiti nakukikata vipande
kwa kufuatana na jumla ya ndugu za marehemu. Mjane huletwa mbele ya wanakijiji huku akiwa
amefunikwa nguo mwili mzima. Mtani huanza kusema, "Bwana Juma kijiti chake ni hiki". Yule mama
huchukuwa kijiti cha Juma na kukitupa chini iwapo hampendi huyo Juma, Halafu kinatolewa kijiti
kingine cha Hamisi, na mjane huchukuwa kile kijiti na kukitia kifuani mwake iwapo yule mama
anampenda Hamisi awe ndiye mume wake mpya baada ya marehemu. Mara akifanya hivyo, basi
vigelegele vyapigwa, na yule ndugu ambaye kijiti chake kimekubaliwa, hushikwa mkono na
kupelekwa mahali pale mama amekaa na kukatishwa hapo. Mwenye shughuli ya kuongoza sherehe
hii ni yule mtani wake. Sherehe ya arusi hufanyika, na yule jamaa huonywa na kukemewa sana ili
aweze kuwatunza vizuri watoto wa ndugu yake marehemu.
Wasagara walipozika maiti walitumia magome ya miti ambayo yalitengenezwa vizuri kama
nguo, na yakatumika kuzikia maiti. Wakati huo ngoma za kuomboleza kifo zilichezwa sana.
60
UFUNDI
Wasagara wanao ufundi wa aina mbali mbali, kwa mfano, Wasagara wana ufundi wa kuchonga
vitanda, wana ufundi wa kuchonga vigoda, mipini ya mashoka na visu, wana ufundi wa kuchonga
vinu, miiko, na kadhalika. Pia Wasagara wana ufundi wa kuvua samaki kwa kutumia migono, nyavu
na ndoano. Vile vile Wasagara wana ufundi wa kutengeneza vilindo vya kuhifadhia nafaka mbali
mbali, wanachonga mizinga na wanafinyanga vyungu wanasuka virago na kufua vyuma na
kutengeneza mashoka na miundu (sengo).
UTANI WA WAKAGURU NA WASAGARA
BABA NA WANA
Baadhi ya Baba na wana kuna wakati wa kutaniana na wakati huo ni baada ya baba kufurahishwa
na kitendo cha mwanawe. Kama kupatiwa pombe, nguo, nyama au tumbaku. Baba huyo anaweza
kumtania mwanawe kwa kumfanya kama rafiki yake. Anamtania kwa kumpa majina ya kiutani utani
kuwa yu Sultani "Mndewa" au Mkombozi - "Muonyi". Majina hayo anayomwita mwanawe ni kwa
wakati ule ule wa ukarimu wake aliyomtendea. Majina hayo ijapokuwa ni ya utani yaani kilemba cha
ukoka, lakini yanampa mtoto moyo mkuu wa kumsaidia baba yake kwa ajili ya ule utani wa kumtaja
kwa majina ya vyeo.
Vile vile mwana anaweza kumtania baba yake iwapo baba huyo amemkaribisha kunywa pombe
au kumpa tumbaku wakati huo huo tu mwana anaweza kumtania baba yake kwa maneno ya kiutani
utani kumwita yu rafiki yake.
Wakati fulani utani unatumika sana jandoni kati ya baba na mtoto iwapo mtoto wake
katahiriwa. Anaambiwa kuwa baba yake ni rafiki yake au ni mtani wake kwani umefanana naye kwa
viungo vyenu vya kiume. Kwa hiyo kutoka katika rika hilo mvulana anajiona ana uhusiano na baba
yake kwa utani hasa wawapo ni wawili tu.
Kwa jumla watoto na wazazi wao wanataniana wakati wa kutendeana matendo mema ya
kiukarimu. Wanaambiana ni marafiki au ni watani. Wasichana vile vile wanataniana na mama zao
kwa ajili ya mambo ya kuvunja ungo. Wakati huo msichana huwa amefanana na mama yake kwa
mawaidha yakimaisha kwa kuvunja ungo, matukio ya miezi na mbinu za kushika mimba na malezi ya
watoto. Vile vile wanaweza kuvaa sare na kufanya kazi za namna moja wakawa ni wa namna moja
kwa kikazi na kwa utani.
MABABU, MABIBI NA WAJUKUU
Kwa kawaida hao ni watani hasa. Majina ya mababu na mabibi ndiyo majina wanayopewa
wajukuu wao. Wavulana hupewa majina ya mababu zao. Wasichana wanapewa majina ya bibi zao.
Wajukuu wana uhuru wa kuwatania babu na bibi zao. Ikiwa wana mapengo watawaita ni vibogoyo
bila ya kuambiwa wanafanya kosa kwa mababu na mabibi zao. Waona hiyo? Wajukuu wanaweza
kulalia vitanda vyao bila ya kukatazwa kwani wao ni watani wao.
VILEMBWE NA BIBI ZAO
Kwa kawaida vilembwe hawana utani na bibi au babu za wazazi wao isipokuwa babu zao ndiyo
waliyo na utani nao, kwa ajili ya cheo cha ubabu na ubibi. Vilembwe ni tabaka la nne kwa hiyo wao
hawana utani na mababu na mabibi wa wazazi wao, ila tu wanaweza kuwatania ikiwa kuna sherehe za
pombe na furaha za ngoma.
61
SIKU ZA UTANI
Kwa kawaida siku ya kwisha kilio na siku ya kuzika ndizo siku maalum za mambo ya
utani. Siku hizo utani hauwi baadhi ya watu wa familia yao ila utani unafanywa na watu wa
ng'ambo ya ukoo. Kwa mfano waliyofiwa kama wana ukoo wa Wampene huwa wenye ukoo wa
mpakani mwao waitwao Wasongo ndiyo watani wa kifo. Ikiwa hakuna mtani wa ukoo wa
Kingambungambu kama akiwapo Mnyamwezi au Msukuma anaweza kuwa ni mtani wa kifo
hicho.
UTANI KIFONI
Mtani kazi yake kifoni ni kutoa maneno yenye porojo ili wenye huzuni ya kifo wasisimke
kusahau huzuni ya kifo. Wakati mwingine anamwambia marehemu analima au anawinda au
ameonana na huyo mtani na kumwagizia mambo fulani fulani. Hizo ni baadhi tu za porojo za
watani ili watu wacheke.
MSHAHARAWA MTANI
Watani wanapewa mshahara wa kuku au vichwa vya mbuzi waliochinjwa pale kifoni
iwapo wenye kifo watawatania. Watani watasomba kuku, mbuzi, vyakula na nguo hata vitanda
bila ya kuambiwa wamefanya kosa.
Kwa kawaida Wasagara na Wakaguru wanathamini sana utani kwa shughuli za vifo. Kwa
hiyo Wasagara na Wakaguru wanafurahia sana maneno yenye kuwachekesha na ikiwa
yamewakolea, basi yanatekelezwa vyema.
MICHEZO YA WASAGARA
Kwa jumla michezo yote ya kijijini walishirikiana vijana na wasichana. Michezo ilichezwa
mara baada ya kukusanya mavuno mashambani. Michezo hiyo ilihusu ujengaji wa vibanda
vidogo vidogo vya majani ambavyo wenyewe huviita (vibunda). Vibanda vilijengwa kwa manyasi,
majani na mabua. Wavulana walishiriki sana katika ujenzi na wasichana walishugnulika na
utayarishaji wa vyakula katika vijumba hivyo. Michezo kama vile kasimbago; michezo ya
kujificha na kutafutana, michezo ya mbio na michezo ya "mafulugwa" - mchezo unaohusu
kupanga miguu mmoja juu ya mmoja na kuupangua - sehemu nyembamba ndipo kamba
hupitishwa na mchezaji huinua kamba juu na kupishana kati ya mkono na mkono - ikianza
kuzunguka vizuri hutupwa juu na kudakwa tena.
Michezo mingine ya kuimba hufanywa wakati wa mbalamwezi. Vifaa vilivyotumika ni
miti; mabua ya mahindi, mtama- udongo, mawe na kadhalika.
KILIMO CHA JADI CHA WASAGARA
Kilimo cha jadi cha Wasagara kilikuwa na faida sana kama wanavyoona Wasagara
wenyewe. Zamani baada ya mvua kunguruma, mkuu wa mji alitoka nje na kukitangazia kijiji
kizima kuwa ni juu ya kila mwanakijiji kutayarisha mashamba mapema kabisa kabla ya mvua
kuanza kunyesha. Kila mtu aliambiwa kutayarisha mashamba mapema kabisa ili mvua
zinyeshapo, wakulima wapande tu kwa sababu mashamba yametayarishwa kabisa kwa hiyo
ilikuwa ni jukumu la mkuu wa Kijiji kuhakikisha kuwa kila mtu katika kijiji alikuwa ametayarisha
shamba lake mapema kabla ya mvua kunyesha. Mkuu wa Kijiji huyo alisema "Humbusa",
yaani "Tuanze kulima wakulima." Katika kuanza kulima kwenyewe kulianzwa kama hivi:—
Kwanza mtani alitafutwa kama vile Mnzelu au Mnyakilo ambaye alichukua jembe, na kwenda
mahali ambapo wanakijiji waliamua kulima mashamba yao, huko huyo mtani alianza kukwatua
nyasi mahali ambapo ni njia panda au kama huko kwenye mashamba hakukuwa na njia
panda, lakini palitafutwa mahali popote penye njia panda na huyo mtani wao.
62
akafanya sherehe ya kukwatua nyasi ikiwa ndiyo sherehe ya kuanzisha rasmi kulima mashamba yao
hao wanakijiji waliohusika. Kila kijiji cha Wasagara kilifanya hivyo. Sherehe hiyo ya kufungua kulima
ilihudhuriwa na kila mwanakijiji wa kijiji kilichohusika. Baada yasherehe hiyo ya uanzishaji rasmi wa
kulima mashamba katika kijiji basi watu wote, wake kwa waume waliyavamia mashamba yao na
kuyalima kwa pamoja.
Wasagara walikuwa hawalimi mtu mmoja mmoja, bali walilima pamoja kama kijiji. Kila familia
ilikuwa na mashamba yake, lakini kulima kulifanywa kwa pamoja kwa kufuata zamu. Sababu ya
kufanya hivi ilikuwa kwamba kwao Wasagara mvua ilikuwa kama mgeni ambaye siku ya kuja kwake
nyumbani haikujulikana hata kidogo bali hutokea wakati wowote. Kwa jinsi hii, iliwalazimu
Wasagara waweze kulima pamoja kwa kufuata zamu mpaka kila shamba la kila mwanakijiji
limelimwa. Mvua ni kitu ambacho hutokea ghafla tu bila kutazamiwa kwa hiyo kwa kulima pamoja,
Wasagara waliweza kumwahi huyo mgeni wao "Mvua."
Walianza kulima shamba la Mkuu wa Kijiji na baada ya kumaliza kulima shamba la mkuu wa
Kijiji ndipo walipoanza sasa kulima shamba moja baada ya moja la kila mwanakijiji. Natunaposema
shamba la mwanakijiji, hatuna maana ya eka moja au mbili hivi, bali ni zaidi ya eka 14 au 15 hivi,
ndiyo shamba la mtu mmoja. Na zama hizo Wasagara walikuwa na ardhi kubwa na safi yenye rutuba
nyingi sana. Kande zilipikwa ill ziliwe wakati wanakijiji wakilima. Kande hizi zilikuwa za
kuwapotezea njaa tu lakini hazikuwa ndiyo chakula chao maalum kilicholiwa baada ya kazi ya
shamba. Pia pombe ilinywewa baada ya kazi ya shamba na mara kwa mara mwanakijiji mwenye
zamu ya kulimiwa shamba siku hiyo ndiye alikuwa na jukumu la kupika chakula cha wafanyakazi.
Wakati wa kulima wanakijiji waliberega kwanza (kukwatua). Wakati huo huo watu wengine
hufuata nyuma wakitapanya (broadcasting) mihindi pamoja na udongo. Mihindi hii ni ya kuota upesi
upesi kabla hawajaanza kupanda rasmi mbegu za mahindi zingine hapo baadaye. Makusudi ya
kufanya hivyo ni kwamba mihindi hii inayotapanywa wakati wa kukwatua ardhi ni kutaka kupona njaa
maana itaota upesi sana na wanakijiji wataepukana na baa la njaa iwapo mihindi mingine
inayopandwa baadaye itakuwa bado kukomaa. Kulima kwa ushirika ndiyo kilimo cha jadi cha
Wasagara. Walikuwa hawajapata kulima kila mtu mmoja mmoja, bali jadi yao kulima kwa ushirika,
na tena mtu yeyote aliye na afya yake timamu ni lazima atoke kwenda kulima labda awe mgonjwa
hapo husamehewa. Pia mtu mvivu hupimiwa ngwe yake mwenyewe ambapo wanakijiji wengine
hulima pamoja kwa furaha na vifijo. Ikiwa yule mvivu hakumaliza ngwe yake aliyopimiwa kwa sababu
ya uvivu wake, wanawake wote wa kijiji chake humcheka na kusema hafai kuwa mwanaume kwa
sababu ya uvivu. Basi Wasagara waliogopa sana kuchekwa na wanawake kwa hiyo walijitahidi sana
waweze kufanya kazi kwa bidii ili wasichekwe na wanawake jambo ambalo linashusha hadhi kwa
wanaume wa Kisagara. Pia Wasagara walikuwa wanalima pamoja, wanaume na wanawake. Kwa jinsi
hii, wanaume kuonekana mvivu na kupimiwa ngwe yake ambapo wanawake walionekana ni wenye
bidii ilikuwa ni adhabu kali kabisa isiyopimika. Kwa hiyo, wanaume wengi wa Kisagara walijitahidi
sana wasionekane wavivu mbele ya wake zao.
Wakati wa kulima, Wasagara waliimba nyimbo za kuwatia nguvu wakulima (work songs). Mfano
wa wimbo wa kulimia ni kama huu hapa: —
"Wakulu mulimile hoi, Manye
wao walimile hoi, Manye wao
walimile kutalitali".
63
Maana yake, "Simameni mbali msije mkakatana mnapolima." Mali kadhalika waliweza kuutumia
wimbo huu wakati wa kuvuna mazao yao na nyimbo nyingine nyingi. Wimbo mwingine wenye
mafunzo mazuri ni kama huu hapa chini. "Kuliga kolojo uhwilehi?" Maana yake, "Unamtukana
mjomba wako unamtumaini nani?" Kwa sababu, mjomba ndiye aliyekuwa anathaminiwa sana kwa
sababu ya urithi, wapwazake walimwogopa na kumheshimu sana mjomba.
Zana walizozitumia katika kutayarishia mashamba yao ni Sengo (Mundu), mashoka na
majembe. Mashoka na Miundi ilitumika kwa kufyekea vichaka na miti lakini majembe ndiyo
yaliyotumiwa kwa kulimia. Majembe yao ya "Msuka" yalikuwa kama plena inavyoonyesha hapa
chini: —
Mti ulichongwa vizuri sana kwa urefu uhaotakiwa halafu, jembe lililotengenezwa na mhunzi
baada ya kuchimba chuma na kukiyeyusha motoni, lilichomekwa katika mpini kwa kutoboa tundu
sehemu ya mviringo ya mpini - hasa kwa kutumia chuma kilichochomwa motoni kwanza.
Katika kutengeneza majembe, kwanza chuma chenyewe kilichimbwa toka ardhini na udongo
wenye chuma ulipatikana huko Mdukwi sehemu ambayo iko katika Wilaya ya Kiiosa na mpaka sasa
udongo hup wa chuma unapatikana huko. Wasagara walipogundua udongo huu wa chuma,
wakaanza kuchimba na kuukusanya na halafu kuyeyusha. Vifaa vilivyotumika katika kuyeyushia
hicho chuma ilikuwa ni kuni nyingi ambazo zilipatikana kwa wingi sana katika nchi ya Usagara zama
hizo. Baada ya kukichoma chuma hicho basi chuma safi kikatoka, na chuma kisichofaa kikatupwa.
Kile chuma safi kikatengenezwa tena katika zana mbalimbali kama vile majembe, mundu na
mashoka na kadhalika. Mipini safi ya kutengenezea majembe yao ilitengenezwa toka miti ya mipingo
ambayo ilipatikana kwa wingi nyakati hizo.
Wasagara waliweza kugundua udongo wenye chuma kwa kuangalia chembechembe zake
ambazo zinametameta kama vile chembechembe za Ulanga (Mica). Basi baada ya kuziona chembechembe hizo, Wasagara waliamua kuchimba chuma hicho ili kiwafaidie katika shughuli zao za
ufundi mbalimbali.
Vifaa walivyotumia katika kuchimbia chuma ni mawe yalichongwa kama majembe. Kabla ya
kuanza kuchimba chuma chao, walichukua majani yaitwayo "Hoza" na wakayafikicha, na baada ya
kuyafikicha, walinyunyiza maji yake juu ya mahali pale walipotaka kuchimba chuma chenyewe ili
kupapooza pasitokee shari yoyote wakati wa uchimbuzi wa chuma. "Hoza" ni dawa ambayo
inatumika kwa mambo mengi ili pasitokee shari au mkosi wowote. Dawa hii yatumika kunyunyizia
mtu anapokuwa amefariki dunia.
64
Kilimo cha Wasagara kilifanyika wakati wa kiangazi na wakati wa masika. Wakati wa kiangazi,
mto wao maarufu sana Mkondoa uliwaletea manufaa mengi sana Wasagara. Mto huu ulikuwa bado
kuchimba sana bonde lake na ulikuwa na matete na magugu mengi sana katika kingo zake. Wakati
ulipofurika maji yake yalisambaa na yalipindukia kingo zake na baadaye yakarudi tena katika njia
yake wakati wa kiangazi huku yakiacha unyevu unyevu na mbolea nyingi sana katika sehemu za
mashamba yaliyokuwa yakilimwa kandokando ya mto huu. Basi Wasagara walilima sana mazao
rnengi wakati huu na kuweza kupata mazao bora licha ya kupata mazao ya wakati wa masika. Kwa
hiyo, baa la njaa katika nchi ya Usagara ilikuwa shida kuwakabili.
Kupanda mbegu shambani Wasagara walipanda pamoja wake kwa waume, kama walivyofanya
katika shughuli za kulima mashamba yao na kilimo chao maarufu sana kilikuwa ni Sesa. Na kupanda
mbegu walianzia shamba la Mkuu wa mji au Mkuu wa kijiji halafu na kuendelea kupanda mbegu
katika mashamba ya wanakijiji wote. Wakati wa kupanda, walichanganya mbegu za mihindi na
mbegu za mtama katika shimo moja. Mtama uliota na mhindi ukatoka katika shimo hilo hilo moja na
walitumia majembe katika kupanda mbegu mashambani. Njia hii ya kupanda mbegu za aina mbili
tofauti katika shimo moja ilikuwa na manufaa sana. Kwanza mbegu zina uwezo unaotofautiana
katika kupambana na wadudu waharibifu, kwa hiyo iwapo mbegu za aina fulani zitashambuliwa na
wadudu mbegu za aina nyingine zitabakia, kwa hiyo mkulima hatapata hasara ya jumla, atapata
mimea kutokana na aina nyingine ya mbegu. Pili, faida nyingine za mbegu zachukuwa muda
mfupi sana kuzaa mazao kuliko mbegu za mimea mingine. Kwa hiyo mkulima atazidi kupata mazao
fulani wakati mazao mengine yanaendelea kukomaa pole pole. Tatu mimea mingine yahitaji mvua
nyingi na mingine yahitaji mvua chache, kwa hiyo iwapo mvua zitakuwa chache mwaka huo,
mkulima atapata mavuno ya mimea yenye kutaka mvua chache tu. Nne, mkulima anapopalilia
shamba lake, anapaiilia shamba lenye aina mbili za mimea. Kwa hiyo mkulima akipalilia shamba
moja, kusema kweli atakuwa amepalilia mashamba mawili yenye mimea ya aina mbili tofauti. Tano,
kwa kufanya hivyo mkulima anaweza kuwa na ardhi nyingi zaidi kwa ajili ya mimea mingine. Sita,
wakati wa kuvuna mkulima anavuna mazao ya aina mbili tofauti.
Mashamba yaliyokuwa karibu na nyumba, Wasagara walipanda mbegu kwa kutumia
"Mwokambiko" au "Mandu". Hiki ni kijiti cha kuchimbia mashimo ya kupandia mbegu ili kuku
waweze kushindwa kuparuaparua mashimo yenye mbegu na kuzila.
MGAWANYO WA KAZI
Kulima na kupanda ilikuwa kazi ya wanaume na wanawake isipokuwa kuchimba mashimo
ilikuwa kazi ya wanaume tu. Kuvuna walivuna pamoja ili chakula kisiharibikie shambani kama
kawaida ya Wasagara, kazi zote zilizofanywa pamoja zilianzia kwa Mkuu wa Kijiji. Kwa kuvuna
walianza shamba la Mkuu wa Kijiji halafu baada ya kumaliza shamba la mkuu wa kijiji, ndipo
wakaendelea kuvuna mashamba ya wanakijiji kwa zamu, wakati wa kuvuna nyimbo nyingi ziliimbwa
shambani.
Baada ya kuvuna chakula chote, kingine kiliwekwa katika maghala ya kila mwanakijiji na
kuhifadhiwa humo. Chakula cha kutumia hakikuwekwa katika ghala hizo bali kiliwekwa katika ghala
tofauti ili kurahisisha kazi ya kukichukua na kukitumia. Chakula kilichowekwa katika ghala,
kilihifadhiwa vizuri sana tena kwa ufundi maalum. Maghala yenyewe yalikuwa ya Msonge na kila
mwanakijiji alikuwa-na ghala yake, hata mkuu wa mji au mkuu wa kijiji alikuwa na ghala yake.
Muundo wa maghaia wenyewe ulikuwa kama inavyoonyesha picha hapa chini.
65
Na hii ndiyo sehemu inayozungushiwa
PLANI YA GHALA
UAABO LA GHALA YENYEWE
nje ya ghala yenyewe nayo yaitwa Herengo. Halafu moto ulikokwa chini ili kuyakausha mazao
yaliyomo ndani ya ghala ili mazao yasishambuliwe na wadudu. Kilichokuwa katika ghala hakikuliwa
mpaka wakati wa shida. Iwapo shida ya chakula ilimkabiii jamaa fulani, basi Wasagara wenziwe
walimgawia chakula bure - hasa mkuu wa mji alitoa chakula toka kwenye ghala yake na kuwagawia
watu wake waliopatwa na shida hiyo. Hakuna aliyeweza kununua chakula katika ki j i ji . Shida ya
chakula ya mtu mmoja ilikuwa ni shida ya kijiji kizima.
Iwapo kijiji kingine kiliingiwa na baa la njaa mtu mmoja kutoka kijiji hicho alitumwa na mkuu wa
mji ili aende katika kijiji cha pili chenye neema na kuwaomba wawagawie chakula.
Basi mkuu wa kijiji chenye chakula humwambia mjumbe huyo kuwa arudi kwao na kwamba
watapata habari kesho yake. Baada ya huyo mjumbe kurudi kwao, mkuu wa kijiji huitisha mkutano
wa watu wote kijijini na kuelezea shida ya wanakijiji wa kijiji cha pili. Basi katika mkutano huo wote
kwa pamoja hutoa uamuzi wa kiasi cha chakula kitakachotolewa. Baada ya hapo Mkuu wa Kijiji
wenye shida huwa na wazo kwamba baadaye watakapopata neema basi chakula walichogawiwa,
ambacho ni mali ya kijiji, watawarudishia. Lakini kama baa hili linahusu wanakijiji wenyewe kwa
wenyewe, chakula chatolewa bure na Mkuu wa kijiji na wala hakuna kulipa hapo baadaye hata kama
neema itapatikana namna gani - kwa sababu wao ndio wenye chakula ndio wenye ghala na mkuu wa
kijiji hutunza hiyo ghala kwa niaba ya wanakijiji.
66
Ghala za kijiji zilijengwa imara kabisa Hi kuzuia panya na wanyama waharibifu. Walitumia miti
na majani ya kuezekea katika kuzijenga ghala zenyewe na zilikandikwa ili zisiweze kuingiliwa na
wanyama waharibifu. Mlango wake ulikuwa imara kabisa na uliweza kutosha barabara katika nafasi
ya tundu lake. Iwapo ilionekana kuwa panya waliingia ndani ya ghala kwa bahati mbaya, basi
wanakijiji wote walialikana siku hiyo na kuzifumua ghala zote na kuwaua panya wote kwa kuwapiga
fimbo. Pombe ilipikwa ili iweze kunywewa baada ya kazi ya kuua mapanya. Wizi ulikuwa hamna
kabisa zama hizo. Mali kadhalika chakula hakikuuzwa kwa mtu yeyote kwa sababu kila mtu alikuwa
nacho, na mtu mwenye njaa aliweza kupewa chakula bure.
CHAMA CHA USHIRIKA CHA WILAYA YA KILOSA
Katika Wilaya ya Kilosa kuna Chama cha Ushirika ambacho ndicho kinachotoa huduma za
kiushirika kwa upande wa watu wa Kilosa. Chama hiki kinaonyesha mfano bora wa ushirikiano wa
kisasa tofauti na ule ushirikiano wa kijadi uliokwisha elezwa hapo juu. Chini ya chama hiki kuna
vyama vingine vidogo vidogo vya wakulima ambavyo vinashughulikia mazao yao moja kwa moja.
Chama cha Ushirika cha Wilaya ya Kilosa kina shughulikia mazao haya: —
(i)
(ii)
(irl)
(iv)
Mpunga;
Nyonyo;
Mahindi;
Alizeti, n.k.
Kutoka kwenye vyama vidogo vidogo vya ushirika vya wakulima chama cha Ushirika cha Kilosa
hununua mazao haya na kuyasafirisha hadi mjini Kilosa na kutunzwa katika maghala ya Chama
mpaka siku yatakaposafirishwa tena kwenda kule yanakotakiwa kama ilivyoelezwa hapo chini.
Chama hutuma magari yao ambayo hukodishwa na kuyasomba mazao yote mpaka kwenye maghala
yao. Gharama zote za uchukuzi hulipwa na mkulima mwenyewe, ndiyo kusema kwamba katika ile
bei ya kununulia ni lazima gharama ya usafirishaji itiwe. Hivyo basi mkulima hulipa kiasi fulani
cha fedha za usafirishaji kwa kilo itakayopimwa. Na vile vile mlaji wa kila zao linaloshughulikiwa
na chama cha Ushirika yampasa kulipia gharama zote hizo.
Maghala yao yako imara kwa kuweza kuhifadhi mazao kuzuia wanyama waharibifu wasipate
nafasi ya kuyaharibu mazao hayo yanapokuwa ghalani. Mali kadhalika mazao hayo yakiwa bado
ghalani hutiwa madawa ya kuzuia wadudu wasiyashambulie. Wakati msimu ni mzito, yaani wakati
mavuno mengi yamepatikana, maghala yao hujaa sana na kusababisha kutunza mazao mengine nje
ya maghala. Lakini wakati mazao mengine yanapotunzwa nje namna hii, tahadhari huchukuliwa ili
mazao hayo yasije yakaharibiwa na mvua, wanyama, wadudu au kuibiwa na watu.
Chama hiki kinapata magari ya kusafirishia mazao toka kwa wakulima kwa kuyakodi. Magari
hayo yapatikana toka kwa: —
(a)
(b)
(c)
UMITA
Chama cha Ushirika cha Mkoa.
Bwana Aziz Kassam, n.k.
Barabara za Kilosa sio imara sana tena ni nyembamba mno. Kwa jinsi hii malori yenye tani
nyingi hayawezi kupita kwa usalama katika barabara hizi; labdatu hayo malori yasipakie hayo mazao
kiasi cha uzito wake. Wakati wa majira ya mvua, kazi ya kusafirisha hayo mazao huwa ni ngumu
zaidi kwa sababu zilizokwisha elezwa hapo juu. Kwa hiyo chama chajitahidi sana kuyasafirisha
mazao hayo wakati wa kiangazi tu kutoka kwa wakulima. Na chama chenyewe sasa huyasafirisha
mazao hayo toka Kilosa hadi Dar es Salaam kwa kutumia reli zaidi. Mazao hayo husafirishwa toka
Kilosa hadi kwenye Mashirika ya Gapex na Usagaji (National Milling) kwa sababu chama cha
ushirika cha Kilosa ni ajenti tu wa mashirika hayo, na gharama zote za usafirishaji wa mazao haya ni
juu ya mashirika hayo.
67
HUDUMA ZA CHAMA CHA USHIRIKA
KWA WAKULIMA WA KILOSA
Kama nilivyosema hapo juu chama cha Ushirika ni namna mpya ya ushirikiano katika shughuli
za uzalishaji mali (Angalia ushirika wa jadi wa Wasagara hapo juu). Ingawa ushirika wa namna hii ni
mpya, lakini si kitu kigeni kwa Wasagara kwa sababu wakulima walikuwa na ushirika wa asili tangu
zamani ushirika ambao uliwaletea manufaa mengi sana kimaisha. Huduma wazipatazo wakulima
kutoka kwenye chama hiki ni kama ilivyoonyesha hapo juu. Kwanza chama kinawasaidia wakulima
kwa kusafirisha mazao yao toka kwenye maghala yao hadi makao makuu ya chama ambako mazao
hayo yanahifadhiwa vizuri mpaka pale yatakapotakiwa kusafirishwa tena hadi Usagaji na Gapex Dar
es Salaam. Pili chama vile vile kinawauzia wanachama wake mbolea kwa bei nafuu, tatu chama
kinawasaidia wanachama wake kwa kuwatafutia madawa bora ya kuulia wadudu waharibifu wa
mimea mbali mbali. Kwa ajili ya huduma hizo, chama cha ushirika kinafanya kazi ya kuwa kama
karakana ya utaalamu wa kutawanya maarifa mbali mbali kwa wakulima na wanachama (As a
workshop of technology for the diffusion of innovations).
Picha hii hapa chini yaonyesha jinsi zao hilo hilo linalolimwa na mkulima linavyoweza kumfikia
mkulima tena. Kwa hiyo gharama huzidi kuongezeka mpaka kumfikia mkulima tena.
Tabia za watu fulani fulani za kuhamahama kutafuta kazi (Labour Migration) hazikujulikana
zama hizo za Wasagara mpaka ukoloni ulipoingizwa na Wazungu. Kila mtu katika Kijiji alikuwa na
kazi yake na kufanya uvivu hakukuwepo, na iwapo kulitokea kwamba watu fulani walikuwa wavivu
hao walipewa adhabu ya kupimiwa ngwe zao na halafu kuchekwa na kudharauliwa na wanawake.
Hizi ndizo namna za adhabu walizopewa kijijini. Lakini baada ya ukoloni kuingia nchini Wasagara
wengi walihamia sehemu za mashamba ya mikonge, wengine wakahamia mijini kutafuta kazi, na
kwa jinsi hii utaratibu wa maisha ukaharibiwa sana na ukoloni na nidhamu waliyokuwa nayo
Wasagara katika Mila na Desturi zao ikaathiriwa kabisa na kuweza kupoteza heshima ya Wasagara ya
Zamani.
68
WANYAMA
Wanyama waliofugwa na Wasagara ni Mbuzi, Kondoo, Bata, Kuku na kadhalika. Ng'ombe
hawajapata kufugwa na jamii ya Wasagara. Mbwa hawakuwapo tangu awali lakini walikuja fugwa
baadaye sana tena watu wachache sana waliwafuga wanyama hawa. Matumizi ya mbwa yalikuwa
kuwafukuzia wanyama waharibifu kama vile nyani. Mbuzi hawakufugwa kwa ajili ya maziwa bali
twaweza kusema wanyama hawa walifugwa kwa ajili ya ufahari tu (Social Prestige) kwa sababu
kufugwa kwa mbuzi hakukuwasaidia sana Wasagara. Tena wanyama hawa hawakuchinjwa ill kupata
nyama yake ambayo ilikuwa ni kitu cha muhimu kwa afya yao. Lakini zaidi mbuzi walitumika kama
mahari kwa kuolea wanawake. Wahindi walipokuja kuishi na kufanya biashara katika nchi ya Kilosa,
basi Wasagara wakaanza kuwakamua mbuzi wao na kuwauzia maziwa Wahindi.
Kondoo walifugwa tu bila ya kuchinjwa ili kupata nyama wala maziwa yao hayakukamuliwa.
Matumizi makubwa ya Kondoo yalikuwa kwa ajili ya tambiko na kufanyia dawa ya kuponyeshea
safura.
FAMILIA
Kwa kawaida kila familia ya Wasagara ilikuwa na Baba, Mama, Wana, na Mabinti. Hii ndiyo
familia maalum ya Kisagara. Lakini kwa sababu za maradhi au uzee mama wa familia fulani, baada
ya kuona kuwa nguvu zake zilipungua sana, na kazi nyingi kumzidi, hasa kazi na mashamba ambayo
yalikuwa ni makubwa sana kuliko mashamba ya siku hizi, aliweza kumwomba bwana yake aoe
mwanamke wa pili aweze kumsaidia katika kazi za kuhudumia familia yao. Basi bwana anayehusika
aliweza kuoa mwanamke wa pili baada ya kupata ruhusa toka kwa mke wake. Iwapo bwana huyo
alioa mwanamke wa pili alilazimika kumjengea nyumba yake huyo mwanamke wa pili mbali kidogo
na nyumba ya mke mkubwa. Ilikuwa ni desturi ya Wasagara waliooa mitara namna hii kuwajengea
nyumba za peke yao. Haikuwa ni desturi kwao kuwaweka wanawake wote katika nyumba moja.
Lakini kwa jumla, mitara ilikuwa nadra sana kupatikana katika majumba ya jamii ya Wasagara kwa
sababu haikuwa jadi yao.
Iwapo mitara ilikaa karibu na ikatokea kwamba bwana wa mitara hiyo kafariki dunia, na iwapo
mama wote wawili walizaa watoto, basi wanakijiji walikusanyika na kuigawanya mali sawa sawa marehemu aligawiwa 6/10 ya mali yote iliyokuwa katika nyumba ya kila mwanamke, na kila
mwanamke alipata 4/10 ya mali iliyokuwa katika nyumba yake aliyochuma pamoja na bwana yake.
Sasa mali yote ya marehemu toka mitara yote miwili ilikuwa 6/10 + 6/10 na ikawekwa pamoja, na
baada ya kufanya hivi watoto wote wa mama wote wawili waligawiwa sehemu ya marehemu. Lakini
iwapo wake zake walikaa mbali mbali sana, yaani kila mtara umbali wa maili kumi au zaidi hivi toka
nyumba ya mtara mmoja hadi mwingine, basi kila mtara ulibakia huko huko pamoja na watoto na
kurithi mali ya nyumba yake.
Katika jamii ya Kisagara, familia - koo - milango au jamii walikuwa hawabaguani wala
kuogopana wala kugombana bali walipendana, hata kati ya jamii na jamii nyingine walikuwa
hawagombani wala kuogopana. Waliweza kusaidiana katika shida mbali mbali zilizowatopea katika
maisha yao. Ingawa walisaidiana namna hirna kutoogopana. Lakini ulinzi wa kabila lao ulikuwa
mkali kabisa. Kwa mfano, mgeni yeyote aliyefika katika mji wa watu ambao si wa kwao ilimlazimu
afikie kwa mkuu wa mji huo ama sivyo alifukuzwa saa ile ile anapogunduliwa kuwa kaingia na kukaa
katika mji wa watu bila idhini ya mkuu wa mji. Pia kila mwanakijiji alikuwa na jukumu la kuhakikisha
kwamba hakuna mtu yeyote mgeni aliyekaa kijijini bila kwanza kukutana na Mkuu wa Kijiji na kupata
ruhusa ya kukaa humo. Kila mgeni aliripotiwa kwa mkuu wa Kijiji. Hii ilikuwa ni kwa ajili ya usalama
wakijiji kizima.
NYUMBA ZA WASAGARA
Nyumba zao zilikuwa za msonge, na zilijengwa kuzunguka nyumba moja ya msonge iliyojengwa
katikati ya kijiji. Nyumba hii ilikuwa ndipo mahali pakulia chakula pamoja kwa wanakijiji. Chakula
chote kutoka kila nyumba kililetwa hapo na wanaume wote wakakaa hapo saa za chakula na kula
chakula chao hapo. Pia hapo hapo katikati, nyumba ya Mkuu wakijiji ilijengwa, pengine madhumuni
69
ya kufanya hivyo ni kumlinda Mkuu wa kijiji asije akadhuriwa na watu wabaya. Vifaa vilivyotumika
kujengea nyumba ni miti, mikambaa, misani, na kamba zake ni gamba la miombo - hasa kamba
hizi zilitoka vizuri sana wakati wa masika ambapo miti mingi ilikuwa imefyonza maji mengi toka
ardhini. Pia kamba za mibungo zilitumika sana katika kujengea nyumba. Fito zilizotumika ni mianzi
ambayo ilipasuliwa katikati na kufanya fito nzuri sana za kujengea nyumba.
Fito za mkole vile vile zilitumiwa kwa kujengea nyumba. Mwamba wa nyumba ulikuwa ni miti,
na kenchi ya paa ilifungwa na mibungo. Vifaa vyote hivi vilipatikana karibu na kijiji. Majani ya
kuezekea yalikuwa majani ya sanje, majani ya motomoto, na kadhalika, ambayo yalifungwa katika
mafungu mafungu wakati wa kuezeka. Majani ya kuezekea yalipofungwa mafungu mafungu kwa
kamba na halafu kuezekwa, yaliweza kudumu muda mrefu sana, hata zaidi ya miaka mitatu.
MILANGO - AINA YA MBILA
Milango hii ilikuwa inasukwa vizuri kabisa na kufanya mlango. Miti ilitafutwa na kupangwa chini
katika safu halafu fito zilitafutwa na kusukwa nje ya hiyo miti pande zote mbili - na baadaye miti hiyo
ikazibwa kabisa na kusukwa kwa fito pande zote mbili - nje na ndani. Kamba za mibungo zilitumika
katika kusukia hizo fito zenyewe juu ya miti iliyokwisha tandikwa chini katika safu moja.
PICHAYAAALANGO
NDOA
Kwa kawaida mwanaume alioa mke kufuatana na maelezo yaliyotolewa katika elimu ya jadi ya
Wasagara. Lakini iwapo mtu aliyekwisha oa anataka kuoa tena mke mwingine, hasa hii ilitokea
wakati mke wa kwanza alionekana mkali kwa bwana wake, alikwenda kwa rafiki yake na kumwelezea
shida yake inayosababishwa na ukali wa mke. Basi yule mshenga wake humwambia rafiki yupi
mwanamke mgani ana sifa safi za kuolewa na bwana. Basi kama rafiki yake akikubaliana na sifa hizo,
mshenga wake huenda kumwita huyo mwanamke mgani wanayemtaka. Baada ya huyo mwanamke
kuambiwa na mshenga kuwa bwana mwenyewe ni huyu anayemtaka kumwoa, humuuliza mshenga
swali huku mama huyu ameinama bila kuwaangalia wale wanaozungumza nao kuwa, "Je ninyi
mwanijuaje?" Basi hao wanaume humwelezea jinsi wanavyomfahamu. Anayetaka kumposa huyo
70
mwanamke hasemi neno lolote ila tu yule mshenga wake ndiyo mwenye kukabili maswali yote
yatokayo kwa mwanamke. Basi mama akisha kubali huvikwa "Kikomo" cha chuma mkononi mwake
na anayefanya kazi ya kumvika mwanamke huyo hicho kikomo ni yule mshenga. Kikomo hicho
ndicho kifunga uchumba.
Basi yule bwana lazima aende nyumbani kwa yule mwanamke mgani na kabla hajaenda
anapatana na yule mwanamke anayetaka kumwoa juu ya alama atakazozitumia wakati wa kubisha
nodi nyumbani kwake. Yule mwanaume maana anatakiwa kwenda huko saa nne za usiku na kulala
huko huko kwa mwanamke mgani. Basi baada ya kupatana juu ya alama atakazozitumia yule bwana,
mwanamke huondoka na kurudi nyumbani kwake. Basi. bwana siku ya kuondoka kwenda kwa yule
mwanamke anayetaka kumwoa, huchukua jembe, mundu na shoka kama ndio alama za kuonyesha
uanaume. Huondoka saa za usiku kama saa nne hivi usiku na kwenda kwa yule bibi anayemtaka.
Anapofika kwa huyo mchumba wake, hubisha mlango kwa kutumia alama alizomwelezea mchumba
wake. Basi yule mwanamke huamka baada ya kusikia kubisha kwa mtu, anajua kabisa zile alama
alizoelezewa. Kabla hajafungua mlango, ni lazima kwanza achungulie kupitia pembeni mwa mlango
wake au kupitia kijidirisha cha nyumba yake. Anapofanya hivyo anahakikisha kama kweli yule mtu
ndiye mchumba wake, lakini kama si yeye basi hawezi kuufungua mlango. Baada ya kufunguliwa
mlango, yule bwana huingia ndani na kulala humo humo pamoja na mchumba wake. Kabla
ya yule bwana kwenda nyumbani kwa yule mwanamke, yule mwanamke huwa ametoa taarifa
kwa Mkuu wa kijiji chake kuwa atapata mgeni usiku huo, na habari hii huzagaa kijiji chote cha yule
mwanamke. Kwa hiyo yule bwana atakapofika kwa yule mwanamke huwa kila mtu anafahamu nini
kinatendeka nyumbani kwake huyo mama.
Bwana huyo hulala kwa mwanamke huyo mpaka asubuhi, na asubuhi hiyo bwana huyo
huchelewa kuamka. Asubuhi na mapema, yule mwanamke huenda kwa Mkuu wa mji na kutoa taarifa
ya kwamba mgeni alilala nyumbani kwake. Basi Mkuu wa kijiji humwambia huyo bibi kuwa aende
akamwambie mgeni wake ya kuwa aende akamwamkie huyo mkuu wa kijiji. Wakati huo watu wote
kijijini hawaendi shambani bali hukaa nje ya nyumba zao ili waweze kumwona huyo bwana. Basi yule
bwana hutoka nje ya nyumba ya mchumba wake huku akichukuwa mundu, shoka, jembe lake na
kwenda kwa Mkuu wa kijiji au mji. Wakati akitoka watu humwangalia na kumpima kama huyo kweli
ni mwanaume au la. Jambo kubwa lililomfanya mwanaume aonekane kama ni mwanaume kweli ni
zile zana anazokuja nazo kwa yule mwanamke, yaani mundu, jembe, na shoka.
Basi yule bwana huondoka pale nyumbani pa mwanamke na kwenda kumwamkia Mkuu wa mji.
Baada ya kumwamkia Mkuu wa mji, huambiwa aje siku ya pili yake ili aonyeshwe kishamba cha
kumlimia yule Mkuu wa mji. Kiasi cha kijishamba chenyewe ni zaidi ya eka mbili hivi. Yule bwana
huenda kwa Mkuu wa mji na kuonyeshwa shamba lenyewe. Basi yule jamaa hushinda huko
shambani akifyeka na kulima. Kazi yenyewe ilimchukuwa siku saba au zaidi, si kazi rahisi. Baada ya
kumaliza kulima lile shamba yule bwana humwambia mchumba wake kuwa amemaliza kulima
shamba na kwamba aende akamwarifu Mkuu wa mji kwenda kuangalia na yeye hurudi nyumbani
kwake na kwamba yeye Mkuu wa mji sasa aende akaliangalie lile shamba lililolimwa na yule
mchumba wake. Mkuu wa mji huenda kuliangalia lile shamba baada ya kuliangalia shamba lenyewe,
humwambia yule bibi kuwa yule ndio bwana wa kumwoa - anafaa kabisa. Basi yule bwana huambiwa
alete mbuzi mmoja iwe ndio posa na mahari ya kwanza. Mahari huendelea na kufikia mbuzi watano.
Mahari haikuthaminiwa sana bali nguvu za mtu katika kufanya kazi ndizo zilizothaminiwa sana kuliko
mahari yenyewe. Siku ya arusi palipikwa pombe nyingi na chakula kwa wingi. Siku hiyo kuku
walichinjwa sana ili kusherehekea arusi hiyo, karibu kila nyumba ilipika pombe ya arusi. Ngoma na
nyimbo kwa wingi ziliimbwa na bibi arusi alipewa kitambi kimoja kama zawadi. Sherehe ilichezwa
kwa kufuatana na wingi wa pombe zilizopikwa siku hiyo.
Nyimbo na ngoma zilichezwa. Mfano wa ngoma zenyewe ni hizi:
Kombe, Kisembe, Ndomole, Segesela na Mbilu. Hizo ndizo ngoma za wanaume. Wanawake
hucheza sana ngoma ya Gubi.
71
Kazi za akina mama katika jamii ya Kisagara ni kusaidia wanaume kujenga nyumba - kutwanga
mahindi - kusuka mikeka - vitunga - majamvi, ufinyanzi - kulima - kupika nakadhalika. Wanaume
wana kazi ya kulima - kujenga nyumba na zinginezo nyingi.
DESTURI ZA KUAMKIANA
Desturi za Wasagara za kuamkiana zilikuwa zinatiliwa maanani kama ni sehemu ya adabu na
nidhamu kwa Wasagara wote. Kwa hiyo kuamkiana ilikuwa ni jambo la lazima na mpaka sasa
Wasagara huamkiana sana kuonyesha adabu, nidhamu na upole. Mwanamke wa Kisagara anapotaka
kuwaamkia wanaume, huenda karibu na nyumba au karibu na mti wowote ulio karibu na hapo
kujificha nusu ya sehemu ya mwili wake kwa kutumia mti huo au ukuta wa nyumba halafu
huchuchumaa chini na kuwaamkia huku jicho moja tu huwaangalia wanaume anaowaamkia na
kusema "Amsindile" - habari za kutwa kama ni asubuhi huamkia "Hamwasile" Mmeamkaje.
Iwapo mwanamke amekutana na mwanaume njiani, basi mwanamke huacha njia - humwachia
njia mwanaume halafu hupiga magoti bila kumtazama na humwamkia huyo bwana. Mwanaume
anapomwamkia mwanaume mwenziwe zaidi itategemea yupi kati yao yu mkubwa kwa umri. Kwa
kawaida mdogo hupiga magoti kumwamkia mkubwa huku akitoa kofia iwapo anayo. Mali kadhalika
mtawala wa nchi ya Wasagara aliamkiwa hivi hivi kama ilivyoelezwa hapo juu.
UTAWALA
Umbo la utawala wa nchi ya Wasagara - Chifu Mzee Kutukutu - Waziri wake - Wandewa wadogo
- wazee - mabaraza ya usuluhisho na kila tarafa ilikuwa na mkuu wake - na mashauri yalipelekwa
moja kwa moja kwa Kutukutu mwenyewe. Adhabu zilitolewa kwa kufuatana na makosa yenyewe.
Makosa makubwa yalipelekwa kwa Kutukutu mwenyewe.
Kodi iliyotolewa haikutolewa kwa kutumia fedha, bali chakula kilichochangwa kwenda kwa
chifu. Kila mtu alifanya hivyo. Mali kadhalika wakati wa kulima kila mtu ilimbidi akalime shamba la
mkuu wa kijiji au chifu. Chakula kilichovunwa katika shamba la chifu kiliwekwa katika ghala ya nchi
au ghala ya kijiji, na wakati wa dhiki, chakula hiki kiligawiwa kwa wananchi wote bure.
Mundewa alitawazwa na mtani wa Wasagara. Mara nyingi Mundewa anayetawazwa lazima awe
ni mtu anayekubalika na wananchi. Kwanza kabla ya kutawazwa mtani anayefanya kazi ya kumtawaza Mundewa huwauliza watu ni mtu wa ukoo gani huyo anayetaka kutawazwa. Basi ndugu za
huyo Mundewa anayetaka kutawala husimulia hadithi yote kuhusu Mundewa huyo na kutoa sifa
zote alizonazo. Halafu mtani huwauliza watu, "Je! Mundewa huyu ni mtumwa, Suria au vipi?"
Basi mtani huyo anahakikishiwa kuwa Mundewa huyo ni Mwuungwana. Katika nchi ya
Wasagara mtu Suria alikubaliwa kutawala nchi hiyo. Sababu kubwa ya kufanya hivi ni kwamba,
Wasagara ni jamii ambayo ilikuwa inafuata urithi kwa upande wa mama (Matrilineal Society) na
waliogopa kuwa iwapo mtu ambaye hakuwa Suria alitawala, utawala huo wakati wa kurithi kwa
mjomba wake ambayo ndiyo iliyokuwa ada yao, angepeleka utawala wote wa Wasagara kwa
wajomba zake, halafu wajomba zake tu ndio wangeweza kurithi utawala huo. Pia Wasagara
waliogopa kumpa utawala mtu ambaye hakuwa Suria kwa sababu baada ya kuupeleka utawala wa
Wasagara kwa wajomba zake, basi wasingeweza kumnyang'anya huyo Mundewa utawala iwapo
alifanya makosa au kukiuka miiko ya utawala wao. Lakini Suria ni mtu asiyekuwa na wajomba
ambako angepeleka ufalme wa Wasagara, pili ilikuwa ni rahisi kwa Wasagara kumnyang'anya
utawala wao iwapo huyo Suria alikiuka miiko ya utawala wa Wasagara.
72
Wakati wa kutawazwa, huyo Mundewa au chifu hukalishwa juu ya kigoda huku amefunikwa
nguo. Shughuli hii hufanywa na mtani - ndiye kasisi wa sherehe zote hizi. Halafu Mundewa huvikwa
kikomo mkononi. Baada ya hapo huyo jamaa anayetawazwa hupewa shoka, mundu, zana za
kufyekea miti na majani shambani. Mkuki - alama ya kuonyesha iwapo vita itatokea aweze kulinda
Taifa lake. Akiwa bado kigodani, mfalme huyo hutemewa pombe kinywani mwake toka kinywani
mwa mtani anayefanya kazi ya kumtawaza siku hiyo na anaimeza pombe hiyo.
KIAPO
Mfalme huyo hula kiapo cha kutawala nchi kama hivi:Uleke ukobo - acha kuwanyima watu. Uleke ugoni
ugoni - acha mambo ya uzinifu. Uleke upekeupeke acha uwongo.
Wewe jina lako liwe "Nifenazo" - yaani "Wewe uwe mtunza siri, cheka na kila mtu". "Mhasemwe
wadala" - usisahau wazee. Halafu mfalme anatiwa mafuta ya nyonyo kichwani pake, halafu mafuta
yale hutiririka kuja usoni - puani mpaka mdomoni; halafu mtani wake wa kike huja na kuyalamba
mafuta yale yaliyotiririka karibu na mdomo wa mfalme na kuyameza.
Mtani anayefanya kazi hii ya kumtawaza mfalme hupewa mbuzi kama zawadi yake kwa kazi
aliyoifanya siku hiyo. Halafu huyo mtani huingia ndani ya nyumba ya mfalme na kulala juu ya
kitanda cha mfalme na kumwita mke wake mtani na kulala naye juu ya hicho kitanda cha mfalme ila
hawatendi jambo lolote. Nyumba ya mfalme hunyunyiziwa hoza ill kuipooza.
MAJI
Maji ya kunywa ilikuwa lazima yatoke kisimani ambacho kilichimbwa katika kila kijiji cha
Wasagara - hasa kisima kilichimbwa chini ya mti mbali kidogo na kijiji kuhakikisha kuwa maji
hayakuchafuliwa na chochote. Maji ya mto Mkondoa hayakutumika kwa kunywa ila kwa kumwagilia
mashamba tu. Kisima chenyewe kilifunikwa na magome ya miti. Maji ya kufulia nguo na kuoga
yalitoka kisimani, na yalitekwa na kutiwa katika chungu kikubwa kilichotengenezwa kilichoitwa
"Ponda".
73
MAVAZI YA WASAGARA
Wasagara
walikuwa
wanatengeneza mavazi ya
wao wenyewe kabla ya kuletwa mavazi mapya na wakoloni. Walitengeneza mavazi yao toka kwenye
magome ya miti ya "Mlenye". Gome la mti huu liliondolewa vizuri sana kwa kutumia shoka na tezo,
halafu likalainishwa vizuri sana kwa kulipon-daponda na jiwe au kipande cha mti na kisha
likavaliwa kiunoni. Kofia vile vile zilitengenezwa kutokana na magome ya miti hii ya "Mlenye".
Mbeleko ya kubebea mtoto na viatu vyote vilitengenezwa kutokana na hayo hayo magome ya
miti. Wakati mwingine viatu vilitengenezwa kutokana na ngozi ya mbuzi.
MAPAMBO
Mwanamke alijipaka mafuta ya nyonyo ambazo zilikuwa zikipandwa sana wakati huo na
ambazo mpaka wakati huu zapandwa sana kama zao la kuwaletea fedha. Masikio ya wanawake
yalitobolewa na kutiwa mpingo. Nywele zao zilikatwa halafu zikatiwa mafuta.
MWISHO
Kama nilivyojaribu kuonyesha mila na desturi za Wasagara katika makala hayo na makala
yaliyokwisha tolewa mwezi wa Oktoba, 1974, ni kwamba watu hawa wana asili ya kushirikiana sana
katika shughuli za kuzalisha mali karibu kila kazi walioifanya walishirikiana pamoja kama kijiji na
kazi zao za kulima mashamba ziliisha mara moja kabla ya mvua kunyesha. Mkuu wa kijiji, baada ya
kusikia ngurumo ya mvua alipiga mbiu ya mgambo na kuwatahadharisha wanakijiji wote kuanza
kulima mashamba yao. Na kazi hii walifanya kwa zamu hata ikatokea kwamba mashamba yao mengi
yalilimwa mapema. Umoja ni nguvu na Utengano ni udhaifu. Kuna haja kubwa ya kufufua desturi hii
ya kufanya kazi pamoja ili wananchi waweze kushirikiana kama zamani katika kutekeleza kazi zao
barabara na upesi zaidi.
Zaidi ya hayo, zamani Wasagara walikuwa hawana shida yachakula-yaani chakula kilipatikana
kwa urahisi wakati wo wote wa kiangazi au wa masika. Wasagara walilima na kupanda mazao ya
chakula mara mbili kwa mwaka. Wakati wa masika mimea yao mashambani ilitumia maji ya mvua na
wakati wa kiangazi mimea yao ilitumia maji yakumwagilia ya mto Mkondoa. Mboga nyingi za majani
zilipandwa wakati huu kwa kutumia maji ya mto lakini jambo hiii sasa halifanyiki hata kidogo kwa
sababu utaalamu ule wa zamani umepotea na pia mto wa Mkondoa sasa uko chini kidogo kuliko
ilivyokuwa hapo zamani. Manufaa yote ya kutumia maji ya kumwagilia ya mto Mkondoa kwa kumwagilia mashamba hamna sasa isipokuwa mto huu unatumika tu kwa kuogelea, kufulia na kuvua
samaki. Mto wenyewe haukauki na tena ni mkubwa, kwa hiyo ingalikuwa vyema zaidi kama mifereji
midogo midogo ingalitengenezwa ili ipeleke maji katika mashamba au bustani wakati wa kiangazi.
Na wakati wa masika mifereji hii ingaliweza kuzibwa kwa sababu wakati huu hakuna haja ya kutumia
maji ya mto wakati ipo mvua. Isipokuwa kama mvua imeshindwa kunyesha. Kitendo hiki kingekuwa
cha manufaa sana kwa Taifa zima kwa kutumia utaalamu wa kisasa.
Jambo jingine la kulifufua ni ulinzi wa Taifa. Wasagara walikuwa na ulinzi mkubwa wa vijiji
vyao kila mwananchi alikuwa najukumu hilo. Tukifanya Kama walivyolinda Taifa lao hawa jamaa
tutaweza kwenda mbali zaidi katika kulilinda Taifa la Watanzania lisiingiliwe na maadui wowote.
74
Katika kufanya kazi, kila mtu katika nchi ya Wasagara alikuwa na wajibu wa kufanya kazi, kila
mtu alipewa kazi ya kufanya na jamii. Mvivu aliadhibiwa na kuzomewa na pia alipewa kazi ya kufanya
kwa kupimiwa ngwe yake Mwenyewe ili aimalize Mgonjwa na mtoto ndio hawakupewa kazi kwa
sababu walikuwa hawajiwezi. Lakini mtu mzima yeyote mwanamke kwa mwanaume, wote walifanya
kazi pamoja bila kutegeana. Desturi hii ilikuwa nzuri sana kwa maoni yangu naona kama
ingalifufuliwa na kuenezwa kila mahali nchini ili kila mtu awe na kazi ya kufanya.
Heshima na adabu vilitiliwa mkazo sana katika jamii ya Wasagara, hasa heshima kwa
wakubwa na viongozi wa Wasagara. Huu ni mfano wa kuiga sana toka kwa watu hao. Heshima na
adabu kwa viongozi wetu ni wajibu wetu. Ni lazima tuwape heshima wanaostahili kupewa na
waliochini yao. Kwa sababu vijana wengi wameanza kupoteza heshima na adabu kwa viongozi wetu,
ingalifaa kama jambo hili lingefufuliwa upesi sana kwa sababu heshima hainunuliwi.
MWISHO
Wafuatao ndio hasa waliotoa habari zilizoandikwa hapo juu:
1.
Mzee Enzi Muhongola- Mwenyekiti waTANU na Diwani.
2.
Mzee Mganga Salum Mjumbe wa Halmashauri yaTANU
na mjumbe wa nyumba kumi kumi.
3.
Mzee Maiko Paulo - Mjumbe wa Halmashauri yaTANU, na
mjumbe wa nyumba kumi kumi.
4.
Mzee Kibwana Mohamed Mkulungwe - Mzee.
5.
Mzee AM Issa-Mzee.
6.
7.
Bwana Saidi Madege - mjumbe wa nyumba kumi kumi.
MzeeMuya-Mtafiti.
ORODHA YA KUMBUKUMBU YA VITABU
1. Wizara ya Utamaduni : Historia fupi ya Utamaduni wa Mtanzania. 1974.
2. CharsleyS.R.: The Princes of Nyakyusa, 1969.
3. Mwakipesile J.S.: Utamaduni wa Wasagara, 1974.
4. A.M.T. Mabeleand Bjarne F.K. Gorm P.. Strategies and methods of the
Development of museal Activities on local Level in Tanzania; 1974.
5. MwakipesileJ.S.: Jamii ya Wasafwa, 1974.
6. Dr. S.A. Lucas & A. F. Masao: The Present State of Research on cultural
Development in Tanzania, 1974.
7. Dr. I.K. Katokeand Dr. S.A. Lucas: Cultural Development as a factor in social
charge, 1975.
75