katuni - The Health COMpass
Transcription
katuni - The Health COMpass
ISSN: 0856-8995 Haliuzwi KATUNI: Kilimo kinalipa Ramani ya Tanzania Kilimo kina thamani na kinaweza kuwa sekta yenye faida kubwa kwa sababu watu wanahitaji kula, soko la bidhaa za kilimo linakuwepo kila wakati hususani mazao cha ya chakula. Changamkia jembe kwa sababu kilimo ni fedha! Kifanye kuwa shughuli yako rasmi ufaidike na kilimo. 2 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo! Huzalishwa na kusambazwa. Si Mchezo! husambazwa. Lilikozalishwa toleo hili. YALIYOMO 4 Stori Yangu: Kilimo kinalipa 6 Mambo Mapya 8 Hadithi ya Picha: Ujanja shambani! Mhariri Majuka Ololkeri 12 Je, Wajua: Maofisa ugani ndiyo nguzo ya kilimo Waandishi Raphael Nyoni Rebeca Gyumi 16 Burudani: Moro All Stars Washauri Timu ya Femina HIP Betty Liduke Mkurugenzi Mtendaji Dr. Minou Fuglesang Mkurugenzi wa Habari Amabilis Batamula Meneja Machapisho Jiang Alipo Meneja Uhusiano Lilian Nsemwa Katuni na Usanifu BabaTau, Inc. Mpiga Chapa Jamana Printers Ltd Usambazaji EAM Logistic Ltd Femina HIP na Washirika Si Mchezo! limefanyika kwa hisani kubwa ya Serikali za Sweden (Sida), Denmark (DANIDA), na mashirika ya HIVOS, RFSU, Marie Stopes, Mama Misitu, TWAWEZA na JHU-CCP/TCCP. Yaliyomo humu ndani ni jukumu la Femina HIP na hayawakilishi maoni au mitazamo ya wafadhili. 14 Sauti yangu 18 Ruka Juu: Ruka juu na jembe 20 Nguvu za mwanaume 21 Nguvu za mwanamke 22 Chezasalama: Jipange, usije ukavuna mabua!... 24 Katuni: Chakarika jembe likutoe 27 Ukweli wa mambo: Kilimo ni tumaini la wengi 28 Sema Tenda: Kilimobiashara ni zaidi ya ujuavyo 30 Marie Stopes: Waelimisharika Zanzibar, walia na utoaji mimba 31 Ushauri TAHARIRI Heri ya Mwaka Mpya wapenzi wasomaji wetu. Mwaka huu tumetuliza vichwa na kubadilisha vitu vingi kwenye jarida lengo likiwa kukuletea vitu adimu kivingine. Yote haya yametokana pia na mawazo yenu mnayotutumia. Toleo hili tumezungumzia masuala ya kilimo. Bila shaka kila mmoja anajua kuwa kilimo ndiyo uti wa mgongo wa Mtanzania. Tufunguke katika kilimo! Karibu. Majuka Ruka Juu kijanja Kijana jitume shambani... ...Peta maishani Wasiliana nasi kwa: S.L.P. 2065, Dar es Salaam Simu: (22) 212 8265, 2126851/2 Fax: (22) 2110842 email: simchezo@feminahip. or.tz Si Mchezo! huchapishwa na Femina HIP. Sms: Andika SM acha nafasi andika maoni yako kisha tuma kwenda 15665 3 STORI YANGU Kilimo kinalipa M tanange wa kusaka maisha nilianza siku nyingi na niliyoyapitia ni mengi lakini nataka nizungumzie machache tu kati ya hayo. Najua vijana wengi tumepitia magumu kama yangu na ni haki ya kila mmoja kuwa huru kutoa historia yake. Nimeamua kufunguka ili kuwaelimisha wengine juu ya umuhimu wa kubadili uamuzi pale ‘unapobugi step’. Naitwa Nesho Festo Madepana (25), mzaliwa wa Kijiji cha Zombo, Kilosa. Nilimaliza elimu ya msingi mwaka 2002 hapa Zombo na sikufaulu kuendelea na elimu ya sekondari. ingawa nilikuwa na nia ya kujiendeleza kielimu. Nilijishughulisha na vibarua mbalimbali nikiwa na lengo la kuwa na pesa ya kianzio kwani wazazi wangu hawakuwa na uwezo wa kunisomesha. Nilipata pesa kiasi ambazo nilitumia kufuatilia kujiunga VETA Mikumi ambapo baba alikubali kunilipia ada. Nilikubaliwa chuoni hapo nikaanza masomo ya ufundi magari mwaka 2003. Baada ya miezi kadhaa nilifukuzwa chuo kwani baba hakuweza kulipa ada na sikuwa na uwezo wa kujilipia. Hapo ndipo nikaanza kuonja ‘joto ya jiwe’ katika maisha. Nilikaa Mikumi kwa kipindi fulani nikisoma ‘ramani’ ya jinsi gani naweza kuendelea. Nilijiunga na Kikundi cha Sanaa cha Wanyonge Family kama mwanamuziki nikawa natunga na kuimba nyimbo. Hatukufanikiwa kiviile kwani hatukuwa na mtaji. Mwaka 2004 nikarudi nyumbani, safari hii nikamuomba baba shamba la kulima na akanipatia hekari moja. Nilianza kulima mahindi peke yake, nilipovuna mara ya kwanza nilipata magunia 12 kwa hekari 4 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013 Mambo yote shambani: Nesho akiwa na mkewe wakionyesha mazao yao. moja. Niliuza yote nikapata 230,000/- nikiwa na lengo la kwenda Bongo kufungua biashara ya kuuza chipsi. Nilitua Jijini mwaka 2005 nikaweka kambi Tabata. Nilijaribu zali la chipsi pale Mwenge lakini niligonga mwamba baada ya kupiga mahesabu na kugundua kuwa gharama za kufungua banda la kuuzia chipsi ni 180,000/- na pesa nitakazobaki nazo hazitanitosha kujikimu Jijini. Nilipoona hivyo nilibadilisha mawazo na kwenda Kariakoo, nikanunua belo la suruali kadhaa za ‘jeans’ kwa ajili ya biashara, nikanunulia na mbegu za matikiti maji, nikaamua kurudi nyumbani. hatua kimaendeleo. Waliniumiza akili sana. Niliuza zile jeans na pesa hiyo nikafungua banda la kuuza chipsi hapa Zombo huku nikiendelea na kilimo. Mwanzoni tulishirikiana na baba kulima pilipili kwa ajili ya biashara. Nilikuwa nikizipeleka Bongo tatizo likawa soko duni. Hatukuwahi kupata faida Niliporudi nyumbani mwaka 2006 niliwakuta kwani bei zilikuwa ndogo sana. Biashara ya chipsi wenzangu ambao tulimaliza wote elimu ya msingi haikuendelea kwani nilishindwa kuendesha zote waliotulia wakaamua kuwa wakulima wamepiga kwa pamoja. Niliamua kulima nyanya maji, huku nikijishughulisha na vibarua ili niweze kupata pesa za kununua dawa ya kuua wadudu shambani. Nilipovuna, nikabahatisha msimu mzuri wa biashara nikauza plastiki moja kwa bei ya 4000/nikapata 280,000/-. Nikaanza kujitegemea mwaka 2007. Nilinunua shamba la hekari tatu. Baadaye nikaweza kununua pampu ya kumwagilia. Mpaka sasa nimegundua siri iliyopo kwenye kilimo kuwa kinalipa! Imenifanya niwe na matumaini ya maendeleo hapo baadaye. Mbali na kilimo hicho pia nafuga nguruwe watatu sasa. Wengine wana fikra potofu kuwa kilimo hakina tija lakini nimekuwa mmoja wa wale wanaoombwa buku kitaani! Hivyo kijana jipange na anza upya sasa. Nina mengi ya kuwashauri vijana. Unapojaribu kitu ukagundua kuwa hakina tija, usione ujinga kuanza upya! Tuepukane na makundi rika yanayotupotosha. Maisha ni kupeta kwa Nesho na mkewe, baada ya kujikita kwenye kilimo. Nimeoa, mimi na mke wangu tunapendana, tunaheshimiana, tunalindana na tunasaidiana kazi. Najipanga ili niweze kujenga nyumba ya kuishi na pia kujiendeleza kielimu ili kuongeza ufanisi kwenye kilimo. JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo! 5 mambo mapya Uchumi Flower Majengo yanakaa bure haya! Hivi Tanzania tutaendelea kutegemea misaada mpaka lini? Yaani inatia uchungu kuona haya majengo ya Ilonga Youth Centre yamekaa tu bila ya hata ya kutumika kwa kukosa fedha na hata yakitumika basi ni kwa kipindi kifupi cha mafunzo ya wiki mbili tu! Majengo haya pamoja na mandhari yake yanafaa yakatumika kwa kuwa chuo cha elimu ya juu kuanzia ngazi ya stashahada ya kilimo kama tu wizara husika itaamua kufanya kweli. Wajumbe walikaa na kuunda kikundi cha Uchumi Flower mwaka 2009 chenye makao yake makuu kijiji cha Mhenda, Kilosa. Jamaa wamejipanga ile mbaya kujikwamua kwa kutumia mashamba ya wanachama kulima alizeti. Penye nia pana njia, wamepata mkopo wa mashine ya kukamua alizeti kutoka halmashauri ya wilaya. Unajua nini? Imesaidia sana wanakijiji kupunguza gharama za kwenda kukamua alizeti na wao wanajiingizia kipato kutokana na kilimo. Boda boda Waendesha pikipiki wa mikoani wanasifika kwa kuzingatia sheria za barabarani, lakini huyu braza wa Gairo yeye sijui vipi? Lori linaovateki na jamaa nae akaona ‘apige mande,. Haraka izingatie usalama na sheria za barabarani. Wakati unawahi ishu zako, kumbuka na majukumu yako kwa watu wanaokutegemea katika jamii. 6 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013 RUKA jUU Young Farmers in Business Kuanzia Machi 2013, Femina itakuletea Ruka Juu TV show Usicheze mbali na luninga yako ITV kila Jumamosi saa 1 usiku TBC1 Kila Jumapili saa 3 usiku Funguka shambani peta maishani na Fema Radio. RFA kila Jumatatu saa 2.45 usiku TBC FM kila Jumanne saa 3 usiku JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo! 7 unauhakika nae? shauri yako! baadae usije lia wakati mwenzio nachekelea mavuno! azikiwe na wanija ni marafiki tangu wanasoma.wanashiriki shana mambo mengi, japo wanasikilizana na wakati mwingine kutofautiana. Wamemaliza kidato cha nne na sasa wameanza maisha ambayo ni funzo kwetu sote kujua ni jinsi gani kila mmoja alivyoanza maisha ya mtaani na sasa anafanya nini. Tufuatilie mchezo huu na tujielimishe haya sasa, azikiwe na wanija wamemaliza masomo na matokeo ya mtihani yameshatoka na wamefeli.Changa moto iko mbele yao juu ya maisha ya baadae, hebu tuwafuatilie kuona nini kitajiri kwao unaonaje tukianzisha bustani ya mbogamboga ili tujipatie kipato? shoga mbona hivyo! subiri majibu yatoke ndio tutajua aku bibi eeh! ya nini kujizeesha na juma ananihudumia kila kitu? …baba hekari moja tu inatosha kwa kuanzia. he, yule sio shoga yako? mbona na jembe jioni yote hii? sawa mwanangu, usihofu umeshapata hilo azikiwe akiwa na bwana shamba wanija akionywa na wazazi bora useme wewe hivi kwa nini umekuwa mazururaji, siku nne sasa hujaonekana hapa nyumbani 8 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013 mtaalamu msaidie mwanangu awe mkulima wa kisasa akizingatia haya, atavuna vizuri baada ya matokeo ya mtihani hata kama nimepata division four. Siwezi nikashika jembe kwani jembe litakataa? kufeli mtihani sio kufeli maisha sasa kulima ndio kufeli maisha? kulima ndio mpango mzima, utaona! basi eti azikiwe alinishauri tulime, mi nkakataa . achana naye, kafulia yule panda mbegu kwenye mstari kwa kuzipa nafasi ili zistawi vizuri ungezeeka, shauri yako haya sasa, kila mmoja yuko bize na maisha yake. kuna aliyepanda kwenye starehe na aliyepanda kwenye kilimo, tuone watavuna nini? kilimo ni suluhu ya ajira kwa vijana duh! kumbe bora nimestuka mapema baada ya miezi kadhaa ameukataa huu ujauzito, sijui nifanyaje jikaze hivyo hivyo mpaka ujifungue mwaya JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo! 9 azikiwe akimshukuru bwana shamba baada ya miezi kadhaa : kila mmoja amevuna alichokipanda Karibuni wageni, wanijaaa,kuna wageni asante sana maana ushauri wako umenisaidia kuongeza mavuno ushauri wa wataalamu wa kilimo ni muhimu kuuzingatia fumanizi!!! karibuni, waoo, na zawadi kabisa asante, hongera jamani nimeshasema mimi na wewe sasa bhaaaas! naomba unisamehe mpenzi usikate tamaa, kwa kilimo unaweza kumudu familia na kujisomesha pia. nimeshajenga,na sasa naenda kusomea kilimo herí yako, mi na hawa watoto siwezi tena 10 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013 dah! sijui kwa nini sikuanza mapema sawa nitajitahidi maisha yananamchapa wanija,. anaamua kujirahisisha kwa wanaume ili aweze kumhudumia mwanae, je hili ndio suluhisho? hebu tujionee mazao yako tayari, tuma gari lije kubeba baada ya kipindi flani acha tu, kwa kuwa sasa ni wapenzi, wewe chukua tu baada ya misukosuko mingi ya kimaisha, wanija ameamua kutafakari upya maisha yake,Je atabadilika? hebu tuendelee na stori mmh! hivi nitaishi maisha haya mpaka lini? baada ya miezi 3 Kilimo kinalipa,ingia shambani tu! …watoto baba zao wamewakataa, maisha yamekuwa magumu sana kwangu miaka miwili baadae huku mambo shwari, na mimi nataka kuja kusoma huko Haya nikiuza yatanisaidia sana asante sana jitahidi na kilimo uje, elimu ndio mpango mzima haya,mambo ya kilimo hayo. Wanija amebadilika na sasa ni mkulima mzuri kabisa.huu ni mfano mzuri vijana wengi wanaona kama kilimo hakilipi. ila ukweli ni kwamba Ukizingatia njia za kilimo cha kisasa unatoka JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo! 11 JE, WAJUA? Maofisa ugani ndio nguzo ya kilimo vijijini K atika mchezo huu tumeona jinsi Azikiwe alivyopiga hatua kwa kujikita katika kilimo. Wanija ‘alibugi step’ alivyokuwa akivinjari kwenye uhusiano, baadaye alijutia uamuzi wake. Kuna mengi tunaweza kujifunza katika mchezo huu lakini ningependa tujadili kidogo kuhusu umuhimu wa maofisa ugani ambao ndiyo waliompiga tafu kubwa Azikiwe katika mafanikio yake. Hawa ndiyo wanaweza kuwa maafisa ugani... Maofisa ugani wapo katika sekta nyingi. Wanaweza kuwa; • Washauri wa misitu • Washauri wa Ukimwi kwenye jamii • Washauri wa kilimo • Maofisa mifugo kwenye jamii • Maofisa afya katika jamii • Wakunga wa jadi Lakini katika stori hii, tunazungumzia wale wanaohusika na kilimo tu. Maofisa ugani ni nani? Ofisa ugani ni mshiriki mkuu, anayeishi na kupata riziki kwenye jamii, lakini si lazima awe mzaliwa wa eneo hilo. Anatakiwa awe anapatikana na anaelewa uwezo, udhaifu na matarajio ya jamii hiyo kwa kutumia utaalamu alioupata na kuwa wakala wa kilimo. Awe anafahamu lugha, awe na uelewa halisi wa utamaduni, kanuni, mila na desturi za jamii hiyo. Awe na uwezo wa kuhamasisha kushawishi au kuwavutia wengine kutumia njia sahihi za kilimo kwa kuwafundisha, kuwatembelea na kuwaonyesha katika mchakato wa kufanya kazi zao za kilimo. Jamii ina nafasi kubwa katika kuchagua ofisa ugani Yapo mambo mengi ambayo jamii inatakiwa kushiriki katika mchakato wa kumchagua ofisa ugani. Haya ni machache tu; • Jamii iwe mstari wa mbele kushiriki kwenye uteuzi, ufuatiliaji na tathmini ya shughuli za maofisa ugani ili kuhakikisha ubora wa utoaji huduma. • Muhimu kujua mipaka ya huduma zinazotakiwa kutolewa na maofisa ugani. • Jamii itoe motisha kwa maofisa ugani kwa kutoa ushirikiano mzuri ili wafurahie kazi zao. Shughuli zao hizi hapa; Pamoja na kwamba maofisa ugani wana shughuli nyingi kwenye jamii, hizi ni baadhi tu; • Kutoa habari na kueneza teknolojia katika jamii • Kuunganisha jamii na masoko, jamii nyingine na watoa huduma • Kuhamasisha jamii kujifunza mambo mbalimbali • Kuwezesha uundwaji wa vikundi • Kutoa mafunzo katika jamii na kufuatilia • Kutoa ufafanuzi kwa kutumia mashamba yao wenyewe 12 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013 Swali; Je unawajua maofisa ugani wa eneo lako? Wanakusaidiaje? Jadili na wenzako na utuambie kwa kutuma ujumbe mfupi; andika SM acha nafasi, andikia maoni yako kisha tuma kwenda namba 15665 JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo! 13 SAUTI YANGU Kama una chochote unachotaka kusema tuandikie ili upate fursa ya kuwaelimisha wengine Si Mchezo! Femina HIP SLP 2065, DSM Maoni yaliyotolewa katika ukurasa huu ni ya wasomaji, si lazima yalingane na msimamo wa Femina. Wadada mnaojiuza badilikeni Migongano ya wafugaji na wakulima itakwisha lini? Serikali itusaidie kutatua suala la uhaba wa maji kwenye wilaya yetu ya Kilosa kwani hali hii inatusababishia kutokuelewana baina ya sisi wafugaji na wakulima pindi tunapotumia chanzo cha maji pamoja. Endapo kitatengenezwa chanzo kingine cha maji kwa ajili ya mifugo, itaepusha migongano na tutaishi kwa amani na upendo. Dani Zakayo Mumbi Kimamba, Kilosa Mabosi wengine ni kero! Kuna mabosi wengine ni wasumbufu sana hasa ukifika wakati wa kutoa posho au mishahara ya wafanyakazi wao. Mara ukatwe mshahara na kutafutiwa sababu zisizo na msingi ili mradi tu asikupe posho yako yote. Wakati mwingine anakuja na vitisho na kutaka ufanye naye ngono ndio akupe mshahara wako. Hii ni kero hasa kwa vijana wa kike walioajiriwa na wanaume. Eda Joseph Ibaraja Kilosa Tabia ya wadada wengine kujiingiza katika biashara ya ngono si jambo jema na linapingana na maadili ya Kitanzania. Mnatoa thamani ya utu wenu na kujidhalilisha kijinsia na kuwa watumwa. Mara nyingi wakihojiwa wanasingizia ugumu wa maisha lakini pesa wanayoipata haibadilishi mfumo wa maisha yao, bali huishia kununua mavazi na mapambo ili kuwavutia wateja wao. Elizabeth J. Mollel Kilosa Jembe ndiyo mpango mzima! Wewe pia unaweza kulonga na vijana wenzako. Tuandike maoni, ushauri, vichekesho,maswali nk, weka anuani yako na tuma ukiambatanisha na picha yako kwa Mhariri, Jarida la Si Mchezo!, S.L.P 2065 Dar es Salaam. [email protected] Au tumbukiza katika boksi la Si Mchezo! kama lipo katika eneo unaloishi. 14 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013 Vijana wenzangu tutumie sana ardhi aliyotupatia Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kilimo ili kitusaidie kwa maisha yetu ya kila siku na siyo kukimbilia mjini bila kuwa na mipango. Serikali iwafuatilie mawakala wa mbegu na dawa ili watusambazie bidhaa zenye ubora pia ikumbuke kuwa vijana ni Taifa la leo na si la kesho. Francis Denis Mtawatawa Kilosa Wazazi Nipende Advert Saumu dhi Buguruni, iu b A ais an , 19 a ak Mi DSM Ana ujauzito wa miezi “Niliamua kuja kliniki kujua kama mtoto aliye tumboni ni mzima, kupima damu pamoja na virusi vya ukimwi, kupewa dawa za malaria na vidonge vya kuongeza damu” “Nilimwambia mume wangu, siku ya kwanza alinileta hapa hospital kufanya vipimo” sita “Wanawake wajawazito waje kliniki kupata chanjo ili kuwakinga watoto kutokupata magonjwa, kujua afya zao kama hawana maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na kujua siku zao za kujifungua” Thuweba Abbas Miaka 27, anaishi Buguruni Kisiwani, DSM Ana ujauzito wa miezi nane na mtoto wa kike aitwaye Nahia mwenye miaka mitatu. ameolewa na Bw. Hassan Rashid mwenye miaka 30. “Nilikuja kliniki kupata huduma za afya na kutaka kujua mwanangu anaendeleaje, pia kupimwa damu na kujua umri wa mimba” “Kwa kuwa nilikuja mara ya kwanza kliniki na wifi yangu, alikuwa wa kwanza kujua nina ujauzito baada ya kupimwa. Niilipofika nyumbani nilimwambia mume wangu” “Akina mama waje kliniki kwa sababu ni hatari. Unaweza kujifungua bila kujua siku yako ila ukija hospitali unajua mambo yote” Salma Ally Tunu RBuagum aMaddenghe,aDSnM i a Saruni,liDSm Hali30,m i run M Miaka 20, anaishi anaishi Bugu Miaka 22, anaish i Buguruni, DSM Ana ujauzito wa miezi mitano. Ana mtoto wa kike Amina mwenye miaka sita, ameolewa na Hamis Said mwenye miaka 30 “Ni muhimu kwenda kliniki mara baada ya kugundua u-mjamzito. Nilikwenda kupata matibabu ili kukilinda kiumbe kilichopo tumboni. Nilipimwa Virusi vya Ukimwi, magonjwa ya zinaa pamoja na kupewa dawa za malaria na za kuongeza kiwango cha damu kwa kuwa nilikuwa na upungufu” Ana ujauzito wa miezi tisa. Ana mtoto Kiume Arafat mwenye miaka mitatu, Salama na mumewe Said Kassim wanaishi Buguruni, Dar es Salaam “Sababu ya mimi kuja kliniki ni kutaka kujua maendeleo ya ujauzito wangu na kufahamu mtoto anavyokua, wingi wa damu, kupima Virusi vya Ukimwi. Baada ya kupatiwa huduma huwa napatiwa kadi ndogo yenye tarehe ya kurudi” “Ushauri wangu kwa akina mama wajawazito na wale wanaopanga kuwa na watoto, waende kliniki kujua afya zao. Hii itawapa fursa kujua kama wana maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na kupewa ushauri wa namna ya kumlinda mtoto asipate maambukizi” “Mtu wa kwanza kumwambia nina ujauzito alikuwa mume wangu kwa sababu ndiye mtu wa karibu sana kwangu na mtu muhimu katika maisha yangu. Mume wangu ndiye mhusika mkubwa wa mimba hii. Lakini nakwenda kliniki peke yangu. Hajawahi kunisindikiza kutokana na kazi yake, mara nyingi huwa anakuwa safarini” “Mume wangu alikuwa wa kwanza kumtaarifu kwamba nina ujauzito. Alifurahi sana ukizingatia kwamba tumekaa muda mrefu bila kupata mtoto mwingine. Alizipokea habari hizi kwa mtazamo chanya” “Nawashauri akina mama wajawazito waende kliniki wapime afya na umri wa mimba zao. Pia wataweza kujikinga na maambukizi ya magonjwa kwa kupata kinga sahihi na ushauri toka kwa watoa huduma” Ana ujauzito wa miezi mitano. Ameolewa na Ramadhani Shabani ambae ana miaka 30 “Niliamua kuja kliniki ili kujua maendeleo ya ujauzito wangu, kupima damu na kujua kama nimeambukizwa VVU. Ningegundulika kuwa nina maambukizi ya VVU, ingekuwa rahisi kumlinda mtoto asipate maambukizi hasa wakati wa kujifungua. Nimepata ushauri mzuri sana kutoka kwa watoa huduma, na nina amani sana baada ya kujua sijaambukizwa VVU” “Hii ni mimba yangu ya kwanza. Nilimweleza mume wangu baada ya kugundua, yeye akamwomba dada yake anisindikize kituo cha afya kwa ajili ya kupima. Imekuwa ni vigumu yeye [mume wangu] kunisindikiza kutokana na majukumu ya kazi kwani inabidi awe dukani na hakuna mtu wa kumsaidia na hawezi kufunga duka” “Ushauri wangu kwa akina mama ni kwamba waende kliniki. Huduma ni nzuri, unapata kujua maendeleo ya afya zao. Pia nimefahamu damu yangu ni kundi gani, na nimeanza kujiandaa kwa kuwa nimefahamu tarehe ya kujifungua” Picha zote na Zechariah Mlacha Miaka Tuma SMS neno “mtoto” BURE kwenda 15001 kwa taarifa zaidi JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo! 15 BURUDANI Wimbo: Moro All Stars Wasanii: Afande Selle, Stamina, O – Ten,Belle 9,Samir, Chriss Wamaria, Nassa, Dynna na Zilla hapa kwetu mtapata furaha, x2 Urithi burudani vyote shwariiiiii, karibu mji kasoro, Udzungwa ujionee ehee hee hee hee hee heee he mwenyewe, Usisubiri usimuliweee, mwenyeweee (Yoo) Njooow Na na na na na na na naa na na na na naaa M-O-R-OOoh, moro town yeah! Home sweet home x2 (uuh) Ubeti wa kwanza - Stamina Chunga usipitilize stendi suka acha watu msamvu, Moro imenipa mengi, washkaji pesa na shavu, hatuna mpango na bahari, Mbona hata mindu ina fukwe, Milima kwetu fahari, mwaka mzima kwetu full kipupwe, Ausindile anoga ndio swagga za waluguru, hata ufunge kwa kuroga ila Moro itaniacha huru, sihitaji tena Baga utamu naupata Gairo, Masai wote huu wana swagga karibu kama upo Njiro, 16 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013 Toka enzi za Mbaraka mpaka wajukuu wa Mwinshehe, Mkude kusimama Pastor, Mbokeleni kuwa sheikh, Nina haki ya kujisifu, Moro imenipa kitalu, Namwaga Pombe kwa Chifu wa Moro Babu Kingalu, Sina bifu na Mngoni, Mpogoro ndio napodeka, Anzisha tifu ulingoni usande tukupe Cheka, Mliotutoka kimwili kiroho tupo pamoja, Karibu Moro mswahili uzalendo uende kwa hoja, (uuuuuh hu huuu) Kiitikio Karibu Morogoro, watu wote wa bara, visiwani mpaka Zanzibar, Bahari sio kasoro, wageni karibuni Ubeti wa pili – O - ten Yeah! mji unaweza poa, niko rock juu mlimani, Na mimi ndio mkuu wa mkoa karibuni madizini, Matonya alifukuzwa Dar breki ya kwanza akaja shaini, Mandela alikuwa shujaa, moro akaifanya maskani, Si unajua? Miji kibao haipati mvua, tofauti kubwa hapa kwetu inanyesha mpaka inaua, Mzinga, Ndigutu, Kichangani, Kiguru nyembe, hapa kwetu haina uzembe, Hata star anashika jembe, Natokea matombo kilosa narudi mzumbe, Nampitia Mkude, makala yuko wapi Msinde, Moro Bambam ila vichwa visivimbe, narudi shamba hata muziki nisiimbe, No, mi na moro tupo kama pacha, yes karibu moro tuishi kama kacha, Mbuga zipo na hata madini yapo, palipo na amani ndo mi nilipo Kiitikio Ubeti wa tatu- Afande Sele Morogoro,mjini kwetu, Karibuni wote rafiki na ndugu zetu(shua) Toka pande zote iwe ndani, mpaka nje ya nchi yetu, Karibuni kwetu mtembeee, harakati zetu mjionee, Kama mimi na mtu chee, kuna mashamba tunalimaga, Mboga mboga na mipunga, kuna mahindi, kuna matunda, viazi miwa na karanga, Karibuni nyote Morogoro mchote, hekima za Selemani mtangaze mataifa yote, Mkawaambie, mlichokiona hapa, mkawasimulie siri ya cheka kuwa chapa, Na habari kibao za wakali wa hapahapa, kwa soka kwa hip hop, ma streika marapa, Maboxer, madensa wote waliotoka hapa, wahapahapa, tangu kitambo kile, Kabla ya Afande Sele, Kabla ya O ten na Belle, kabla ya Supa Ngedere Moro Bado Chapa Ilale Ngoma inogile, tuna historia tele, hata Mwalimu Nyerere alikuwaga mbunge wa kwanza wa Moro miaka ile, kwa wasiotambua hilo. Karibuni Moro, hata tommorow karibuni mjionee maajabu ya mzimu wa Kolelo, Ifakara Kilombero, Turiani, Mvomero, Kilosa na Msowero, Masombo mpaka Gairo Yeaaah hii ndio Morogoro mpaka Nyachiro kwa mjomba Kobelo Na Mahenge kwa shangazi wa kipogoro, twende mahewaa Kiitikio Kibwagizo Morogoro mji kasoro bahari kwetu bado shwari Morogoro, Mgeta Mzumbe Mlali Moro imetulea Nilipokula gimbi na kachumbari, mwenzenu mimi naona fahari Hata ninapokwenda mbali nitarudi moro nyumbani Nimelelewa angali bado kichanga, bado mimi sijajua kuimba Mpaka sasa mimi natamba, tena Moro nimepata Mchumba mie x2 Nitazikwa Moro, Nitakufa Moro, Naipenda Moro, nitaishi Moro !! !! Muulize mama’ko... J Baba flani mlevi alirudi nyumbani mwake jioni akamkuta mwanawe anafanya ‘homework’. Mtoto akamuuliza babake, “Baba Indian ocean iko wapi?” Baba akajibu “Muulize mamako sababu ye ndio anapenda kusafisha nyumba saa zote,hata mimi viatu vyangu sivioni!” J Nakusaidia hata nikiwa gerezani Mzee mmoja alimtumia mjukuu wake aliyefungwa gerezani barua, na ilisomeka hivi:- Nafata chenji yangu! J Basi lilipata ajali katika daraja likazama kwenye mto...watu wakaanza kuogelea kujitoa nje. Jamaa mmoja akajitahidi kujitoa. Alipofika nje ya mto ghafla akavua nguo na kujitupa tena kwenye mto. Rafiki yake alipomuona akashangaa akamuuliza,”JUMA unaenda wapi?” JUMA,”Nataka kumtafuta konda... hajanirudishia chenji yangu!” “Mjukuu wangu mpendwa nina huzuni sana mwaka huu sitoweza kulima viazi kwenye shamba kwa sababu wewe uko gerezani na sina uwezo wa kulima shamba lote peke yangu”. Mjukuu alipopata barua akajibu hivi:“Babu usijaribu hata kidogo kulima hilo shamba...zile pesa zote nilizoiba nilizificha kwenye hilo shamba”. Mapolisi wa gereza walipoona ile barua kesho yake wakaenda kwenye shamba la mzee wakalilima lote wakitafuta pesa. Baada ya wiki mjukuu akamuandikia babu yake barua nyingine:“Unaweza kupanda viazi vyako sasa babu...unaona jinsi ninavyoweza kukusaidia hata nikiwa huku gerezani? JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo! 17 RUKA JUU Ruka Juu na jembe! Unakumbuka shindano la ujasiriamali la Ruka Juu, kwenye luninga mwaka 2010? Habari ya mjini ndio hii, Ruka Juu imerudi tenaaa… na sasa ni kuhusu vijana wanaofanya kilimo kama biashara. Kipindi kipya cha radio pia kitazinduliwa kikilenga kuelimisha kwenye masuala haya haya ya kilimo. Kilimo ni utajiri: Kila mtu ni lazima ale ili aishi, hakuna kazi nyingine yenye umuhimu kuliko kilimo. Soko la kilimo haliishi, kuna kipato kwenye kilimo. Lima kwa usahihi na ubora. Kilimo ni maisha: Chakula kinajenga miili yetu, kinatupa nguvu. Kwa kutumia chakula tunakua, tunakidhi njaa zetu, tunaponya magonjwa mbalimbali. Tupo tulivyo kwa sababu ya chakula. 18 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013 Kilimo ni uti wa mgongo: Unafahamu kuwa 85% ya Watanzania wanaishi kwa kutegemea ardhi? Muda umefika wote tuweke msisitizo kwenye kilimo na kukifanya kiwe na faida. Msimu mpya Msimu mpya utakaoanza kurushwa Machi, 2013, umejaa mambo kibao ya kijanja, tumezunguka sehemu mbalimbali Tanzania na kukutana na vijana wakulima ambao wako tayari kukushirikisha mbinu za kutoka na kilimo. Amabilis Batamula, mtangazaji wako wa msimu uliopita amerudi tena akiwa na Bwana Ishi anayetaka kuingia kwenye kilimo. Bila kumsahau Bahati, atawabahatisha wote watakaowasiliana nasi kupitia Wasiliana na Bahati Ubahatike. Kwenye redio utakutana na vijana wenzako; Michael Baruti na Rebeca Gyumi wakiwa tayari kukuelimisha kuhusu masuala mbalimbali ya kilimo. Hii si ya kukosa. Ardhi kubwa yenye rutuba: Nchi yetu imebarikiwa ardhi yenye fursa kibao za kuendeleza kilimo. Wakulima wajanja wanaofahamu nini cha kupanda wanaweza kubadilisha ardhi hii kuwa pesa. Kilimo Bomba! J Kum b uk a Unaweza kuita kilimo bomba au Kilimo Kwanza, kama kampeni inayoendeshwa na serikali. Tuungane wote na kukipa kilimo kipaumbele. Tulishe kizazi kijacho, tujenge maisha yetu. Kilimo siyo ushamba, kilimo ni ajira na kinaweza badili maisha yako. JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo! 19 NGUVU ZA MWANAmUME Imeshalipiwa hiyo, unaitaka? P wani kuna msemo unaosema “Ushalipiwa weye”ambao watu wengi wakiambiwa, hung’aka na kuwa wakali kama vile wamekula pilipili mbuzi. Ndiyo. Hata wewe unapopewa ofa zisizoeleweka na watu unaowafahamu au usiowafahamu. Kuwa makini. Chunga sana hizo ofa, wengi huwa wanakuja kudai vyao na kutaka vyako pia. Vijana wengi wa kiume hudhani kuwa ofa kwao ni “zali la mentali” na ni akina dada peke yao ndiyo wanaohongwa na hizo ofa huwatokea puani hao kina dada, Hapana! Hata wewe kidume unaweza kukumbwa na madhara yale yale ambayo yanaweza kuwakumba akina dada ukiangukiwa na hilo zali la ofa, mentali. Kupenda ofa husababisha: • Kuwa mtumwa wa ngono, hasa pale unapolazimishwa kulipa vitu ambavyo ulipewa kama ofa na huna uwezo wa kuvilipa, hii inakuweka katika mazingira hatarishi. • Vijana wengi kudhani kuwa zali la mentali litawadondokea na kufanikiwa kimaisha bila ya kufanya kazi na kuwajibika kikamilifu na matokeo yake ni kukosa ubunifu wa kukabiliana na changamoto za maisha na ‘fainali’ ni uzeeni. • Kutokuwa na misimamo thabiti juu ya maisha yako. • Kujiingiza katika tabia hatarishi. 20 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013 Jihadhari • Kama mtu usiyemfahamu anakupa ofa, kabla ya kukubali muulize kwanza ana lengo gani hadi anatoa ofa kwako. • Ni muhimu kutafakari mahusiano uliyonayo na huyo mtu anayekupa ofa J Ku m b uk a Ofa zinatengeneza mazingira ya kukosa utashi na ufinyu wa maamuzi. Tafakari kabla ya kutenda. NGUVU ZA MWANAMKE Wazazi nipendeni! Huzuni kubwa imetanda. Ni vilio huku na kule, wakubwa kwa watoto, wote wanalia. “Mama Wawili umetutoka, Mama Wawili” wanasikika wanawake wakilia. Mama Wawili, mwanamke mcheshi, mama wa watoto wawili amefariki wakati akijifungua mtoto wa tatu. Mtoto pia amefariki. Mama na mtoto kufariki wakati wa uzazi si mara ya kwanza kutokea katika kijiji hicho; na wala si jambo jipya nchini kwetu, lakini si jambo la kuvumilia. Ni wajibu wetu sote Pamoja na juhudi za serikali kuimarisha huduma za afya kwa wajawazito, mafanikio bado ni kidogo. Kina mama na watoto wengi wanaendelea kufa kutokana na matatizo wakati wa ujauzito na kujifungua! Ila serikali haiwezi kufanya juhudi za kupambana na tatizo hilo peke yake. Ni wajibu wa kila mmoja wetu, kama taifa zima, jamii, familia, baba wa mtoto na mama mjamzito pia. Kuhudhuria kliniki mapema ndiyo usalama wako! Kwa mjamzito ni muhimu kutambua mapema kwamba u-mjamzito. Hii itakusaidia kujiwekea mikakati ya jinsi ya kutunza mimba yako na maandalizi ya kuhakikisha kwamba unajifungua salama. Tufanyeje? Hakuna anayependa kifo, hasa pale uhai mpya unapotazamiwa kuchipua. Wazazi na jamii nzima mpendeni huyo mtoto kabla na baada ya kuzaliwa. Kliniki kwanza Mjamzito anatakiwa kuhudhuria kliniki katika wiki 16 (miezi minne) za kwanza za ujauzito. Pia mjamzito anatakiwa ahudhurie kliniki angalau mara nne katika kipindi chote cha ujauzito. Mahudhurio ya kliniki kwa wakati unaofaaa yatamuweka mjamzito pamoja na mtoto wake katika nafasi bora zaidi ya uzazi salama. Wazazi Nipendeni ni nini? Kampeni ya “Wazazi Nipendeni” ina lengo la kutekeleza kampeni ya kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi Afrika, kwa kuwawezesha wajawazito na wenza wao kuchukua hatua muhimu kwa afya ya mama mjamzito na uzazi salama. J Kum b uk a Maandalizi ni kitu muhimu kwenye kila kitu. Kwa mama mjamzito, maandalizi ya uzazi salama yanaanza kwa kuhudhuria kliniki mapema. JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo! 21 CHEZASALAMA Jipange, usije ukavuna mabua!... Baada ya kuisha kwa msimu wa mavuno, wakulima hupata muda wa kufanya tathmini na kupumzika kwa ajili ya kujiandaa na msimu mwingine wa kilimo. Kipindi hiki mara nyingi hutawaliwa na chereko chereko kwani mazao yanakuwa yameshauzwa na watu wameshavuta mkwanja wao na kuusunda kibindoni. Kinachofuata… Msimu wa sherehe Hapa ndio utasikia ‘vishughuli’ kila nyumba; • kumtoa mwali, • ngoma, • ndoa/harusi • Safari za kwenda mjini kusalimia ndugu Na siyo kwamba huwa zinafanyika hivihivi tu, bali wengine hutafuta hata sababu ili mradi tu wafanye sherehe. Hatari ipo jirani! Ushauri wa bure Utumiaji wa vileo kama vile pombe huongezeka sawa sawa na idadi ya wapenzi, ukizingatia pesa ipo. Kipindi hiki ndio utasikia, Tumia pesa ikuzoee, jenga heshima baa! Vipi lakini jembe, umeshajiandaa kwa kilimo katika msimu unaofuata? Una uhakika msimu unaokuja utakuwa wa neema kama huu ulioisha? Jihadhari kabla ya hatari! Ukilima na kuvuna, pesa inayopatikana ni bora ikaongezewa katika mtaji wa kilimo kwa kununua mbegu na pembejeo nyingine za kilimo. Kumbuka kuwa msimu wa kilimo ni mrefu zaidi kuliko msimu wa mavuno. Ni vyema basi ukajiandaa mapema kwa msimu unaofuata badala ya kujisahau na kujirusha kwa sana. 22 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013 Muhimu kuzingatia Baada ya kuuza mazao na kudaka huo mkwanja, tuliza ubongo na kujiongeza kifikra namna ya kujiletea maendeleo. Fikiria kuhusu biashara nyingine ambazo zinalipa msimu wa mavuno ili kujazia kwenye kilimo. Achana na mawazo potofu ya ushawishi kutoka kwa marafiki wanaokutaka mkapige ‘tungi’ au kushinda kijiweni kutwa nzima bila kuwa na shughuli ya kufanya. Msimu wa kilimo ni mfupi lakini ni mrefu kama hautakuwa makini upande wa matumizi ya fedha, Usije ukashtuka wakati jua ndio linaanza kuchwa, pasua kichwa. J K umb u ka Kuna mabadiliko ya hali ya hewa, mabadiliko ya bei ya mazao sokoni, mabadiliko ya bei za zana za kilimo na magonjwa ya mazao. Jipange kwa msimu ujao! JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo! 23 chakarika na jembe likutoe! K Michoro: babatau cartoons 2013 ijana Chema anatafuta jinsi ya kutoka kimaisha na washkaji. Ametoka kijijini kwenda mjini kucheza mdundo wa muziki wa mjini. Ni muziki gani huo? Je, atatoka? Fuatilia... baada kushindwa muziki wa mjini 24 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013 chama akikomaa na mteja balaa! kilimo kimejibu, chema anasafirisha mazao kwenda kuuza mjini JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo! 25 anakutana na washkaji, bado wanahangaika na mdundo wa muziki wa mjini Umeonaeee? Michongo ya maisha si lazima kuifukuzia mjini, hata kijijini ipo. Umemwona Chema? Wengine tulibugi kama Chema, tuko mjini tunasota, kila kukicha afadhali ya jana! Umeshafikiria kuhusu kilimo? Tafakari! 26 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013 UKWELI WA MAMBO Kilimo ni tumaini la wengi W engi wetu tumekuwa tukiimba nyimbo lakini hatuujui tunachezaje, kwa kuwa hata mdundo wake hiyo inatupiga chenga. Kwa kawaida kila wimbo una uchezaji wake na hivyo kama wimbo utabadilishwa ghafla basi ni wazi kuwa hata uchezaji utabadilika.Vijana wanakimbilia mjini wakidai kuwa eti kilimo hakilipi wakidhani mjini ndiko maisha bora yaliko. Twende sawa basi; • Vijana tukiachana na vurugu za mgambo wa jiji na kurudi mashambani tutakuwa na wimbo mmoja, tutacheza pamoja na kitaeleweka. • Tuanze kubadilika tuchangamkie kilimo cha umwagiliaji na kuacha kutegemea mvua za msimu • Tukope pesa kwenye asasi mbalimbali ili tuwekeze katika kilimo. J Ku m b uk a Tudadisi haya yanayotokea • Vijana kukimbilia mjini kumefanya kilimo kudumaa na kusababisha wakulima wengi na wengine ambao maisha yao yanategemea kilimo wakaanza kubadilisha wimbo • Wakati kilimo kinadumaa kutokana na vijana wenye nguvu kukimbilia mjini mambo yakabadilika na kutokea kwa nyimbo mbili tofauti. Ukaanza ule wimbo wa ukitaka maisha mazuri yapo mjini • Huko mjini nako vijana walikimbilia kazi ya kuuza nguo yaani umachinga, ulinzi n.k baadaye wakajikuta wakilazimika kuimba wimbo mmoja na askari wa jiji yaani Jeshi la Mgambo. • Sasa wimbo huu wa mgambo si wa kawaida kwani uliwafanya baadhi ya vijana kuukumbuka ule wa shambani ambao ulikuwa rahisi hata kuucheza. Wapo vijana ambao wameweza kunufaika kupitia kilimo na sasa wanaendesha maisha yao vizuri. Usikubali kuachwa nyuma, kilimo ndio mdundo wa uhakika! JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo! 27 sema. tenda! Kilimobiashara ni zaidi ya ujuavyo M engi yanasemwa kuhusu kujihusisha na kilimo. Wengine wanakandia kilimo na saa nyingine wana sababu ambazo zinaweza zikakushawishi kukubaliana nao. Tulitia timu Kilosa na tukachonga na vijana kuhusiana na kilimo, soko lake, namna ya kujiendeleza katika kilimo na kadhalika. Changamoto zinazo wakabili wakulima ni hizi • Wakulima wengi wanalima bila kuwa na malengo • Hakuna mfumo wa taarifa za masoko kuwawezesha wakulima kujua watauza wapi • Elimu ndogo juu ya jinsi ya kuongeza thamani mazao wanayolima kama vile usindikaji • Hakuna utunzaji mzuri wa mazao • Kutojua umuhimu na faida za kujihusisha kwenye vikundi na taasisi za kifedha kama vile SACCOS na VICOBA • Kutokuwa na uwezo wa kupanga bei ya mazao • Miundombinu duni hasa ya barabara na mawasiliano mbovu • Ukosefu wa vyombo vya usafirishaji kutoka maeneo ya uzalishaji • Kutojua namna ya kutumia simu za mikononi kibiashara katika kupata taarifa • Ubora wa mazao kupungua pale yanapofika sokoni Mbegu mbalimbali za mahindi Moja ya pembejeo za kilimo ambao ni mbolea ya chumvi chumvi kwenye moja duka la pembejeo za kilimo, katika Kijiji cha Msalabani, Kilosa 28 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013 Nini kifanyike? Kikundi cha Jitegemee wakiwa mbele ya duka la mmoja wa wanakikundi hicho. Hawa wanajihusisha na kilimo biashara Matokeo yake ni nini? • Vijana wengi hukata tamaa kujishughulisha na kilimo kwa madai kwamba hakilipi • Wakulima hukata tamaa kuendeleza kilimo hata kuuza mashamba • Vijana kukimbilia mijini bila kuwa na malengo • Wengi hulima kwa ajili ya chakula tu • Sekta zinazohusika zitoe elimu ya kilimo biashara ili wakulima wanufaike na kilimo • Kuwe na msukumo wa matumizi ya teknolojia sahihi za kilimo kama vile kilimo cha umwagiliaji, mbegu sahihi kulingana na udongo na hali ya hewa ya eneo lako. • Wakulima wajifunze namna ya kutafuta masoko na biashara juu ya kilimo stahiki kinacholenga hitaji la soko na walaji • Kuwaunganisha wakulima kwenye masoko kwa kutumia teknolojia na mawasiliano mfano vipindi vya redio na simu za mkononi • Kufanye tafiti za kuendeleza kilimo biashara • Miundombinu ya barabara, vyombo vya usafiri n.k iboreshwe • Elimu ya usindikaji itolewe kwa wakulima • Suala la kilimobiashara lipewe kipaumbele katika ngazi zote ili wakulima waweze kuingia katika soko la ushindani • Huduma za pembejeo za kilimo zisogee zaidi vijijini na ziwalenge wakulima Swali Je, ni changamoto zipi wanazokutana nazo wakulima wa eneo lako? Unadhani nini kifanyike kutatua changamoto hizo? Tuambie kwa kutumia mawasiliano hapa chini: Barua pepe: [email protected] Sms: andika SM acha nafasi, andikia maoni yako kisha tuma kwenda namba 15665 S.L.P. 2065, Dar es Salaam. JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo! 29 MARIE STOPES Waelimishaji rika Zanzibar, walia na utoaji mimba Suala la utoaji mimba kwa njia zisizo salama, limekuwa likipigiwa kelele kila mara hapa Tanzania. Vijana waelimishaji rika huko Zanzibar wamefunguka na kuwaomba wazazi, viongozi wa dini na Serikali kuwasaidia kupambana na vifo vitokanavyo na utoaji mimba usio salama. Kuna madhara ukijihusisha na uhusiano wa kimapenzi kwenye umri mdogo • Kupata mimba katika umri mdogo • Kujiingiza katika mazingira hatarishi ya kutoa mimba kwa njia zisizo salama. • Kujishushia heshima mbele ya jamii yako • Kujiongezea majukumu katika umri mdogo Vijana hao wametoa ushauri huu... Muelimisharika akizungumza na wazazi kuhusu madhara ya utoaji mimba. Kuna usiri mkubwa “Vijana wengi hushirikiana kutoa mimba kwa kutumia miti shamba,” alisema mmoja wa waelimishaji rika. Akaongeza, “vitendo hivi hufanyika kwa kificho sana ili wazazi na jamii kwa ujumla isijue. Hii hupelekea hatari ya vifo pale watoaji wanapozidiwa.” Walizungumzia pia kuhusu mila na desturi za jamii yao kuwa zinamzuia kijana kuanza mapenzi kabla ya ndoa, kwa hiyo vijana hutoa mimba mafichoni na kwa usiri ili kuepuka aibu na adhabu. Kwa huduma za kuokoa maisha kwa walioharibikiwa mimba fika kituo cha Marie Stopes Tanzania kilichopo Kilimani Mnara wa Mbao au kliniki yoyote ya serikali. Kwa mawasiliano piga 0767160038 au tuma ujumbe au kwa njia ya baruapepe [email protected] 30 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013 • Wazazi kuwa karibu na vijana ili kuwafundisha kuhusu afya ya uzazi kwa kuwaruhusu kupata elimu hiyo kwenye vituo vya afya ya uzazi. • Serikali na viongozi wa dini mbalimbali walihimizwa kuweka sera itakayomlinda kijana hasa wa kike kupata huduma bora hasa baada ya mimba kuharibika ili wasipoteze maisha. Jamii pia ielimishwe juu ya matumizi ya njia za uzazi wa mpango. J Ku m b uk a Maandalizi ya mafanikio ya baadaye ya kijana, huanza akiwa mdogo. Sote tuwalinde vijana ili tuwe na Taifa lenye vijana wanaofaidi matunda ya malezi ya wakubwa wao. USHAURI Mimi ni msichana wa miaka 24. Nilibahatika kumpata mvulana ambaye tulianza Swali uhusiano. Katika uhusiano wetu sikuwa na haraka ya kutambulishwa kwani nilijua kila kitu kinakwenda na wakati. Mpenzi wangu aliniambia anakaa na mama yake na dada yake na mimi nilimweleza kuwa naishi na mama. Baada ya miaka miwili pamoja ndipo nilipogundua kuwa mpenzi wangu ameoa na ana mtoto mmoja. Mama alinishauri niachane naye lakini nampenda sana huyo kijana na sidhani kama kuna mwanamume atakayechukua nafasi yake. Naomba ushauri. Msomaji wa Si mchezo, Mburu-Manyara. Tafuta muda ukae naye, muulize kama yupo tayari kuendelea na mwanamke aliyezaa naye au kuwa na wewe na akupe sababu za msingi kwa nini amemchagua aliyemchagua, ndipo ufanye maamuzi. Abdulrazaaq Ngowo Kilosa Nashukuru kwa swali. Ukweli ni kwamba mtu anayekupenda kwa dhati hawezi kukudanganya huyaweka mambo yake wazi ili muweze kuyajadili pamoja. Ingawa unampenda sana jiulize; ‘kwa mfano mimi ningekuwa mke wa huyu bwana nitakaposikia habari hizi nitajisikiaje?’ Pia kumbuka kwamba mahusiano na watu wengi, kama anavyofanya huyo mwanaume huchangia sana katika kueneza magonjwa ya zinaa pamoja na VVU. Tafakari kabla ya kuchukua hatua hata kama unampenda. Asante. Ningependa kukwambia uondoe mawazo kwake na amini kuwa yupo mvulana mwenye mapenzi ya kweli, na muaminifu na huyo ndiye atakayekufaa. Vumilia tu utampata. Mwanahamisi Rajabu Kilosa SWALI LA TOLEO LIJALO Nina miaka 21, nina rafikiwa kike ambaye tumejuana kwa muda wa mwaka mmoja hadi sasa. Nampenda ila naogopa kumueleza kwani nitavunja urafiki wetu. Pia kuna mwanamke anayenipenda sana ila mie simpendi na yupo jirani sana na mimi kuliko yule nimpendae ambaye ni rafiki yangu, vijana wenzangu naomba mnishauri nifanye nini katika suala hili? Hantish Jozack Njombe. Huyo hana mapenzi ya kweli kwako, mpe nafasi mwingine, utampata anayekupenda. Umeshajifunza, kwa huyo mwingine utakuwa makini zaidi. Pili George Kilosa Kama unaishi naye sehemu moja ondoka ili kumsahau kirahisi. Jishughulishe na kazi na siyo mapenzi. Ukisema ukae nae bado itakusumbua kwani bado utakuwa kama mke mwenza na utaumia zaidi. Steven F. Mbwiss Kilosa Betty Liduke ni rafiki mkubwa wa vijana, hata wewe unaweza kulonga naye. Ni msambazaji mkubwa wa Jarida la Si Mchezo! Mkoani Njombe. Ni mshauri nasaha na ni Mratibu wa Kitengo cha Udhibiti Ukimwi katika Kampuni ya TANWAT, Njombe. Mwandikie kupitia Jarida la Si Mchezo! Si Mchezo! S. L. P. 2065 Dar es Salaam SMS; andika SM acha nafasi andika ujumbe wako kisha tuma kwenda namba 15665 na utuambie kama ungependa uchapishwe. JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo! 31