NORTH EASTERN DIOCESE
Transcription
NORTH EASTERN DIOCESE
NORTH EASTERN DIOCESE EVANGELICAL LUTHERAN CHURCH IN TANZANIA CLINICAL OFFICERS TRANING CENTRE BUMBULI Tel: +255-27-2640360 Tel:+255-27-2640360 Fax: +255-27-2640360 P.O.Box 9, Bumbuli, Tanzania. Email:[email protected] Kumb Na: COTC/BK/1/____________ 01ST /08/2014 _________________________________________ _________________________________________ _________________________________________ Yah: MAFUNZO YA KUJIENDELEZA KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015 Napenda kukuarifu kuwa umechaguliwa kujiunga na mafunzo ya Clinical Officer katika chuo hiki. Mafunzo yaha ni ya miaka miwili. Mafunzo yaataanza tarehe 6th, Oktoba, 2014. Unatakiwa ufike chuoni siku mbili kabla ya masomo kuanza. Napenda ieleweke kwamba nafasi yako itahesabika kupotea kabisa na kujazwa na mtu mwingine endapo hautafika katika kipindi kilichotajwa. Gharama za mafunzo, unatakiwa kulipa ada kiasi cha shilingi (TZS.1, 900,400.00) kwa mwaka. Unaweza kulipa gharama hii kwa awamu moja au mbili. Malipo yote ya Ada ni kupitia Benki katika akaunti ya chuo, NMB Lushoto, ELCT NED CLINICAL OFFICERS TRAINING CENTRE A/C.No: 4161300005. Kabla ya kwenda choni hakikisha afya yako imepimwa na kupata cheti (medical certificate) kutoka kwa Daktari., Cheti hicho itakubidi ukikabidhi kwa Mkuu wa Chuo mara tu ufikapo chuoni. Wakati wote utakapokuwa chuoni unatakiwa kutii sheria za nchi na za chuo. Vilevile ieleweke kwamba masuala yote ya mwanfunzi anapokuwa chuoni yatashuhulikiwa na Uongozi wa chuo, endapo itakuwepo lazima ya suala la mwanafunzi kughulikiwa na Wizara makao makuu, basi maombi au matatizo yote yapitie kwa Mkuu wa Chuo kabla ya kuwasilishwa. Utaratibu wa matibabu yote yatagharamiwa na mwanafunzi mwenyewe kupitia bima ya taifa ya afya. Page 1 of 3 Usafiri wa kwenda na kurudi chuoni ni gharama ya mwanafunzi na wala si jukumu la Chuo. Hakikisha unakuwa na fedha za kutosha kwa asjili ya mwatumizi yako madogo madogo kwa kipindi utakapokuwa chuoni. Kila mwanafunzi anatakiwa kufika chuoni na vifaa vifuatavyo:SARE ZA CHUO: Mwanamke: Magauni mawili (2) meupe ya mikono mifupi, viatu vyeupe, vyeusi au kahawia vyenye visigino vifupi. Mwanaume: Suruali mbili (2) za rangi ya khaki na mashati mawili rangi nyeupe ya mikono mifupi. Viatu vya ngozi nyeusi au kahawia. UNATAKIWA KUJA NA MAHITAJI YAFUTAYO: 1. Nguo za michezo mbalimbali 2. Ndoo ya maji aina ya “Plastic” 3. Picha nne(4) Passport size kwa ajili ya kumbukumbu. 4. Cheti halisi cha cha kuhitimu kidato cha nne 5. Vitabu katika kozi husika inapowezekana. 6. Vifaa vya kuandikia kwa mfano madaftari, kalamu, rula n.k. 7. Mwamvuli au koti la mvua. 8. Viatu aina ya Buti za mvua 9. Shuka - 4, mto -, blanketi -1, chandarua -1, taulo na foronya MWONGOZO WA GHARAMA/AINISHO LA ADA S/R ITEM 1 TUITION FEES 2 GHARAMA YA MITIHANI WA KUHITIMU 3 IDENTITY CARD 4 PRACTICAL PROCEDURE BOOK 5 PRACITICUM GUIDE BOOK 6 HEALTH INSURANCE 7 SPORTS 8 CAUTION MONEY 9 NACTE STUDENT REGISTRATION FEES 10 APPLICATION FORM TOTAL AMOUNT COST 1,550,000.00 150,000.00 5,000.00 50,000.00 30,000.00 50,400.00 10,000.00 10,000.00 15,000.00 30,000.00 1,900,400.00 Page 2 of 3 2 MAHALI PA KUISHI MWANAFUNZI 3 Kila mwanafunzi atagharamia mahali pa kuishi kipindi chote atakapokuwa chuoni. Gharama kwa mwezi ni shilingi hamsini elfu tu (TZS.50, 000.00). Kwa muhula ni shilingi laki mbili hamsini elfu tu (TZS.250,000.00) Hivyo basi gharama kwa miezi kumi mwanafunzi atakapokuwa chuono ni shilingi Laki tano tu (TZS.500, 000.00). Fedha hizo zitalipwa katika akaunti ya chuo. Fedha hizo zaweza kulipwa kwa mara moja au awamu mbili kupitia akaunti ya chuo kama ilivyoelekezwa katika ukurasa wa kwanza. CHAKULA CHA KILA SIKU Kila mwanafunzi atagharamia chakula chake kwa kununua katika mgahawa wa chuo kwa fedha tasilim. MAELEKEZO KUHUSU MAHALI CHUO KILIPO Chuo kinapatikana Bumbuli katika halmashauri ya Bumbuli wilaya ya Lushoto. Ukiwa Dar es Salaam pakia Basi la Bumbuli Ukiwa Arusha/Moshi/Tanga pakia basi la Bumbuli Au pakia basi hadi Mombo au Soni halafu panda mabasi ya kuelekea Bumbuli Nakutakia kila kheri katika mafunzo yako Dr. Ronald Erasto Msangi MKUU WA CHUO Page 3 of 3