de pita tangas
Transcription
de pita tangas
THE UNITED NATIONS CHILDREN'S FUND – UNICEF TANZANIA KIVUNGE CHA MKAKATI WA MAWASILIANO KATIKA KUKABILIANA NA MAAFA FEBRUARI, 2013 YALIYOMO DIBAJI ...................................................................................................................................................... 1 WILAYA YA MAGHARIBI, UNGUJA- MAFURIKO ........................................................................ 16 WILAYA YA KINONDONI, DAR ES SALAAM-MAFURIKO ......................................................... 24 WILAYA YA HANDENI, TANGA-MLIPUKO WA KIPINDUPINDU .............................................. 28 WILAYA YA KILOSA, MOROGORO-MAFURIKO .......................................................................... 32 WILAYA YA MICHEWENI, PEMBA-UKAME.................................................................................. 36 WILAYA YA KINONDONI, DAR ES SALAAM-MAFURIKO ......................................................... 40 WILAYA YA LONGIDO, ARUSHA-UKAME .................................................................................... 44 WILAYA YA MAGHARIBI, UNGUJA-MAFURIKO ......................................................................... 48 KIAMBATANISHO No 1: UJUMBE MHIMU NA NJIA ZA MAWASILIANO ZINAZOTUMIKA KWA SASA NA NJIA MPYA ZILIZOPENDEKEZWA KUTUMIKA ................................................... 51 ii DIBAJI Kivunge hiki kimetayarishwa kutokana na mkakati wa mawasiliano wa kukabiliana na maafa uliotayarishwa kwa ajili ya wilaya sita ambazo ni Micheweni, Pemba (Ukame), Magharibi Unguja (Mafuriko), Longido, Arusha (Ukame), Handeni, Tanga (Milipuko ya kipindu pindu), Kilosa, Morogoro (Mafuriko) na Kinondoni, Dar es Salaam (Mafuriko). Kivunge hiki kimetayarishwa ili kusaidia kupashana habari muhimu na walengwa ambao wengi wao ni waathirika wa ukame, mafuriko na milipuko ya magonjwa ya kipindupindu kabla, wakati na baada ya majanga hayo kutokea. Kivunge hiki pia kinatoa taarifa ambazo zinaweza kutumiwa moja kwa moja na walengwa ambazo zitaweza kuwasilishwa kupitia njia mabali mbali za mawasiliano kama vile Redio, Televisheni, mtandao wa intaneti, simu za mkononi, magazeti, vipeperushi na posta ambazo zinaweza kuwekwa kwenye mabango makubwa. Kivunge hiki kina jumla ya skripti (script) 24, kila skripti inabeba ujumbe mhimu ambao unaweza kuwasilishwa na kuwafikia walengwa kwa njia ya Redio na Televisheni. Kivunge hiki pia kimesheheni vikaragosi (Cartoons) 24 ambavyo vimeandaliwa kufikisha ujumbe kwenye wilaya zote sita. Kivunge hiki kimeandaliwa kwa lugha ya Kiswahili ili kuweza kuwafikia walengwa wengi kwa urahisi. 1 WILAYA YA HANDENI, TANGA – MILIPUKO YA KIPINDUPINDU TANGAZO LA REDIO 1 WAHUSIKA : SAMBONI NA LUKA MAHALI : KIBANDA CHA CHIPS/BAR SAUTI NA MILIO : HONI NA NGURUMO ZA MAGARI NA KELELE ZA WATU 1. SEKIMWEI : Hizo Chips vipi? 2. SAUTI NA MILIO : MTU AKINAWA MIKONO 3. SEKIMWEI : Wewe mbona haya maji baridi? 4. LUKA : Kwani yana tatizo gani?, nawa mzee nina wateja wengine wananisubiri. 5. SEKIMWEI : Wewe mgonjwa nini? Unataka kutuua wenzio na kipindupindu. Hao wateja wote watakuwa hawaji hapa kwako kama wataugua Kipindupindu na magonjwa ya kuhara. 6. LUKA : Mzee unanizingua bwana. Hii biashara bwana! Maji ya kunawa ya moto nyumbani kwako. 7. SEKIMWEI : Unasemaje? Wewe mjinga tunatakiwa kunawa mikono kwa maji ya moto na sabuni kabla ya kula ili kuua vijidudu vya Kipindupindu na magonjwa ya kuhara,…lazima ujue kijana wangu la sivyo Kipindupindu hakitakoma hapa kwetu au naongea uongo ndugu zangu? 8. WATU : Uko sawa kabisa mzee mwenzetu. 2 TANGAZO LA REDIO 2 WAHUSIKA : SEKIDIA NA MA’ MHANDO MAHALI : KWA SEKIDIA SAUTI NA MILIO : MILIO YA KUKU NA MBUZI 1. MA’MHANDO : Shemeji uani ni wapi? Naona tumbo haliko vizuri. 2. SEKIDIA Subiri kidogo shemeji nakuja : 3. SAUTI NA MILIO: MLANGO UNAFUNGULIWA. 4. MA’MHANDO : Haaaaa!!! Shemeji unanipa jembe maana yake nini? 5. SEKIDIA Zunguka hapo nyuma kwenye migomba kule, chimba : jisaidie huko utuwekee mbolea. Hatujachimba choo shemeji……. wenyewe tumezoea. Watu wote huku wanajisaidia porini. 6. MA’MHANDO : Shemeji….shemeji haaaaa, karne hii ya digitali bado mnajisaidia porini…… aaaaah ndio maana huku kwenu Kipindupindu na Magonjwa ya Kuhara hayaishi, Shemeji Sekidia… ili muweze kuepukana na milipuko ya Kipindu pindu ni kutumia choo… Kipindupindu husambaa kwa haraka kupitia uchafu na vinyesi. Shemeji chimba choo, hii ni hatari kwa usalama wa maisha yenu. 7. SEKIDIA : 8. MA’MHANDO : Nimekusikia Shemeji yangu, nitalifanyia kazi Choo ni muhimu sana kwa maisha yenu, siondoki mpaka nihakikishe umechimba choo, uwe mfano kwa wana jamii wenzio. 3 TANGAZO LA TELEVISHENI 1 NJE : KIBANDA CHA CHIPS : JIONI : MJI : Kinaonekana Kibanda cha Chips, wanaonekana watu kadhaa wakiwa wamekaa wanakula Chips, mishikaki na Kuku. Mmoja wapo wa watu hawa ni mzee Samboni, amekaa akionekana akiwa anasubiri huduma, anaonekana Kijana muuza Chips Luka akimletea Chips Mayai na Mishikaki Miwili, anaweka sahani kwenye Meza na kuanza kumnawisha. SAMBONI Wewe mbona haya maji Baridi LUKA Kwani yana tatizo gani, nawa mzee nina wateja wengine Wananisubiri. SAMBONI Wewe mgonjwa nini? Unataka kutuua wenzio na kipindupindu. Hao wateja wote watakuwa hawaji hapa kwako kama wataugua Kipindupindu na magonjwa ya kuhara. LUKA Mzee unanizingua bwana. Hii Biashara bwana. SAMBONI Tunatakiwa kunawa mikono kwa maji moto na sabuni kabla ya kula ili kuua vijidudu vya Kipindupindu na magonjwa ya kuhara, lazima ujue kijana wangu la sivyo Kipindupindu hakitakoma hapa kwetu au naongea uongo ndugu zangu? Anawaangalia wateja wengine huku na wenyewe wanaonekana kukubaliana nao, Luka nae anaonekana kukubaliana na Mzee Samboni. 4 TANGAZO LA TELEVISHENI 2 NJE : JIONI : MBELE YA NYUMBA YA SEKIDIA : MTAANI : KIJIJINI : Inaonekana Nyumba ya kawaida tu ya udongo lakini imepigwa Lipu, anaonekana mama Mhando akiwa anaongea na Mzee Sekidia, anaonekana mama Mhando akisimama, MAMA MHANDO Shemeji uani ni wapi? Naona tumbo haliko vizuri. SEKIDIA Subiri kidogo shemeji nakuja Anaonekena Sekidia akiingia ndani, Kisha anatoka akiwa na Jembe mkononi na kopo la maji, Mama Mhando anaonekana Kushangaa. SEKIDIA Zunguka hapo nyuma kwenye migomba kule, chimba. Hatujachimba choo. Wenyewe tumezoea. MAMA MHANDO Shemeji….shemeji haaaaa, karne hii ya Digitali bado Mnajisaidia porini…… aaaaah ndio maana huku kwenu Kipindupindu na Magonjwa ya Kuhara hayaishi, Shemeji Sekidia… ili muweze kuepukana na milipuko ya Kipindu pindu ni kutumia choo… Kipindupindu husambaa kwa nguvu na haraka kwa kupitia uchafu na vinyesi. Shemeji chimba choo, hii ni hatari kwa usalama wa maisha yenu. SEKIDIA Nimekusikia Shemeji yangu. 5 WILAYA YA MICHEWENI, PEMBA – UKAME TANGAZO LA REDIO 1 WAHUSIKA : MWINCHANDE NA KIDAU MAHALI : SHAMBANI SAUTI NA MILIO : SAUTI ZA NDEGE NA WADUDU 1. SAUTI NA MILIO: MLIO WA PANGA AU SHOKA LIKIKATA MTI 2. KIDAU We Mwinchande weye … mzima kweli weye? : 3. MWINCHANDE : Kwani vipi? Waniona natakiwa pelekwa kwa Dokta au kwa Fundi. 4. KIDAU : Yaani weye ukame wote huu bado wakata mti, wenzio twasisitiza watu wapande miti mpaka kwenye majumba yao wewe wakata, mtumeeee…. Halafu mwembee wazaa huu ! 5. MWINCHANDE : Huu mti ni wangu, nimechoka fukuzana na watoto na watu wazima wanaokuja niibia embe zangu, bora niukate tuu…mwenbe wangu lakini wanao faidi wengine. 6. KIDAU : Huo ni uamuzi wa kitoto….. 7. MWINCHANDE: Kwa hiyo waamua ntukana sasa? Si ndiyo? 8. KIDAU Wala sikutukani, ila ntaka nikuambie, ili kuepukana na ukame : twatakiwa panda miti kwa wingi, hata mpaka kwenye maeneo ya majumba yetu, tupande miti kila mahala….. acha hasira weye. Au wewe huoni ukame huu. 9. MWINCHANDE : Nauona, ni kweli jua la waka, basi nauacha, ahsante sana Bwana Kidau. 6 TANGAZO LA REDIO 2 WAHUSIKA : MAMA JUMBE NA MAMA CHANDE MAHALI : KWA MAMA JUMBE SAUTI NA MILIO : SAUTI ZA KUKU 1. MA’CHANDE : Hodi hapa…… za hapa? 2. MA’JUMBE : Hapa kwema, haya mwanamke weye na kikapu watokea wapi? 3. MA’ CHANDE : Natokea hapo kwa duka la pembejeo natoka nunua mbegu za mahindi, kesho nipande. 4. MA’JUMBE : Na ukame huu bado tu unapanda mahindi, unachekesha. 5. MA’CHANDE : Sasa wewe ulitaka nipande nini? miwa? 6. MA’JUMBE : Mazao yanayovumilia ukame mwanamke wewe, si unaona mwenzio hapa, nina mtama hapa na pale nina mihogo, haya mazao yanavumilia ukame, kwa hali kama hii ni vizuri tupande mazao yanayo himili ukame. 7. MA’CHANDE : Mmmmh!!! Lakini kweli maana hali si hali, jua kali kama nini sijui, lakini tutakula nini sasa mihogo tu na mtama? 7 TANGAZO LA TELEVISHENI 1 NJE : ASUBUHI : SHAMBANI : Aaonekana Bwana Mwinchande akiwa na Panga lake mkononi akiwa Shambani kwake akikata Mti mkubwa wa mwenbe, anaonekana Bwana Kidau akiwa anapita mkononi na yeye akiwa na Panga na kiroba kimekunjwa kunjwa, anasimama na kushangaa, anasogea kabisa alipo Mwinchande, KIDAU We Mwinchande mzima kweli weye? MWINCHANDE Kwani vipi? Waniona natakiwa pelekwa kwa Dokta au kwa Fundi KIDAU Yaani weye ukame wote huu bado wakata mti, wenzio twasisitiza watu wapande miti mpaka kwenye majumba yao wewe wakata, mtumeeee. MWINCHANDE Huu mti ni wangu, nimechoka fukuzana na watoto na watu wazima wanaokuja niibia Embe zangu, bora niukate tuu… mwenbe wangu lakini wanao faidi wengine. KIDAU Huo ni uamuzi wa kitoto….. MWINCHANDE Kwa hiyo waamua ntukana sasa? KIDAU Wala sikutukani, ila ntaka nikuambie, ili kuepukana na ukame twatakiwa panda miti kwa wingi, hata mpaka kwenye maeneo ya majumba yetu, tupande miti kila mahala….. acha hasira weye. Au wewe huoni ukame huu. MWINCHANDE Nauona, basi nauacha, ahsante sana bwana Kidau. 8 TANGAZO LA TELEVISHENI 2 NJE : JIONI : KANDO YA NYUMBA : Ni nyumbani kwa Mama Jumbe, anaonekana amekaa kwenye kivuli cha nyumba, anapeta Mtama, kwa kando yake kunaonekana lundo la miti ya Mihogo, ikiwa imekatwa katwa vipande, anaonekana Mama Chande akiwa anaelekea alipo kaa Mama Jumbe, akiwa na kikapu mkononi. MAMA JUMBE Haya mwanamke weye na kikapu watokea wapi? MAMA CHANDE Natokea hapo kwa duka la pembejeo natoka nunua mbegu za Mahindi, kesho nipande. MAMA JUMBE Na ukame huu bado tu unapanda mahindi, unachekesha. MAMA CHANDE Sasa wewe ulitaka nipande nini? MAMA JUMBE Mazao yanayovumilia ukame mwanamke wewe, si unaona mwenzio hapa, nina mtama hapa na pale nina mihogo, haya mazao yanavumilia ukame, kwa hali kama hii ni vizuri tupande mazao yanayo himili ukame. 9 WILAYA KILOSA, MOROGORO – MAFURIKO TANGAZO LA REDIO 1 WAHUSIKA : MAMA MKUDE, WATU NA MTU 1 MAHALI : MKUTANONI SAUTI NA MILIO : KELELE ZA WATU 1. MWENYEKITI WA KIJIJI : Tusikilizane jamani, tumeitisha mkutano huu ili tuweze kuzungumzia athari za mafuriko katika eneo letu na hapa tunaye kiongozi kutoka wilayani. 2. MA’MKUDE(Afisa Tawala Wilaya): Jamani tunaomba sana ushirikiano wenu, bila nyinyi sisi serikali tutakuwa tunafanya kazi bure, ndugu zangu Mjenga nchi……….. 3. WATU : Ni Mwananchi 4. MA’MKUDE : Na mvunja nchiiiiiiiiiiii!!!!!!! 5. WATU : Ni huyo huyo Mwananchi 6. SAUTI NA MILIO : WATU WANAPIGA MAKOFI NA VIGELEGELE 7. MA’MKUDE : Jamani tunawaomba sana acheni kulima kankando ya mto Mkondoa, acheni kuchungia mifugo yenu kando ya mto Mkondoa, hayo yote yana sababisha mmomonyoko wa udongo na hatimae husababisha mafuriko. 8. MTU 1 : (KWA KUROPOKA) Sasa unataka tulime wapi na kuchungia wapi wakati yale ndio maeneo yenye rutuba na majani mazuri! 9. MA’MKUDE : Jamani sikilizeni maeneo ya Kulima na kuchungia yapo mengi sana. Sasa nasema hivi atakaye kwenda kinyume na amri hii akikamatwa sheria itachukua mkondo wake, tumetunga sheria ngumu ili tuweze kuulinda mto wetu. Tumechoshwa na mafuriko katika Wilaya yetu; 10 tukiachia tabia hii iendelee ni sawa na kulipa dudu liumalo………… 10. WATU : Kidole 11. MA’MKUDE : Si ndio jamani………..? 12. HADHARA : Ndiooooooooooooooooooooo!!! 11 TANGAZO LA REDIO 2 WAHUSIKA : SEKULU, MLOKA NA MAMA MLOKA MAHALI : KWA SEKULU SAUTI NA MILIO : MBUZI NA KUKU 1. SEKULU : Mloka na Shemeji Ahsanteni sana kwa ushauri wenu. 2. MLOKA : Tunakushauri mengi Sekulu lipi hasa unalotushukuru? 3. SEKULU : Hili mliloniambia kwamba kusombewa vitu na mafuriko sio mwisho wa maisha, nikakakope kamkopo kadogo, imenisaidia nyumba ndio hii na biashara zangu zinaendelea vizuri maana mafuriko ya mto Mkondoa yalinisombea kila kitu. 4. MA’MLOKA : Umeamini sasa Shemeji kukumbwa na mafuriko, sio mwisho wa maisha. 5. SEKULU : Ni kweli, Shemeji…. Binadamu hutakiwi kukata tama, na mimi nitawashauri wenzangu wakikutwa na hali kama yangu ya kukumbwa na mafuriko wasikate tama, maisha yanatakiwa kuendelea……….kukatika kwa koleo sio mwisho wa………….. 6. MLOKA NA MAMA MLOKA: Uhunzi……….. 12 TANGAZO LA TELEVISHENI 1 NDANI : JIONI :UWANJANI : CHINI YA MTI : SHULENI MKUTANO Ni mkutano mkubwa wa watu, wanaonekana Wake kwa Waume wakiwa katika Mavazi ya aina Mbalimbali. Mbele yao anaonekana Mwanamama mmoja akiwa amesimama jukwaani akiwa ana hutubia, huyu ni Mama Mkude, ni Afisa Tawala wa Wilaya…………. MAMA MKUDE Jamani tunaomaba sana ushirikiano wenu, bila nyinyi Sisi serikali tutakuwa tunafanya kazi bure, ndugu zangu mjenga nchi WATU WOTE Ni Mwananchi MAMA MKUDE Na mvunja nchiiiiiiiiiiii!!!!!!! WATU WOTE Ni huyo huyo Mwananchi. Watu wanapiga makofi na Vigelegele. MAMA MKUDE Jamani tunawaomba sana acheni kulima kando kando ya mto Mkondoa, acheni kuchungia mifugo yenu kando ya mto Mkondoa, Jamani hii ni amri ya Serikali, kufanya hayo yote kuna sababisha mmomonyoko wa udongo na hatimae husababisha Mafuriko. MTU 1 (KWA KUROPOKA) Sasa unataka tulime wapi na kuchungia wapi wakati yale ndio maeneo yenye rutuba na majani mazuri. MAMA MKUDE Nimesema hii ni amri toka Serikalini, na maeneo ya Kulima na kuchungia yapo mengi sana. Sasa nasema hivi atakae kwenda kinyume na amri hii akikamatwa Sheria itachukua mkondo wake, tumetunga sheria ngumu ili 13 tuweze kuulinda mto wetu. Tumechoshwa na mafuriko katika Wilaya yetu… tukiacha tabia hii iendelee ni sawa na kulipa dudu liumalo….!! WATU WOTE Kidoleeeeeeeeee MAMA MKUDE Si ndio jamani………..? HADHARA Ndiooooooooo!!! 14 TANGAZO LA TELEVISHENI 2 NDANI : JIONI : NYUMBANI KWA SEKULU Anaonekana Bwana Sekulu akiwa amekaa na Bwana Mloka na mkewe sebuleni, kwenye Makochi ya kawaida, ni kajumba kazuri. SEKULU Mloka na Shemeji Ahsanteni sana kwa ushauri wenu. MLOKA Tunakushauri mengi Sekulu lipi hasa unalotushukuru.? SEKULU Hili mliloniambia kwamba kusombewa vitu na mafuriko sio mwisho wa maisha, nikakakope kamkopo kadogo, imenisaidia nyumba ndio hii na biashara zangu zinaendelea vizuri, maana mafuriko ya mto Mkondoa yalinisombea kila kitu. MAMA MLOKA Umeamini sasa Shemeji kukumbwa na mafuriko, sio mwisho wa maisha. SEKULU Ni kweli, Shemeji… Binadamu hutakiwi kukata tama, na mimi nitawashauri wenzagu wakikutwa na hali kama yangu ya kukumbwa na mafurio wasikate tamma, maisha yanatakiwa kuendelea…kukatika kwa koloeo siyo mwisho wa…….. WOTE Uhunzi…….. 15 WILAYA YA MAGHARIBI, UNGUJA- MAFURIKO TANGAZO LA REDIO 1 WAHUSIKA : HABIBA NA SHARIF MAHALI : NYUMBANI KWAO SAUTI NA MILIO : MUZIKI KWA MBALI 1. HABIBA Mimi kuendelea kukaa hapa, unajidangaya, siwezi. Mabondeni : utakaa peke yako. 2. SHARIF : Mimi ndio baba, tutaendelea kuishi hapa, sipengine. 3. HABIBA : Hata kama, wewe ambae unaona kuendelea kukaa hapa ni sawa endelea, tulipoteza vitu vyetu kibao, wewe mwenyewe kama sio waokoaji ulikuwa una bebwa na mafuriko, hukomi tu, mimi na wanangu tutakwenda kukaa huko huko waliko tuhamishia. 4. SHARIF : Kwa hiyo tunabishana, si ndiyo? Tutaishi hapa hapa. Kama kawaida, nimesha weka doti. 5. HABIBA : Kuishi mabondeni ni hatari kwetu na familia nzima. Ili kuilinda familia yako na jamii nzima ni kuhakikisha unaisaidia kuwashawishi watu wasijenge mabondeni. wewe baki peke yako. wanangu twendeni…. Twendeni, siwezi kukubali kupoteza maisha ya familia yangu huku naona….. haya twendeni……. 6. SHARIF : Habiba….. wee Habiba…. Rudi hapa. 7. HABIBA : Habiba ni jina langu, kwa heri 8. SAUTI NA MILIO : Mlango unafunguliwa nakufungwa. 16 TANGAZO LA REDIO 2 WAHUSIKA : MTENDAJI NA WANANCHI MAHALI : OFISI YA SERIKALI YA MTAA SAUTI NA MILIO : KELELE ZA WATU 1. SAUTI NA MILIO: KELELE ZA WATU HUKU WAKIIMBA 2. MTU 1 (KWA KUPAYUKA ) Kama hataki kuvunja nyumba yake : mwenyewe turuhusuni wananchi tuivunje. 3. MTU 2 : Atajengaje Nyumba yake kwenye mkondo wa mto? 4. MTU 3 : Kwa nini azibe mifereji ya maji machafu na mto kwa kujenga jumba lake. Aliondoe haraka. 5. MTU 1 : Tunataka tumjue ni nani alimpa Kibali cha kujenga kwenye njia ya mfereji wa maji machafu. 6. MTU 3 : Avunje yeye mwenyewe kabla hatuja chukua sheria mkononi, tumechoshwa na mafuriko na maji kujaa ndani ya nyumba zetu wakati wa mvua. 7. MTU 4 : Viongozi tunataka maelezo ya kina, kiburi cha kujenga na kuziba Mfereji na njia ya maji anakitoa wapi? 8. MTENDAJI : Tumeona jamani, kweli ni kosa kubwa kujenga na kuziba njia ya maji, amekubali kuanzia kesho ataanza kuivunja nyumba yake. 9. WOTE : WATU WANAPIGA MAKOFI NA KUSHANGILIA 10. MTU 1 : Asipofanya hivyo kuanzia kesho, tutamuonyesha cha mtema kuni. 11. SAUTI NA MILIO: WANASIKIKA WAKIIMBA NYIMBO ZA KUHAMASISHANA 17 TANGAZO LA TELEVISHENI 1 NDANI : JIONI : KWA BWANA SHARIF : MABONDENI : Ni ndani nyumbani kwa bwana Sharif, anaonekana amekaa na wanawe wanne, wawili wa kiume na wawili wa kike, anaonekana mke wa Sharif, Habiba anaonekana amesimama huku anaongea kwa hasira. Huku akiwa anatoa mabegi na masanduku. HABIBA Mimi kuendelea kukaa hapa, unajidangaya, siwezi. mabondeni utakaa peke yako. SHARIF Mimi ndio baba, tutaendelea kuishi hapa, sipengine. HABIBA Hata kama, wewe ambae unaona kuendelea kukaa hapa ni sawa endelea, tulipoteza vitu vyetu Kibao, wewe mwenyewe kama sio waokoaji ulikuwa Una bebwa na mafuriko, hukomi tu, mimi na wanangu Tutakwenda kukaa huko huko waliko tuhamishia. SHARIF Kwa hiyo tunabishana, si ndiyo? Tutaishi hapa hapa. Kama kawaida, nimesha weka doti. HABIBA Kuishi mabondeni ni hatari kwetu na familia nzima. ili kuilinda familia yako na jamii nzima ni kuhakikisha unaisaidia kuwashawishi watu wasijenge mabondeni. Wewe baki peke yako. Wanangu twendeni. Anaonekana akitoka na mizigo huku watoto wakimfuata, SHARIF Habiba….. wee Habiba…. Rudi hapa. HABIBA Habiba ni jina langu, kwa heri Mlango unafungwa na kumuacha Sharif amesimama hajui afanye nini. 18 TANGAZO LA TELEVISHENI 2 NJE : MCHANA : MBELE YA OFISI YA SERIKALI YA MTAA (SHEHIA) : Wanaoneka watu wengi kiasi wakiwa mbele ya Ofisi ya Serikali ya Mtaa (SHEHIA) Wakiwa na mabango wameyashika mikononi, wengine wameshika wawili wawili, wengine mmoja mmoja huku wanaimba…mabango yanasomeka hivi. 1. Kama hataki kuvunja nyumba yake mwenyewe turuhusuni wananchi tuivunje. 2. Atajengaje Nyumba yake kwenye mkondo wa mto, 3. Kwa nini azibe mifereji ya maji machafu na mto kwa kujenga jumba lake. 4. Tunataka tumjue ni nani alimpa Kibali cha kujenga kwenye njia ya mfereji wa maji machafu. 5. Avunje yeye mwenyewe kabla hatuja chukua sheria mkononi, tumechoshwa na mafuriko na maji kujaa ndani ya nyumba zetu wakati wa mvua. 6. Viongozi tunataka maelezo ya kina, kiburi cha kujenga na kuziba njia ya maji anaitoa wapi? MTENDAJI Tumeona jamani, kweli ni kosa kubwa kujenga na kuziba njia ya Maji, amekubali kuanzia kesho ataanza kuivunja nyumba yake. Watu wanapiga makofi na kushangilia MTU 1 Asipofanya hivyo kuanzia kesho, tutamuonyesha cha mtema kuni. Wanatawanyika huku wanaimba kwa furaha. 19 WILAYA YA LONGIDO, ARUSHA – UKAME TANGAZO LA REDIO 1 WAHUSIKA : OLE MUDIKI NA MOLLEL MAHALI : KWA MOLLLEL SAUTI NA MILIO : MILIO YA NGOMBE NA MBUZI 1. O’MUDIKI : Nasema hivi, nataka mifugo yangu isssei, utaniusi. 2. MOLLEL : Mfugo hata mmoja sikupi, nenda shambani kwangu kaangalie walivyo nitenda, 3. O’ MUDIKI : Hayo mimi sijui ninachotaka nataka munyama yangu la sivyo nitachukua kwa ngufu. 4. MOLLEL : (KWA HASIRA) Jaribu nikuonyese, unaleta utani kwa mali yangu , kila siku tunaambiwa, fuga wanyama wachache wenye tija, ni hivi tunatakiwa kufuga kisanyansi, unaporuhusu ng’ombe na mbusi wanatembea tembea tena wengi, huichakaza Ardhi yenye rutuba na kusababisha Jangwa na ukame. 5. O’MUDIKI : Mimi hayo sijui nataka munyama yangu 6. MOLLEL : Kuchunga hovyo ni makosa, Ng’ombe wote hao wa nini?Ng’ombe alfu mbili wa nini wote hao, wakipita mahali kwenda machungani, wanasababisha mmomonyoko wa udongo ambao huleta ukame, acha kuchunga hivyo mifugo yako, umesikia? 7. O’MUDIKI : Nimesikia mzee wangu, ...sasa nitapata mufugo yangu au sipati? 20 TANGAZO LA REDIO 2 WAHUSIKA : EDWARD, OLE MOLOIMETT NA MA’MOLOIMENT MAHALI : SHAMBANI KWA MOLOIMETT SAUTI NA MILIO : SAUTI ZA NDEGE 1. EDWARD Bwana Moloimett naona unapanda miti, huoni ni kama : unapotesa muda wako tu. 2. MOLOIMETT : Kwa nini nasema hivyo? Huoni kama ukame nasidi 3. EDWARD Sasa kwani ukame nasababishwa na miti, hii ni laana. : Lazima tuchinje munyama tutoe kafara. 4. MOLOIMETT : Huko ni kujidanganya, laana hiyo tumeitafuta sisi wenyewe kwa kukata miti, la muhimu ni sisi wote kama jamii nzima kuhakikisha tunapanda miti kama vile hatuna akili nzuri, na hili ni jukumu langu mimi, wewe, yule na wana Longido wote. 5. MA’MOLOIMETT: Hilo ndilo tunalotakiwa kufanya, tuhamasishane kuhakikisha tunapanda miti tuondokane na hili Janga la ukame,…, hali inatisha. 6. EDWARD : Ni kweli hata mimi taungana na nyinyi katika hilo hali natisha, jua nawaka kama moto ya jehanamu 21 TANGAZO LA TELEVISHENI 1 NJE : JIONI : KWA MOLLEL : NJE YA NYUMBA : Anaonekana Mollel akiwa anaongea na Ole Mudiki, Ole Mudiki anaonekana kuongea kwa hasira OLE MUDIKI Nasema hivi, nataka mifugo yangu isssei, utaniusi. MOLLEL Mfugo hata mmoja sikupi, nenda shambani kwangu kaangalie walivyo nitenda, OLE MUDIKI Hayo mimi sijui ninachotaka nataka munyama yangu la sivyo nitachukua kwa ngufu. MOLLEL (KWA HASIRA) Jaribu nikuonyese, unaleta utani kwa mali yangu,kila siku tunaambiwa, fuga wanyama wachache wenye tija, ni hivi tunatakiwa kufuga kisanyansi, unaporuhusu ng’ombe na Mbusi wanatembea tembea tena wengi, huichakaza Ardhi yenye rutuba na kusababisha Jangwa na ukame. OLE MUDIKI Mimi hayo sijui nataka munyama yangu MOLLEL Kuchunga hovyo ni makosa, Ng’ombe wote hao wa nini? Ng’ombe alfu mbili wa nini wote hao, wakipita mahali kwenda machungani, wanasababisha mmomonyoko wa udongo ambao huleta ukame, acha kuchunga hivyo mifugo yako, umesikia? OLE MUDIKI Nimesikia mzee wangu, …….sasa nitapata mufugo yangu au sipati? 22 TANGAZO LA TELEVISHENI 2 NJE : ASUBUHI : SHAMBANI : KIJIJINI : Anaonekana Bwana Ole Moloimett akiwa na Mkewe Martha wakiwa wanapanda Miti, kando yao anaoneka Bwana Edward akiwa anapita anasimama na kuwaangalia. EDWARD Bwana Moloimett naona unapanda miti, huoni ni kama unapotesa muda wako tu. MOLOIMETT Kwa nini nasema hivyo? Huoni kama ukame nasidi EDWARD Sasa kwani ukame nasababishwa na miti, hii ni laana. lazima tuchinje munyama tutoe kafara. MOLOIMETT Huko ni kujidanganya, laana hiyo tumeitafuta sisi wenyewe kwa kukata miti, la muhimu ni sisi wote kama jamii nzima kuhakikisha tunapanda miti kama vile hatuna akili nzuri, na hili ni jukumu langu mimi, wewe, yule na wana Longido wote. MAMA MOLOIMETT Hilo ndilo tunalotakiwa kufanya, tuhamasishane kuhakikisha tunapanda miti tuondokani na hili janga la ukame, hali inatisha. EDWARD Ni kweli hata mimi taungana na nyinyi katika hilo hali natisha, jua nawaka kama moto ya jehanamu 23 WILAYA YA KINONDONI, DAR ES SALAAM-MAFURIKO TANGAZO LA REDIO 1 WAHUSIKA : KAKA, MGAMBO, DADA1, DADA 2 NA MWENYEKITI MAHALI : MTAANI SAUTI NA MILIO : HONI NA NGURUMO ZA MAGARI 1. DADA 1 Mwenzangu wee tupa haraka hizo takataka zako, nasikia : wakikukamata …… heeeeee 2. DADA 2 : Achaaaaa wewe 3. KIJANA : Wanazuga tu 4. MGAMBO : Hatuzugi tuko makini, kwa hiyo mko chini ya ulinzi, wachafuzi wakubwa wa Mazingira… simama hapo. 5. DADA 1 : Kosa letu ni lipi? mlitaka tukatupie wapi takataka? 6. M’KITI : Nyumbani kwako unajiwekea pipa, unajaza uchafu ukisubiri magari ya kusomba taka ya pite. Hapa umetupa kwenye mfereji tena ndani ya mfereji. Wakati wa mvua ndio hu sababisha mafuriko. Na huu ni uchafunzi mbaya sana wa………….. 7. DADA 2 : (Akiingilia) Lakini sio sisi peke yetu, mtaa wote huu tunatupa Takataka hapa. 8. MGAMBO : Aliyeshikwa na Ngozi ndio Mwizi wa Ng’ombe, twende. Sheria ikachukue nafasi yake……. 9. M’KITI : Dawa ya watu kama hawa ni kuwakamata na kuwapeleka mahakamani, hali kama hii haikubaliki, mafuriko yaliyo pita watu wengi walipoteza maisha na mali zao, kwa ujinga huu huu…….Nasema uongo jamani…….? 24 TANGAZO LA REDIO 2 WAHUSIKA : HAMADI NA MWAKITUTA MAHALI : NJIANI SAUTI NA MILIO : SAUTI ZA NDEGE 1. HAMADI : Karibu ndugu yangu….. Mwakituta karibu. 2. M’TUTA : Hamadi ndugu yangu si tulihamishwa huku mabondeni yaani na nyumba ndio umeamua kuijenga vizuri zaidi. 3. HAMADI : Siwezi mimi kuhama hapa nikaishi porini kule, mambo yote mjini, liwalo na liwe. 4. M’TUTA : Hayo sio maneno, hapa unaiweka familia yako na wewe mwenyewe kwenye hatari kubwa, mafuriko yakija hapa nani atapona, haya maeneo ya mabondeni hayafai jamani. Hamadi umesahau uliponea tundu la Sindano,….. umesahau ee, ama kweli sikio la kufa….. halisikii dawa 5. HAMADI : Bwana wewe yaliyopita si ndwele……… 6. M’TUTA : Tugange kifo chako na familia yako kwa kusombwa na mafuriko. Si ndio…… jamani tuambiwe mara ngapi maeneo ya mabondeni ni hatari kuishi, hayafai…… hapa ni kifo mkononi….. 7. HAMADI : Najua lakini sasa mimi nifanyeje na huku ndio biashara zangu ziliko, nifanyeje……. Mwakituta? 25 TANGAZO LA TELEVISHENI 1 NDANI : MTAANI : JIONI : USWAHILINI : Unaonekana mfereji wa maji machafu ukiwa umejaa uchafu mpaka juu, unaonekana kabisa kwamba maji yakija hayataweza kupita, yanaonekana maeneo zaidi yaliyo jaa uchafu mpaka kuziba njia za kupitia maji. Wanaonekana akina dada wawili na Kijana mmoja wakija wakiwa na viroba vilivyo jaa uchafu na kutupa kwenye mfereji ule ule, wakati wanamalizia kutupa tu wanaonekana Mgambo kama watatu na watu wengine wawili wakiwa wamevaa kiraia, wanawakamata wale wanawake na yule kijana, MGAMBO 1 Mko chini ya ulinzi, wachafuzi wakubwa wa Mazingira DADA 1 Kosa letu ni lipi? Mlitaka tukatupie wapi takataka? MWENYEKITI Nyumbani kwako unajiwekea pipa, unajaza uchafu ukisubiri magari ya kusomba taka ya pite. Hapa mnapotupa hivi wakati wa mvua ndio kuna sababisha mafuriko. Na huu ni uchafunzi mbaya sana wa mazingira DADA 2 Lakini sio sisi peke yetu, mtaa wote huu tunatupa takataka hapa. MGAMBO 1 Aliyeshikwa na ngozi ndio mwizi wa Ng’ombe, twende. sheria ikachukue nafasi yake……. MWENYEKITI Dawa ya watu kama hawa ni kuwakamata na kuwapeleka mahakamani, hali kama hii haikubaliki, mafuriko yaliyo pita watu wengi walipoteza maisha na mali zao, kwa ujinga huu huu. Nasema uongo jamani…….? Anageuka kuwaangalia wenzie na watuhumiwa wao, wanaonekana wanamuangalia na kukubaliana nae, Kisha anageukia Kamera. 26 TANGAZO LA TELEVISHENI 2 NDANI : JIONI : MBELE YA NYUMBA : MTAANI : USWAHILINI : Anaonekana Bwana Hamadi na Bwana Mwakituta wakiwa wanatembea kwenye maeneo ya Mabondeni, zinaonekana nyumba zikiwa zimejengwa kwenye Bonde, wanafika mbele ya nyumba moja na yenyewe iko Bondeni. HAMADI Karibu ndugu yangu….. Mwakituta karibu. MWAKITUTA (ANAONEKANA AKIANGALIA HUKU NA KULE) Hamadi ndugu yangu si tulihamishwa huku mabondeni yaani na nyumba ndio umeijenga vizuri zaidi. HAMADI Siwezi mimi kuhama hapa nikaishi porini kule, mambo yote mjini, liwalo na liwe. MWAKITUTA Hayo sio maneno, hapa unaiweka familia yako na wewe mwenyewe kwenye hatari kubwa, mafuriko yakija hapa nani atapona, haya maeneo ya mabondeni hayafai jamani. Hamadi umesahau uliponea tundu la Sindano, umesahau ee ! HAMADI Bwana wewe yaliyopita si ndwele……… MWAKITUTA Tugange kifo chako na familia yako kwa kusombwa na mafuriko. Si ndio…… jamani tuambiwe mara ngapi maeneo ya mabondeni ni hatari kuishi, hayafai. HAMADI Najua lakini sasa mimi nifanyeje na huku ndio biashara zangu ziliko, nifanyeje….. 27 WILAYA YA HANDENI, TANGA-MLIPUKO WA KIPINDUPINDU Ujumbe: Kuripoti mapema milipuko ya kipindupindu, dalili zake na matibabu ya mapema pamoja na kumpa mgonjwa mchanganyiko wa maji, chumvi na sukuri (ORS) husaidia kuokoa maisha. MCHORO NAMBA 1 28 Ujumbe: Jilinde mwenyewe, familia yako na jamii yako ili kuepuka maambukizi ya kipindupindu kwa kuchemsha maji ya kunywa MCHORO NAMBA 2 29 Ujumbe: Wakinge uwapendao kwa kutunza mazingira yako: uchafu hueneza kipindupindu. MCHORO NAMBA 3 30 Ujumbe: Kipindupindu kinauwa: njia salama ya kujilinda wewe na familia yako ni kuepuka kunywa na kula vyakula vya barabarani vya baridi. MCHORO NAMBA 4 31 WILAYA YA KILOSA, MOROGORO-MAFURIKO Ujumbe: Mafuriko yanauwa, mara upatapo taarifa ya kuondoka kwenye eneo hatarishi ondoka haraka ili uokoe maisha yako na familia yako. MCHORO NAMBA 1 32 Ujumbe: Mafuriko yanaua; jilinde mwenyewe, familia yako na jamii yako kwa ujumla kwa kutunza kingo za mto Mkondoa. MCHORO NAMBA 2 33 Ujumbe: Ikinge jamii na familia yako na hatari ya mafuriko kwa kupanda miti kandokando ya mto Mkondoa. MCHORO NAMBA 3 34 Ujumbe: Upatikanaji wa mikopo midogo midogo husaidia kujenga nyumba zilizoharibiwa na mafuriko na kuendeleza biashara ndogondogo. MCHORO NAMBA 4 35 WILAYA YA MICHEWENI, PEMBA-UKAME Ujumbe: wanaume na wanawake wote kwa pamoja tujiunge kwenye shughuli za kilimo ili tuongeze upatikanaji wa chakula katika familia zetu. MCHORO NAMBA 1 36 Ujumbe: Vuna maji ya mvua na anzisha kilimo cha umwagiliaji ili kuongeza kipato na kuondoa njaa katika familia yako MCHORO NAMBA 2 37 Ujumbe: Ikinge jamii na familia yako dhidi ya ukame kwa kupanda miti MCHORO NAMBA 3 38 Ujumbe: Panda mazao yanayostahimili ukame ili kupambana na upungufu wa chakula MCHORO NAMBA 4 39 WILAYA YA KINONDONI, DAR ES SALAAM-MAFURIKO Ujumbe: Maeneo yanayokumbwa na mafuriko mara kwa mara ni hatari, jikinge wewe na familia yako, usijenge na kuishi maeneo hayo MCHORO NAMBA 1 40 Ujumbe: Jikinge wewe na familia yako, usijenge na kuishi kwenye mkondo wa maji MCHORO NAMBA 2 41 Ujumbe: Ikinge jamii yako na mafuriko; usichimbe mchanga katika mto Msimbazi MCHORO NAMBA 3 42 Ujumba: Weka mazingira yako safi usitupe taka katika mifereji; kuepuka mafuriko MCHORO NAMBA 4 43 WILAYA YA LONGIDO, ARUSHA-UKAME Ujumbe: Punguza namba ya mifugo kwenye kaya yako kuepuka uharibifu wa mazingira MCHORO NAMBA 1 44 Ujumbe: Ili kupunguza uhaba wa chakula kwenye familia yako, panda mazao yanayostahimili ukame MCHORO NAMBA 2 45 Ujumbe: Kufuga mifugo mingi kunasababisha uharibifu wa mazingira; tunza mazingira kwa kupunguza idadi ya mifugo MCHORO NAMBA 3 46 Ujumbe: Ikinge jamii yako dhidi ya ukame kwa kupanda miti MCHORO NAMBA 4 47 WILAYA YA MAGHARIBI, UNGUJA-MAFURIKO Uumbe: Ikinge familia yako dhidi ya mafuriko, usizibe mifereji ya asili kwa kujenga nyumba kwenye maeneo hayo MCHORO NAMBA 1 48 Ujumbe: Maeneo yanayokumbwa na mafuriko mara kwa mara ni hatari, jikinge wewe na familia yako, usijenge na kuishi maeneo hayo MCHORO NAMBA 2 49 Ujumbe: Weka mazingira yako safi; usitupe taka katika mifereji ya maji ya mvua MCHORO NAMBA 3 50 KIAMBATANISHO No 1: UJUMBE MHIMU NA NJIA ZA MAWASILIANO ZINAZOTUMIKA KWA SASA NA NJIA MPYA ZILIZOPENDEKEZWA KUTUMIKA Wilaya Handeni Ujumbe Njia za mawasiliano Televisheni Kuchemsha maji ya kunywa ni moja ya njia bora za kuikinga familia yako kutokana na maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu Wakinge uwapendao: uchafu hueneza ugonjwa wa kipindupindu, weka mazingira yako katika hali ya usafi Kuripoti mapema dalili za ugonjwa wa kipindupindu pamoja na matibabu ya mapema na kumpatia mgonjwa mchanganyiko wa maji, chumvi na sukuri (ORS) huokoa maisha Hii ni dharura: njia sahihi ya kujilinda wewe na familia yako na ugonjwa wa kipindupindu ni kuepuka misongamano isiyo ya lazima pamoja na kutokunywa na kula vyakula vya baridi vya barabarani Jikinge wewe mwenyewe pamoja na Kipaza Sauti Magazeti Broshua Posita Mbao za matanga zo Redio DVD 51 Mabango Simu za mkononi Mtandao wa Intaneti Uso Kwa Uso Mawasi liano ya kijadi familia yako na ugonjwa wa kipindupindu kwa kunawa mikono na maji ya moto na sabuni kabla ya kula na baada ya kutoka chooni Tumia choo siku zote uepuke kueneza ugonjwa wa kipindupindu Jikinge wewe, familia yako na jamii yako kwa ujumla kutokana na maambukizi ya ugonjwa wa kipindu pindu: chemsha maji ya kunywa kila siku Michewen i Ilinde jamii yako na familia yako kutokana na athari za janga la ukame kwa kupanda miti Ikinge jamii yako na uharibifu wa mazingira: usifanye shughuli za kuchimba mchanga na kutengeneza tofali za mawe Epuka uchimbaji wa mchanga pamoja na utengenezaji wa tofali za mawe ili kupunguza athari za uharibifu wa mazingira 52 Kinondoni Wanaume na wanawake sote kwa pamoja tujishughulishe na kilimo ili kuongeza upatikanaji wa chakula katika familia zetu Panda mazao yanayostahimili ukame ili kukabiliana na madhara yatokanayo na ukame kama vile upungufu wa chakula Jishughulishe na kilimo ili kupunguza tatizo la njaa na kuondoa utapiamlo katika familia yako Vuna maji ya mvua na kujishughilisha na kilimo cha umwagiliaji ili kuongeza upatikanaji wa chakula na kuondoa njaa katika familia yako Maeneo ya mabondeni ni hatari sana kwa mafuriko: ilinde familia yako na wewe mwenyewe usijenge nyumba na kuishi katika maeneo hayo Ilinde jamii yako na janga la mafuriko: Usichimbe mchanga kando kando ya mto msimbazi Iweke jamii yako katika hali ya 53 usafi,usitupe taka ngumu kwenye mifereji ya maji ya mvua Kilosa Mafuriko yanaua: mara usikiapo tahadhari ya mafuriko ikitolewa, ondoka haraka sana eneo hatarishi na uende eneo salama Tafuta mikopo midogo mdogo ili ikusaidie kukarabati nyumba yako na biashara yako iliyo athirika na mafuriko, kuna maisha hata baada ya mafuriko Ilinde jamii yako na familia yako kutokana na mafuriko kwa kupanda miti na matete kando kando ya mto mkondoa Kuchungia kando kando ya mto Mkondoa kunasababisha mmomonyoko wa udongo na kupungaza kina cha mto na hatimaye kusababisha mafuriko:Ilinde jamii yako kwa kuacha kuchungia mifugo kando kando ya mto Mkondoa Mafuriko yanaua: usilime kando ya mto Mkondoa kwani shghuli za kilimo 54 zinachangia kuongeza hatari ya kutokea kwa mafuriko Mafuriko yanaua: mara upatapo tahadhari ya mafuriko, tafadhari ondoka haraka sana eneo hatarishi na uende eneo salama Jitahidi upate mikopo midogo midogo ili uweze kukarabati nymba yako na biashara yako iliyoathirika na mafuriko: Kuna maisha hata baada ya mafuriko Jilinde wewe na familia yako na jamii yako kwa ujumla kutokana na mafuriko kwa kulinda tuta na kingo za mto Mkondoa Magharibi Maeneo ya mabondeni ni hatari sana kwa mafuriko, jilinde wewe na familia yako: usiishi na kujenga katika maeneo hayo Ilinde jamii yako na mafuriko: usizibe mifereji ya asili ya maji kwa kujenga nyumba katika maeneo hayo Iweke jamii yako katika hali ya usafi: usitupe taka ngumu 55 katika mifereji ya maji ya mvua Mafuriko yanaua: mara upatapo tahadhari ya mafuriko ondoka haraka sana eneo hatarishi na uende eneo salama Jitahidi upate mikopo midogo midogo ili uweze kukarabati nymba yako na biashara yako iliyo athirika na mafuriko; Kuna maisha hata baada ya mafuriko Uchungaji holela wa mifugo unasababisha uharibifu wa mazingira: ilinde jamii yako kwa kufuga kisasa na kuacha kuchunga mifungo hovyo Fuga kisasa kwa kupunguza idadi ya mifungo yako ili kupunguza athari za uharibifu wa mazingira Ili kuongeza upatikanaji wa chakula katika familia yako panda mazao yanayostahimili ukame Ilinde jamii yako na athari za ukame kwa kupanda miti Angalizo: Rangi nyeusi inaonyesha njia zilizopo za mawasiliano na rangi nyekudu inaonyesha njia mpya za mawasiliano zilizo pendekezwa Longido 56