Uk. 4 Uk. 18 Uk. 14
Transcription
Uk. 4 Uk. 18 Uk. 14
Toleo NO. 039 Julai –Septemba 2011 Uk. 4 Bei Shs. 500/= Uk. 14 Wakulima wapongeza MVIWATA kwa kuhabarisha wakazi wa vijijini ISSN 0856-5937 Uk. 18 Maonesho ya NaneNane 2011 Kijana mbunifu atengeneza mitambo ya radio kunufaisha wanakijiji Tahariri Toleo NO. 039 Julai Septemba 2011 Bei Shs. 500/= ISSN 0856-5937 WAHARIRI Susuma Msikula Susuma Stephen Ruvuga BODI YA MVIWATA Mwenyekiti – Yazid Makame Makamu Mwenyekiti – Lydia Ruliho Katibu - Stephen Ruvuga- (Mkurugenzi Mtendaji) Mweka Hazina - Grace Runkulatile I WAJUMBE Cosma Bulu Sylvester Yatuba Joseph Kilowoko Samweli Maseke Julius Mbago Habibu Simbamkuti MSHAURI WA MVIWATA Prof. Amon Mattee LINATOLEWA NA KUSAMBAZWA NA Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) S.L.P 3220 Morogoro, Tanzania Simu:023 261 41 84 Faksi:023 261 41 84 Barua pepe: [email protected], [email protected] Tovuti: www.mviwata.org MICHORO Godwin Chipenya USANIFU NA UCHAPISHAJI PENplus Ltd – 022 2182059 Toleo NO. 039 Julai –Septemba 2011 Uk. 4 Bei Shs. 500/= Uk. 14 Wakulima wapongeza MVIWATA kwa kuhabarisha wakazi wa vijijini ISSN 0856-5937 Habari za vijijini zipewe kipaumbele ngawa juhudi na mchango wa jamii za vijijini nchini Tanzania ndiyo vinavyoiendeleza Taifa, habari za vijijini haziandikwi kwa umuhimu huo. Mara nyingi, habari za vijijini zinazopewa nafasi kwenye vyombo vya habari ni zinazohusu maafa, kesi, vimbwanga na hotuba za viongozi wanapotembelea maeneo hayo. Wanahabari wanafanya kazi kubwa ya kuuelimisha umma, hata hivyo kwa sehemu kubwa habari hizo zimekuwa ni zile zinazohusu watu wa mijini. Toleo hili linalozungumzia habari za vijijini ni sehemu ya utekelezaji wa ajenda ya upashanaji habari inayotekelezwa na MVIWATA kwa muda mrefu sasa. Tunafahamu kwamba pamoja haya umuhimu wa upatikanaji wa habari kwa watu wa vijijini, ziko changamoto kadhaa zinazokwamisha ufanisi wake. Miongoni mwa changamoto hizo ni ukosefu wa vitendea kazi ikiwemo usafiri, kamera na vinasa sauti ambapo hata waandishi wachache wenye nia ya kwenda kukusanya habari vijijini wameshindwa kufanya hivyo kwa kukosa usafiri na wengine kuishia kutegemea usafiri wa viongozi wanapotembelea maeneo ya vijijini. Kulingana na kubanwa na ratiba za viongozi hao, waandishi hawawezi kukusanya habari nzuri zenye kuchochea maendeleo ya vijijini zaidi ya kuishia kuandika hotuba na maagizo ya viongozi. Changamoto nyingine ni ya waandishi wa habari kukosa taaluma ya kutosha yenye kuwawezesha kudadisi na kuibua kero na changamoto halisia za vijijini na siyo vimbwanga. Tunaamini ziko changamoto nyingi na lengo letu siyo kuziainisha zote isipokuwa tunawakumbusha wadau wa sekta ya habari kuwa vijijini ndiko kwenye chimbuko la wazalishaji na kwamba hatupaswi kuwatenga. Tunashauri kuwepo na jitihada za makusudi za kutatua changamoto hizi na vilevile kuwe na juhudi za kuhimiza vyombo vya habari kuzipa kipaumbele habari za vijijini. Ni wakati muafaka ambapo Tunawakumbusha wana habari juu ya umuhimu wa kuzingatia maadili ya taaluma ya uandishi wa habari kwa kuandika habari zilizofanyiwa utafiti wa kina na kuhakikisha jamii zote vijijini na mijini wananufaika na huduma hii muhimu. Tusaidie kuchochea maendeleo vijijini kwa kuhakikisha tunawapatia habari za kutosha na zilizofanyiwa utafiti. Uk. 18 Maonesho ya NaneNane 2011 Kijana mbunifu atengeneza mitambo ya radio kunufaisha wanakijiji Picha ya Jalada: Bw. Benjamini Nziku mkulima wa kijiji cha Lusala kata ya Lupanga wilayani Ludewa akipata habari kupitia gazeti la wakulima la Pambazuko. b Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011 MADA MAALUM Upatikanaji wa habari vijijini, kichocheo cha maendeleo? teknolojia ya habari, nchi za Kusini mwa Afrika bado zinakabiliwa na tatizo kubwa la kukosekana kwa habari za umma hasa kwenye maeneo ya vijijini ambazo ni muhimu kwa wananchi kutoa maamuzi mbalimbali ambayo ni sahihi kwa maisha yao. maeneo hasa ya vijijini. Mfumo wa upashanaji habari uliopo sasa siyo utokana na kupiga hatua wa kuridhisha kwani haumfikii kila mwananchi wa kijijini mahali alipo. za kimaendeleo katika Kwa mfano magazeti yanayofika teknolojia hasa ya habari, kwa nadra vijijini ndani yake yanakuwa wigo wa upatikanaji wa habari yamejaa habari zinazohusu vuguvugu hivi sasa umepanuka ukilinganisha la maisha ya mjini. Habari hizo nyingi na miaka ya nyuma hasa wakati Hata ni zile zinazohusu malumbano na tunapata uhuru. siasa za chuki baina ya viongozi radio za kijamii Hivi sasa watu wanauwezo wa vyama, foleni za barabarani, wa kutumia kompyuta na zilizoanzishwa kwa lengo michezo ambayo pengine mtu simu za mkononi zenye kijijini hajawahi kuiona na la kuhudumia wakazi wa vijijini, wa huduma ya intaneti na burudani kama vile miziki kuweza kupata taarifa zimeacha misingi ya kuanzishwa na picha kubwa kubwa za mbalimbali zinazotokea wasanii ambazo ki uhalisia kwake na kuegemea zaidi ulimwenguni kwa wakati hazimuongezei tija mtu wa huo huo ama kulipia huduma kutangaza mambo ya kijijini katika harakati zake za mbalimbali kama vile matibabu, kupambana na umasikini kupitia mijini. maji na umeme. Lakini pia wanaweza kilimo, ufugaji ama uvuvi. hata kufanya manunuzi ya bidhaa Bado Tunashuhudia ongezeko la mbalimbali kupitia intaneti na hivyo kuna changamoto zinazoikumba vyombo vya habari vya kielektroniki kupunguza gharama na muda na sekta hii ya habari ikiwemo uhaba kama vile radio na televisheni na kurahisisha biashara. wa upatikanaji wa habari sahihi ukuaji wake kutoka kwenye mfumo Hata hivyo mbali na kukua kwa na zenye manufaa kwa baadhi ya Endelea Uk wa 2 Na Goodness Mrema, Morogoro K Mwekahazina wa MVIWATA Ruvuma Bibi Immaculata John akitekeleza shughuli za MVIWATA za kusambaza habari za wakulima kwa wadau Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011 1 MADA MAALUM Upatikanaji wa habari vijijini Inatoka uk. wa 1 wa analogia kwenda digitali. Ongezeko na ukuaji wa teknolojia bado hauwanufaishi vya kutosha wakazi wa vijijini. Kilichobadilika ni kuwepo kwa usikivu mzuri wa matangazo ya radio kwenye baadhi ya vijiji tofauti na ilivyokuwa awali. Habari zenye mlengo wa kuchochea maendeleo vijijini bado hazipewi kipaumbele. Hata radio za kijamii zilizoanzishwa kwa lengo la kuhudumia wakazi wa vijijini, zimeacha misingi ya kuanzishwa kwake na kuegemea zaidi kutangaza mambo ya mijini. Japokuwa televisheni na redio zinajitahidi kurusha matangazo yake na kuwafikia kwa wakati watu wa vijijini, lakini bado habari zake zinakosa mguso kwao, ingawa serikali inajinadi kuwa matumizi ya mfumo wa digitali yameongeza upatikanaji wa habari maeneo ya vijijini. Kwa ujumla habari zinazohusu mafundisho ama mafanikio ya wananchi vijijini haziandikwi wala kusikika vya kutosha na kwamba kuna haja ya kubadili mfumo ili waandishi wa habari wapate msukumo wa kuwafikia wananchi vijijini na kuandika habari zao. Siku hizi umekuja utaratibu mpya wa upashanaji habari kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii (tovuti, blogs, facebook, twitter) ambayo kwa hakika mkulima au mfugaji mdogo anayeishi kijijini hafahamu hata jinsi ya kuitumia na wachache wenye uelewa hawawezi kuitumia kwa kukosa nishati ya umeme. Changamoto ya miundombinu Ziko sababu nyingi zinazotajwa kuchangia habari kutowafikia watu wa vijijini. Sababu mojawapo ni ubovu wa miundombinu ya barabara katika maeneo mengi ya vijijini ambako kuna asilimia 80 ya Watanzania wazalishaji wanaochangia pato la taifa. Kulingana na miundombinu duni ya barabara zetu hasa maeneo 2 ya vijijini, ni vigumu kwa mwananchi wa kijijini kupata gazeti kwa wakati na kulisoma. Wauzaji na wasambazaji wa magazeti ya kila siku wanajikuta wakishindwa kuyafikia maeneo hayo kwa wakati. Kwa mfano gazeti la kila siku linalosambazwa asubuhi katika maeneo ya mijini huchukua wakati mwingine siku mbili kufika eneo la Mrimba Kilombero mkoani Morogoro kutokana na barabara ya kuelekea sehemu hiyo kuwa mbaya. Huu ni mfano wa sehemu moja iliyo katika mkoa jirani na mji ambapo magazeti mengi huchapishiwa, swali ni je vipi kwa watu waishio Kigoma vijijini, Karagwe ama Murugwanza huko Ngara, wao hulipata gazeti hilo siku ngapi baada ya kuchapishwa? Ukosefu wa nishati nalo ni tatizo kubwa kwa wakazi wa maeneo ya vijijini ambalo linazuia wananchi wa vijijini kununua televisheni au radio kwa sababu ya kukosa nishati itakayowawezesha kuvitumia vyombo hivyo. Maisha magumu ya vijijini yanayosababishwa na ukosefu wa huduma muhimu za kijamii pia yanadhoofisha kasi ya upatikanaji wa habari vijijini. Kwa mfano mtu anayesumbuliwa na maradhi kwa kukosa huduma sahihi za matibabu, hawezi kukaa na kusikiliza radio huku akigugumia kwa maumivu makali. Mtu huyu pia hawezi kutenga fedha ya kununua gazeti linalomfikia baada ya siku mbili Akina mama wengi vijijini wanakosa muda wa kusikiliza taarifa za habari ama matangazo mengine muhimu kwa kuwa muda ambao radio na televisheni zinatangaza taarifa za habari wao wanakuwa kwenye shughuli za kupika, kutafuta maji na kuni na shughuli za shamba. Ukiachana na tatizo la miundombinu duni, iko sababu nyingine ya baadhi ya wananchi kukosa mwamko wa kutafuta ama kutoa habari. Wananchi kwenye baadhi ya maeneo ya vijijini hawajaelimishwa vya kutosha juu ya umuhimu wa kutoa na kupokea habari kuhusiana na masuala mbalimbali hivyo baadhi yao kuona kwamba kununua gazeti ama kununua televisheni ni kuwa na matumizi ya anasa. Habari zinachochea maendeleo? Wakazi wa vijijini wengi wao wakiwa ni wakulima waliopata fursa ya kuzungumzia hoja hii, walikiri kuwa upatikanaji wa habari sahihi vijijini umesaidia kuchochea maendeleo, japokuwa kiwango cha upatikanaji wake siyo cha kuridhisha. Walieleza kuwa habari chache zilizowafikia ziliwasaidia kupata elimu ya kilimo bora, taarifa za upatikanaji wa pembejeo, masoko, mwelekeo wa hali ya hewa na mwenendo wa uchumi na hali ya kisiasa nchini pamoja na kufahamu jitihada za maendeleo zinazofanywa na makundi mbalimbali. Mbali na vyombo vya habari, ziko njia nyingine za asili zinazotumika kufikisha habari kwa jamii kwenye maeneo ya vijijini ikiwemo mikutano ya vijiji, kwenye nyumba za ibada na kwenye mikusanyiko kama vile sokoni na kwenye minada. Walisema habari hizo pia zinawapatia uwanja mpana wa mjadala na kubadilishana uzoefu kuhusiana na masuala mbalimbali yanayowakabili ikiwemo uwezo wa kudai haki zao za msingi.Wanafahamu mahali pa kupata mahitaji muhimu na fursa zinazopatikana kwa ajili yao na Endelea Uk wa 3 Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011 MADA MAALUM Inatoka uk. wa 2 njia muafaka za kufikia suluhu kwa changamoto zinazowakabili katika shughuli zao. “Suala la upatikanaji wa habari linahusika zaidi na maisha ya kila siku ya mwananchi. Ni suala la maendeleo ya kila mwanadamu hapa ulimwenguni, endapo wananchi hawa wa vijijini watapata habari sahihi na kwa wakati zitachochea bidii katika kujiletea maendeleo,” alisema Bw Andrew Hepelwa, Katibu Mkuu Mstaafu wa MVIWATA taifa. Aliongeza kuwa maendeleo ni jambo la muhimu ambalo kila mwanadamu analitegemea katika maisha yake kuanzia ngazi ya familia hadi ngazi za kitaifa. Kama hupati taarifa kamili kuhusu kitu fulani, huwezi kujua uzito wake na huwezi kuchukua hatua za kimaendeleo na kwa upande mwingine jamii ikipata taarifa na habari sahihi inaweza kuchukua hatua ya kujikwamua katika matatizo. Matumizi ya habari Kwa ujumla jamii ya vijijini kutokana na kutengwa kwa muda mrefu na mfumo wa habari, nayo kwa namna fulani imekuwa kama imejiengua na kuyaona masuala ya habari kama siyo sehemu yao. Jamii hii inahitaji kujengewa ufahamu wa kutosha kuhusu umuhimu wa kupashana habari na matumizi sahihi ya vyombo vya habari katika kujiletea maendeleo. Vyombo vya habari katika hili vina mchango mkubwa wa kuwafumbua macho wakazi wa kijijini ili wafahamu umuhimu wa matumizi sahihi ya habari katika mchakato wa kujiletea maendeleo. Mbali na vyombo vya habari, ziko njia nyingine za asili zinazotumika kufikisha habari kwa jamii kwenye maeneo ya vijijini ikiwemo mikutano ya vijiji, kwenye nyumba za ibada na kwenye mikusanyiko kama vile sokoni na kwenye minada. Hata hivyo taarifa nyingi muhimu hutolewa katika mikutano ya vijiji, lakini kutokana na kukosa mwamko huko nako mahudhurio ni madogo na hivyo kukosesha wananchi habari muhimu. Miongoni mwa wakulima waliohojiwa wamekiri wazi kuwa hawajawahi kuhudhuria mkutano wa kijiji kwa zaidi ya miaka miwili. Hili ni tatizo na ni tabia inayopaswa kuachwa kwa sababu inadidimiza maendeleo. Miongoni mwa wakulima hao pia wamekiri mapungufu kwamba walipata habari lakini hawakuzitumia ipasavyo jambo ambalo wamelijutia na baadaye kujirekebisha. Kwa mfano Bw. Charles Ndugulile mkulima wa kijiji cha Mwamala Kata ya Mwamala wilaya ya Shinyanga Vijijini alisema “mwaka 2008 kupitia matangazo ya radio nilipata taarifa za kutokea mabadiliko ya tabia ambayo yatasababisha ukame na mlipuko wa wadudu lakini nilipuuzia na baadaye msimu wa kilimo uliofuata nililima shamba kubwa kama kawaida, nikapata hasara baada ya mazao kukauka kwa ukame.” Bw. Ndugulile akafafanua kwamba kutokana na hali hiyo amekuwa mhamasishaji mkubwa kwenye mkoa wa Shinyanga akiwahimiza wakulima umuhimu wa kutafuta habari na kuzitumia, lakini pia wawe wamezipata kutoka katika vyanzo vya uhakika na vinavyoaminika ila wasipotoshwe kwa kupata habari ambazo si sahihi. Hitimisho Ili kuboresha upatikanaji wa habari vijijini, serikali na wadau wa habari kwa ujumla wanapaswa kushirikiana kuondoa kasoro zilizopo na kuweka mfumo wa usawa wa utoaji taarifa na upatikanaji wa habari kwenye Endelea Uk wa 5 Upatikanaji wa habari sahihi unapanua wigo wa mijadala kama hii ya wakulima Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011 3 MADA MAALUM Maoni ya wakulima na wataalam Na Goodness Mrema C hangamoto kubwa inayowakabili wakulima vijijini kwa kukosa habari ni kuachwa nyuma kimaendeleo, kuibuka kwa migogoro mingi baina yao na viongozi wao ama makundi mengine katika jamii. Baadhi ya wakulima na wataalam wamekuwa na maoni tofauti kuhusiana na suala hili la upatikanaji wa habari vijijini. Wakulima kutoka mikoa mbalimbali walieleza jinsi wanavyokabiliwa na changamoto katika kupokea na kutoa habari katika maeneo mengi ya vijijini kutokana na miundombinu mibovu. Yafuatayo ni maoni waliyoyatoa baada ya kuulizwa swali lililosema hali ya upatikanaji wa habari kijijini ukoje? Bibi. Mariam Mmanga kutoka kijiji cha Kivulini wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro alieleza kwamba japokuwa kijijini kwake hawatembelewi na waandishi wa habari mara kwa mara wala kufikiwa na magazeti, lakini wanawake kijijini kwake wamejiunga katika vikundi wanavyovitumia kupashana habari kupitia mikutano na vikao mbalimbali na sasa wamehamasika na wanaelewa umuhimu wa kupata habari, jambo ambalo linawatia moyo na wanaimani kwamba hawataweza kubaki nyuma kwani wanafahamu na wanaelewa nini kinaendelea katika nchi yao. Hata hivyo akaongeza kuwa wanaomba kutembelewa na wanahaabari ili habari za vikundi vyao pia zitangazwe. Bibi. Mariam Hassan kutoka kijiji cha Magamba, wilayani Kibondo mkoani Kigoma anaeleza kwamba magazeti kijijini Magamba yanawafikia baada ya siku tatu ama nne, tena lazima awepo mtu ametoka mjini siku hiyo. Kwa upande wa radio wanakamata zaidi radio za Burundi na kwamba hupokea matangazo ya radio moja tu ya Tanzania ambayo nayo husikika usiku tu, jambo ambalo linawafanya washindwe kupiga hatua kimaendeleo. Ameiomba serikali kuwakumbuka Endelea Uk wa 5 Miongoni mwa machapisho yanayotolewa na MVIWATA ambayo yamewanufaisha wakulima wengi kwa kuwapata habari sahihi za kilimo 4 Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011 MADA MAALUM Inatoka uk. wa 4 na kuhakikisha kwamba nao pia wanapata huduma hii muhimu kwani wanaonekana wamesahaulika kama vile wako nje ya Tanzania kutokana na kijiji chao kuwa mpakani mwa nchi ya Burundi. “Kuhusu habari za kijijini kwetu zinaandikwa pale tu kiongozi anapokuja kututembelea ama wakati mwingine waandishi hufika kijijini hapo kunapokuwa na matukio ya maafa kama vile mauaji. Tatizo hili linatuathiri zaidi sisi wanawake kwani muda mwingi tuko ndani, afadhali wenzetu wanaume wanakutana kwenye vikao na kuhabarishana na wengine wanamiliki simu za mkononi.” Bw. Hamad Abdallah Salimin kutoka Zanzibar yeye alieleza kukerwa na waandishi wa habari wanaokurupuka na kutangaza mambo yasiyo sahihi na kuupotosha umma. Akashauri ni vyema wanataaluma hawa kuthibitisha habari wanazozikusanya kabla ya kuzitangaza kwa umma. Hata hivyo aliwashauri wakulima wenzake wakabiliane na changamoto ya upatikanaji wa habari katika maeneo ya vijijini kwa kutosubiri tu hadi magazeti yawafikie ndipo wajue wamepata habari kumili kujua nini kinaendelea, bali wanaweza pia kupata habari zinazowahusu kwa kupitia majarida yanayochapishwa na mashirika yanayojihusisha na shughuli za kilimo kama vile MVIWATA ili kutambua fursa walizo nazo. Lakini akasema kwamba wakulima wasiishie kusoma habari na kuziacha tu katika makaratasi bali wazifanyie kazi na pia wasiogope kutumia vyombo vya habari kuwasilisha kero na kufichua maovu. Bw. Joseph Msagama kutoka Tanga alikiri kuwa changamoto kubwa ipo katika upokeaji wa habari kutokana na uhaba wa rasilimali fedha ambayo inamwathiri kila mkulima. “Jambo la kusikitisha ni kwamba wananchi wa vijijini wanaonekana kuwa tabaka la watu waliosahaulika katika kila kitu kuanzia kipato, elimu na hata haki zao mbalimbali ikiwemo hii ya kupata habari” alisema Bw. Msagama. Alishauri Halmashauri za wilaya ziweke utaratibu wa kutenga mafungu ya kuwawezesha usafiri maaalum waandishi wa habari ili wafike maeneo ya vijijini na kuwasaidia wananchi kufahamu nini kinaendelea na kwa kiasi gani kinaathiri uchumi wa wakulima. Kwa upande wake Bw. Abdala Ramadhani kutoka wilaya ya Misungwi, Mwanza alisema wakulima wengi vijijini wanakabiliwa na uhaba wa habari na kushauri vituo vya taarifa vijijini viimarishwe ili kuziba pengo lililopo. “Kupitia vituo hivyo vichache vilivyopo sasa wakulima na wajasiriamali wanapata habari kuhusiana na bei za mazao na wapi wanaweza kuuza lakini habari hizo haziwafikii wengi kutokana na uhaba wa rasilimali fedha unaozikabili,” alisema Ramadhani. “Tunashukuru kuwapo kwa gazeti letu wakulima la Pambazuko, linatuwezesha kufahamu wenzetu katika maeneo mengine wanafanya nini na ni njia gani wanazozitumia kutatua changamoto zao, jambo ambalo linatupa ari ya kufanya kazi kwa bidii ili kuzalisha kwa tija.” Bw. Ramadhani alisema kupitia mtandao wa wakulima wanajipanga ili kuweka utaratibu mzuri wa kuwezesha habari za wakulima wa Mwanza zinamfikia mhariri wa Pambazuko kwa wakati. Bw. Paul Mossama kutoka Serengeti mkoani Mara, anaeleza kuwa mfumo wa upashanaji habari uliopo nchini hivi sasa ni mzuri kuliko miaka ya nyuma, japokuwa una kasoro ya kutotangaza habari nyingi za kuwasaidia wakulima kuboresha shughuli zao na akashauri vituo vya radio na televisheni vinavyoanzishwa na halmashauri za wilaya vitangaze zaidi habari hizo badala ya kuwa na Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011 Endelea Uk wa 6 Upatikanaji wa habari vijijini Inatoka uk. wa 3 maeneo ya vijijini na mijini. Kwa upande wa radio matangazo yaboreshwe yasikike vizuri vijijini ili wananchi wetu walioko mipakani kama vile Kigoma pia waweze kunufaika na matangazo ya radio za nchini mwao badala ya radio za nchi jirani ya Burundi na Kongo ambazo kila kukicha zinatangaza vita na mauaji kutokana na mapigano yanayoendelea nchini mwao. Kadhalika waandishi wenyewe wanakabiliwa na changamoto ya kujiendeleza kitaaluma ili kuweza kuwa na upeo zaidi wa kuandika na kuchanganua habari zao kwa weledi hasa zinazohusu maendeleo vijijini badala ya kuwa mawakala ama mashabiki wa siasa tu. Kuna matatizo mengi vijijini ambayo kimsingi yanahitaji nguvu ya wanahabari kuyatatua. Kwa mfano wanahabari wanapaswa kuijengea uwezo jamii kuhusu elimu ya afya vijijini, elimu ya ukatili wa wanawake na vitendo vya unyanyasaji, elimu juu ya umiliki na matumizi bora ya ardhi, elimu ya kilimo bora na ufugaji, ujasiriamali, masoko na umuhimu wa elimu kwa watoto wao. Ipo haja kubwa ya tasnia ya habari kutilia mkazo suala la kuielimisha jamii ili iepukane na imani potofu za kwenda kwa waganga wa kienyeji kupiga ramli badala ya kuwapeleka wagojwa kutibiwa kwenye zahanati na vituo vya afya. Wanakijiji ambao kwa sehemu kubwa ni wakulima wanapaswa kujengewa uelewa wa masoko ya mazao yao, taarifa za bei na mbinu bora za kuongeza tija katika uzalishaji na kuboresha uchumi. Maendeleo vijijini yanachelewa kwa sababu wananchi hawapati habari sahihi kwa wakati muafaka. Hivyo yanapaswa kuchochewa kwa kuwapatia habari za kina. 5 MADA MAALUM Maoni ya wakulima... Inatoka uk. wa 5 vipindi vingi vya miziki na salamu. Akashauri pia magazeti kutenga kurasa maalumu zitakazoandika habari za wakulima wadogo angalau mara moja kwa wiki. “Magazeti mengi sasa yamefungua kurasa za udaku, urembo na muziki, hivyo hata kwa habari za wakulima jambo hili linawezekana.” Aliwashauri wakulima wadogo kutumia mitandao ya wakulima waliyonayo katika maeneo yao kwa ajili ya kupashana habari hadi pale wanapokuwa wanaona wameshindwa kufanya hivyo wenyewe ndipo waweze kumtafuta mwandishi ambaye atawasaidia kutangaza taarifa zao ili nao wapate nafasi ya kupaza sauti zao na kusaidiwa pale wanapohitaji msaada. Bw. Benardi Maiko kutoka Kasanga, wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa alisema wakulima wanayo mambo mengi ambayo ni vyema wakayatangaza ikiwemo mazao yao na bidhaa zingine wanazozalisha, changamoto ya uhaba wa pembejeo na zana bora za kilimo pamoja na mahitaji ya masoko ya kuuzia mazao yao. Aliongeza pia, wakulima wanahitaji kuwezeshwa kuwasiliana wao kwa wao kupitia vyombo vya habari ili kurahisisha mawasiliano kwani badala ya wao kufunga safari kwenda maeneo mengine kuwatembelea wenzao wataweza kusoma tu kwenye magazeti ama kusikiliza radioni na kujifunza. “Endapo habari zingekuwa zinafika maeneo ya vijijini kama ilivyo kwa maeneo ya mijini hakika wakulima leo tungekuwa kundi lenye nguvu kiuchumi na tusingekandamizwa wala kunyanyaswa” alisema Bw. Maiko Bw. Charles Ndugulile mkulima wa kijiji cha Mwamala Kata ya Mwamala wilaya ya Shinyanga Vijijini alieleza kwamba 6 upatikanaji wa habari unategemeana na watafutaji wa habari kwamba wanataka habari za namna gani na zinazohusu nini na kutolea mfano wa jarida la Pambazuko kwamba kila anayetaka kupata habari kuhusiana na wakulima anaweza kuzipata kutoka ndani ya jarida hilo. Akizungumzia matumizi sahihi ya habari Bw. Ndugulile alisema “mwaka 2008 kupitia matangazo ya radio nilipata taarifa za kutokea mabadiliko ya tabia ambayo yatasababisha ukame na mlipuko wa wadudu lakini nilipuuzia na baadaye msimu wa kilimo uliofuata nililima shamba kubwa kama kawaida, nikapata hasara baada ya mazao kukauka kwa ukame.” Bw. Ndugulile alifafanua kwamba kutokana na hali hiyo amekuwa mhamasishaji mkubwa kwenye katika mkoa wa Shinyanga akiwahimiza wakulima umuhimu wa kutafuta habari na kuzitumia, lakini pia wawe wamezipata kutoka katika vyanzo vya uhakika na vinavyoaminika ila wasipotoshwe kwa kupata habari ambazo si sahihi. Alifafanua kwamba katika mkoa wa Shinyanga wamewahamasisha wakulima umuhimu wa kutafuta habari kutoka katika vyanzo vya uhakika na vinavyoaminika ili wasipotoshwe kwa kupata habari ambazo si sahihi. Alisema kuwa wakulima wanaumia waonapo habari mara kwa mara zinazoeleza kuwa wameshindwa kufanya jambo ama wana mgogoro fulani wakati habari za mafanikio waliyopata kupitia kilimo ikiwemo kuongeza uzalishaji na kuweza kulipa ada za watoto wao, kujenga nyumba, kuongeza idadi ya mifugo na hata kufanikiwa kununua zana za kilimo, haziandikwi. “Kwa msingi huu ndiyo maana mara nyingi nimekuwa nikishauri kwamba ni muhimu wakulima tuimarishe chombo chetu cha habari kama Pambazuko kinachoweza kutusemea habari zetu.” Bw. Ndugulile ambaye pia ni mwenyekiti wa MVIWATA Shinyanga, alisema vyombo vingi vya habari nchini hivi sasa vinafanya shughuli zake kibiashara na hivyo kujikita katika matukio yenye habari zinazouzika na kutupa kando jukumu la kuwaelimisha wakulima kilimo biashara ama ufugaji na uvuvi wa kisasa. Maoni ya wataalam Bibi Mary Nsemwa, ni mkuu wa Idara ya Ushawishi na Ujenzi wa Nguvu za Pamoja katika Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), anasema asilimia kubwa ya wananchi wa vijijini wanaoathirika na upatikanaji wa habari ni wanawake. Bibi Nsemwa alisema wanawake wanahitaji kuhabarishwa kuhusiana na kilimo, ujasiriamali, sheria ya ardhi na mambo mbalimbali yanayoendelea mijini na duniani, lakini haki hiyo wanaikosa kutokana na kutokuwepo kwa miundo mbinu inayofika maeneo ya vijijini hususan barabara kwa ajili ya magazeti. “Hata kwa familia zenye radio nyingi zinamilikiwa na wanaume, hivyo wanawake kukosa taarifa muhimu ndiyo maana wanazidi kukandamizwa”. Bw. Marcossy Albanie wa Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu yeye anasema “kwa ujumla wakulima ni kundi lililoachwa nyuma na hata wakizungumza watu wanawapuuza na ndiyo maana hata vyombo vingi vya habari vimeegemea zaidi mjini, ingawa kisingizio kikubwa kimekuwa ni miundombinu mibovu vijijini. “Suala hili linamfanya mkulima mdogo abaki kwenye kiza na watu wachache waendelee kunufaika na rasilimali za nchi. Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011 MAKALA Soko huria lilivyoathiri upatikanaji wa habari vijijini Na Rashid Kejo Tulikotoka Nchi ya Tanzania tangu ilipopata uhuru wake mwaka 1961, ilikuwa ikitumia mfumo wa vyama vingi hadi mwaka 1965 ilipoamua kuachana nao. Hata hivyo mwaka 1992, Tanzania iliridhia mageuzi makubwa ya kurejea katika mfumo wa vyama vingi vya siasa. Sababu iliyotolewa mwaka 1965 wakati wa kuachana na vyama vingi ni kwamba pamoja na mambo mengine, vyama vya upinzani ambavyo vilikuwapo kama vile African Independence Movement (AIM) na People’s Democratic (PDP), havikuwa na nguvu. Lakini pia wakati ule, kulikuwa na vuguvugu kubwa la mataifa mengi ya Afrika kuendeshwa chini ya utawala wa chama kimoja kutokana na kile kilichoelezwa kwamba ni kuleta umoja wa kitaifa na kuondoa mifarakano na migogoro kwa lengo la kujiletea maendeleo. Licha ya kuwa na chama kimoja kilichokuwa kimeshika hatamu, hata nyanja nyingine kuu na muhimu za kiuchumi na kijamii, kwa kiwango kikubwa zilikuwa chini ya umma. Vyombo vya habari kadhalika, vilikuwa katika mfumo dola. Redio, televisheni (kwa Zanzibar) na magazeti, ama vilimilikiwa moja kwa moja na Serikali, taasisi zake au chama na jumuiya zake. Tunakumbuka vyombo kama Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD), Sauti ya Tanzania Zanzibar (STZ), Magazeti ya Daily News/Sunday News, Uhuru/Mzalendo, Mfanyakazi na Mkulima wa Kisasa. Kutokana na uchache na umiliki wake, maudhui ya vyombo hivi yaliratibiwa na dola yakilenga masuala kadhaa ambayo Serikali ilikuwa imeyapa kipaumbele. Pamoja na changamoto zake, habari za wakulima zilipata fursa katika vyombo hivyo. Achilia mbali gazeti, kulikuwa na vipindi vya redio vya Mkulima wa Kisasa ambavyo vilitoa mafunzo na maelekezo mbalimbali ya kilimo bora. Kulikuwa pia na mkakati maalumu kupitia Taasisi ya Vielelezo wa kupeleka sinema vijijini kuelimisha wakulima juu ya ukulima na ufugaji bora. Kimsingi, kulikuwa na upatikanaji wa taarifa hasa zile za msingi kwa umma wa vijijini. Wahenga walisema, kila masika yana mbu wake. Katika mabadiliko ya mwaka 1992 yaliyoruhusu mfumo wa vyama vingi na soko huria, Serikali ilijitoa katika biashara na kulegeza masharti hivyo kuiwezesha sekta binafsi kushiriki moja kwa moja katika masuala ya kiuchumi na kijamii. Mabadiliko yalichochea kuanzishwa kwa Sera ya Habari na Utangazaji ya mwaka 1993. Hata hivyo, haikujitoa katika usimamizi na uendeshaji wa vyombo vyake vya habari, bali iliruhusu sekta binafsi nayo kuingia katika biashara hiyo. Hivyo, kuanzia mwaka 1992, magazeti, vituo vya televisheni na redio na baadaye mitandao ya mawasiliano vilianza kwa kasi. Tofauti na awali ambako mwelekeo wa habari ulilenga zaidi propaganda, safari hii mtazamo ulikuwa wa kibiashara zaidi na hali hiyo imekuwa na athari kubwa katika upatikanaji wa habari za vijijini. Kutokana na msukumo huo wa nguvu ya soko, vyombo ambavyo vilishindwa kujiendesha kibiashara vilikufa na hivyo ndivyo ilivyotokea kwa Gazeti la Mkulima wa Kisasa. Vipindi vingi vilivyoanzishwa katika redio na televisheni vililenga zaidi kuwavutia watangazaji (advertisers). Kwa upande mwingine, asilimia kubwa ya magazeti na machapisho Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011 husomwa zaidi mijini ambako usambazaji ni rahisi na kiwango cha kujua kusoma na kuandika ni kikubwa na hilo likawa na athari kubwa kwa upatikanaji wa habari za vijijini. Hiyo ilimaanisha kwamba wakulima na wananchi wengine waishio vijijini walianza kupewa habari ambazo hazikuwa na uwiano wa moja kwa moja na matatizo au vipaumbele vyao. Kwa mfano, mwaka 1995 wakati taifa likiwa katika kampeni za kwanza tangu kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi, baadhi ya vituo vya televisheni vilitumia fursa hiyo vibaya kwa kuonyesha picha za mauaji hivyo kuwatishia wananchi. Mabadiliko makubwa Hata hivyo, kadri miaka inavyosonga kumekuwa na mabadiliko makubwa. Kukua kwa teknolojia ya mawasiliano na dhana ileile ya soko kumevifanya vyombo vya habari kuanza kubaini umuhimu wa kulitazama soko la vijijini waliko asilimia 80 ya Watanzania. Halmashauri za wilaya na wawekezaji wengine wa ndani wameanzisha redio za jamii (community radio) ambazo zinatoa huduma ya habari katika maeneo yao. Hili limekuwa na mchango mkubwa kwa wananchi wa vijijini kwani taarifa, kero na shida zao zimekuwa zikipata fursa ya kusikika. Lakini siyo kusikika tu, kumekuwa na fursa kubwa zaidi ya kupata habari zinazokidhi mahitaji yao kwa kiwango kikubwa na hivyo kuchochea maendeleo yao. Ingawa wilaya zilizoanzisha radio hizi za jamii ni chache mno, lakini wilaya zilizobahatika kuwa na redio hizi, zimekuwa zikitumia fursa hiyo kufikisha ujumbe muhimu katika maeneo husika kama vile bei ya bidhaa na huduma nyingine muhimu. Endelea Uk wa 11 7 MFUMO WA TAARIFA ZA MASOKO WA MVIWATA (MAMIS) ANA KWA ANA/MAKALA PATA BEI ZA MAZAO KWENYE SIMU YAKO POPOTE ULIPO!! Jinsi ya kupata taarifa kwenye simu yako: Taarifa ya BEI ZA MAZAO 1. Andika neno BEI acha nafasi 2. Andika zao unalotaka bei yake mfano; MAHINDI 3. Kisha tuma kwenda namba 0654 555 884 Taarifa ya WAUZAJI 1. Andika neno NANUNUA acha nafasi 2. Andika zao unalotaka kununua mfano; MAHINDI 3. Kisha tuma kwenda namba 0654 555 884 Taarifa ya WANUNUZI: 1. Andika neno NAUZA acha nafasi 2. Andika zao unalotaka kuuza mfano; MAHINDI 3. Kisha tuma kwenda namba 0654 555 884 Masoko yaliyopo mpaka sasa: MOROGORO, TAWA, TANDAI, NYANDIRA, KIBAIGWA, DODOMA, IGUNGA, TABORA, SHINYANGA, MASWA, BARIADI, BUKOMBE, KAHAMA, KILOMBERO (ARUSHA), KARIAKOO, BUGURUNI, TEMEKE, IGURUSI (MBEYA), MKURANGA, MAKAMBAKO, SIMANJIRO, TAVETA, MKATA, IGAGALA, MATAI (RUKWA), KASANGA, HIMO, HOLILI, n.k Mazao yaliyo kwenye mfumo huu: MAHINDI, MCHELE, MAHARAGE, CHOROKO, KUNDE, MBAAZI, NJEGERE, MTAMA, UWELE, ULEZI, UFUTA, ALIZETI, NDIZI MBIVU, NDIZI MBICHI, MAGIMBI, MUHOGO, NANASI, CHUNGWA, PAPAI, EMBE, PARACHICHI, NYANYA, VITUNGUU MAJI, VITUNGUU SAUMU, TANGO, KAROTI, KABICHI, HOHO, LUBABU, SELELI, BITRUTI, ZUKINI, SALADI, KOLIFLAWA, TANGAWIZI, PILIPILI MTAMA, MDALASINI, ILIKI. ...meseji moja kwa kila zao moja Kwa Mawasiliano zaidi piga SIMU NAMBA 0659250317 8 imedhaminiwa na; Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011 MAKALA Taaluma ya habari ni wito Na Susuma Susuma V yombo vya habari ni jina la jumla la mfumo wa mawasiliano unaojumuisha utangazaji wa redio, televisheni, majarida na magazeti. Vyombo hivi vina wajibu mkubwa wa kuhudumia matakwa ya jamii katika maisha yao ya kila siku. Vyombo vya habari vinaelimisha, vinatoa burudani na kutoa changamoto kwa wananchi na viongozi kuhusu mambo mbalimbali. Kadhalika taaluma ya habari ni tasnia nyeti inayoheshimika katika jamii yoyote inayothamini ustaarabu, umoja na utangamano wa kitaifa. Kuandika makala kwenye magazeti, kusoma taarifa ya habari au utayarishaji wa vipindi vya siasa, jamii, utamaduni, dini, burudani ama matukio yanayohitaji jamii kupewa taarifa, ni shughuli zinazohitaji ushirikiano wa kutosha baina ya wadau yaani waandishi, watoa habari na walaji (wasikilizaji/wasomaji). Kwa mantiki hiyo, ushirikiano madhubuti kati ya wadau wa habari na waandishi wa habari ni nguzo ya maendeleo katika jamii. Aidha, kufanikisha masuala haya kunahitaji umakini, weledi, mazingatio ya kufuata miiko, maadili na heshima kwa mwandishi ama mtangazaji husika. Utendaji kazi wa vyombo vya habari Ukilinganisha miaka 50 iliyopita hali ya utendaji kazi wa vyombo vya habari na hali ilivyo hivi sasa nchini kwetu ni tofauti kabisa. Uandikaji wa habari, makala, utangazaji na utayarishaji wa vipindi hivi sasa hauzingatii ujuzi, taaluma na kuheshimu miiko, kama ilivyokuwa miaka ya awali. Fani hii imeshuhudia watu wanahitimu uandishi wa habari ngazi ya shahada ya kwanza au ya uzamili, lakini bado wakashindwa kuandika habari kwa usahihi. Kwa mfano eneo moja linalowashinda ni jinsi ya kufahamu mahitaji halisi ya wasomaji, wasikilizaji ama watazamaji wao, kushindwa kufahamu habari ilipo ama kushindwa kutofautisha habari, uzushi na fitina. Wapo wanaosema fani hii ni rahisi kuliko zote na hawa ndiyo wanaovamia fani hii na kudhani kwamba wanafanya vizuri bila kufahamu kuwa wanachangia kuua taaluma. Fani hii siyo rahisi kama inavyodhaniwa na wengi, na pengine ndiyo maana kila kukicha vyombo vya habari vinalaumiwa kwa kukiuka miiko na maadili kwa kuwa wengi wanaamua kujiunga wakidhani ni kuandika tu, matokeo yake wanafanya upotoshaji. Tumeshuhudia pia utitiri wa vyombo vya habari vinavyoanzishwa kila leo, lakini cha kushangaza vingi vinaanzishwa mijini na kuhudumia watu wa mijini tu na kuwaacha kando watu waishio vijijini. Kwa mujibu wa takwimu za Msajili wa Magazeti mpaka sasa amekwishasajili zaidi ya magazeti na majarida 350 ingawa ni asilimia 15 tu ya machapisho hayo ambayo yanaonekana mitaani kwa wakati huu na asilimia kubwa yakiwa mijini. Idadi kubwa ya magazeti yaliyosajiliwa yanamilikiwa na watu au makampuni binafsi isipokuwa magazeti ya ”Daily News, Sunday News na Habari leo” ambayo yanamilikiwa na Serikali na gazeti la Uhuru linalomilikiwa na chama tawala CCM. Ukipekuwa kwa undani utendaji kazi wa magazeti haya sasa yako kibiashara zaidi kinyume na matarajio ya kutoa huduma ya kuhabarisha umma. Vyombo vya habari vinapoanzishwa vikiwa na mlengo wa kibiashara zaidi, ni moja ya sababu inayochangia vyombo vingi virundikane mjini ambako wamiliki wanaamini watauza na kupata matangazo ya kutosha. Na hoja hapa ni Je, jamii ya huko vijijini ambako biashara ya radio, televisheni na magazeti hazilipi, itafikiwaje na habari zenye kuchochea maendeleo? Kufanya hivi vyombo vya habari vinakiuka sheria na kuwanyima haki Endelea Uk wa 10 MVIWATA katika kusaidia wakulima kupaza sauti zao, imekuwa ikiwawezesha wanahabari kuyafikia maeneo ya vijijini na kuchukua habari za kero zao Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011 9 MAKALA Taaluma ya habari ni wito... Inatoka uk. wa 9 ya msingi wananchi wa vijijini. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) ambayo ilifanyiwa marekebisho mwaka 1984, imeweka kifungu maalum kinachotaja wazi kuwa habari ni haki ya msingi ya raia. Kifungu hicho cha 18 cha Katiba kinasema: (1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati. (2) Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wowote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani kote, ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi; na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii. Wajibu wa vyombo vya habari Njia muhimu za kuwezesha wananchi kufurahia haki ya kupasha na kupashwa habari na kujieleza kwa kutoa maoni hadharani bila bughudha,vitisho na ukandamizwaji ni kupitia vyombo vya habari. Kutokana na umuhimu wa kipekee wa haki hii ya msingi, nafasi ya vyombo vya habari katika utekelezaji wake pia ni ya kipekee. Kwa kuwa vyombo vya habari vinawawezesha wananchi kutumia haki hii ili isibaki nadharia au kwenye maandishi tu, hakuna budi wamiliki wa vyombo vya habari pamoja na serikali, watambue na kukiri kwamba nafasi yao ni ya kutoa huduma au mahitaji ya lazima kwa jamii, huduma kwa umma. Hadhi ya huduma ya kijamii inazidi sana ile ya bidhaa ambazo huuzwa kuingiza faida. Ndiyo maana wajibu wa wamiliki wa vyombo vya habari kwa jamii ni mkubwa kuliko wa mfanyabiashara ama mwekezaji ambao msukumo wao mkubwa ni 10 kutengeneza faida. Hata vyombo vya habari vya serikali vinapaswa kuwajibika kwa umma na sio utashi wa kisiasa wa wanasiasa na watawala. Wanahabari pamoja na kwamba huajiriwa na wamiliki wa vyombo, bado huwajibika kwa umma. Na ndiyo maana ili vyombo vya habari viweze kutekeleza majukumu yao, hakuna budi kwa wahariri na wanahabari kuwa na uhuru wa kutosha kukusanya, kuchambua na kusambaza habari bila woga, shinikizo au ushawishi wa wamiliki na washiriki wao kibiashara. Habari ni huduma Kazi ya uandishi wa habari ni fani ambayo pamoja na kuwa na ujuzi lakini inahitaji zaidi wito. Ni fani ambayo inahitaji zaidi mtu kutanguliza utu na upendo ama dhana ya kutoa huduma kuliko malipo ama kufanya biashara. Ni fani isiyojali sana malipo yenye kulingana na kadhia, ugumu wala masuala mengine kwa kuwa kuna wakati unakuwa unashughulikia tatizo la kijamii iliyo masikini ambayo malipo yake ni asante. Kinachosikitisha zaidi ni kuona baadhi ya waandishi wa habari wakishabikia zaidi kuandika habari za migogoro na kuwachafua watu, wakati mwingine wakiishia kudai posho bila hata kuandika chochote. Hali hii inaonesha walivyokosa ushirikiano na jamii. Pia zipo sheria ambazo zinaonekana kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari nchini, ambazo wanahabari wamekuwa wakizipigia kelele kwa kuitaka serikali kuzirekebisha ama kuzifuta kabisa. Hizi ni pamoja na sheria ya magazeti ya Tanzania ya mwaka 1976 ambayo inampatia uwezo waziri anayehusika na habari wa kulifungia gazeti lolote lile kama ataridhika kuwa limekiuka kwa kiasi kikubwa matakwa ya sheria hiyo. Sheria hizi pia zinakwamisha upatikanaji wa habari sahihi zenye maslahi umma. Mfano halisi ni wa taarifa zinazohusiana na kashfa kwenye migodi ya madini na kwenye sekta ya uwindaji wanyama kwenye mbuga za wanyama ambazo zinaakisi uchumi wa nchi. Serikali inapaswa kupitisha sheria rafiki kwa vyombo vya habari na ambazo zinaweka mazingira huru ya upatikanaji wa habari, kwani kuvifunga minyororo vyombo vya habari ni kuwafunga minyororo wananchi. Kwa upande mwingine wapo waandishi wa habari wanaotishiwa maisha pale wanapofuatilia ili kupata habari za kina kuhusiana na jambo fulani lenye maslahi kwa jamii. Lakini hiyo siyo sababu ya wao kufanya shughuli zao kinyume cha sheria na maadili ya taaluma yao kama vile kutoa na kupokea rushwa, upotoshaji na udanyanyifu, uchochezi, ushabiki, kutunga ama kutia chumvi habari. Hata hivyo changamoto ni sehemu ya maisha, ni chachu kwa maendeleo yoyote, wanahabari ni vyema tukajenga tamaduni ya kwenda vijijini kuzungumza na kutangaza habari za mafanikio, ubunifu, uzoefu na mbinu wanazotumia wanavijiji kutatua changamoto za maisha yao ya kila siku. Kwa kuwa tumeamua kuwatumikia wananchi wenye uhitaji wa huduma yetu, hatuna budi kuzikabili changamoto zote za kutafuta, kuandaa na kuzifikisha habari kwa wadau bila kujali zinapatikana kutoka mazingira yenye changamoto nyingi. Kwa upande mwingine liko kundi dogo la wanahabari nchini ambao wamepungukiwa utu na upendo, wametanguliza zaidi maslahi binafsi, ndiyo maana wameigeuza fani hii kuwa biashara badala ya huduma kwa jamii. Kundi hili japokuwa ni dogo lakini laweza kuwa na madhara makubwa kwa jamii hasa kipindi hiki ambao vitendo vya ufisadi vinazidi kushika kasi ndani ya nchi yetu. Wakialikwa kwenda kuchukua habari Endelea Uk wa 11 Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011 MAKALA Soko huria lilivyoathiri... Inatoka uk. wa 7 Inawezekana bado kuna vikwazo vya hapa na pale katika kuwafikia wananchi wa vijijini walio wengi, lakini muhimu ni kuviimarisha zaidi vyombo hivi ili walau viweze kuziba pengo lililosababishwa na kutoweka kwa majarida kama ya mkulima wa kisasa. Mamlaka za miji na wilaya nchini ni mali ya wananchi kupitia mabaraza ya madiwani ambao wanatokana na kura za watu katika ngazi za kata. Kwa maana hiyo basi ni fursa kwa viongozi hawa wawakilishi wa umma (madiwani), kuimarisha usimamizi wa vituo vya redio na televisheni vinavyomilikiwa na halmashauri zao ili viweze kukidhi matakwa ya jamii husika, ziwe za wakulima, wafugaji, wavuvi, wachuuzi au wengineo. Hii ni moja ya hatua muhimu zinazoweza kuwarejesha wazalishaji wadogo wa sekta mbalimbali nchini katika dunia ya mawasiliano. Intaneti na simu za mkononi Tunapozungumzia habari, hatuwezi kuacha kuzungumzia njia nyingine za kisasa za mawasiliano kama vile intaneti na simu za mkononi. Hizi kwa ujumla wake zimekuwa na mchango mkubwa kwa wananchi wa vijijini katika mambo mbalimbali. Intaneti kwa mfano, imewawezesha wananchi kutafuta masoko, masomo na kuwasiliana kwa sababu mbalimbali na taasisi, ndugu, jamaa na marafiki zao walio mbali. Zamani ilikuwa ni gharama kubwa na usumbufu kuwasiliana kwa njia ya barua na ndugu walio mbali. Lakini sasa, katika baadhi ya maeneo ya vijijini kuna vituo vya mawasiliano ambako wananchi huenda na kupata huduma hizo za mtandao (simu/ intaneti) na hivyo kupata taarifa mbalimbali za shughuli zao na pia kuwasiliana na watu mbalimbali. Magazeti mengi ya ndani na nje na hata redio zimeunganishwa pia katika mitandao hii ya intaneti, hivyo wananchi popote walipo wanaweza kusoma habari za leoleo hivyo kujiweka katika nafasi nzuri ya kuujua ulimwengu na yanayoendelea na kutumia taarifa hizo kujiongezea maarifa na kujiendeleza. Njia hii ya simu ndiyo imekuwa na athari chanya kubwa. Idadi kubwa ya Watanzania mijini na vijijini hivi sasa wanafaidika kwa huduma hii iwe moja kwa moja au kupitia kwa ndugu na jamaa zao. Upashanaji wa habari ulikwaza mambo mengi ya watu waishio vijijini lakini baada ya mapinduzi ya teknolojia hii, si ajabu hivi sasa kwa mfano, mtu aliye kijijini kumweleza au kumpa taarifa aliye mjini juu ya tukio lililotokea huko huko mjini. Mara ngapi tumesikia watu waishio Dar es Salaam wakipewa taarifa za msiba uliotokea hukohuko Dar es Salaam na mtu aishie kijijini? Kimsingi mawasiliano hayo yamevunja umbali baina ya watu wa maeneo haya. Japokuwa haya yanatokea kwenye maeneo machache mno ya vijijini ambayo yamebahatika kuunganishwa na huduma za simu za mkononi. Mapinduzi mengine chanya yaliyotokana na uwepo wa mawasiliano haya ya simu ni utumaji na upokeaji wa fedha kupitia mitandao ya simu. Usumbufu wa kuwatumia wazazi kijijini fedha au kuwalazimu wakulima na wafanyabiashara kusafiri kwenda mjini au kijijini kununua au kuuza bidhaa siku hizi hauna ulazima. Baada ya kuingia makubaliano, mkulima anaweza kufungasha mazao yake na kuyatuma mjini na kutumiwa fedha kwa njia ya simu na hayo hufanyika ndani ya muda mfupi mno. Zaidi ya hayo huduma za mawasiliano ya simu zimepanua wigo wa ajira kwa vijana vijijini na kuongeza kipato, hivyo basi wananchi wanapaswa kuitumia vyema fursa hiyo kwa kuifanya kuwa kichochocheo cha maendeleo yao. Taaluma ya habari ni wito... Inatoka uk. wa 10 kijijini, swali la kwanza wanalouliza ni watalipwa? nani atawalipa? kiasi gani watalipwa? Wakishapewa majibu kuwa hakuna malipo kwa kuwa kazi hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yao, wanaishia kutoa visingizio vya kutoenda kufanya kazi hiyo. Wanahabari tunapaswa kujitambua kuwa sisi ni nguzo muhimu ya maendeleo katika jamii hivyo tunatakiwa kujenga ushirikiano madhubuti baina yetu na wadau wa habari wakati wa kutekeleza majukumu ya kuipasha habari jamii kwa uaminifu na kudhihirisha kuwa tulioko kwenye taaluma hii tuna wito. Aidha ni muhimu kwa umma kuwa na imani na wanahabari kuwa wanachofanya ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu kama ilivyo kwa watumishi wa sekta nyingine na kwamba hawana sababu ya kuwaogopa, kujenga chuki ama kuwapa taarifa za uongo na uchochezi, bali washirikiane nao kwa ukaribu. Ni vyema kila kundi likajali na kuheshimu uhuru wa kutoa na kupata habari kama ilivyo ndani ya katiba ya nchi. Jihadhari na maambukizo ya UKIMWI jikinga na umlinde mwenzako Mwandishi wa Makala hii ni Mhariri wa Habari wa Gazeti la Mwananchi Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011 11 KAMERA KAMERA YA MVIWATA MITANDAONI Wakulima wa kata ya Mlangali wilayani Ludewa wakioneshana jambo lililowavutia kwenye gazeti la Pambazuko linaloandika habari za wakulima na kusambazwa vijijini Bibi HotensiaThomas, mwenyekiti wa Bodi ya Soko la Wakulima Nyandira akisikiliza swali kwa mmoja wa wadau wa masoko ya Igurusi, Matai na Kasanga walipofanya ziara sokoni hapo Julai 21, 2011 Moja ya mikutano ya mitandao ya wakulima ambayo imekuwa ikitumika kupashana habari vijijini Wana-MVIWATA walioshiriki Tamasha la Jinsia Septemba 2011 wakimsikiliza mwenzao wakati wa majadiliano Picha ya pamoja ya baadhi ya viongozi na watumishi wa MVIWATA na wawakilishi wa ubalozi wa Ireland nchini Bibi Aileen D’donovan, Dkt Sizya Lugeye na Bw.Vicent Akuluyuka (wa nne hadi wa sita kutoka kushoto waliosimama), baada ya ujumbe huo kutembelea makao makuu ya MVIWATA yaliyoko Morogoro Julai 5, 2011. Wana-MVIWATA Kiteto Manyara walioshiriki mafunzo ya kujengea uwezo viongozi Julai 28-29, 2011, wakiwa na baadhi ya watumishi wa MVIWATA taifa waliowezesha mafunzo hayo 12 Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011 KAMERA KAMERA YA MVIWATA MITANDAONI Ukosefu wa habari sahihi za masoko vijijini unasababisha bidhaa za wajasiliamali kama hawa wa Kwekanga Lushoto kukosa soko ‘Natangaza kazi za mikono’, ndivyo anavyoelekea kusema mama huyu mkazi wa kijiji cha Kwalei wilayani Lushoto Wakulima wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kushiriki Jukwaa la Wakulima mkoani Ruvuma Bibi Elizabeth Lagwen (kulia) Mwenyekiti wa mtandao wa msingi Mamire Babati Vijijini akiwasikiliza wageni kutoka shirika la TRIAS Ubeligiji waliomtembelea kujifunza shughuli anazozifanya Wanawake jamii ya wafugaji wilayani Monduli, wakishiriki kazi ya kuchimba msingi na kuweka mawe ya msingi ya jengo la kukusanyia la kituo cha kibiashara Licha ya kuwa na historia ya ufugaji pekee, jamii ya Wamasai sasa wamebadlika na kuanza kushiriki kilimo kama wanawake hawa walivyokutwa na kamera yetu wakipanda mazao shambani Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011 13 KUTOKA MITANDAONI Maonesho ya NaneNane 2011 Wakulima wazungumzia matumizi na faida za bidhaa walizoonesha Na Goodness Mrema, Morogoro M tandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA) katika kuhakikisha kwamba unatekeleza vyema majukumu yake umekuwa na utaratibu wa kuwawezesha wakulima toka mikoa mbalimbali kushiriki kuonesha bidhaa zao kwenye maonesho ya kilimo maarufu kama NaneNane. Mwaka 2011 katika maonesho hayo ya wakulima MVIWATA iliwawezesha wakulima zaidi ya 40 kushiriki maonesho hayo kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Morogoro na Themi Arusha, kwa lengo la kuwapatia fursa ya kujifunza, kubadilishana uzoefu na kutangaza bidhaa zao. Katika maonesho hayo MVIWATA ilipata ushindi wa kwanza kwa upande wa vyama na mashirika yasiyo ya kiserikali kwenye uwanja wa maonesho ya NaneNane kanda ya Mashariki wa Mwalimu Nyerere Morogoro na katika kanda ya Kaskazini kwenye viwanja vya Themi Arusha na kukabidhiwa zawadi ya Kombe na Cheti vilivyotolewa na Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda. Aidha kwenye viwanja vya Themi Arusha mkulima Bw. Richard Kipara ambaye ni katibu wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Ekenywa (MVIWAEKE) alishinda kuwa ‘Mkulima Bora’ wa wilaya mpya ya Arusha Vijijini. Katika maonesho hayo mfugaji Bw. Moses Ndoipo kutoka wilaya ya Longido, alileta mbuzi bora aina ya Isiolo wa uzito wa kilo 240 aliyekuwa anauzwa Sh. 300,000 na kuwa kivutio kwa wageni waliotembelea maonesho. Miongoni mwa wakulima waliopata fursa ya kushiriki maonesho haya ya NaneNane kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Morogoro, walielezea umuhimu wa bidhaa walizoonesha na faida ya maonesho kwa ujumla. Kakao na Mawese Bibi Lain Mwakatundu kutoka Kyela, Mbeya alikuwa na zao la mawese na kakao ambapo alisema usindikaji wa mawese unawezesha utengenezaji wa bidhaa mbalimbali muhimu kama vile sabuni ya kufulia na kuogea. Lain Mwakatundu “Vile vile kutokana na mawese unaweza kupata mbosa ambayo hutengeneza mafuta ya kupikia na kupaka. Mafuta haya ya kupaka yanafaida kubwa ikiwemo ya kuponya mba wa ngozi katika mwili wa binadamu. Aidha magamba ya mawese hutumika kwa ajili ya kuni. Kwa upande wa zao la kakao alisema lina matumizi mengi ingawaje matumizi yanayofahamika zaidi kwa watu ni utengenezaji Endelea Uk wa 15 Mwenyekiti wa MVIWATA Morogoro Bw. Stanford Chabonga aliyenyanyua juu kikombe, akiungwa mkono na wana-MVIWATA wenzake kusherehekea ushindi 14 Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011 KUTOKA MITANDAONI Inatoka uk. wa 14 wa kinywaji na kitafunwa aina ya chocolate. Akaongeza kuwa “ndani ya tunda la kakao kuna mbegu zenye ladha ya sukari ambazo hutumika kutengeneza juisi lakini pia juisi hiyo waweza kuichachusha na kupata kilevi baada ya kuiweka kwa muda wa siku tatu hadi nne.” “Mbegu hizi za kakao pia zikikaushwa na kusagwa hupatikana unga laini ambao unafaa kwa matumizi mengi ikiwemo kuweka kama kiungo kwenye mboga na wengine hutafuna unga pekee maan unaradha nzuri,” anafafanua. Bibi. Mwakatundu anafafanua zaidi kuwa zao la kakao ni dawa nzuri ya kupunguza kasi ya ugonjwa wa kisukari mwilini na pia hupunguza mafuta ndani ya mwili wa binadamu, hivyo anawahimiza watanzania kulitumia zaidi. Anaeleza kuwa katika mkoa wa Mbeya hususan wilaya ya Kyela mazao ya Kakao na Mawese hulimwa kwa ajili ya chakula na biashara japokuwa soko lake kwa sasa siyo zuri. Hata hivyo anaongeza kuwa maonesho ya mwaka huu yamemsaidia kupanua wigo wa soko kwani hivi sasa amepokea maombi ya wateja wengi wanaohitaji bidhaa na wengine wameomba aende kuwafundisha kilimo cha mazao hayo. Tiba asili Mzee Hassan Nundu kutoka kijiji cha Chamkoroma wilaya ya Kongwa - Dodoma, yeye alionesha dawa za asili zinazotokana na magome na mizizi ya miti ambazo zinaaminika kutibu magonjwa mbalimbali ya binadamu kama vile meno, tumbo, athma pamoja na kideri cha kuku. Akielezea matibabu ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo, anasema mgonjwa anayetumia dawa hiyo anapona kwa muda mfupi hata kama vidonda ni vya muda mrefu. “Dawa hii ambayo ni mchanganyiko wa mizizi ya miti mbalimbali, mtumiaji huchanganya na maziwa mabichi kwa kuweka kijiko kimoja cha dawa katika kikombe cha maziwa na kunywa mara tatu kwa siku kwa muda wa siku kumi na tano tu.” “Dawa nyingine ni ya fangasi ambapo fangasi hawa huwa tumboni na kwenye mapacha ya vidole vya miguu kutokana na joto linalokuwepo ndani ya kiatu kufuatia msuguano wa miguu ya mtu anapotembea. Dawa hii ya unga inampasa mgonjwa kuiweka kwenye maji baridi na kisha kuichuja ili kupata mabaki ambayo atayapaka sehemu zilizoathirika na baadaye kunywa dawa iliyochujwa mara tatu kwa siku kwa muda wa siku tatu na atapona kabisa.” Bw. Nundu anafafanua kuwa athma ni ugonjwa ambao hauna tiba hospitalini bali hutulizwa lakini yeye anayo dawa ya kutibu ugonjwa huu ambayo inapatikana kwenye vipaketi vitatu. Mgonjwa anapaswa kuiloweka na kuichuja kisha kunywa mara mbili kwa siku asubuhi na jioni. “Ninawashauri Watanzania kurudia dawa zao za asili zinazotokana na mizizi na magome ya miti kwani hazina kemikali zitakazowadhuru kiafya tofauti na dawa za hospitalini ambazo nyingi sasa ni bandia na kuongeza kuwa anazo dawa nyingi za asili zinazotibu maradhi ambayo hayawezi kutibiwa hospitalini kama vile kukojoa kitandani pamoja na meno ambayo mara nyingi hung’olewa badala ya kutibiwa. Mzee Nundu anasema maonesho ya NaneNane ambayo amekuwa akishiriki yanamsaidia kupata wateja wapya na kukutana na wagonjwa aliowatibu miaka ya nyuma ambao wanashuhudia kuponywa na dawa zake. Bibi Hortenzia Thomas kutoka kijiji cha Nyandira Mvomero, mkoani Morogoro alifika katika maonesho hayo kutangaza tiba asili itokanayo na matunda na mbogamboga zikiwemo njegere, sereri, cornflower, maharagwe, redishi, boga, nzukini, pasili na kabichi. Anaeleza kuwa kabichi huponya ugonjwa wa kisukari. Hii ni baada ya mgonjwa kuchukua mti wa katikati ya kabichi kuukatakata na kuuchemsha, kisha kunywa maji yake mara tatu kwa siku. Pia mboga mboga kama Radishi na tenepsi hutumika kutibu vidonda vya tumbo na shinikizo la Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011 damu. Bibi Mwajuma Mwiyoha, ni mkulima kutoka Chamkoroma ambaye alifika kwenye maonesho haya akiwa na zao la Alizeti ambalo ni maarufu kwa kutengeneza mafuta ya kupikia. Hata hivyo, kwa mkulima huyo zao la Alizeti siyo kwa ajili ya kukamua mafuta pekee bali pia hulitumia kutengeneza dawa ya kuhifadhia mazao galán, dawa ambayo haina madhara kwa watumiaji. Mwajuma Mwiyoha “Dawa hii ya kuhifadhia mazao hutokana na masuke ya alzeti hutengenezwa kwa teknolojia rahisi tu ambayo mkulima yeyote anaweza kumudu kwani cha kufanya ni kuyachoma masuke ya alizeti kwenye chombo kisafi, yakishaungua vizuri hutwangwa na kuchekechwa ili kupata majivu laini ambayo ndio dawa yenyewe. Dawa hii hunyunyizwa juu ya magunia yenye mazao na ina uwezo wa kuzuia mazao yasishambiliwe na wadudu kwa muda wa miaka miwili hadi mitatu. Bibi. Mwiyoha anasema dawa hii ni nafuu kwani haimwingizii mkulima gharama na ni salama kwa afya ya binadamu. Ufugaji wa nyuki wadogo Bw. Hassan Haji kutoka Zanzíbar ni mkulima mdogo anayefuga nyuki wadogo wasiouma. Mkulima huyu ameanza ufugaji wa nyuki wasiouma miaka 15 iliyopita. Alianza ufugaji wa nyuki hao kama mradi wa kiuchumi lakini pia kwa lengo la kuwahifadhi baada ya kuona kwamba wako hatarini kutoweka kutokana ukataji wa miti katika maeneo ya misitu vitendo ambavyo vinawafanya viumbe hao kukimbia na hivyo kizazi hicho kupotea. Endelea Uk wa 17 15 KUTOKA MITANDAONI Ludewa wahimizwa kuwekeza kwenye kilimo cha miti Na Susuma Susuma, Ludewa W akulima wilayani Ludewa na nchini kote wametakiwa kuwekeza zaidi katika upandaji wa miti kibiashara ili kuhifadhi mazingira na kujiongezea kipato kutokana na soko la miti kuongezeka kila mwaka. Wito huo umetolewa na Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Swedish Cooperative Center (SCC) Kanda ya Mashariki mwa Afrika Bw. George Onyango alipokuwa akizungumza na wakulima wa kata za Mlangali na Milo wilayani Ludewa katika mkoa mpya wa Njombe. Bw. Onyango alikuwa kwenye ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wenye lengo la kuwawezesha wakulima wadogo kuwa na uzalishaji wenye kukuza na kuongeza kipato na uhifadhi wa mazingira na bioanuai Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Swedish Cooperative Center (SCC) Kanda ya Mashariki mwa Afrika Bw. George Onyango (aliyenyosha mkono) akizungumza na wakulima wa kata ya Mlangali ya chakula wanayolima. Aidha aliwataka wakulima hao kuunda mitandao imara itakayofanya kazi ya kutafuta na kusimamia soko la mazao ya miti ili kuondokana na walanguzi ambao sasa wananeemeka kwenye biashara ya mazao ya chakula Uharibifu ya wakulima. huu tuliufanya sisi katika Naibu mkurugenzi huyo alisema licha ya harakati za kujitafutia riziki, na kuwaingizia utajiri, tunaoathirika na uharibifu huu ni sisi, hivyo kilimo cha miti ni sisi wenyewe ndiyo tunapaswa kurejesha kitasaidia kwa kiwango kikubwa uhai wa mazingira yetu kwa kuwekeza kwenye katika utunzaji upandaji miti na kwa kufanya hivi tutasaidia wa mazingira ya kupunguza athari za mabadiliko ya wilaya hiyo ambayo yameharibiwa kutokana tabia ya nchi na shughuli za kibinadamu zikiwemo ukataji miti kwa ajili ya katika Ziwa Nyasa unaotekelezwa na kupata nishati ya mkaa na kuni. “Uharibifu huu tuliufanya sisi Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Wadogo Tanzania (MVIWATA) kwa katika harakati za kujitafutia riziki, na tunaoathirika na uharibifu kushirikiana na SCC. Bw. Onyango alisema biashara ya huu ni sisi, hivyo ni sisi wenyewe miti na mazao yake, inakuwa kila siku ndiyo tunapaswa kurejesha uhai na kupanda bei, hivyo kwa kuwekeza wa mazingira yetu kwa kuwekeza zaidi kwenye upandaji miti wakulima kwenye upandaji miti na kwa kufanya hao watapata mapato mazuri kuliko hivi tutasaidia kupunguza athari za hata wanayoyapata kwenye mazao mabadiliko ya tabia ya nchi,” alisema Bw. Onyango. Aliwahimiza wakulima hao kutumia vyema elimu ya uhifadhi wa mazingira, ujasiriamali na usimamizi wa vikundi inayotolewa kupitia mradi huo. Kwa upande wake afisa anayesimamia mradi huo wilayani Ludewa Bw.Remmy Urio alisema matokeo ya mafunzo yaliyotolewa kwa wakulima yameanza kuonekana baada ya wengi wao kuanza kupanda miti kwenye maeneo ya wazi na wameimarisha usimamizi wa sheria zinazolinda mazingira. Bw. Urio alisema wakulima wengi pia wameibua miradi ya kiuchumi ikiwemo uanzishaji wa SACCOS ili kuwawezesha kuboresha kipato badala ya kutegemea kipato kutoka kwenye kazi zinazochangia uharibifu wa mazingira. Afisa Programu wa MVIWATA Bw. Laurent Kaburire alisema, utafiti uliofanywa na MVIWATA kwenye wilaya zinazounganishwa na Ziwa Nyasa kwa upande wa Tanzania, umebaini kwa shughuli nyingi zinazoathiri ziwa zinatekelezwa na wavuvi, wafugaji na wakulima Endelea Uk wa 17 16 Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011 KUTOKA MITANDAONI Maonesho ya NaneNane 201... Inatoka uk. wa 15 Miongoni mwa faida anazozipata Bw. Haji ni pamoja na kujipatia kipato kwa ajili ya familia yake kwani kwa sasa anao wateja wengi wanaotumia asali ya nyuki hawa wasiouma na kwamba asali yake ina soko zuri. Kwa sasa ana jumla ya mizinga 20 ya nyuki ingawaje changamoto anayokutana nayo katika kupanua ufugaji huo ni ugumu kuwapata kutoka msituni kwani huwa wanajificha sana. “Ninawashauri watanzania kupenda kutumia zaidi asali kwani ni kinga ya maradhi mengi kwenye mwili wa binadamu. Hiki ni chakula kizuri mno hasa kwa watoto, nawaambia wazazi wasiwape watoto pia badala yake wawape asali,” anasisitiza. Ukaushaji matunda na mbogamboga Bw. Zuberi Sultani kutoka Korogwe Tanga kwenye maonesho haya yeye alionesha utaalamu wa kuhifadhi matunda na mboga mboga kwa njia ya ukaushaji. Miongoni mwa matunda yanayosindikwa ndizi, mananasi, maembe pamoja na zikiwemo mbogamboga kama vile mchunga na kisamvu. Anafafanua kuwa usindikaji wa matunda na mboga unafanyika ili kuyahifadhi na kutumika kwa msimu wote wa mwaka, wakulima wengi wa matunda hawanufaiki na kilimo hicho kwa sababu msimu wa mavuno matunda hushuka bei na mengine kuoza kwa kuwa wakulima hawana ujuzi wa kuyahifadhi. Anasema ukaushaji huu hutumia teknolojia rahisi, ambayo yeye amekuwa akiwafundisha wakulima wenzake bure ili nao wanufaike. “Tunakausha kwa kutumia chombo maalum ambacho hufunikwa na turubali jeusi juu kwa lengo la kupunguza ukali wa mionzi ya jua na kuhakikisha kwamba haileti madhara kwa watumiaji. Matunda haya yanapokaushwa huzidishiwa ubora kwani sukari yake huongezeka mara dufu ukilinganisha na tunda linavyokuwa katika hali ya kawaida.” “Mtanzania yeyote anaweza kusindika matunda na hata mboga Watazamaji wakitoka kwenye banda la MVIWATA kwani si kazi ngumu bali inahitaji usafi na uangalifu wa karibu ili kuhakikisha bidhaa inakuwa katika kiwango cha juu cha ubora ili isilete madhara kwa binadamu,” anaeleza. Bw. Sultani anasema kwamba utaratibu wa kusindika matunda huanzia katika utafutaji wa matunda mazuri yaliyoiva kiasi, unayaosha kuyakata vipande vidogo vinavyoweza kukauka upesi, kisha kuyaweka kwenye chombo kinachotumia mwanga wa jua kukaushia na baada ya hapo huhifadhiwa kwenye vifungashio maalum tayari kwa kuuzwa. Utaratibu huu unafanana vile vile katika mboga za majani ambapo huoshwa na kuchemshwa kidogo jikoni kisha huanikwa katika chombo kinachotumia mwanga wa jua kukaushia mazao na baada ya kukauka huwa tayari kufangashwa kwa ajili ya kuuzwa ama kuliwa. Usindikaji zao la Muhogo Bw. Juma Nyamgunda kutoka Mkuranga Pwani anasema katika kuhakikisha kwamba zao hili la muhogo linaongezewa thamani wakulima wa Mkuranga wameanza kusindika muhogo na kupata unga ambao huutumia katika kutengeneza Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011 vitu mbalimbali ikiwemo keki, biscuti, tambi, chinchin, chapati na maandazi kazi ambayo hufanywa kwa wingi na kina mama kwa lengo la kuongeza kipato cha familia. Bw. Nyamgunda anasema usindikaji unawapa faida kubwa wakulima ukilinganisha na walivyokuwa wakiuza muhogo ghafi kwa walanguzi na katika maonesho ya NaneNane amepata wateja wengi wanaohitaji kiwango kikubwa cha unga wa muhogo. Ludewa wahimizwa... Inatoka uk. wa 16 wadogo ambao kipato chao ni kidogo ama cha wastani. Alisema katika hatua ya awali ya miaka mitatu ya majaribio, mradi unatekelezwa kwenye wilaya mbili ambazo ni Kyela mkoani Mbeya na Ludewa mkoani Njombe. Katika hatua ya pili ya mradi utajumuisha wilaya za Mbinga mkoani Ruvuma na Makete mkoani Njombe. Kwa ujumla mradi unalenga kuwafikia na kuwanufaisha wakulima,wafugaji na wavuvi wapatao 15,000 wa hapa nchini. 17 MAKALA Mtweve: Ubunifu wangu wa redio umenufaisha wengi Anamiliki Mlangali Coconut FM H atimaye ndoto ya siku nyingi ya Bw. Ditrick Mtweve (18) mkazi wa Kata ya Mlangali wilayani Ludewa mkoa mpya wa Njombe imeweza kutimia baada ya kutumia ubunifu wake kutengeneza mtambo wa redio unaowanufaisha wakazi wengi wa wilaya hiyo. Mtambo huo uliotokana na kuunganishwa kwa vifaa mbalimbali kutoka katika redio mbovu na vifaa vinginevyo kama miti ya mianzi, boksi na vyuma vya baiskeli, ulianza kurusha matangazo yake mwaka jana katika kijiji cha Lufumbu na kwa sasa matangazo hayo yanawafikia wakazi wa vijiji sita katika Kata ya Mlangali. Kwa sasa redio hii ambayo ameipa jina la ‘Mlangali Coconut FM’ imekuwa ikitumiwa na viongozi wa vijiji vya kata ya Mlangali kutangaza taarifa muhimu kama vile mikutano ya vijiji, kampeni ya chanjo pia shughuli muhimu za kijamii. Vile vile imekuwa kichocheo kikubwa cha biashara na burudani kwani watu binafsi hutumia redio hiyo kutangaza biashara na huduma wanazotoa bila kusahau wapenzi wa muziki wa kisasa na nyimbo za injili ambao pia hupata fursa ya kupiga simu na kuchagua wimbo waupendao. Bw. Mtweve ambaye ni mtoto pekee kwenye familia na yatima (aliyefiwa na baba) alisema kuwa alitamani siku moja katika maisha yake awe mtangazaji maarufu wa redio kubwa hapa nchini na ikiwezekana aweze kumiliki redio yake mwenyewe na mapema mwaka 2009 akiwa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Lufumbu ndoto yake ilianza kutimia ambapo kwa kutumia maarifa madogo aliyoyapata shuleni alianza kubuni na kutengeneza mtambo huo wa redio. “Wakati naanza ilikuwa kama mchezo, kwanza nilichukua muda nikitafakari kwanini ‘Microphone’ zisizo na waya zinasafirisha sauti na kuupeleka katika mitambo. Baadaye nilichukua kifaa ‘transistor’ kilichotumika katika ‘Microphone’ hizo na vifaa vingine nilivichukua katika redio mbovu na kuviunganisha,” alisema Bw. Mtweve. Baada ya kukusanya vifaa mbalimbali kutoka kwenye redio mbovu na maeneo mengine pia alitumia betri za kawaida hatimaye kufanikiwa kuwasha mtambo wake na redio yake kuanza kusikilizwa na wananchi waishio jirani. Uwezo huu wa redio kusikilizwa na watu wa jirani ulianza baada ya Mwanachama na mhamasishaji wa MVIWATA Mlangali akizungumza kwenye kipindi cha karibu mgeni 18 kuboresha baadhi ya vifaa vyenye uwezo mkubwa zaidi ili kuwezesha mawimbi ya sauti kufika mbali zaidi na hatimaye alifanikiwa kufunga mnara wa mlingoti wa miti iliyounganishwa wenye antena ya waya wa kawaida juu yake na kuutundika juu ya kilele cha mlima uliokuwa jirani na nyumbani kwao. “Haikuwa kazi ndogo kwani mwanzoni niliweka mtambo huu nyumbani kwetu ambako ni bondeni ikawa inasikika nyumba kadhaa za jirani tu. Ilibidi kutumia muda mwingi na kuumiza akili ili kuweza kufikia mafanikio, baadaye nikapata wazo la kuhamia hapa mlimani kwenye nyumba ya rafiki yangu ambaye amenipangishia chumba kimoja,” alisema Bw. Mtweve alipozungumza na Pambazuko ndani ya studio yake kijijini Lufumbu. Bw. Mtweve alisema anafurahia ubunifu wake lakini bado anakabiliwa na changamoto nyingi sana ikiwemo kutokujua sheria “mpaka sasa redio hii naimiliki kienyeji kwa lengo la kukuza kipaji changu na kuiwezesha jamii inayonizunguka kunufaika na kipaji hicho, sijui taratibu za kuisajili zikoje,” alisema Bw. Mtweve. Tatizo jingine ni kukosa mtaji wa kuweza kununua vifaa vya kisasa na kuwa na jengo maalumu la studio ya utangazaji. Kwa hivi sasa Bw. Mtweve anaishi na mama yake baada ya baba yake kufariki wakati yeyé akiwa na umri wa miaka 10 na alikuwa akisoma darasa la tatu wakati huo. Endelea Uk wa 19 Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011 MAKALA Inatoka uk. wa 18 Alisema hali hiyo ya kubakia na mzazi mmoja imechangia kwa kiasi kikubwa umasikini katika familia yao baada ya mama yake kutokuwa na uwezo wa kifedha na hata afya yake kutokuwa thabiti kutokana na maradhi yanayomsumbua na hivyo wakati mwingine hulazimika kusimamisha kazi za redio ili kumsaidia mama yake shughuli za shamba. “Redio hii huwa hewani kwa masaa 24 kila siku kwa kurusha muziki hewani na salamu, short time za muziki wa bongo flava na chaguo la msikilizaji, na inapofika 4.00 usiku hurudi nyumbani na kuuacha mtambo ukipiga muziki mpaka alfajiri ninapoingia kuendelea na vipindi,” alisema Bw. Mtweve. Awali kabla ya kufikia kiwango cha kurusha matangazo saa 24, alikuwa akitumia redio inayotumia kanda za kawaida na baadaye alipata redio yenye kutumia ‘memory card’ ambayo imekuwa ikimwezesha kupiga muziki muda wote. Hata hivyo eneo hili la Mlangali bado halijafikwia na huduma ya umeme waTanesco hali inayomlazimu kutumia betri za kawaida za redio kuendeshea mtambo wake. “Nimekuwa nikiwategemea watu mmoja mmoja ambao wanavutiwa na huduma hii, kuninunulia betri, kuna wakati zinapoisha na hakuna mtu wa kununua ninalazimika kuzima matangazo kwa siku kadhaa, hadi ninapoenda kufanya kibarua mahali Hii ndiyo mitambo ya kurusha matangazo ya COCONUT FM na kupata fedha, nitafurahi kama kijijini kwetu tutapata umeme.” Wakazi wa vijiji vya kata hiyo ambao hawakuwa wakimiliki redio majumbani mwao kwa sasa wameanza kumiliki redio na kusikia matangazo na burudani kutoka katika mtambo wa redio ya kijana huyo. Wafanyabiashara wa Mlangali nao kwa uchache wameanza kuitumia fursa ya redio hii kujitangaza na humlipa kati ya Sh 500 na 1,000 ili kuweza kurushiwa matangazo yao redioni kwa siku kiwango ambacho kijana huyo anasema kuwa kimekuwa kikimsaidia kwa mahitaji binafsi yeye na mama yake. Anasema hata hivyo kuwa kwa sasa yeye ndiye mtangazaji na fundi mitambo wa redio hiyo.Anawaomba wananchi wenye uwezo na ambao wanaguswa na kipaji chake kumsaidia kuweza kwenda kusoma katika chuo cha ufundi stadi (Veta) ili kuongeza maarifa. Sambamba na hilo, kijana huyu anaeleza kuwa kamwe ndoto zake Afisa programu wa MVIWATA Bw. Laurent Kaburire akimtambulisha Bw.Ditrick Mtweve kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 16 wa MVIWATA Oktoba 24, 2011 mjini Morogoro Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011 hazitaishia hapo, bali ataendelea kubuni mbinu mbalimbali na kuboresha kazi yake hiyo na kiu yake ni kuona siku moja redio hiyo inasikika katika wilaya nzima ya Ludewa. Bw. Mtweve anaishukuru jamii inayomzunguka kwani pamoja na kukosa fedha sambamba na ufinyu wa elimu ya ufundi alionayo, bado jamii hiyo imekuwa msaada mkubwa sana kwake kwani wameweza kutambua umuhimu wake katika jamii kwa kumpati redio mbovu ili aweze kutoa vifaa muhimu kwa kazi yake. Hii ndiyo studio ya COCONUT FM Kwa kutambua mchango mkubwa anaoutoa katika kuhakikisha jamii ya vijijini inafikiwa na habari, Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA), ulimwalika Bw. Mtweve na kuwezesha kushiriki kwenye Warsha ya Kitaifa na Mkutano Mkuu wa 16 wa MVIWATA uliofanyika Oktoba 24 na 25, 2011 mjini Morogoro. Mojawapo ya mada iliyojadiliwa kwenye warsha hiyo na kugusa hisia ni “haki ya upatikanaji wa habari vijijini” ambapo wakulima kutoka vijiji mbalimbali walieleza jinsi ambavyo wanakabiliwa na changamoto katika kupokea na kutoa habari katika kutokana na vyombo vingi vya habari kuegemea zaidi mijini. Hivyo washiriki hao walipongeza ubunifu wa kijana huyo na kuomba MVIWATA kama taasisi kuendelea kumuunga mkono na kumtumia kutangaza zaidi habari za wakulima. Jambo hilo limetekeleza na hivi sasa baadhi ya vipindi vya SAUTI YA MVIWATA vinarushwa kupitia redio hiyo Mlangali Coconut FM. 19 KUTOKA MITANDAONI Viongozi wa masoko ya wakulima wapewa ushauri Na Susuma Susuma, Morogoro V iongozi wa masoko ya wakulima wametakiwa kutojenga uhasama na viongozi wa awamu zilizopita bali wawatumie kujifunza na kupata mbinu za kuyafanya masoko hayo kuwa endelevu. Wito huo umetolewa Julai 30,2011 mjini Morogoro na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Soko la Wakulima la Kibaigwa Kongwa mkoani Dodoma Bw. Richard Kapinye kwenye kikao cha pamoja cha wakurugenzi wa bodi za masoko sita yaliyojengwa na MVIWATA kwenye vijiji mbalimbali hapa nchini. Bw. Kapinye alisema “tuepuke uhasama unaofanywa na wanasiasa kwamba akishamuondoa mwenzake madarakani wanakuwa maadui wanaotafuta kuharibiana kila wakati, sisi tuwe tofauti tuwatumieni wenzetu waliotutangulia ili tuweze kufanikiwa.” Kadhalika Bw. Kapinye ambaye pia ni mkulima mdogo na Diwani wa Kata ya Kibaigwa, aliwataka wajumbe wenzake kutumie vyema dhamana waliyopewa kwa kusimamia haki na maslahi ya wakulima huku akitahadharisha tabia inayojitokeza ya baadhi ya wakulima wanaopata nyadhifa za kisiasa, kusahau walikotoka na kuanza kuwakandamiza wenzao. Akawahimiza pia wakulima ili kupanua uelewa wawe na hamasa ya kujifunza mambo mapya kwa kusoma magazeti na machapisho mengine likiwemo jarida la wakulima la Pambazuko (Sauti ya Wakulima) linalochapishwa na MVIWATA. Kwa upande wake mratibu wa kikao hicho ambaye pia ni Afisa Masoko wa MVIWATA Bw. Jimmy Mongi aliwahimiza wakurugenzi hao wa bodi, wawatumie wajumbe wenye uzoefu walioko masoko ya jirani ili kuwafundisha na kuwajengea uwezo wajumbe wapya wanaochaguliwa. “Tunaamini kuwa wajumbe wa mwanzo kwenye bodi hizi, walijengewa uwezo mkubwa kielimu kwa kupelekwa ziara mbalimbali za mafunzo, hivyo tunapofikiria kupata mafunzo kwa wajumbe wapya tuwafikirie kwanza hawa, ni wenzetu watatupatia elimu hiyo kwa gharama ndogo na pale panapohitajika utaalamu zaidi ndipo tuombe msaada wa MVIWATA ofisi kuu,” alisema Bw. Mongi Kwa upande wake Bibi. Honolata Blass, mjumbe wa bodi ya Soko la Nyandira alisema bodi za wakurugenzi zinapaswa kuwa na ubunifu ili kuongeza ufanisi wa masoko. “Kwa upande wetu ubunifu wa bodi umesaidia kuongeza mapato ya soko kila mwaka na kulifanya soko kuwanufaisha wakulima wengi,” alisema Bibi Blass. Bodi hizo za wakurugenzi wa masoko hukutana mara kwa mara kwa lengo la kuwapa wadau hao fursa ya kushirikishana uzoefu wa mafanikio, changamoto na kuweka mikakati ya uendelevu wa masoko hayo ya wakulima. Kikao hiki kilikutanisha wakurugenzi 25 wa bodi za masoko ya Kibaigwa wilaya ya Kongwa, Nyandira wilayani Mvomero, Tandai na Tawa Morogoro Vijijini, Mkata wilaya ya Handeni na Igagala wilayani Njombe. Masoko hayo yalijengwa na MVIWATA tangu mwaka 2004 na kukabidhiwa kwa halmashauri za wilaya na uendeshaji wake kubakia mikononi mwa bodi za wakurugenzi ambazo zinaundwa na wakulima na wawakilishi wa halmashauri. Kufunga mipaka ya kuuza mazao nje ya nchi kunamsababishia hasara mkulima Na Martin Pius, Babati S erikali imetakiwa kutotoa amri za kuzuia mazao ya chakula yakiwamo mahindi kuuzwa nje ya nchi kwani kufanya hivyo inawasababishia hasara wakulima na kuwakatisha tamaa ya kuongeza uzalishaji. Rai hiyo imetolewa Julai 13, 2011 na Mjumbe wa Bodi ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bibi Rehema Mwateba wakati akifungua Mkutano Mkuu wa nne wa MVIWATA Manyara uliowashirikisha wanachama wa wilaya tano za mkoani Manyara. Bibi Mwateba alisema Serikali itambue kwamba inatumia mfumo kandamizi kwa mkulima kwa kufunga mipaka ya kuuza mazao ndani na nje ya nchi bila ya kujali kuwa hilo ni hitaji la mkulima la kuendesha maisha yake yanayotegemea hasa bei nzuri ya mazao. Alisema kuzuia biashara ya mazao kwa kutumia kisingizio cha kinga ya njaa hakitavumilika kwani wakati utafika wakulima watachukua hatua ambazo huenda zikawa na madhara makubwa kwa taifa. “Serikali inatakiwa kufanya utafiti wa haraka kubaini maeneo yaliyoathirika na njaa na kupeleka chakula cha msaada na kwa maeneo mengine yasiyokuwa na uhaba wa chakula wakulima waruhusiwe kuuza mazao yao nje ya nchi ili kuweza kupata faida,” alisema. Makamu Mwenyekiti wa MVIWATA Manyara, Bibi Fatuma Kimolo, akizungumza kwenye mkutano huo alisema kama serikali Endelea Uk wa 21 20 Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011 KUTOKA MITANDAONI Wakulima washauriwa wasidai posho za mafunzo Na Ledis Kigala, Kyela B aadhi ya wakulima wilayani Kyela mkoani Mbeya wamewaasa wenzao kutanguliza mbele manufaa ya elimu wanayopata katika kshiriki kwao kwenye mafunzo badala ya kudai posho. Wamesema mtindo wa kudai posho kwanza, unawafanya wakulima kushindwa kupata elimu muhimu kwa ustawi wa maisha yao. Walitoa wito huo wakati wa kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo katika uzalishaji bora wa mazao ya mpunga, mahindi, kokoa na ufugaji wa wanyama. Mmoja wa wakulima hao Bw. Goden Mwantimwa wa kijiji cha Lutusyo kata ya Muungano wilayani Kyela alieleza kufurahishwa na elimu na mafunzo yanayoendelea kutolewa na Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) na kuahidi kuwa ataendelea kushiriki kwa sababu kwake elimu ni muhimu kuliko posho. “Mimi niko tayari kujitolea kushiriki mafunzo mengine hata kama itakuwa nje ya hapa, nawaombeni wenzangu tuithamini sana elimu hii ili itusaidie katika kuboresha kilimo chetu,” alisema Bw. Mwantimwa. Kwa upande wake Bw. Musa Mwangongolo mkulima wa kijiji cha Makwale kata ya Makwale, alisema tabia ya kudai posho kutoka kwa waandaaji wa mafunzo imesababbisha wadau mbalimbali wa maendeleo kuwakimbia wakulima wa eneo hilo. Alisema matokeo yake ni waandaaji kuhamishia mafunzo hayo katika maeneo mengine na kuwaacha wakulima wa Kyela wakiwa hawana la kufanya. Alisema kimsingi wakulima siyo masikini wa kipato, na kwamba umasikini wao ni maarifa ambayo MVIWATA imeonyesha njia ili kufikia azma ya kuboresha kilimo ili kiwe chenye tija zaidi. Mafunzo hayo yaliyofanyika kuanzia tarehe Septemba 21 hadi Oktoba 11, 2011 kwenye vijiji 18 vilivyoko kwenye kata 10 za wilaya ya Kyela yalilenga kuwapa elimu wakulima ya kuongeza Bibi Edina Mwakipesile mkulima wa kijiji cha Mwiyonde wilayani Kyela akielezea dhana ya MVIWATA kwa wakulima wenzake walioshiriki mafunzo ya kujengea uwezo vikundi, yaliyoandaliwa na MVIWATA mjini Kyela. Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011 uzalishaji pamoja na ubora wa mazao na mifugo. Mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Uhifadhi Mazingira na Kukuza kipato kwa wakulima wadogo waishio kandokando ya ziwa Nyasa, unaotekelezwa na MVIWATA kwa ufadhili wa Shirika la Swedish Cooperative Center (SCC). Afisa Mradi huo Bw. Ledis Kigala, alisema, mradi huo unatekelezwa kwenye kata 10 kati ya kata 20 za wilaya ya Kyela ambazo ni Bujonde, Ikolo, Ngonga, Ikimba, Katumbasongwe, Ipande, Mwaya, Ipinda, Muungano na Makwale. Kufunga mipaka ya kuuza mazao nje ya nchi... Inatoka uk. wa 20 imeamua kufunga mipaka ya kuuza chakula inatakiwa sasa ijipange kununua mazao hayo ya wakulima kwa bei yenye tija badala ya kupanga bei yake isiyokuwa na maslahi kwa mkulima. Bibi Kimolo alisema kufungwa mipaka kipindi hiki kumesababisha bei ya mahindi kushuka kutoka Sh. 45,000 na kufikia Sh 30,000 kwa gunia, hali ambayo inarudisha nyuma maendeleo ya mkulima. Alihoji kuwa iweje watumishi wa Serikali wapandishiwe mishahara kila mwaka kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha, huku mkulima akiwekewa masharti ya kupata ujira stahiki ili aweze kukabiliana na hali ngumu ya maisha magumu kwa kuuza mazao kwenye soko lenye bei nzuri? Alisema umefika wakati sasa, serikali iache kutumia raslimali nyingi kwenye kutoa na kusimamia matamko ambayo hayana tija kwa ustawi wa wakulima badala yake nguvu na raslimali hizo zitumike kuimarisha miundombinu ya kilimo ili kiweze kuwa na uzalishaji wa kutosheleza mahitaji ya chakula na ziada ya biashara. 21 KATUNI MUDA MREFU NAONA UNASOMA HILO GAZETI LINA HABARI GANI? AH! GAZETI LENYEWE LINA HABARI ZA MJINI TU, SIONI HATA HABARI INAYOGUSIA KERO ZETU. OH! KWELI NDIO SABABU WAANDISHI WENGI WANAJISHUGHULISHA NA MAMBO YA MJINI TU. WEWE UTAZIPATA VIPI HABARI ZA MJINI WAKATI GAZETI LINACHUKUA SIKU 4 KUFIKA HAPA AHA HAHA SIO HIVYO, NI MFUMO WA TAARIFA YA MASOKO MVIWATA. NAPATA TAARIFA KUPITIA SIMU YANGU YA MKONONI TU. 22 SI NINATUMIA SIMU YANGU YA MKONONI ONA SASA MIMI SIJUI HATA KUTUMIA HUO MTANDAO, HEBU FIKIRIA NI WATU WANGAPI HAWAPATI HIZO HABARI? HIVI KWANINI SISI WATU WA VIJIJNI HABARI ZETU HAZIANDIKWI? NDIO MAANA HAKUNA HABARI ZA KILIMO KWENYE MAGAZETI MENGI! NANI ATAKUJUA HUKU KIJIJINI AH! MBONA MWAKA JANA WAANDISHI WALIKUJA WENGI TU HUKU HABARI ZITAFIKAJE YAANI UNAWAULIZA WATU WA MJINI KWA SIMU!? LAKINI MIMI NAONA BADO HIZO HABARI UNAZOPATA KWENYE SIMU HAZIZUNGUMZII KILIMO WE UMESAHAU!? SI KWA SABABU WALILETWA NA WAHESHIMIWA KWENYE KAMPENI LAKINI MIMI NAPATA TAARIFA NYINGI ZA MASOKO YA MJINI KILA SIKU. HAPANA NATUMIA MTANDAO MTANDAO WA WAKULIMA MVIWATA? HAWA WAANDISHI WANAUPENDELEO BWANA! Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011 KATUNI HUKU HABARI ZA KILIMO HAZIANDIKWI NA WAKIANDIKA GAZETI LINACHELEWA KUFIKA AU LISIFIKE KABISA. NDIO, BARABARA SIYO NZURI KUWEZA KUSAFIRISHA MAGAZETI YAFIKE HARAKA LAKINI TUSIWALAUMU SANA WAANDISHI, MIMI NAFIKIRI SERIKALI YETU IANGALIE NA MIUNDO MBINU YETU SASA HUKU KWETU BARABARA NI TATIZO LABDA TUTAPATA HIZO HABARI KWENYE RADIO NA TV KWELI TUTAPATAJE MAENDELEO KAMA HATUJUI TAARIFA YA KILA SIKU YA MASOKO, UCHUMI NA SIASA?! WATU WENGI WANAKUFA KWA KUKOSA ELIMU YA AFYA NA KUAMINI IMANI POTOFU ZA KWENDA KWA WAGANGA. ACHA UCHUMI TU, IDADI KUBWA YA WATANZANIA WANAISHI VIJIJINI NA UMEME HAKUNA HAYO MATANGAZO WATAYAONA VIPI? HATA KAMA ZIPO KUTOKANA NA HALI YA UCHUMI JE, TUTAWEZA KUNUNUA HIZI TV NA UMEME TUTAPATA WAPI? HAPO MAENDELEO YATACHELEWA SANA WANAHABARI WANA NAFASI KUBWA SANA YA KUELIMISHA WATU KUHUSU MATUMIZI BORA YA ARDHI, UFUGAJI BORA, BEI KATIKA MASOKO EH HAYO YOTE YANATOKEA SABABU HATUPATI HABARI SAHIHI! Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011 SASA NAFIKIRI MUDA MUAFAKA KWA WAHUSIKA KULIANGALIA HILI, SABABU VYOMBO VYA HABARI NDIO VINAWEZA KUWAELIMISHA WATU NA KULETA MAENDELEO HARAKA. ITATUSAIDIA KUPATA ELIMU SAHIHI YA AFYA, UKATILI DHIDI YA WANAWAKE HILI TATIZO LIFANYIWE KAZI, SABABU HATA RADIO ZENYEWE HAZIFIKI VIJIJINI NA ZINATANGAZA UDHAIFU TU WA WATU WA KIJIJINI INGAWA KUNA MAFANIKIO NA UBUNIFU WANAOUFANYA. Kwaherini KWELI BARABARA NI TATIZO KWA SABABU HATA MTOTO WA MZEE KIPARA ALIFARIKI KWENYE GARI KWA UBOVU WA BARABARA. JUZI NILIKUWA MJINI NIMEONA MATANGAZO MENGI YANAYOONESHA UDHAIFU WA WATU WA KIJIJINI TU INA MAANA HUKU HATUNA MAMBO MAZURI YA KUTANGAZA NA TV? wasalimie rafiki zangu’ 23 KUTOKA MITANDAONI Mfumo shirikishi unaharakisha maendeleo Na Gratian Cronery, MUCCoBS Shinyanga M aendeleo na ustawi wa miradi ya kijamii yanategemea zaidi ushirikishwaji wa jamii husika katika hatua zote. Katika nchi yetu hali ni tofauti ambapo miradi mingi wanayopelekewa wananchi hawakushirikishwa kikamilifu na kwamba kinachofanyika ni wao kupokea amri ya bwana mkubwa na kutekeleza wasichokijua. Hali hii ya kuwapelekea wananchi maamuzi badala ya wao kushiriki kuibua wazo na kuamua, imesababisha miradi mingi kutotoa matokeo chanya licha ya kugharimu fedha nyingi. Serikali katika kuwasaidia wananchi kutekeleza mipango ya maendeleo imekuwa ikianzisha miradi ikiwemo ya kujenga majengo kwa lengo la kuwasaidia wananchi, ila ukweli ni kwamba fedha na raslimali nyingi zimekuwa zikipotea bure. Iko mifano mingi ya miradi ya aina hii ambayo wananchi wanaipa jina la ‘miradi ya serikali’ kwa kuwa hawakushirikishwa na haikuwa kipaumbele chao. Miradi hii ni kama vile ya majengo ya masoko kwenye vijiji vya Ruvu Darajani mkoani Pwani, Buigiri wilaya ya Chamwino, Ruaha mkoa wa Iringa na kwingineko ambayo yametelekezwa na kuwa vichaka vya wezi ama nyumba ya wanyama na wadudu, baada ya wananchi kususa kuyatumia kwa kuwa haikuwa kipaumbele chao na kwingineko uchaguzi wa eneo haukuwa sahihi. Huu ni mmoja wa mifano ya 24 miradi mingi ambayo imeanzishwa na serikali pasipo kuwashirikisha wananchi katika kutoa mawazo yao na kupendekeza nini wanahitaji na ni kwa matumizi gani, na kama ni jengo likae sehemu gani. Mfumo uliotumika kuanzisha na kutekeleza kauli mbiu ya “kilimo kwanza” ni ule ule wa amri kutoka kwa bwana mkubwa, mkulima hana hiari cha kuchagua kukataa hata kama kilicholetwa ni mwiba kwake. Vile vile serikali imekuja na mpango wa zana bora za kilimo ikiwemo matrekta madogo (power tiller) na ambapo kwenye maeneo mengi hazihitajiki kutokana na aina ya udongo na mazingira. Baada ya wakulima kulazimishwa kuzinunua wamezigeuza matumizi na kuwa mashine za kufua umeme, kusukuma maji, kulanda mbao na kusaga unga. Hii ni changamoto kwa serikali na wadau wengine ambao wanatazamia kupeleka miradi kwa wananchi, kwamba ni vyema kuzingatia ushirikishwaji wa wananchi na mawazo yao yakaheshimiwa ili baadaye wakithamini wanachopelekewa. Watanzania wanakabiliwa na kero nyingi ambazo wangetarajia serikali kuwekeza nguvu zake zaidi kwa kutumia mfumo wa ushirikishwaji katika kuzitatua. Kwa mfano kuondoa kero ya ushuru mkubwa wa mazao unaotozwa kwenye vizuizi vya kila barabara ya nchi hii inayoelekea mjini. Kuna maana gani kumpa ruzuku ya pembejeo mkulima na baadaye kumkamua faida yote inayotokana na mavuno hayo? Kama ushuru unatozwa ili kufidia fedha za ruzuku, ni bora ruzuku hiyo ifutwe wakulima wajitafutie pembejeo na wawe huru kusafirisha mazao yao. Hili linaweza kutatuliwa kwa njia shirikishi ya majadiliano. Kwa kufanya hivyo tunaweza kutengeneza mipango na miradi endelevu kwa vizazi na vizazi ambayo italeta tija katika nyanja zote za maisha kisiasa, kiuchumi na kijamii. Kwa upande mwingine tumeona mfano wa miradi ya ujenzi wa masoko inayotekelezwa na MVIWATA kwa mfumo shirikishi imefanya vyema na wakulima wanathibitisha matokeo yake. Mwenyekiti wa MVIWATA Shinyanga Bw. Charles Ndugulile anasema siri kubwa ya mafanikio ya masoko ya MVIWATA ni kuzingatiwa kwa dhana ya ushirikishwaji. “MVIWATA imefanikiwa kufanya hivyo kwa hutoa mafunzo mazuri ya jinsi ya kushirikisha jamii kuanzia ngazi ya kaya hadi taifa ambayo huambatana na mafunzo ya andiko la mradi, uendeshaji na usimamizi wa miradi, uhasibu wa vikundi na mashirika pamoja na taasisi pamoja na mifumo ya masoko na biashara,” anasema Bw. Ndugulile. Endapo serikali na wadau wengine wa maendeleo watatumia dhana hii ya ushirikishwaji wa jamii kwa mapana na kuiona kama fursa ya kuleta mabadiliko chanya kwa jamii ya Watanzania, hakika taifa litapiga hatua ya ukuaji wa kasi wa maendeleo. Jamii kwa upande wao pia wanapaswa kujipanga vyema kushiriki katika mradi kwa kuibua wazo, kupanga, kutekeleza na kusimamia na baadaye kujipima kiwango cha uwajibikaji wao kwenye miradi husika. Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011 MAWAKALA Jipatie nakala ya Jarida la Pambazuko katika ofisi za MVIWATA ngazi za kati zifuatazo Mratibu MVIWATA Morogoro S.L.P 3220 Morogoro Mahali: Uwanja wa Maonyesho NaneNane mkabala na ofisi za TASO Simu/Faksi: 023 261 41 84 Barua Pepe: [email protected] Mratibu MVIWATA Rukwa S.L.P 468 Sumbawanga Mahali: Jengo la Bethlehem Center – Barabara ya Msakila Faksi: +255 25 280 25 58 Simu: +255 764 232 747, +255 784 940 606 Barua pepe: [email protected] Mratibu MVIWATA Mbeya S.L.P 3015 Mbeya Mahali: Jengo la Bima na CRDB Bank (Ghorofa ya mwisho Simu: +255 784 979 397, +255 652 835 568 Barua pepe: [email protected] Mratibu MVIWATA Chunya Mahali: Jengo la Halmashauri, chumba Na.3 Barua pepe: [email protected] Mratibu MVIWATA Iringa S.L.P 918 Njombe Mahali: Jengo la Njoluma, Njombe mjini Simu: 0782 241 224, +255 767 241 224 Barua pepe: [email protected] Mratibu MVIWATA Kilimanjaro S.L.P 7389 Moshi Mahali: Mbuyuni sokoni- ghorofa ya GOLDEN GROWN LODGE Simu: +255 27 275 16 39, +255 784 720 320 Barua pepe: [email protected] Mratibu MVIWATA Kagera S.L.P 1753 Bukoba Mjini Mahali: Ofisi za Mayawa-Mtaa wa Rwamishenyi, Barabara ya Uganda Simu: +255 788 685818, +255 782 154961, +255 755 522 447 Barua pepe: [email protected] Mratibu MVIWATA Dodoma S.L.P 3293 Dodoma Mahali:Area C Dodoma eneo la INADES Formation Tz,mkabala na msikiti wa Area C Simu:255-26-2350013, +255 782 257 783, +255 767 881 352 Faksi: +255 26 2350744 Barua pepe: [email protected] Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011 Mwenyekiti MVIWATA Monduli (MVIWAMO) S.L.P 47 Monduli Mahali: Barabara ya Boma-Moringe Sekondari, Monduli Mjini Simu: 255-27-253 8029, +255 27 253 8337 Faksi: +255 27 253 8338 Barua pepe: [email protected] Mratibu MVIWATA Manyara S. L. P. 446, Babati Manyara Mahali: Barabara ya Nyerere SIMU: +255 27 253 0385 Faksi: +255 27 253 0707 Baruapepe: [email protected] Mwenyekiti MVIWATA Tabora S.L.P 175 Igunga Mahali: Mtaa wa Uarabuni Simu: +255 784 398 414, +255 782 219 551 Barua pepe: [email protected] Mratibu MVIWATA Zanzibar S.L.P 149 Zanzibar Mahali: Mwana kwerekwe- mkabala na shule ya sekondari M’kwerekwe A Simu: +255 773 926 955, +255 777 470 518 +255 783 651 135 Barua pepe: [email protected] Mratibu MVIWATA Ruvuma S.L.P 696 Songea Manispaa Mahali: Jengo la TTCL ghorofa ya 2 Simu: +255-25-2600626, +255 756 096 291 Barua pepe: [email protected] Mratibu MVIWATA Mkuranga S.L.P 56 Mkuranga Mahali: Karibu na Stendi ya Kimanzichana Simu: 0786 158 646 Barua pepe: [email protected] Mwenyekiti: MVIWATA Shinyanga S.L.P 1024 Shinyanga Mahali: Chuo cha Ushirika Moshi tawi la Shinyanga (Kizumbi) Simu: +255 763 740 675, +255 755 546 311 Barua Pepe: [email protected] Mwenyekiti MVIWATA Kigoma S.L.P 1144 Kigoma Mahali: Ndani ya ofisi ya KIKANGONET, Lumumba road jengo la NHC chumba 205 Simu: 0713 565 252, 0762 565 252 Barua pepe: [email protected] 25 IJUE MVIWATA Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania- MVIWATA Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) ni chombo cha kuunganisha wakulima wadogo ili kuwa na sauti moja katika utetezi wa maslahi yao ya kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na kisiasa. Mtandao huu ulianzishwa mwaka 1993 na wakulima wadogo. Kauli mbiu ya MVIWATA ni ‘Mtetezi wa Mkulima ni Mkulima Mwenyewe’. Falsafa, utume na dira ya MVIWATA Falsafa ya MVIWATA inajengwa katika ya misingi ya ushawishi na utetezi wa maendeleo ya wakulima wadogo katika nyanja za kiuchumi na kijamii; kuwezesha mawasiliano na kujifunza kwa kubadilishana uzoefu miongoni mwa wakulima. Utume wetu: Kuimarisha mawasiliano na kuwaunganisha wakulima wadogo kupitia vikundi na mitandao yao katika ngazi mbali mbali ili kujenga mtandao wa kitaifa wenye nguvu ya kuwezesha ushiriki na uwakilishi wa kweli wa maslahi ya wakulima wadogo katika ngazi zote za maamuzi. Dira yetu: MVIWATA ni kuwa chombo imara chenye nguvu za ushiriki na uwakilishi wa mawazo ya mkulima katika mchakato wa maamuzi ya kiuchumi, kijamii na kisiasa. Kuwa na uwezo wa kutekeleza na kufuatilia michakato na shughuli za maendeleo ya kiuchumi na kijamii yanayogusa maslahi ya wakulima wadogo. Malengo ya MVIWATA 1. Kuwezesha mawasiliano miongoni mwa wakulima wadogo ili kujenga kwa pamoja mbinu na mikakati ya ushawishi na utetezi kwa maslahi ya wakulima wadogo, kiuchumi na kijamii. 2. Kubadilishana mawazo, ujuzi na uzoefu juu ya kilimo na shughuli mbalimbali za wakulima ili kuboresha maisha na kuinua hali yao kiuchumi na kijamii. 3. Kuwakilisha wakulima wadogo katika mashauriano na serikali juu ya masuala mbalimbali yanayohusu au yanayoathiri ufanisi na maslahi ya wakulima wadogo wa Tanzania. Maeneo makuu ya mpango mkakati 1. Ushawishi na Utetezi: Kuwezesha wakulima wadogo kuwa na uwezo wa kutetea maslahi yao. 2. Uwezo wa kiuchumi: kuwezesha wakulima wadogo kuwa na uwezo wa kiuchumi kupitia njia za akiba na mikopo, kuunganisha wakulima na masoko na elimu ya ujasiliamali 3. Kuimarisha vikundi na mitandao ya wakulima kwa lengo la kujipanga na kujitetea. 4. Masuala mtambuka: Kujenga uelewa wa wakulima juu ya Ukimwi, Jinsia, Mabadiliko ya Tabia ya nchi. 5. Ujenzi wa kitaaasisi kwa lengo la kuimarisha shirika Muundo Muundo wa MVIWATA una ngazi tatu ambazo ni Ngazi ya Taifa, Ngazi ya Kati na Ngazi ya Msingi. Ngazi ya Kati inaundwa na mitandao ya kimkoa na kiwilaya wakati Ngazi ya Msingi inaundwa na mitandao ya Kata na Vijiji. Shughuli kuu 1. Kujenga uwezo wa wakulima wadogo kwa kupitia mafunzo shirikishi juu ya mbinu za ushawishi na utetezi, mbinu za kuimarisha uchumi wa wakulima wadogo na uendelevu wa rasilimali kwa njia za warsha, mafunzo, mikutano na ziara za mafunzo. 2. Kuhamasisha wakulima wadogo kujiunga katika vikundi vya kijamii na kiuchumi, mitandao ya msingi (kata na vijiji) na mitandao ya kati (mikoa na wilaya). Mpaka sasa MVIWATA imeanzisha mitandao ya kimkoa katika Mikoa ya Dodoma, Iringa, Kagera, Kilimanjaro, Manyara, Mbeya, Morogoro, Rukwa, Ruvuma, Shinyanga, Tabora na Tanga kwa Tanzania Bara. MVIWATA pia imeanzisha mitandao ya kiwilaya katika Wilaya za Monduli (Arusha) na Chunya (Mbeya). Tanzania Visiwani, MVIWATA Zanzibar imeanzishwa na kusajiliwa (Usajili namba 401). Mkakati unaendelea wa kuimarisha mitandao iliyopo na kuanzisha mitandao mipya. 3. Kukusanya, kuweka katika kumbukumbu na kusambaza habari zinazohusu ujuzi na uzoefu wa wakulima, sera za kitaifa na kimataifa kwa kupitia jarida la Pambazuko Sauti ya Wakulima, vipindi vya radio, vipeperushi, vijitabu na machapisho mengine. 4. Kuhamasisha na kuwezesha wakulima kubuni na kuendesha miradi shirikishi ya kiuchumi na uzalishaji kwa lengo la kuboresha uchumi wa wakulima wadogo kama vile vyama vya mazao, vyama vya kuweka na kukopa na masoko ya mazao. 5. Kuandaa mikutano na warsha kuhusiana na mada zinazowagusa au kuathiri maslahi ya wakulima wadogo. Uanachama na jinsi ya kujiunga na shirika MVIWATA ina wanachama wa aina tatu (3). Aina ya kwanza ni Wanachama wa Kawaida ambao wamegawanyika katika makundi mawili; a) Kikundi cha wakulima wadogo au b) Mkulima mdogo binafsi aliye mwanachama katika Kikundi au Mtandao. Mkulima atakuwa mwanachama wa kawaida wa MVIWATA mara tu Kikundi au Mtandao wake utakapokubaliwa kuwa mwanachama. Atapewa kadi ya uanachama na kikundi au mtandao utapewa cheti cha utambulisho. Aina ya pili ni Vyama, Mashirika na Mitandao ya Wakulima Wadogo. Vyama, Mashirika na Mitandao ya Wakulima Wadogo vinavyojishughulisha na utetezi na ushawishi wa maslahi ya wakulima wadogo vilivyosajiliwa chini ya sheria yoyote ya Tanzania katika Ngazi za Wilaya, Mkoa au Taifa vinaweza kuomba kuwa mwanachama wa MVIWATA iwapo vinakubaliana kwa dhati na malengo na madhumuni ya Shirika. Aina ya tatu ni Wanachama Washiriki Ni mtu yeyote, taasisi au kikundi cha watu ambacho kinaunga mkono malengo na madhumuni ya Shirika. Mwanachama mshiriki anatamkwa na Mkutano Mkuu wa MVIWATA. Kila mwanachama, isipokuwa mwanachama mshiriki atalipa kiingilio na ada ya kila mwaka. Maelezo zaidi juu ya utaratibu wa kujiunga na ada yanapatikana kutoka kwa kiongozi au ofisi ya MVIWATA. Kwa mawasiliano zaidi Ofisi Kuu ya MVIWATA Mkurugenzi Mtendaji MVIWATA S.L.P 3220 Morogoro Simu: 023 261 41 84 Faksi: 023 261 41 84 Barua pepe: [email protected], [email protected]